Wednesday, 28 January 2015

Re: [wanabidii] PROFESSA LIPUMBA 'UMEBUGI MEN'

Happiness tumia lugha yenye staha katika maandishi yako kwani unabeba haiba ya chuo kikuu cha Bagamoyo. Wewe ni mwanafunzi wa sheria na siyo msomi wa sheria. Huu ni ushauri wangu kwako utaheshimika kwa kujenga hoja na siyo kwa kutukana.

Sent from Yahoo Mail on Android



From: 'lucas haule' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] PROFESSA LIPUMBA 'UMEBUGI MEN'
Sent: Wed, Jan 28, 2015 11:26:58 AM

Maumivu ya kichwa huanza polepole.
--------------------------------------------
On Wed, 1/28/15, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] PROFESSA LIPUMBA 'UMEBUGI MEN'
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, January 28, 2015, 2:24 PM

PROFESSA LIPUMBA 'UMEBUGI MEN'

Na Happiness Katabazi

JANUARI 27 Mwaka huu, jeshi la Polisi Mko wa Kipolisi
Temeke, liliamua kutumia Nguvu kuwatawanya wafuasi wa Chama
cha Wananchi (CUF) na kufanikiwa kumkamata Mwenyekiti wa
Taifa wa Chama hicho Profesa Ibrahim  Lipumba na
wenzake .

Polisi walidai wamekiuka sheria za nchi ikiwemo Kutenda
kosa  la kukaidi amri ya Jeshi Hilo iliyozuia
wasiandamane.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi , ilisema CUF il
iliandika barua ya kuomba Kibali cha kufanya maandamano na
mkutano eneo la Mbagala Zakhem Jana lakini Jeshi Hilo
lilikataa ombi Hilo na Kabla ya kufika siku ya Jana Jeshi
Hilo lilikuwa limeishakipelekea Chama cha CUF, barua ya
Jeshi Hilo inayozuia CUF isifanye maandamano Jana na CUF na
Lipumba hadi Jana alikuwa hajawasilisha maandishi pingamizi
la amri hiyo ya Jeshi la Polisi.

Matokeo yake Profesa Lipumba na wafuasi wake Jana waliamua
kutoka ofisini Kwao huku wakitembea  kwa miguu kwa
kisingizio Kuwa wanaenda kuairisha mkutano huo.

Lakini Wakati Lipumba na wenzake wakitumia mbinu hiyo ya
kutoti waliyofikiti itawasaidia kuwapiga chenga ya mwili
Polisi ,na CUF wakisahau Msemo usemao 'katika msafara wa
Mamba,Kenge Pia wamo'.

Jeshi la  Polisi kupitia 'mawashawasha wao' yaani
makachero wao ,muda mrefu sana Kumbe walikuwa wameishaibini
mbinu hiyo ya Lipumba na wafuasi wao ya kukaidi kiaina amri
ya jeshi la Polisi iliyotaka CUF wasiandamane.

Hiyo Polisi gani kwenye akili timamu angeshindwa kubaini
hiyo mbinu ya CUF waliyoitumia Jana ilikuwa na Lengo la
kukaidi amri ya Jeshi la Polisi iliyowataka za
wasiandamane?


Ndipo Jeshi la Polisi lipoutangazia umati ule wa CUF Kuwa
watawanyike kwasababu wanachokifanya ni kinyume cha Sheria
lakini baadhi ya wafuasi waliokaidi ndiyo Polisi waliamua
kutumia mabomu ya Machozi na kuwaadhibu waliokaidi na Kisha
Kumtia nguvu ni  Lipumba Ambaye ndiye alikuwa Kinara wa
maandamano hayo haramu.

Ieleweke wazi kuna taarifa Kuwa Lipumba anataka Kugombea
Ubunge jimbo la Temeke kwasababu amechoka Kugombea nafasi ya
urais ambayo ameishagombea zaidi ya Mara Tatu na amekuwa
akishindwa.

Kwa hiyo kumbukizi hiyo ya Mauji ya waliokuwa wanachama wa
CUF kule Pemba ambayo alikuwa akiyaongoza Jana ,ilikuwa ni
Karatasi ya kisiasa iliyokuwa imepangwa kutumiwa na Lipumba
kuanza kujipitisha kwa wakazi wa Jimbo la Temeke lakini
wajuzi wa mambo wamelibaini Hilo Mapema wanamcheka Ujinga.

Wafuatiliaji wa siasa za nchi hii tunajiuliza  ni
kwanini kabla ya mwaka Huu wa uchaguzi mkuu , Lipumba na CUF
yake imekuwa haifanyi kumbukizi hiyo kwa Maandalizi makubwa
kiasi hicho hadi Mwaka huu wa uchaguzi Mkuu wa 2015 ndiyo
Lipumba na Chama Chake kiwe na kimuemue cha kufanya
kumbukizi hiyo kwa Maandalizi kabambe?

Kuna ajenda gani ya siri ya kumbukizi hii ya mauji ya
Pemba.Yaani msiba utoke Pembe - Zanzibar halafu maandamano
ya kumbukizi ikafanyiwe Mbagala - Dar es Salaam, wakati
wakazi wa Mbagala siyo wafiwa wa Msiba wa kumbukizi hiyo ya
Mauji ya Pemba?

Watoto wa mjini tunasema Profesa Lipumba una Lako jambo na
Si jingine ni unataka Ubunge wa Jimbo la Temeke. Lipumba
Umebugi Men.

Hao marehemu mnaowafanyia kumbukizi nao waliotuhumiwa
kuwachinja Askari wa Jeshi la Polisi huko Zanzibar , Mbona
CUF haifanyi kumbukizi ya kukumbuka Askari wale
waliochinjwa?

  Kila siku wabunge Bungeni wanaomba Jeshi la polisi
liongezewe fedha za kununulia vitendea kazi kama mabomu,
silaha za kisasa, virungu, uniform Na Polisi waboreshewe
mishahara na makazi Yao.

Nauliza mnataka hivyo virungu Vya Polisi,mabomu ya Machozi
yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi  hayo mabomu ya
Machozi yakatumike kufanyia Uvuvi haramu wa Samaki? Au hivyo
virungu Vya Polisi mnataka Wapewe watu wa Kabila la Wamasai
wakatumie virungu hivyo kuchungia Ng'ombe na Mbuzi?

Virungu na Mabomu ya Machozi ni matumizi sahihi kwa watu
wakorofi Kama Lipumba na wenzake .

Cha Msingi hapa ni wananchi watii Sheria bila shuruti
.Ukitii Sheria bila shuruti utakuwa umeepuka kupigwa virungu
na mabomu ya machozi,mitama,nakozi na Matoke na kung'atwa na
Mbwa wa Polisi.

Binadamu wote ni sawa Mbele ya Sheria na Ibara ya 13(1) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ,
inasomeka HIvi; ' Watu wote ni sawa mbele ya Sheria  na
wanayo haki , bila ya ubaguzi wowote ,kulindwa  na
kupata haki sawa  Mbele ya Sheria'.

Kwa Tafsiri nyepesi ya Ibara hiyo ,Jeshi la polisi
limetekeleza matakwa ya ibara hiyo kwa kukukamata wewe na
wenzako licha unayo madaraka makubwa na kukufikisha katika
mkondo wa sheria kwasababu watu wote ni sawa mbele ya
sheria.

Kwani wasomi wa sheria tunaposema  Usawa mbele ya
sheria  basi usawa huo auangalii umri wa ,elimu
,itikadi wala rangi kwani binadamu wote ni sawa mbele ya
jicho la sheria.

Nalipongeza Jeshi la Polisi chini ya IGP- Ernest Mangu kwa
kuzinduka usingizini sasa kuanza kuwatia 'displine' viongozi
wa juu wa vyama Vya siasa Kama Lipumba Jana mlivyomtia adabu
.

Nalipongeza sana mAana hawa viongozi wa juu wa baadhi ya
vyama siasa ni Kama mashetani wamekuwa na tabia chafu ya
kuwana na ajenda zao binafsi za kuleta Uvunjifu wa Amani
nchini ambazo wafuasi wao Wengi hawazijui wanaamua kuwaunga
mkono mwisho wa siku wafuasi wao Ndio wanaishia
kushughulikiwa na Jeshi la Polisi.

Rais wa Zimbambwe  Robert Mugabe na Rais wa Uganda
,Yoweri Mseveni  huwa hawataki kuendekeza viongozi wa
aina hiyo, wanausalama wa majeshi hayo uwa wanaanza
kuwashughulikia kwa vipigo vitakatifu Hao viongozi wa juu wa
vyama Vya upinzani na viongozi wa juu wa Makundi mengine
ambayo yanaamasisha wafausi Hao washiriki maandamano
haramu.

Tulimshuhudia Rais Mugabe alivyotoa adabu aliyekuwa kiongozi
wa upinzani nchini Zimbabwe ,Tsvangirai na rais Mseveni
alipomtia adabu Besige hadi Leo hii hao vinara wa Chokochoko
wamefyata Mkia.

Enzi za Utawala wa Rais Benjamin Mkapa wakati jeshila Polisi
likiongozwa na IGP- Omar Mahita aliweza kudhibiti na
kumaliza Nguvu za baadhi ya wanasiasa wa upinzani na
wanaharakati uchwara waliokuwa hawana ajenda zenye mashiko
waliokuwa wakikaidi amri ya Jeshi la Polisi .


Mchana wa Leo ,Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia aliliomba
Bunge liairishwe ili waweze kujadili hoja ya kwanini Jeshi
la Polisi limempatia ' mkong'oto heavy ' Lipumba Jana Kwani
eti Lipumba ni kiongozi mkubwa,watoto na waandishi wa Habari
walioumizwa Jana.

Spika Anne Makinda akitumia mamlaka yake na Kusema ametumia
madaraka yake kuimuru serikali Kesho ije kujieleza bungeni
kuhusu tukio Hilo.

Wakati Makinda akitoa agizo Hilo, baadhi ya wabunge 
kwakweli mi nadiriki kuwaita ni wendawazimu na ambao hawana
nidhamu wala staha,waliinuka na kuanza kupinga agizo Hilo la
Makinda tena bila kutoa kipengele gani kinawaruhusu kufanya
hivyo hali iliyosababisha zogo Kuzuka bungeni utafikiri watu
wapo Sokoni.

Jamani, Kama Bunge la Tanzania ambalo wabunge wake ndiyo
watunga Sheria na Ndio baadhi Yao wanakuwa wakwanza
kutoheshimu na kutii maagizo ya kiongozi wao yaani Spika,
HIvi tunaweza Kusema tunawatunga Sheria kweli ?

Nikisema kuna baadhi ya wabunge wa upinzani ni wendawazimu
nitakuwa nakosa?Nidhamu na busara kwa wabunge Hao wa
upinzani Iko wapi? Eti hawa ndiyo Watanzania turuhusu vyama
Vya upinzani kiongozi taifa hili kwa tabia Kama hizi za
kiuwenda wazi?haiwezekani.

Mbatia aliyoyasema Leo Bungeni HIvi haramu Mbele ya
Wanasheria wa namuona ni Mtu wa ajabu sana?

Maana Kifungu cha 8 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka
2002, inasema kutofahaumu Sheria siyo kinga yakutoadhibiwa.

Mbatia haelewi Sheria na Huyo Lipumba hawaelewi Sheria hivyo
ndiyo mAana wanafikiri hawawezi kufadhiliwa.Mnajidanganya.
Mbatia Leo bungeni Kasema eti waliwahi kuzungumza na Rais wa
Nchi wakasema eti viongozi wa juu nawatapigwa?

HIvi rais wa nchi, IGP ni Sheria?Rais wa nchi, IGP wote
Taasisi zao zimeanzishwa kwa mujibu wa Sheria na wanatakiwa
wafanyakazi zao kwa mujibu wa Sheria.Kama kweli mlikubaliana
hiyo basi waliamua kuwageuza viongozi wa upinzani
'Mambululala' kwasababu hamfahamu Sheria na Nyie kwa Ujinga
wenu mkakubaliana.

Mbatia acha Sheria Ufuate mkono wake , Mbona Halima Mdee,
Sheikh Ponda Issa Ponda walivyoamua tea na kufikishwa
mahakamani Mbona hatukukona ukisimama bungeni kuomba Bunge
liarishwe ili Mjadili kwanini Mdee ,Ponda wamepigwa na
kufikishwa mahakamani?

Na kwa taarifa yenu Nyie wabunge ambao mmezusha zogo Bunge
Leo kwa Shinikizo la kutaka ombi la Mbatia la kujadili
kipigo kwa Lipumba lijadiliwe Leo, kwa taarifa yenu sisi
wasomi wa Sheria tunasema imekula kwenu, Kwani Tayari
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga
kaishamwandilisha hati Mashitaka Lipumba na atafikishwa
mchana huu Katika Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam .

Na akishasomewa Mashitaka ya nayomkabili ndiyo basi tena
Bunge linakuwa limefungwa mikono kujadili Kesi iliyopo
mahakamani. Kwa Tafsiri nyepesi  Nyie wabunge
'wendawazimu' mliozusha zogo Leo Bungeni mmejiaribia wenyewe
.

Mlijiona mnaakili sana kuliko Spika Makinda.Mnamzarau
kwasababu ni mwanamke? Sasa mjanja nani Kati ya Nyie wabunge
'machizi' na Makinga?Mjanja ni Makinda na Jeshi la Polisi na
Ofisi ya DPP.

Kama mnampenda sana Lipumba jichangisheni Fedha
kumuwekee  Mawakili wazuri au pandeni  Ndege
nendeni makamuwekee dhamana Katika Mahakama ya Kisutu.

Nashauri Kanuni na sheria ya Bunge ifanyiwe mabadiliko
ambayo yataingizwa kipengele cha kuruhusu matumizi ya
virungu na mabomo ya machozi  yatumike ndani ya bunge
pindi wabunge wakorofi wanapozusha ukorofi ndani ya bunge n
kusababisha muda wa bunge kuairishwa kwasababu ya vuugu
hizo.

Tumeishabaini Sababu ya wewe Lipumba kuamisha  msiba wa
Pemba Kuja Mbagala ni kwasababu  wewe Lipumba
umeanza  kampeni za Ubunge jimbo la Temeke Kama
mlivyokubalana na viongozi wenzio wa UKAWA katika vikao
vyenu vya siri  kuwa nyie viongozi wa juu wa vyama
vinavyounda UKAWA  mgawane majimbo yaani mkagombee
ubunge badala ya urais kwani tayari mmeishaona nafasi ya
urais hampati.Hilo limejulikana.

Profesa Lipumna Kama una huruma na Marehemu  wale
siungeenda Pemba ukawakusanya wafiwa Ukawapikia  Pilau
na Biliani na Tende na Haruwa ungewapatia na ungeita na
viongozi wa dini na Kisomo mngewasomea marehemu wale.

Fanya Kama Mwenyekiti wa Makampuni  ya IPP, Reginal
Mengi yeye anawaonea huruma Maalbino,walemavu wa viungo
hivyo kila Mwaka amenitengea siku Moja kuwaandalia Mlo wa
Mchana anakula nao na kuwasaidia.

Lipumba Janja yako ya kutaka Ubunge jimbo la Temeke
imejulikana, na siyo kosa kisheria kutaka Kugombea jimbo ila
kosa ni kukaidi amri Hali za mamlaka husika.Usitumie
Kumbukumbu za misiba ya watu kujifanyia kampeni katika jimbo
ka Temeke, mizimu ya marehemu Hao itakusurubu. Lipumba
umebugi  Men.

Chanzo: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
Januari 28 Mwaka 2015.
0716 774494


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment