Comrade Elisa;
Nakuunga mkono kwa dhati kabisa Mkuu bila SHURUTI.
Obvious this is the way this Nation is heading to,tuna kazi kubwa ya kutafuta nini cha kufanya kurinusuru hili.
Changamoto iliyopo ni kwamba,haya yalitakiwa yawe yanafanywa na watu binafsi then Serikali itafute mustakabali,hapo ingekuwa suala dogo lkn sasa yanafanywa na Utawala hivyo kwa kutokea na kunusurika ni tundu la sindano.
Ukiangalia vitendo hivi vya utawala vinalifanya Taifa siku hadi siku kuendelea kuzoea na kuona fujo na machafujo ni njia ya kawaida ya maisha,hivyo sio mbali labda ni mwishoni mwa mwaka huu (Mwenyezi atuepushe) hali inaweza kuwa mbaya sana.
Katika hali ya ukosefu mkubwa wa ajira kwa kundi la vijana,hili ni hatari sana. Vijana kulingana na uzoefu wetu/wao mdogo katika maisha na kuhimila mambo,ni wepezi sana kushawishika na kweli tutaliingiza taifa hili katika historia nyingine.(Mwenyezi tuepushie balaa hili)
Reuben
On Wednesday, January 28, 2015 8:24 AM, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Kwa maswala yahusuyo Nchi yetu niliwahi kulia mara nne hadi sasa.
Mara ya kwanza nilitoa machozi na kulia sana wakati wa kifo cha Edward Moringe Sokoine. Nchi hii ilipoteza kiongozi mmoja bora. Kuna wanaofikiri kuwaa Kama Sokoine asingekufa basi Mwalimu Nyerere asingeacha amebadili Katiba ya kuweka vipindi viwili vya uongozi ngazi ya Rais. Ni vigumu kudhibitisha hilo maana wote wawili hawapo.
Mara ya pili ni pale Mwalimu Nyerere alipokuwa anashushwa na DAHACO kama mzigo. Nilikumbuka jinsi alivyokuwa anateremka kutoka ziara chache alizofanya nje ya nchi alizoea mlango wa ndege ukifunguliwa anatokeza na kupunga mkono kwa tabasamu lake la nadra lakini lenye ujumbe. Siku hiyo alikuwa anarufishwa akiwa amefariki. Nililia na kutokwa machozi.
Mara ya tatu ni leo nilipofungulia ITV na kwenye taarifa nikamuona Lipumba kuanzia anawatuliza wafuasi wake na kuwataka warudi nyumbani na yeye anaelekea uwanjani kuwaelekeza hivyo wananchi waliokuwa wametangulia kabla ya kujua kuwa Polisi wamekataza mkutano na maandamano. Nikaona msafara huo uliokuwa unajulikana lengo ni kutimiza matakwa ya amri ya polisi. Nikaona Polisi wanauingilia msafara huo. Nikaona sehemu ya majibizano. Nikaona walinzi wa Lipumba wakimzunguka na kutaka kumuingiza kwenye gari jekundu lililokuwa likijitahidi kusogea kumpakia. Nikaona Polisi wanatafuta namna ya kutumia kwa shida mabumu ya machozi. Nikaona wanajilazimisha kuanza kuyafyatua. Nikaona wanawapiga mateke walinzi wa Lipumba ili wamchukue asiendelee na wajibu wake kuwatawanya kwa amani wananchi waliokuwa uwanjani BAADA YA HAYO YOTE NIKATOKWA NA MACHOZI.
Mara ya nne ni baada ya kuona taarifa hiyo nikapiga magoti kumuomba Mungu alinusuru taifa hili. Nilimkumbusha Mungu jinsi Tanzania ilivyozisaidia nchi za AFRIKA KUPATA UHURU WAKE. Nikamkumbusha Mungu jinsi Tanzania ilivyokuwa makao makuu ya nchi zilizo Mstari wa mbele na makambi ya wapigania uhuru. Nikamkumbusha Mungu usemi wa Nyerere kuwa Tanzania haitajisikia huru kama jirani zake hawajawa huru. Nikamkumbusha Mungu jinsi watu fulani wanavyoliombea taifa hili usiku na mchana na watu hao yeye tu (Mungu) ndiye anayewajua na wao wanajijua. Nikamkumbusha mambo mengi. NIKATOKWA NA MACHOZI KWA UCHUNGU. Nina kawaida ya kujituliza sana ninapomuomba Mungu ili nihisi jibu analonipa. Leo nimeshindwa na Amina ya mwisho nimeisema nimeisha amka. Niliwaza mbali kweli. Niliona kwa sasa hata tumaini la kutumia uchaguzi kuleta mabadiliko nchini linayeyuka. Nani hakumbuki jinsi uchaguzi wa Serikasli za mitaa mapingamisi yasivyokuwepo na bila misingi ya kisheriza
limewaondolewa kugombea uchaguzi. Jinsi ambavyo baada ya kuhesabu kura mtu anatangaza mtu tofauti. Jinsi ambavyo waliapishwa watu tofauti na waliotangazwa kushinda.
Nikajiuliza tunakwenda wapi kama taifa. Nikafikiri itakuwaje siku wajumbe kutoka pande mbili au zaidi za Tanzania zinaenda Nairobi au Maputo kutafuta suluhu. Nikafikiri jinsi viongozi wetu (ambao wala sijui wanatuongoza kwenda wapi) wasivyoliona hilo Nikalia sana. Nimefikiri jinsi katika umri huu ninajiandaa kuwaacha wanangu na wajukuu zangu katika mazingira machafu ambayo wao hawakuwahi kuyaona yakitokea Afrika ya Kusini au kweingine lakini sasa wanayaona nchini mwetu. Nikawahurumia sana. Nikalia sana.
Ni mara hizo tu mimi nimewahi kutokwa na machozi kwa sababu za taifa letu hili tukufu.
Elisa Muhingo
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are
subscribed to the
Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment