Tuesday, 4 October 2016

[wanabidii] Kinachoendelea ndani ya CUF ni sawa na chama cha Labour nchini Uingereza

Mtafuruku unaoikumba CUF kwa sasa hauna tofauti sana na kinachoendelea ndani ya chama cha upinzani cha Labour nchini Uingereza. Tofauti yake ni namna ambavyo labour wanatumia katika kukabiliana na changamoto/tatizo. Wakati viongozi wa CUF wanalaumu nguvu za nje, viongozi wa Labour wanalaumu nguvu za ndani.

Wabunge wengi na baadhi ya viongozi wa chama cha Labour hawamtaki kiongozi mkuu wa chama cha upinzani Labour, Jeremy Corbyn wakati wanachama wengi kutoka upande wa England wanamtaka.

Marumbano hayo yamepelekea kuitishwa tena uchaguzi mwingine ndani ya chama ambapo matokeo yake ameshinda tena kwa zaidi ya kura ambazo alishinda katika uchaguzi wa mwanzo uliofanyika Septemba 2015. Sina shaka kuwa hata Prof. Lipumba anaweza kushinda tena kiti cha Mwenyekiti kama uchaguzi utafanyika.

Kwa sasa wabunge wengi wa CUF na baadhi ya viongozi hawamtaki Prof. Lipumba wakati wanachama wengi hasa upande wa Tanzania bara wanamtaka aendelee kuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa.

Wabunge wengi na baadhi ya viongozi wa Labour wamesikika wakitoa malalamiko kwenye vyombo vya dola kuwa wanafanyiwa fujo na kundi la wanachama wanaomuunga mkono kiongozi Mkuu wa chama kama tunavyosikia kwa wabunge na viongozi wa CUF wakitoa malalamiko kwa vyombo vya dola nchini.

Prof. Lipumba inawezekana kwa sasa ni 'spend force' kwenye siasa za kitaifa kama ilivyo kwa kiongozi wa chama cha Labour lakini kama kuna mtu alidhani Prof. Lipumba amekwisha ndani ya CUF atakuwa alikuwa anaota ''ndoto za mchana''.

Mapokezi kutoka kwa wafuasi wake aliyopata katika ofisi ya CUF Makao Makuu baada ya ushauri na tamko la Msajili wa Vyama vya Siasa yanadhihirisha nguvu zake ndani ya CUF.

Katika mapokezi yake, wafuasi wake walijipanga kuanzia Barabara ya Buguruni (Rozana) inayoingia Ofisi Kuu za chama hicho na kuimba huku wakipuliza matarumbeta.

Uwingi wa wafuasi wake uliwafanya walinzi wa ofisi ya Makao Makuu CUF kukimbilia huku wengine wakiruka ukuta ili kusalimisha maisha yao. Hii inaonyesha katika siasa za Tanzania kinachoshinda si maneno mengi bali ni uwingi wa wafuasi kwa vitendo. Kama Prof. Lipumba angekuwa hana wafuasi wengi, ninaamini asingeweza kukanyaga Makao Makuu na kuingia ofisi kufanya kazi huku viongozi wengine wakikimbia.

Ukisoma kwenye mitandao bila kufanya uchambuzi makini unaweza kuamini kuwa Prof. Lipumba is finished ndani na nje ya CUF kama ilivyo kwa kiongozi wa Labour ambapo media nyingi zinazomilikiwa na mabepari zinamponda na kusema hafai ndani ya chama kwa sababu mtazamo wake niwa kidemokrasia ya kijamaa (democratic socialist).

Kwa jinsi Katiba za vyama vya siasa zilivyowapa Wenyekiti nguvu kubwa za kidikteta ndani ya vyama vya siasa. Kwa sasa Prof. Lipumba akisaidiwa na wafuasi wake wengi Tanzania bara amekabidhiwa rungu ambalo viongozi wengine waandamizi ndani ya CUF hawana.

Hata kejeli za kina Julius Mtatiro walizokuwa wanasema mbele ya vyombo vya habari kwa dharau ''We are nothing to talk with Prof. Lipumba'' itabidi kwa sasa waseme kwa upole na unyenyekevu, ''We have something to talk with Prof. Lipumba''.

Ninafahamu kuna baadhi ya watu watasema Prof. Lipumba anatumiwa na baadhi ya watu nje ya CUF lakini locus of control inabainisha, People with a strong external locus of control tend to blame external factors. Hii husababisha Self-handicapping katika kukabiliana na kutatua changamoto na matatizo ambayo yako ndani ya uwezo wao..

Kundi la Maalim Seif lazima likubali kuwa Prof. Lipumba amewapiga bao la kisiasa na kilichobaki kwa sasa ni kuukubali ukweli na kukaa pamoja kwa faida ya CUF kama walivyofanya wabunge na viongozi wa chama cha Labour nchini Uingereza.

Bila kundi la Maalim Seif kukubali kukaa chini na Prof. Lipumba na kumaliza mgogoro kwa amani, wasitegemee kama wataweza kumuondoa Prof. Lipumba bila CUF kumeguka kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa sababu Prof. Lipumba anawafuasi wengi kutoka Tanzania bara wakati Maalim Seif anawafuasi wengi kwa upande wa Zanzibar.

kWA HISANI YA JF

0 comments:

Post a Comment