Tuesday 4 October 2016

Re: [wanabidii] Chadema yatenga mamilioni kummaliza Prof. Lipumba. Wamuhofia kuvuruga mpango wao wa kuimeza CUF

Sounds like habari hii ni ya kupikwa. Who is Tazama?
em

2016-10-04 13:22 GMT-04:00 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
CHAMA cha demokrasia na maendeleo (chadema), kimeelezwa kutenga mamilioni ya shilling kwa lengo mahususi la kummaliza kisiasa mwenyekiti wa Cuf, Profesa Ibrahim Lipumba.

Habari za uhakika kutoka vyanzo kadhaa vya taarifa hivi zinabainisha wazi chadema kutenga mamilioni hayo kwa lengo la kuhahikisha, pamoja na mambo mengine Profesa halejei katika uongozi wa juu wa Cuf.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, hofu kuu ya chadema kwa profesa Lipumba iwapo ikatokea akarejea kwenye nafasi yake ya mwenyekiti, ni kuvurugika kwa mpango wao kabambe wa wa kuimeza CUF, ambao ulianza kuratibiwa kwa mafanikio na aliyekuwa mgombea urais wao katika uchaguzi wa mwaka wa jana, Edward Lowassa.

Mpango huo mpya wa kuimeza Cuf, chadema yenye nguvu ya kisiasa kwa upande wa Tanzania Bara na ilikuwa na mpango wa kuunganisha nguvu za kisiasa za chama hicho kwa upande wa Zanzibar ili ikiwezekana, kufikia mwaka 2020 vyama hivyo viwe vimeungana na kuwa chama kimoja.

Mpango huo mpya ulilenga kuunganisha umaarufu wa wanasiasa kisiasa wa wanasiasa wawili pande mbili za muungano, Edward Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad, ili kukiwezesha chadema kukamata dola katika pande zote mbili za muungano 2020.

Hata hivyo hatua ya sasa kurejea profesa Lipumba kutaka kurejea kwenye uongozi wa CUF na kwa sababu ya kulindwa nakatiba ya chama hicho, huku pia msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, akionekana kubariki hatua hiyo, imezidi kuuchanganya uongozi wa juu wa chadema, hali iliyowalazimu kutenga mamilioni ya shilling katika kuhakikisha kuwa suala hilo haliwezekani.

Mbali na kutenga fedha hizo zinazodaiwa kutoka kwa wale wanaoitwa marafiki wa Lowassa ili kummaliza kisiasa profesa Lipumba, uongozi wa chadema unadaiwa kujipanga kutumia kila aina ya silaha, ikiwemo vyombo vya habari na baadhi ya wasomi nchi kumdhalilisha Profesa Lipumba ili aonekana hafai machoni mwa jamii ya kitanzania.

Hata hivyo, pamoja na mikakati hiyo ya chadema kummaliza kisiasa Profesa Lipumba, kambi ya mwanasiasa huyo, ambayo tayari inakalia ofisi ya kuu ya Buguruni, Dar es Salam, imeapa kupambana hadi mwisho, huku ikiweka bayana "daima haki itashinda".

Kwa mujibu wa kambi ya Profesa Lipumba mgogoro wa sasa ni baina ya kundi la waasi nan a wavunjaji wa katiba wakiongozwa na katibu mkuu Maalim Seif Sharif Hamadi na kundi la watetezi, walinzi na walinzi wa katiba ya chama hicho wakiongozwa na Profesa Lipumba.

Kutokana na hali hiyo kundi la Profesa Lipumba linasema wazi kwamba hata kama uongozi wa chadema utaamua kukusanya mamilioni ya shilingi kwa ajili kwa ajili ya kufadhili kundi la la waasi linaloongozwa na Maarif Seif Sharifu Hamadi, ni wazi fedha hizo zitateketea bure kwa maelezo kuwa hakuna mahala popote duniani ambako dhulma ikashinda.

Afisa mmoja wa Cuf, aliyeko kambi ya Profesa Lipumba, Abdul Kambaya, amekiri kufahamu mpango huo wa chadema kutenga mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kummaliza mwenyekiti wao, ikiwa ni pamoja kuhakikisha harejei tena kwenye uongozi wa juu wa chama hicho.

"Tunafahamu sana kundi la maarim Seif linaendeshwa na chadema na wao ndio wanaoamua cha kufanya. Tunafahamu chadema wametenga fedha nyingi sana kwa ajili ya kuhahikisha profesa Lipumba harejei kwenye uongozi wa juu wa Cuf, lakini niwahakikishie daima haki itashinda dhulma tu" anasema Kambaya na kuongeza

"sisi tupo ofisini, wao wapo msituni. Hii ni vita kati ya watetezi wa katiba, hivyo basi kamwe hawaezi kushinda vita hii, na ndio maana Profesa Lipumba anaendelea na majukumu yakle ya kukisuka upya chama chetu, huku wao wakihangaika huko nje, wakidhani Chadema itawasaidia.

Chanzo Tazama
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment