Sunday, 18 January 2015

[wanabidii] Poleni chadema na Hongereni ACT

Poleni chadema na Hongereni ACT.

Baada ya chama cha Chadema kushindwa propaganda ya kumchafua Mzalendo namba moja Zitto zuberi Kabwe kuwa anatumiwa na ccm,waliamua kuwatumia waandishi wa Tanzania Daima pamoja na wazee mashuhuri ili kumbakisha chadema.

Hofu kubwa ya chadema ni kuhofia endapo Zitto atajiunga na chama cha Kizalendo cha ACT,basi itakuwa mwisho wa chadema.

Pamoja na jitihada za kumbakisha chadema Zitto alitoa Masharti Magumu ambayo chadema walishindwa kuyatekeleza.

Moja ya sharti la Zitto kubaki chadema ni wale waliomzushia tuhuma kuwa anatumiwa kuhujumu chadema basi warudi kwenye vyombo vya habari na kukanusha maneno yao(Sharti gumu)

Sharti lingine ni kuwa yupo tayari kubaki chadema endapo tu wapiganaji wake watarudishwa kwenye chama,(Prof Mkumbo,Mwigamba ,na wengine wengi)

Chadema baada ya kushindwa kumshawishi,wakaja na plan B.

Katika plan hii waliamua kumrubuni Mwenyekiti wa muda Bw.Kadawi Limbu ili asikubali kuitisha uchaguzi wa chama na kisha akiendeshe chama kwa maelekezo toka makao makuu ya chadema (Ufipa)

Limbu kwa kushawishiwa na pesa kidogo zilizoletwa na mtu anaeitwa Saidi Kubenea,akaapa kuwashughulikia wote wanaodai uchaguzi ndani ya chama

Akamfukuza Katibu Mkuu wa chama na viongozi wandamizi wa chama bila kufuata katiba wala taratibu za chama.

Lengo ni kuhakikisha chama kinasambaratika ili kumkatisha tamaa Zitto Kabwe ambae muda wowote atatua ACT kujenga demokrasia kwa vitendo.

Hatimae Plan B nayo imeshindwa,Maana mission kupewa mtu mwenye shule ya Form four (Kubenea)kukabiliana na Think tank za ACT kama Prof Mkumbo,Zitto na Mwigamba ni sawa na kumtisha kuku ndoo ya maji.

Kubenea kumshinda Prof Mkumbo ni sawa na Kabati kuangushwa na Mende.

Nilitegemea tu kuwa plan B nayo ingeshindwa maana akili ndogo haiwezi kuishinda akili kubwa.

Kushindwa kwa mipango hiyo dhidi za Zitto Kabwe ,kumewagharimu mamilioni ya fedha chadema ,pamoja na hayo yote chadema wameibuka na plan C.

Hii nikumwaga pesa kwa wahariri wa vyombo vya habari ili kuhakikisha habari chanya za Mzalendo Zitto hazitolewi kwenye vyombo vya habari.

Lakini pamoja jitihada hizo za chadema kumhujumu Zitto,lakini Zitto anazidi kuchanja Mbuga.

Ni katikati ya zengwe hilo ,Zitto alihutubia mkutani Mkubwa huko mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Mchumi wa Dunia Prof Lipumba.

Lakin kwa upande wa chama cha ACT-Tanzania imekuwa neema,chama kimepata coverage ya kutosha katika vyombo vyote vya habari.
Chama kimejitangaza bila kutumia gharama,chakufurahisha nikuwa wamaoitangaza ACT ni chadema.

Huenda kutokana na uelewa mdogo wa viongozi wao hawajagumdia kama wanazidi kuifanya ACT kufahamika mbele ya macho yawanyonge.

Hapa ndipo unapokubali kuwa chama kikiwa na viongozi makini kazi ya kurangaza chama huwa rahisi.

Ni ukweli usiopingika kuwa chadema ilitangazwa na CCM baada ya kuwa inasemwa kila ccm walipohutubia.

Pia ni ukweli usiopingika kuwa ACT inatangazwa na chadema

Hongereni ACT kwa kupata covarage kwenye vyombo vya habari kwa kutumia gharama za chadema.

Asanteni chadema kwa kuijenga ACT kupitia magazeti yenu ya Tanzania Daima na Mawio.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment