Thursday 27 October 2016

Re: [wanabidii] Re: [TPN] China Rise fall and rise again

Kaka Olomi umeongea vyema. Huu ulinganisho unaotolewa ya nchi zetu na za Asia ni wa kisiasa zaidi, pengine kwa nia njema ya kuhamasisha watu kuanza kufikiri, lakini siyo wenye uhalisia  Ni lazima kabla ya kulinganisha kuangalia historia ya pande zote mbili. Historia ya nchi za Asia ni ya karne nyingi sana za mabadiliko. Ni nchi zilizofanya biashara na nchi za bara la ulaya kwa muda mrefu.... Na kuna ushahidi kuwa ustaarabu mwingi tunaouona kwa wazungu wa bara la ulaya ulikuwepo Bara la Asia karne nyingi sana. Kwa bara la Afrika, historia iliyoandikwa ya mahusiano na Ulaya ni ya nchi ya Misri, ambayo ndiyo iliyorutubisha uchumi, utamaduni na hata siasa za ulaya. Afrika haikuwepo kama bara lenye utambulisho wa pamoja kiutamaduni, uchumi na hata kiutawala. Hata nchi ya Tanganyika, Rwanda, Kenya, Somalia nk hazikuwepo kwenye tramani  katika ulinganisho unaofanywa leo hii. 

Mahusiano au ulinganisho unaofanywa kwa sasa ni mwendelezo wa fikra za kutawaliwa na wakoloni tu... Kwa wenzetu wa baadhi ya mabara ya Asia uhuru kwao ilikuwa ni ukombozi kurudi kwenye taifa, utamaduni na uchumi wao. Tofauti na Tanzania ambapo kupata uhuru ndiyo ulikuwa kama mwanzo wa kujenga taifa jipya la Tanganyika isiyo na mila, utamaduni, lugha uchumi, na utawala. Kujenga taifa ni mchakato wa muda mrefu. Kwa bahati mbaya nchi za Afrika wakati zinapata uhuru zilikuwaa na changamoto ya kuanza kujenga haya yote.... Lugha (kwa bahati nzuri Mwalimu alitambua na kusimamia Kiswahili), Utamaduni (hadi leo sina uhakika kama tunao utamaduni wa Watanzania), Uchumi (kwa bahati mbaya tuliendeleza uchumi wa misingi ya mahitaji ya mkoloni... kuzalisha tusichokula na kubeza tunachokula), Utawala (tiliendeleza yale ya mkoloni), elimu (ilijengwa katika mahitaji na ustaarabu wa mkoloni) nk.

Katika mkutadha huu, hatuhitaji kujilinganisha bali kuweka nguvu kujenga misingi mikuu ya utaifa kiutamaduni, lugha, uchumi, elimu nk. Kwa maoni yangu tunatakiwa kuweka nguvu kwenye utamaduni na elimu itakayotambua haya mengine badala ya kuendeleza na mfumo unaotugawa.  Nionavyo bado hatujaandika historia ya Tanganyika/Tanzania.... historia ambayo ikielezwa majumbani na wazazi, ikifundishwa shuleni na vyuoni itawajenga vijana wetu kukua katika uzalendo na hamu ya kujitambua kama taifa. Leo hii kua vijana wanasoma wakiota siku  watakayoondoka nu kuenda kuishi sehemu zingine hasa ulaya, pengine siyo mbaya, lakini wanakwenda huko na misingi gani itakayowafanya waendelee kutambulika kama Wayahudi wanavyotambulika? Kuna baadhi wanaobeza kuwa "I wish I was not born on this poor continent"  Leo tunaona wimbi kuwa la vijana wanahatarisha maisha kufuata maisha yaliyo bora Ulaya. Kwa nini? Kwa nini? na kwa nini viongozi wetu wamekaa kmiya tu na badala yake wanatuimbia eti Tanzania ilipata uhuru kipindi kimoja na nchi hii au ile?

Wasomi na waandishi, wagani wa tenzi, wahubiri na wanasiasa waendeleze kuijenga historia ya Tanzania, ikiwemo na kipindi hiki cha mpito ambao tumekengeuka na kutaka kukumbatia mila ze wengine. Kwa bahati nzuri bado tunayo rasmali ya asili ya kujenga uchumu, Hapoa Dr Olomi na wengine tuangalie njoa za kukimbia kuzitumia kwa kulind maslahi ya vizazi vijavyo. Kama Mwalimu alivyosema "Wakati ni huu, timiza wajibu wako.

Makongo     
----------------------------------------------------------------
Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32670, Dar es Salaam,
TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +253 24 2732125+253 24 2732125, Mobile:+253 758 270 254+253 758 570 253


On Thursday, October 27, 2016 3:06 PM, Donath R.Olomi <olomi@imedtz.org> wrote:



Wanazuoni,

Ni kweli huna nasikilizia watu wakiwemo wasomi wanavyolinganisha nchi za
Africa na Asia zilivyokuwa zinafanana miaka ya 60 kwa kipato na pengine
kupata uhuru na sasa jinsi tulivyoachwa.

Ukiingia ndani kidogo tu utakuta nchi za Afrika zilikuwa nyuma sana
kimaendeleo ya kiutamaduni, kisiasa, kiutawala, kielimu, nk na watu wake
walikuwa masikini mno.... uchumi uliokuwa unagawiwa ulikuwa wa wazungu
wachache na wahindi. Kulikuwa hakuna lugha, taifa, utamaduni wenye sura ya
kitaifa, mfumo wa utawala wa kitaifa, mfumo wa kielimu uliacha ule wa
mzungu, nk. Mataifa tunayojilinganisha nayo yalishakenga utamaduni wa
kitaifa kiasi cha kuwa la lugha iliyoandikwa, utawala wa asili wa kitaifa,
mila na desturi za kitaifa, kwa mamia hadi maelfu ya miaka

Hivyo tumeanza nyuma sana ukilinganisha na wenzetu

Tusipotambua mambo kama haya ya msingi na kuyajenga tunaishia kusema
Mwafrika kalongwa!



On Thu, October 27, 2016 01:14, Andrew R. Kwayu wrote:
% kwa wale wanaofikiri kwamba China imeanza jana, someni hapa. pia ona
% ni kwa nini ushirikiano na china ni bora zaidi kuliko magharibi.
%
http://www.globalresearch.ca/china-rise-fall-and-re-emergence-as-a-global-power/29644
%  ____________________________
% Andrew R. Kwayu,
% Head of ICT,
% MALF, Department of Agriculture
% Kilimo Complex,
% 1 Kilimo Road
% P.O. Box 9192,
% 15471 DAR ES SALAAM.
% Phone: +255 22 2861533
% www.kilimo.go.tz/[1] www.agriculture.go.tz[2]
%
%
% Links:
% ------
% [1] http://www.kilimo.go.tz/
% [2] http://www.agriculture.go.tz
%
%
% ----
%
% --
% You received this message because you are subscribed to the Google
Groups "Wanataaluma wa Tanzania" group.
% To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send
an email to wanataaluma+unsubscribe@googlegroups.com.
% For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
%


--
"Give your energy to things that give you energy.",

"Learn enough to begin and then learn as you go."


Dr. Donath R.Olomi
Chief Executive Officer
Institute of Management and Entrepreneurship Development (IMED)
Baraka Plaza 3rd Floor, Mikocheni, Old Bagamoyo Road
P.O. Box 35036 Dar es Salaam, Tanzania E-mail: info@imedtz.org, website:
www.imedtz.org
Mobile +255-754-296660

Publications available on the Internet

http://www.repoa.or.tz/documents/RR_12-2.pdf

http://www.businessenvironment.org/dyn/be/docs/31/BETanzania02.pdf

http://www.tanzaniagateway.org/docs/EnhancingSMEcontributiontoempandpovertyreduction.pdf

http://econpapers.repec.org/article/wsijecxxx/v_3a17_3ay_3a2009_3ai_3a01_3ap_3a103-125.htm

http://www.fek.umu.se/forskning/pub/Business.Studies/babsonpaperversion.pdf

http://www.sbaer.uca.edu/research/icsb/2011/763.pdf

http://fusionmx.babson.edu/entrep/fer/babson2001/I/I-R/I-R/i-r.htm

http://www.theigc.org/sites/default/files/EnterpriseMapofTanzania.pdf

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment