Wednesday, 28 January 2015

[wanabidii] TANZANIA: WITO WA MAOMBOLEZO

Bwana Mungu aliye Hai anatuita kwamba tufanye maombolezo, na kulia kwa machozi. Kwa maana anaachilia hukumu zake za kutisha juu ya nchi. Kutakuwa na huzuni nyingi, kutakuwepo na kulia kwingi kwa machozi na kusaga meno, lakini itakuwa imechelewa mno. Kwa maana alipowaita, hawakutubu, hawakusikia, walimkataa kwa hivo watapokea ukali wa ghadhabu na  hasira ya Mungu.
Uko kwenye starehe, fanya maombolezo, kwa maana umedhania kuwa huna tatizo. Umedhania kuwa kila kitu kuhusu wewe kiko sawa, na hutajua sikitiko, lakini Mungu aliye Hai atakuteketeza na huzuni nyingi. Utalia na wala haitakusaidia kwa kuwa wewe ni mwovu na uko mbali na Mungu. Mungu atamtuma aharibuye kwako. Funza watakutafuna, magonjwa na tauni zitakuangamiza wewe na uloo wako.
Usipomsikiliza Mungu utajipeleka mwenyewe kwenye kifo. Haimpendezi Mungu kufa kwa wale wanaojiita kwa jina lake. Lakini wakati wawapo wagumu wa kusikia na wana shingo ngumu, muda huja ambapo wanakumbana na ghadhabu na hasira ya Mungu. Wakati inapomwagwa, sio kitu kizuri, lakini ni kikali na cha kutisha.
Wale wanaoipokea itashangaza kwa maana ghadhabu ya Mungu haikomi, hakuna mtu asitishaye ghadhabu ya Mungu. Tufanye maombolezo, tuwe na majonzi kwa maana siku za kuvaa magunia zinaenda kutujia, na tutakapovaa magunia tutakuwa tumeshachelewa sana. Kwa maana  hatukumsikiliza Bwana.
Tufanye maombolezo, tufanye kilio, kwa maana yale tunayoyafikiri kuwa ni yetu, tutanyang'anywa na hatutabaki na kitu na tutakuwa utupu, na wapweke. Mungu atatuondolea yote yaliyotupa furaha, kwa maana Mungu ametukasirikia na tumeipata ghadhabu ya Mungu.
Siku nzima Mungu ametusihi na amemtuma Roho wake kukaa juu yetu. Kwa mfululizo tumemkataa Mungu, kwa mfululizo tumemkataa Roho wa Mungu, na tumetafuta njia yetu wenyewe na tumefanya ukahaba mwingi.
Tumekuwa kama mwanamke kahaba anayejiuza kwa kila kitu kichafu, bado tunapangusa midomo yetu na tunamtamkia Mungu kwamba hatujafanya uovu. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuthubutu kumwambia Mungu aliye Hai kuwa hatujafanya uovu wowote mbele zake? Mungu anajua kazi za kila mwanamume na mwanamke, na mengi ya vitu tulivyovifanya mbele zake, ni viovu.
Bado tumekuwa sugu, tumekuwa na kiburi, na tumedhania kuwa hatuna uovu. Lakini Mungu atakufunua katikati ya uovu wako mwenyewe, na atakuvua uchi na wengine watakuangazia macho na watashtushwa.
Wale waliokataa kutubu na wale waliokataa maombolezo na kulia machozi, na wale wanaoendelea katika ugumu wa mioyo yao na shingo zao na ukorofi wa akili zao, Mungu atawaangusha chini. Watavunja meno yao kwenye vumbi, na watalia kwa uchungu na watachana vichwa vyao wenyewe kwenye udongo.
Lakini hiyo haitawasaidia  kwa maana watakuwa ukiwa na wasiofanikiwa. Watumishi wa Mungu, wale wanaokwenda kwa agizo la Roho wa Mungu, watatangaza haki ya Mungu na watatangaza utakatifu wa Mungu.  Tusiwe kama wajinga wanaosubiri sana, lakini hata siku hii ya leo fanya maombolezo.  Ona uchungu, fanya kilio kwa ajili ya dhambi zako na za ukoo wako.
Omboleza kwa ajili ya dhambi zako na dhambi za ndugu zako.  Lia kwa machozi kwa ajili ya dhambi zako na dhambi za watoto wako. Kweli kama hakutakuwepo na mtu atakayelia kwa machozi kwa ajili ya dhambi na kufanya maombezi, na kufanya maombolezo, ndipo wote watakapopotea. 
Tusimwondoe Mungu na tusifikirie kwamba tutampendeza kesho. Na ingawaje tumezoea kujiridhisha, na starehe, Mungu atayapasua makochi yetu ya madaha, na atapasua kitakachoonekana na tutabakiwa uchi na tutaachwa utupu. Kila mtu atatuangalia na kuona aibu tuliyoifanya mbele za Mungu.
Kwa maana kweli wale waliomwaibisha Mungu, je, Mungu hatasababisha kadhalika wao kuaibika? Tufanye maombolezo, tuuruhusu uchungu ule uliopo katika Roho wa Mungu uje juu yetu. Tusikitike kwa ajili ya dhambi zetu na sikitika kwa ajili ya dhambi za koo  zetu, na dhambi za ndugu zetu, na dhambi za watoto wetu.
Tuzungumzie uchungu mkubwa. Kwa maana dhambi nyingi zimefanywa mbele za Mungu kwa kujiridhisha, kwa ukorofi, kwa wale wajipendao wenyewe, kwa wale waliopo chini ya mvuli wa udanganyifu, kwa wale walio katika hali ya kuashiria umuhimu wao wenyewe. Tumefanya dhambi, na kuongeza dhambi dhidi ya dhambi. Tumekuwa chukizo kwa Mungu.
Je, Mungu hatawafunua watu hao katika uovu wao, hatawafanya utupu, hatawafanya ukiwa na hatawafanya aibu na tamasha? Atawafanya, na watageuziwa watesi wao na kwa maadui wa kusudi la Mungu. Watageuzwa na kuwa watumwa wa wale watu waliowadharau.
Wakati watu wa Mungu watakapokataa kuomboleza, wakati watu wa Mungu watakapokataa kutubu, na kukataa kumfuata Mungu aliye Hai, je hatalipiza kisasi chake dhidi ya watu wake? Atalipiza. Hii ni siku ya kisasi chake, na kimekuja.
Wakati watu wanaendelea katika furaha ya ulevi wao, atawafanya kubiringika kwenye matapishi yao wenyewe na atawasababisha kushindwa kusema hata kwa lugha zao wenyewe. Wakati walinena upotofu wao na uwongo kinafiki kiasi kwamba Mungu aliye Hai hakulala.
Mungu anaona mbele ya uso wake kila nafsi iliyomezwa, na kila mtu aliyemwuliza Mungu na wakamlisha uwongo na kila mtu aliyemtamani Mungu na wakamlisha uchafu. Mungu aliye Hai ataachilia kisasi cha haki juu ya waovu, na juu ya waliorudi nyuma na juu ya wale wanaodai kuwa ni watu wa Mungu kumbe sio.
Mungu ataachilia kisasi chake cha haki. Kutakuwepo na marundo ya mifupa ya wafu, kwa maana Mungu atatuma kifo nchi nzima. Wengi watamezwa na kifo na hawatasimamisha kifo. Hakitaletwa na mwanadamu, lakini kitaletwa na kutembea kwa Roho wa Mungu.
Mifupa itajirundika juu, na anayepita njiani atahema kwa majonzi na kulia na kuonyesha kwa kushangaa. Lakini haitakuwa inawezekana kusitishwa kwa nguvu za mwanadamu, bali itakuwa katika mikono ya Mungu. Wakati mkono wa Mungu atakapokuja kupiga kama ngumi, wengi watatawanyika wakiwa wamegongwa. Wengi watakufa.
Kwa kipindi kirefu sana wengi wasemao kuwa ni mali ya Mungu wamemkanyaga Mungu, wamemtukana Mungu, wamepuuza kumtumikia Mungu. Wameishi kitukutu na kijinga. Wako kama makahaba walionenepeshwa, wakijilisha wenyewe kutwa nzima, wakifanya uasherati wao na uzinzi na kila nguvu ijayo.
Ni chukizo mbele za Mungu na aibu. Hakuna tendo lao hata moja lililojificha katika uso wa Mungu kwa maana Yeye ni Mungu aliye Hai na kila kitu ni dhahiri kwake. Wengi watadhoofika katika siku za huzuri na wengi wao watakufa, na mifupa yao itachomoza kwenye ngozi zao kwa ajili ya njaa. Mungu hatawasikia.
Ingawaje wanaweza kuponda vichwa vyao juu ya nchi mpaka kutokwa damu, damu zao zitamwajika chini bure. Kisasi cha Mungu kimekuja. Wapeipata ghadhabu ya Mungu na hasira yake na imemiminwa. Usiwe kama wajinga ambao hufumba macho yao na kuziba masikio yao na kushupaza shingo zao na kufanya migumu mioyo yao.
Kwa maana huzuni yao itakuwa kubwa katika siku zijazo. Na maombolezo yao yatakuwa makubwa, lakini itakuwa imechelewa sana kwa maana wataombolezea upepo. Usiwe kama wao kwa maana wamefungwa katika maovu yao na chakula chao kitakuwa matapishi yao wenyewe mpaka kutakapokuwa hakuna kilichobakia tumboni mwao, na wengi wao watakufa katika ujinga wao.
Usiwe kama walivyo kwa maana wamechagua upofu wao, wamechagua uziwi wao, na wamejeuza mioyo yao wenyewe kuwa jiwe. Ilikuwa uasi wao wenyewe uliofanya shingo zao kuwa ngumu kwa sababu wamekataa, na kukataa, na kukataa na katika siku ya maombolezo Mungu atawakataa.
Ingawaje wanaweza kuhuzunika sana na ingawaje wanaweza kunung'unika, watanung'unikia upepo. Hata ndege hawatawajali kwa maana Mungu atawaacha mahali pa ukiwa. Tubu sasa hivi Mungu akupapo maonyo. Usimdharau Mungu, usimshtaki Mungu, piga magoti mbele zake kwa maana Yeye ni Mungu wako.
Mungu akupapo siku hii ya leo, hata kuomboleza, katika huzuni kubwa anza kulia.Usidharau, usimtolee Mungu nje, piga magoti, piga magoti, piga magoti. Kwa maana muda iwapo kamba ya matumaini kwako, piga magoti. Fanya maombolezo. Frank






0 comments:

Post a Comment