allan
Mimi siku hizi hata sisomagi tena story za huyu dada coz ni keeero kero .......nadhani hata anaaibisha hicho chuo kiukweli anashindwaje kutulia....mapro wa vyuo vikuuu ni watu makini na wasio watu wa kukurupuka kama happy.....Walikuwepo kina mr Saule wa Udsm miaka yetu ya practical journalist nikiwa family mirror cjawahi kuwaona wakijiingiza ktk arguments za ajabu ajabu akiwa biased kama huyu dada amejaa mitusi tupu na dharau, kusoma law kawa bingwa.....so hua sisomagi zinaboa hoja zake
From: "'allanlawa@yahoo.co.uk' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, January 28, 2015 12:06 PM
Subject: Re: [wanabidii] PROFESSA LIPUMBA 'UMEBUGI MEN'
Happiness tumia lugha yenye staha katika maandishi yako kwani unabeba haiba ya chuo kikuu cha Bagamoyo. Wewe ni mwanafunzi wa sheria na siyo msomi wa sheria. Huu ni ushauri wangu kwako utaheshimika kwa kujenga hoja na siyo kwa kutukana. |
From: 'lucas haule' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] PROFESSA LIPUMBA 'UMEBUGI MEN'
Sent: Wed, Jan 28, 2015 11:26:58 AM
Maumivu ya kichwa huanza polepole. -------------------------------------------- On Wed, 1/28/15, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote: Subject: [wanabidii] PROFESSA LIPUMBA 'UMEBUGI MEN' To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com> Date: Wednesday, January 28, 2015, 2:24 PM PROFESSA LIPUMBA 'UMEBUGI MEN' Na Happiness Katabazi JANUARI 27 Mwaka huu, jeshi la Polisi Mko wa Kipolisi Temeke, liliamua kutumia Nguvu kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) na kufanikiwa kumkamata Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake . Polisi walidai wamekiuka sheria za nchi ikiwemo Kutenda kosa la kukaidi amri ya Jeshi Hilo iliyozuia wasiandamane. Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi , ilisema CUF il iliandika barua ya kuomba Kibali cha kufanya maandamano na mkutano eneo la Mbagala Zakhem Jana lakini Jeshi Hilo lilikataa ombi Hilo na Kabla ya kufika siku ya Jana Jeshi Hilo lilikuwa limeishakipelekea Chama cha CUF, barua ya Jeshi Hilo inayozuia CUF isifanye maandamano Jana na CUF na Lipumba hadi Jana alikuwa hajawasilisha maandishi pingamizi la amri hiyo ya Jeshi la Polisi. Matokeo yake Profesa Lipumba na wafuasi wake Jana waliamua kutoka ofisini Kwao huku wakitembea kwa miguu kwa kisingizio Kuwa wanaenda kuairisha mkutano huo. Lakini Wakati Lipumba na wenzake wakitumia mbinu hiyo ya kutoti waliyofikiti itawasaidia kuwapiga chenga ya mwili Polisi ,na CUF wakisahau Msemo usemao 'katika msafara wa Mamba,Kenge Pia wamo'. Jeshi la Polisi kupitia 'mawashawasha wao' yaani makachero wao ,muda mrefu sana Kumbe walikuwa wameishaibini mbinu hiyo ya Lipumba na wafuasi wao ya kukaidi kiaina amri ya jeshi la Polisi iliyotaka CUF wasiandamane. Hiyo Polisi gani kwenye akili timamu angeshindwa kubaini hiyo mbinu ya CUF waliyoitumia Jana ilikuwa na Lengo la kukaidi amri ya Jeshi la Polisi iliyowataka za wasiandamane? Ndipo Jeshi la Polisi lipoutangazia umati ule wa CUF Kuwa watawanyike kwasababu wanachokifanya ni kinyume cha Sheria lakini baadhi ya wafuasi waliokaidi ndiyo Polisi waliamua kutumia mabomu ya Machozi na kuwaadhibu waliokaidi na Kisha Kumtia nguvu ni Lipumba Ambaye ndiye alikuwa Kinara wa maandamano hayo haramu. Ieleweke wazi kuna taarifa Kuwa Lipumba anataka Kugombea Ubunge jimbo la Temeke kwasababu amechoka Kugombea nafasi ya urais ambayo ameishagombea zaidi ya Mara Tatu na amekuwa akishindwa. Kwa hiyo kumbukizi hiyo ya Mauji ya waliokuwa wanachama wa CUF kule Pemba ambayo alikuwa akiyaongoza Jana ,ilikuwa ni Karatasi ya kisiasa iliyokuwa imepangwa kutumiwa na Lipumba kuanza kujipitisha kwa wakazi wa Jimbo la Temeke lakini wajuzi wa mambo wamelibaini Hilo Mapema wanamcheka Ujinga. Wafuatiliaji wa siasa za nchi hii tunajiuliza ni kwanini kabla ya mwaka Huu wa uchaguzi mkuu , Lipumba na CUF yake imekuwa haifanyi kumbukizi hiyo kwa Maandalizi makubwa kiasi hicho hadi Mwaka huu wa uchaguzi Mkuu wa 2015 ndiyo Lipumba na Chama Chake kiwe na kimuemue cha kufanya kumbukizi hiyo kwa Maandalizi kabambe? Kuna ajenda gani ya siri ya kumbukizi hii ya mauji ya Pemba.Yaani msiba utoke Pembe - Zanzibar halafu maandamano ya kumbukizi ikafanyiwe Mbagala - Dar es Salaam, wakati wakazi wa Mbagala siyo wafiwa wa Msiba wa kumbukizi hiyo ya Mauji ya Pemba? Watoto wa mjini tunasema Profesa Lipumba una Lako jambo na Si jingine ni unataka Ubunge wa Jimbo la Temeke. Lipumba Umebugi Men. Hao marehemu mnaowafanyia kumbukizi nao waliotuhumiwa kuwachinja Askari wa Jeshi la Polisi huko Zanzibar , Mbona CUF haifanyi kumbukizi ya kukumbuka Askari wale waliochinjwa? Kila siku wabunge Bungeni wanaomba Jeshi la polisi liongezewe fedha za kununulia vitendea kazi kama mabomu, silaha za kisasa, virungu, uniform Na Polisi waboreshewe mishahara na makazi Yao. Nauliza mnataka hivyo virungu Vya Polisi,mabomu ya Machozi yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi hayo mabomu ya Machozi yakatumike kufanyia Uvuvi haramu wa Samaki? Au hivyo virungu Vya Polisi mnataka Wapewe watu wa Kabila la Wamasai wakatumie virungu hivyo kuchungia Ng'ombe na Mbuzi? Virungu na Mabomu ya Machozi ni matumizi sahihi kwa watu wakorofi Kama Lipumba na wenzake . Cha Msingi hapa ni wananchi watii Sheria bila shuruti .Ukitii Sheria bila shuruti utakuwa umeepuka kupigwa virungu na mabomu ya machozi,mitama,nakozi na Matoke na kung'atwa na Mbwa wa Polisi. Binadamu wote ni sawa Mbele ya Sheria na Ibara ya 13(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 , inasomeka HIvi; ' Watu wote ni sawa mbele ya Sheria na wanayo haki , bila ya ubaguzi wowote ,kulindwa na kupata haki sawa Mbele ya Sheria'. Kwa Tafsiri nyepesi ya Ibara hiyo ,Jeshi la polisi limetekeleza matakwa ya ibara hiyo kwa kukukamata wewe na wenzako licha unayo madaraka makubwa na kukufikisha katika mkondo wa sheria kwasababu watu wote ni sawa mbele ya sheria. Kwani wasomi wa sheria tunaposema Usawa mbele ya sheria basi usawa huo auangalii umri wa ,elimu ,itikadi wala rangi kwani binadamu wote ni sawa mbele ya jicho la sheria. Nalipongeza Jeshi la Polisi chini ya IGP- Ernest Mangu kwa kuzinduka usingizini sasa kuanza kuwatia 'displine' viongozi wa juu wa vyama Vya siasa Kama Lipumba Jana mlivyomtia adabu . Nalipongeza sana mAana hawa viongozi wa juu wa baadhi ya vyama siasa ni Kama mashetani wamekuwa na tabia chafu ya kuwana na ajenda zao binafsi za kuleta Uvunjifu wa Amani nchini ambazo wafuasi wao Wengi hawazijui wanaamua kuwaunga mkono mwisho wa siku wafuasi wao Ndio wanaishia kushughulikiwa na Jeshi la Polisi. Rais wa Zimbambwe Robert Mugabe na Rais wa Uganda ,Yoweri Mseveni huwa hawataki kuendekeza viongozi wa aina hiyo, wanausalama wa majeshi hayo uwa wanaanza kuwashughulikia kwa vipigo vitakatifu Hao viongozi wa juu wa vyama Vya upinzani na viongozi wa juu wa Makundi mengine ambayo yanaamasisha wafausi Hao washiriki maandamano haramu. Tulimshuhudia Rais Mugabe alivyotoa adabu aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe ,Tsvangirai na rais Mseveni alipomtia adabu Besige hadi Leo hii hao vinara wa Chokochoko wamefyata Mkia. Enzi za Utawala wa Rais Benjamin Mkapa wakati jeshila Polisi likiongozwa na IGP- Omar Mahita aliweza kudhibiti na kumaliza Nguvu za baadhi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati uchwara waliokuwa hawana ajenda zenye mashiko waliokuwa wakikaidi amri ya Jeshi la Polisi . Mchana wa Leo ,Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia aliliomba Bunge liairishwe ili waweze kujadili hoja ya kwanini Jeshi la Polisi limempatia ' mkong'oto heavy ' Lipumba Jana Kwani eti Lipumba ni kiongozi mkubwa,watoto na waandishi wa Habari walioumizwa Jana. Spika Anne Makinda akitumia mamlaka yake na Kusema ametumia madaraka yake kuimuru serikali Kesho ije kujieleza bungeni kuhusu tukio Hilo. Wakati Makinda akitoa agizo Hilo, baadhi ya wabunge kwakweli mi nadiriki kuwaita ni wendawazimu na ambao hawana nidhamu wala staha,waliinuka na kuanza kupinga agizo Hilo la Makinda tena bila kutoa kipengele gani kinawaruhusu kufanya hivyo hali iliyosababisha zogo Kuzuka bungeni utafikiri watu wapo Sokoni. Jamani, Kama Bunge la Tanzania ambalo wabunge wake ndiyo watunga Sheria na Ndio baadhi Yao wanakuwa wakwanza kutoheshimu na kutii maagizo ya kiongozi wao yaani Spika, HIvi tunaweza Kusema tunawatunga Sheria kweli ? Nikisema kuna baadhi ya wabunge wa upinzani ni wendawazimu nitakuwa nakosa?Nidhamu na busara kwa wabunge Hao wa upinzani Iko wapi? Eti hawa ndiyo Watanzania turuhusu vyama Vya upinzani kiongozi taifa hili kwa tabia Kama hizi za kiuwenda wazi?haiwezekani. Mbatia aliyoyasema Leo Bungeni HIvi haramu Mbele ya Wanasheria wa namuona ni Mtu wa ajabu sana? Maana Kifungu cha 8 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002, inasema kutofahaumu Sheria siyo kinga yakutoadhibiwa. Mbatia haelewi Sheria na Huyo Lipumba hawaelewi Sheria hivyo ndiyo mAana wanafikiri hawawezi kufadhiliwa.Mnajidanganya. Mbatia Leo bungeni Kasema eti waliwahi kuzungumza na Rais wa Nchi wakasema eti viongozi wa juu nawatapigwa? HIvi rais wa nchi, IGP ni Sheria?Rais wa nchi, IGP wote Taasisi zao zimeanzishwa kwa mujibu wa Sheria na wanatakiwa wafanyakazi zao kwa mujibu wa Sheria.Kama kweli mlikubaliana hiyo basi waliamua kuwageuza viongozi wa upinzani 'Mambululala' kwasababu hamfahamu Sheria na Nyie kwa Ujinga wenu mkakubaliana. Mbatia acha Sheria Ufuate mkono wake , Mbona Halima Mdee, Sheikh Ponda Issa Ponda walivyoamua tea na kufikishwa mahakamani Mbona hatukukona ukisimama bungeni kuomba Bunge liarishwe ili Mjadili kwanini Mdee ,Ponda wamepigwa na kufikishwa mahakamani? Na kwa taarifa yenu Nyie wabunge ambao mmezusha zogo Bunge Leo kwa Shinikizo la kutaka ombi la Mbatia la kujadili kipigo kwa Lipumba lijadiliwe Leo, kwa taarifa yenu sisi wasomi wa Sheria tunasema imekula kwenu, Kwani Tayari Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga kaishamwandilisha hati Mashitaka Lipumba na atafikishwa mchana huu Katika Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam . Na akishasomewa Mashitaka ya nayomkabili ndiyo basi tena Bunge linakuwa limefungwa mikono kujadili Kesi iliyopo mahakamani. Kwa Tafsiri nyepesi Nyie wabunge 'wendawazimu' mliozusha zogo Leo Bungeni mmejiaribia wenyewe . Mlijiona mnaakili sana kuliko Spika Makinda.Mnamzarau kwasababu ni mwanamke? Sasa mjanja nani Kati ya Nyie wabunge 'machizi' na Makinga?Mjanja ni Makinda na Jeshi la Polisi na Ofisi ya DPP. Kama mnampenda sana Lipumba jichangisheni Fedha kumuwekee Mawakili wazuri au pandeni Ndege nendeni makamuwekee dhamana Katika Mahakama ya Kisutu. Nashauri Kanuni na sheria ya Bunge ifanyiwe mabadiliko ambayo yataingizwa kipengele cha kuruhusu matumizi ya virungu na mabomo ya machozi yatumike ndani ya bunge pindi wabunge wakorofi wanapozusha ukorofi ndani ya bunge n kusababisha muda wa bunge kuairishwa kwasababu ya vuugu hizo. Tumeishabaini Sababu ya wewe Lipumba kuamisha msiba wa Pemba Kuja Mbagala ni kwasababu wewe Lipumba umeanza kampeni za Ubunge jimbo la Temeke Kama mlivyokubalana na viongozi wenzio wa UKAWA katika vikao vyenu vya siri kuwa nyie viongozi wa juu wa vyama vinavyounda UKAWA mgawane majimbo yaani mkagombee ubunge badala ya urais kwani tayari mmeishaona nafasi ya urais hampati.Hilo limejulikana. Profesa Lipumna Kama una huruma na Marehemu wale siungeenda Pemba ukawakusanya wafiwa Ukawapikia Pilau na Biliani na Tende na Haruwa ungewapatia na ungeita na viongozi wa dini na Kisomo mngewasomea marehemu wale. Fanya Kama Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginal Mengi yeye anawaonea huruma Maalbino,walemavu wa viungo hivyo kila Mwaka amenitengea siku Moja kuwaandalia Mlo wa Mchana anakula nao na kuwasaidia. Lipumba Janja yako ya kutaka Ubunge jimbo la Temeke imejulikana, na siyo kosa kisheria kutaka Kugombea jimbo ila kosa ni kukaidi amri Hali za mamlaka husika.Usitumie Kumbukumbu za misiba ya watu kujifanyia kampeni katika jimbo ka Temeke, mizimu ya marehemu Hao itakusurubu. Lipumba umebugi Men. Chanzo: Happy Katabazi Blog: www.katabazihappy.blogspot.com Januari 28 Mwaka 2015. 0716 774494 Sent from my iPad -- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/d/optout. -- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/d/optout. |
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment