mbona karimjee alikuwepo lowasa na hapakuwa na katazo lolote? hilo la udom ndio lifanye ccm kuwa mkoloni mweusi? au kuna jingine?
2016-06-19 11:51 GMT+03:00 'Gikaro Ryoba' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
--Mwishoni mwa karne ya 19 mabepari wa kikoloni waliketi huko Berlin nchini Ujerumani wakapanga mikakati ya kuligawana na kulitawala Bara la Afrika kwa maslahi yao binafsi. Juhudi zao zilifanikiwa kwa 99% na unyama waliowafanyia waafrika kila mtu anaufahamu – tulinyonywa, tukaonewa, na kudhalilishwa kwa kiwango cha mwendokasi..Ni jambo la kusikitisha kuona CCM nao wanataka kuiga mtindo huu wa "Divide And Rule" uliotumiwa na wakoloni kututawala. Siku za karibuni CCM na serikali yake wameanza kuwagawanya watanzania kwa malengo yale yale ya kikoloni.Jana tumeshuhudia wanafunzi wa UDOM amabo ni wafuasi wa CHADEMA/UKAWA wakizuiwa kufanya mahafali yao huku wale wa CCM wakiruhusiwa kuendelea na mahafali yao huko Iringa bila kubughudhiwa. Aidha, maandamano na mikutano ya kisiasa ya UKAWA imepigwa marufuku wakati mikutano na maandamano ya CCM yanaendelea kama kawaida. Juzi kati wafuasi wa CCM waliandamana huko Mwanza na mpaka leo hatujasikia wakitiwa msukosuko wowote na polisi wao..Ninachoona sio tu kwamba CCM wanagawanya na kutawala lakini pia wanajaribu kulifanya kundi moja liwe na chuki dhidi ya serikali na kulijengea mentality ya kulipiza visasi. Ikiwa kundi kandamizwa litaona linaonewa sana kwa kutumia CCM militia, nao hawakawii kufikiria kuanzisha vyombo vyao vya kujilinda. Ndio. Sasa wewe unadhani wataendelea kunyanyaswa mpaka lini? Haiwezekani kundi moja likawa na vyombo vyao vya ulinzi vinavyomiliki kila aina ya silaha wakati kundi la pili halimiliki hata kirungu kimoja..Hii mbegu ya ukabila ilianza kumea kwa miaka mingi huku CCM wakishuhudia na kuchekelea kwa kuwa wanafurahia uwepo wa mgawanyiko huu. Tujiulize tumefikaje hapa. Hadi leo hii kuna vikundi vya kikabila na kikanda katika vyuo vikuu ambavyo hufanya mahafali yao kwa misingi ya kikabila na kikanda. Utaratibu huu umefumbiwa macho na uongozi wa vyuo vikuu na serikali kwa muda mrefu sasa. Baada ya mihemko ya kisiasa kuingizwa vyuoni na CCM, sasa ukanda na ukabila huu umehamia kwenye vyama vya siasa. Na kinachoudhi zaidi ni kuona kundi moja linaandamwa na kunyanyaswa huku kundi la pili likiendelea na shughuli zao bila kubughudhiwa..Mwanzo wa ngoma ni lele. Ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuacha kamwe. Ulaji wa nyama ya mtu ni sawa na ubaguzi. CCM imelea mgawanyiko wa kikanda na kikabila katika vyuo vikuu hadi umezaa mgawanyiko wa kiitikadi za vyama (CCM vs UKAWA). Kuna taarifa kuwa mgawanyiko huu umeingia hadi kwa wahadhiri wa vyuo vikuu – kuna wahadhiri wenye muelekeo wa CCM na wahadhiri wenye muelekeo wa UKAWA. Ikiwa mgawanyo huu utazidi kufumbiwa macho, tutafika hadi kugawana madarasa ya mihadhara (lecture theatres). Kutakuwa na madarasa wanayosoma wanaCCM wakifundishwa na wahadhiri wa CCM na kutakuwa na madarasa ya UKAWA yanayofundishwa na wahadhiri wa UKAWA. Bila shaka huku ndiko CCM wanakotaka kutupeleka..Dhambi ya ubaguzi haitaishia hapo tu bali itasamabaa hadi hapa mitaani. Kule Zanzibar sasa tunashuhudia mgawanyiko mkubwa sana. Watu hawashirikiani katika misiba, harusi, na matatizo mengine kwa misingi hiyo hiyo ya kisiasa iliyoasisiwa na kupaliliwa na CCM kwa ajili ya Divide And Rule. Baada ya kufanikwa kuwagawanya wazanzibar sasa wanataka kuhamishia ubaguzi wao huko Tanganyika. Watanganyika kuweni makini. Msikubali kugawanywa kizembe hivyo.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment