Thursday 29 January 2015

[wanabidii] Scholarships for Masters Degree Programmes in the UK - September 2015 Intake

Tarehe April 24, 2014 nilituma barua pepe (forwarded) kuhusu nafasi za masomo "Scholarships for Masters Degree Programmes in the UK - September 2015 Intake" ambazo zilikuwa zinadhaminiwa na "Global Academy for Mining, Oil & Gas".

Maelezo yalikuwa wazi na mepesi kueleweka kwamba usaili ulipangwa kufanyika tarehe 7 na 14 Mei, 2014 Kigali na Mombasa. Kwa maana rahisi ili uitwe kwenye usaili ulipaswa kutuma maombi kabla ya tarehe 7 Mei 2014.

Kuna watu ama kwa uzembe, uvivu, makusudi au ukaidi tu wa kutokusoma maelezo yote wameamua kutuma maombi mwaka huu 2015.

Wahusika/waandaaji wamenitumia ujumbe nifute tangazo kwa kuwa muda wa kutuma maombi umekwisha! Ni aibu kwa kweli. Nimewajibu kwamba tangazo lilitumwa kwenye kundi na watu walipata kwenye anuani zao za barua pepe kabla ya tarehe ya mwisho ya kutuma maombi.

Ombi langu kwenu ni kwamba kabla hujatuma maombi sehemu soma maelekezo vizuri. Usipofanya hivyo utakuwa unapoteza muda wako, gharama zako na hutoipata nafasi uliyoiomba.

Natumaini hatutoendelea kuaibishana.

Yona naomba ufute (delete) hizi posti kwenye "server" 



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment