Friday 30 January 2015

Re: [wanabidii] TAARIFA MAALUM KUHUSU KAMPUNI YA NDEGE YA TANZANIA (ATCL)

I believe Muhigo will read this without shedding tears.

2015-01-30 12:18 GMT+03:00 Kazi Bongo <worldngojobs@gmail.com>:

TAARIFA MAALUM KUHUSU KAMPUNI YA NDEGE YA
TANZANIA (ATCL)

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Ndege ya Tanzania
(ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya
Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la
Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika
Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA)
lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo
ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya
kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti
2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia
100.

2.8.1 Hali halisi ya ATCL kwa sasa
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Msajili
wa Hazina kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,
2013 na kwa kuzingatia Taarifa ya Wizara ya
Uchukuzi, imebainika kuwa ATCL kwa sasa ina Ndege
moja tu aina ya Dash 8 – Q 300, Wafanyakazi 142 na
Jengo la ATC House lililoko mtaa wa Ohio, Dar es
Salaam huku ikiwa na madeni makubwa kama
itakavyofafanuliwa hapo baadae.

2.8.2 ATCL imefikaje hapo ilipo kifedha na kuwa na
Madeni makubwa?

Mheshimiwa Spika, baada ya kuvunjika kwa mkataba
wa ubia baina ya SAA ana ATC, mnamo mwezi Machi
2008, Wizara ya Miundombinu kwa wakati huo iliingia
katika makubaliano na Kampuni ya China Sonangol
kuwa Kampuni hiyo ya China ingeleta ndege mpya 7
kwa ATCL ikiwamo Ndege 5 aina ya Airbus ambazo
zingewasili mwaka 2012 na 2013.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Msajili wa Hazina
na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, Wakati ATCL
ikisubiri ndege hizo mpya, Kampuni ya China
Sonangol iliitambulisha Kampuni ya Wallis Trading Inc
kwa ATCL na kisha Kampuni hizi mbili (Wallis Trading
Inc na ATCL) zikaingia mkataba wa Ukodishaji ndege
aina ya Airbus 320 kwa kipindi cha miaka 6 kwa
Malipo ya USD 370,000 kila mwezi.

Mheshimiwa Spika, huu ndio ulikuwa mwanzo wa
mwisho wa ATCL, kwani baada ya Ndege hiyo
kuwasili ilifanya kazi kwa muda wa miezi sita tu na
baadae ilifungiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA) kwa kushindwa kutekeleza matakwa
ya usafiri wa anga. Ndege hiyo ilipelekwa kwa
matengenezo makubwa mwezi Julai, 2009 nchini
Ufaransa na haijawahi kurudi hadi leo wakati ambapo
Serikali kama mdhamini wa ATCL anadaiwa fedha
nyingi na Kampuni ya Wallis.

Mheshimiwa Spika, kutokana na deni la ATCL kwa
Wallis linalofikia USD 42,459,316.12 hadi tarehe 31
Oktoba, 2011 na kufuatia majadiliano mbalimbali
baina ya Serikali na Kampuni hiyo, Serikali
imekwishalipa jumla ya USD 26,115,428.75 hadi sasa
wakati bakaa inayodaiwa ni USD 23,996,327.82.

Mheshimiwa Spika, Kamati inasikitishwa sana na
upotevu huu wa fedha za Umma ambao umetokana
na mkataba mbovu ulioingiwa na watumishi wa Umma
wasiokuwa waaminifu na uchungu na Taifa lao.
Mabilioni ya fedha yanaoendelea kulipwa kwa
Kampuni ya Wallis kwa huduma ya ndege iliyofanya
kazi hapa nchini kwa miezi sita tu na kisha ndege
hiyo kupelekwa Ufaransa kwa matengenezo ni
fedheha kubwa kwa wazalendo wa Taifa letu. Aidha,
Taarifa zinasema ndege hiyo ikiwa Ufaransa ilipakwa
rangi na kukodishwa kwa Shirika la ndege la nchi ya
Guinea wakati Serikali yetu ikiendelea kulipia tozo ya
ukodishaji wa ndege husika.

Mheshimiwa Spika, ni wakati sasa kwa Serikali
kuamua kwa dhati kushughulikia suala la ATCL kwa
mapana yake ikiwa ni pamoja na kuangalia uhalali wa
kulipa deni la Wallis (ambalo lipo chini ya dhamana ya
Serikali, hivyo ni fedha za Umma) ambaye kimsingi
naye alikiuka makubaliano ya Mkataba kwa kukodisha
ndege iliyokuwa imekodishwa tayari kwa ATCL. Aidha,
ni muhimu wahusika wa uingiaji wa mkataba husika
wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili haki
itendeke.

Mapendekezo kuhusu deni la USD 23,996,327.82
ambalo ATCL inadaiwa na Wallis Trading Inc.

KWA KUWA, Serikali haikunufaika na mkataba wa
kukodisha ndege aina ya Airbus kutoka kwa Kampuni
ya Wallis baada ya ndege hiyo kugundulika ni mbovu
ndani ya miezi sita na kupelekwa kutengenezwa kwa
muda mrefu,

NA KWA KUWA, Serikali inaendelea kulipa tozo ya
ukodishaji wa ndege hiyo ambayo haifanyika kazi,
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza yafuatayo;

a) Serikali kuangalia uhalali wa kulipa deni la Wallis
ambaye kimsingi naye alikiuka makubaliano ya
Mkataba kwa kukodisha ndege iliyokuwa imekodishwa
tayari kwa ATCL.

b) Serikali ihakikishe inawafikisha kwenye vyombo vya
Sheria ili haki itendeke kwa wahusika wa uingiaji wa
mkataba huo unaoendelea kuipa hasara Serikali kwani
hadi sasa hakuna kesi iliyopelekwa mahakamani
mahususi kwa waliongia mkataba husika.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment