Monday, 13 June 2016

Re: [wanabidii] Will Clinton Or Trump Change US- Africa Relations?

Bora aje Trump kutubamiza. Tumezidi kuacha kujituma nchini kwetu na kukimbilia nchi za wenzetu. Viongozi kukaa madarakani karne na kusababisha vita. Akili kweli-kuna kila kitu ila tumebweteka. Ukipewa surveyed plot eneo la viwanda, hadi miliki na mkopo ujenge kiwanda-unajenga Hall la sherehe na viongozi wakusanya kodi wanapita wanakusanya kodi.

Eti jengo la NHC la ghorofa mtu kapangishwa-anaongeza vyumba, uwanja anazungusha ukuta watoto wanakosa pa kucheza yeye anaweka parking ya magarina karakana na stoo ya mitumba. Wakusanya kodi wanapita na leseni ya frame za biashara anapata ila kaziba pia na feeder road na mapito ya miguu. Tunamwangalia. Ni Tanzania pekee utakuta Bar ya vileo au restaurant mradi wa kituo cha polisi na upo hapo hapo mjengoni na kila mtu anakwenda hapo kula na kunywa!

Watu mamia wamejazana katika boat wamelipa madola kibao wanahamia Ulaya na wanajua boat imebeba watu beyond uwezo wake na bahari ni kubwa yenye mawimbi makali. Yupo tayari rhayo madola apoteze hata kama atakufa kuliko kuyatumia nchini kwao kununua mahitaji ya kilimo au ujasiriamali mwingineo.

Mkogombana wenyewe kwa wenyewe-mnakimbilia ulaya eti wawaamulie. Huku Africa kuna maraisi wangapi na wazee wa mila na wasomi waliobobea-kujipendekeza na kujidhalilisha kama Kawa. Hiyo multi-party ideology kwetu sisi ni malumbano kabla na baada ya uchaguzi na kukomoana kwa kutoka bungeni na vikao vya pamoja sio kujadiliana kufikia maamuzi kidemokrasia-tupo baada ya MISIFA kuonekana unabwata, unapayuka, unaandamana kutaka demokrasia. Huangalii hizo hela na muda unaopoteza ungetumia jimboni kwako kuleta maendeleo ya kiwango fulani na kutoa huduma kwa wapiga kura wako. Halafu-toka Chama kianze (na Hata NGO nyingine zianzishwe) kiongozi ni wewe tu toka iwe 1995 au NGO ianze 1980 ni wewe tu hubadilishiki lakini unaona chama tawala hakina demokrasia. Unazeeka na kuanguka jukwaani kama Mugabe, unasinzia vikaoni uchovu na uzee-hubadilishiki ukawaachia vijana uliowalea-labda umwachie mwanao au mkeo uongozi au rafikio-umeng'ang'ania madaraka.

Mwache ajenge kuta na kutuacha baharini tuzame-mbona tukifika kule tunapigana na kuchoma makambi na kubaka vitoto eti pia tunataka waweke himaya za dini zetu. Lakini-hatukukimbilia kwene nchi ambazo ni salama na wana mpaka katiba za dini zetu tutakazo zitawale. Tunakimbilia kule ambazo dini tusizozipenda ndio zoipo mpaka ktk katiba za nchi zao. Kulikoni usikimbilie kule ambako utapata amani kijamii, kidini upendavyo wewe? Yaani umekimbilia kwa jirani anakusaidia halafu unamwamulisha utakavyo wewe-rudi kwako ulikokimbia!

Sasa hapa kazi tu, kusimamia good governance kusiwe na rushwa, upotevu wa hela, kuwe na utendaji vema na kujituma-tunagundua miradi ta Teleza kuingia na kubaka wamama au kuwakata mapanga wakikataa kubakwa; tunakata mapanga na kuua watu tunaohizi walitoa siri za uvamizi wetu; tunavamia vituo vya polisi kuchoma moto na kuua polisi; tunasaidia wauwaji wanyama pori; majambazi waporaji mali za watu; kubeba na kuficha wahamiaji haramu na kupangisha watu wanaoweka viwanda vya siri majumbani ktk nyumba zetu kimya tunakula jiwe. Ukikamatwa-Nchi haina demokrasia!
Akili za nyumbu-badala ya kumsaidia Rais tupate maendeleo tunaanzisha maandamano nchi nzima ila-hatutangulizi wake, waume na watoto wetu ktk mstari wa mbele wa maandamano. Akija mgeni au mwekezaji kuwekeza-tunamsaidia kuiibia nchi mipesa tunakwenda kuiweka bank za ulaya! Trump tunamhitaji-arudishe mihela hiyo, na vibaka hao wakikimbilia huko-asiwapokee. Hata wanaohamia huko kukimbia kulima kwani mbona wakienda huko ulaya waliowengi huishiakufagia barabara, kudeki mahotelini na kulima mashamba ya maua na ngano? Kulima na kuzoa takataka bongoland-No!?

Wakati umefika wa Africa kuacha vita na malumbano bali kufanya kweli kwa kushirikiana ili kuleta maendeleo.

Ninapenda sana TRUMP achaguliwe alipige tarumbeta lake kwetu mpaka akili zibadilike na lkuona mbali.
Kama Kawa




--------------------------------------------
On Mon, 13/6/16, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Will Clinton Or Trump Change US- Africa Relations?
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, Wanazuoni@yahoogroups.com
Date: Monday, 13 June, 2016, 13:21

( My article,
Africa Bloggers Network)http://www.africablogging.org/will-clinton-or-trump-change-us-africa-relations/




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment