Wednesday, 19 November 2014

Re: [wanabidii] JENGO LA KIHISTORIA LAPOROMOKA HUKO ZANZIBAR

hatuna thamani na utalii japo twaitaka hela yake

On Nov 19, 2014 2:32 AM, "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Ninakumbuka yakuwa-kwa upande wa miji mikongwe na majengo yao hasa miji inapopata status ya kuwa UNESCO historical sites nyumba za zamani za historia zinatakiwa zikibomolewa zijengwe kwa design ya zamani na material zile zile lakini kamili za kisasa ili kuweka historia. Hivyo, wale waliorithi zile jumba kutoka kwa ndugu zao au Mabwana zao (Masters wao wakiwa watumwa) wengi wao hawana uwezo. Idara ya mambo ya kale haina uwezo kukarabati majengo hayo ingawaje ni kivutio vha utalii. Majengo mengi ya Bagamoyo mji mkongwe wa biashara ya watumwa njia ya kuwapeleka ZNZ enzi hizo; mji wa majengo ya mwarabu na mjerumani na mitaa iliyopangika toka zama za mwarabu yameporomoka na mitaa sasa inajengwa hovyo majuka, frame kila kona na kuzima mitaa. Miti iliyotumika kunyonga watu, minyororo ya bandari ya zamani na katika makaburi au platforms za mjerumani imeibiwa. Zamani ukifa na unatumikia kifungo kaburi lako linafungwa mnyororo mpaka miaka ya kifungo iishe (Mjerumani huyo). Huko Tongoni Tanga maporomoko ya majengo, makaburu ya Persians. Makaburi ya Kaole Bagamoyo nayo ni kivutio lakini yanapakatika na yalijengwa kwa limestones tu lakini hatuwezi kuyajenga upya ila posho za mabilioni poa. Majengo ya Persians wakwanza kuingia na kuitawala Kilwa, Mafia mwaka 600 misikiti mikubwa ya ajabu, magereza, visima vya maji yanaporomoka eti hela za kukarabati mpaka zitoke UNESCO, Ufaransa etc. Aibu!!

Kwani maghorofa ya DSM posta yamejengwa kurudishia design ya mwarabu na mjerumani si wanabomoa na kujenga ukisasa zaidi na baadhi yanaporomoka lakini yale ya kale yapo?

Kuna uwezekano kabisa wa matajiri wetu kuchukua kisiwa tajiri akafanya adoption, kutengeneza masterplan ya ukarabati majengo na plan ya kutoa mafunzo ya utalii kwa vijana kushiriki kutembeza watalii, kulinda majengo watu wasibomoe matuwawe na kufanya uharibifu. Yeye analipa hela itakiwayo Wizara ya utalii na kodi halmashauri kuliko kuachia majengo yaishie kama kule Kilwa kisiwani. hela za utalii hazitoshi kuyajenga maana zinaingia kulipa mishahara.

Makaburi ya ras Kisimai Mafia yameporomoka mengine kuliwa na bahari mifupa inaonekana. Visima vinaonekama maji yakikupwa. Mijengo ya ajabu ya Kisiwa cha Juani na Ras Kisimani  Mafia Island na Kilwa Kisiwani inaporomoka misikiti mikubwa ajabu Kilwa.

Wazee wataalamu wa Kuita popo-vampire bats na kuita samaki, tuyuri zikaja na watalii kuangalia. Yote haya yapo bongoland visiwani na ni sehemu ya utalii. Kisima cha maji cha toka muajemi kuja kinategemewa zaidi Mafia kuliko cha kujenga kwa msaada wa idara ya maji na handpump yake ilikwisha kubomolewa. Cha kushusha ndoo kipo toka karne hiyo hadi ujio wa mwarabu wa Oman ZNZ na vasco dagama.

Tukiambiwa tunaweza uwekezaji katika SODA-tunakasirika. kasema kweli Mh Muhongo!! Mbona hatujengi mijengo hiyo inayoporomoka? Tunasifiwa ubilionea kinchi na kibara? Lakini, tunaachia mali na raslimali hizi zinaporomoka na kuua watu au kupotea. Akija mchina kuchukua apajenge-wageni kushika raslimali, uchumi haki ya wazawa...?

Kwa nini matajiri hawajiungi wakakarabati, kushika na kufufua viwanda na mashamba ya mamlaka za serikali ambayo yanaota magugu? Mananasi yanaoza, maembe, machungwa, nazi hazipati usafiri ila twaleta vipodozi hadi vya sumu kutoka ulaya sio kufufua mashamba na viwanda kununua mazao yaozayo kijijini na sokoni tandale, kariakoo, tandika. Nyanya za kopo na chupa sio natural.

Sera za PPP na sheria zipo na sector mbali mbali. Ruksa ya local firms na matajiri kuwekeza haitumiwi ila kulalamika ajapo mwekezaji kutoka nje na kupewa eneo ndipo kila mbunge kachachamaa na kujaza maneno na kuchochea raia kuvamia wawekezaji na kuharibu mali. Mijengo inatoka mpaka gazetini- wanasiasa CCM, CUF wapo huko ZNZ.  Hela za donors kwa chama chao ni malipo yake ya posho sio maendeleo jimboni jimbo lake liwe mfano.

*L-) loserTIC ipo kwa ajiri ya uwekezaji na mjengo wao upo, maelekezo sera na sheria na process kama unataka kuchukua eneo kuwekeza unaanzaje  hadi upate eneo hile na kufaidika wananchi inakuwaje. ukiambiwa hata OBC mwarabu wa kuwinda Loliondo aligharimia nini kiwilaya ni mamilioni mangap kila mwaka, milioni ngapi vijiji vinavyozunguka eneo, police, airport, msikiti wa Loliondo kafanya nini, kasomesha mtoto wa mbunge gani kwenda nchi gani na raia gani kama mafao-hawatosimama kubwata. Ukiangalia kilimo kinavyofanyika ndani ya wildlife conservation area ya Loliondo kwa trekta na plough, uingiaji mifugo kutoka Kenya na ulimbikizaji mifugo na wildlife kukosa malisho na expansion ya kilimo-waache wapiga KURA wangu (nipate Kula) ila mkosa-Mwekezaji aliyesanya rehabilitation ya eneo na kuweka tented camp, hotels, wildlife ranchi ambao wenyeji wanaoharibu mazingira yao wanaivamia wapate malisho kule kulikotunzwa). Conservation with development strategy ya nchi na ya dunia inatutaka wote tuwajibike.

Ni hivyo hata Chole Island Mafia mwekezaji from South Africa kakarabati soko la watumwa kawajengea soko jipya-halijai; kazuia uingiaji hovyo majengo mazee ya zamani ambayo amweka vibao-usiingie bila ruksa na kama sio mgeni wa hoteli (wakapiga kelele wanaonewa). Ameunda na kutoa mafunzo kwa vijana kulinda magofu ya Juani island na Chole yasibomolewe na watakao matumbawe/mawe yake. kajenga nyumba za watalii juu ya mibuyu (kwa waswahili ni nyumba ya mashetani)  wageni wanalala juu ya vibanda mibuyuni. Mbona kuna waarabu matajiri wenye ndugu zao Uarabuni-Oman etc na koo zao zipo Chole, ras Kisimani, Kilindoni hawajitumi mijengo inaporomoka na wao koo wanauza kwa wawekezaji wageni kwa bei poa? wanauza nyumba za NHC kariakoo kwa mabilioni mighorofa inapanda. Ukimuambia awe mbia/partner and shareholder-anakuambia mimi ninataka pesa yangu taslimu nisepe nihame hapa hayo mengine sina haja. Hela bilioni 2 nyumba ya 60,000/= 1974 wanagawana na kucheza mwali, arusi ya ufahari na kuhamia mchikichini au suna, vingunguti, mkwajuni bonde la mto msimbazi. Wakihamishiwa Kiwarani na kupimiwa-wanauza; mabwe pande sasa uzunguni-wanauza plots, mabati, simenti-tumezoa jangwani, mchikichini.
Kinakuja daraja la Salander litavuta wengi kurudi biashara inakua.

Lalamiko kubwa-raslimali zetu kutekwa na wageni. lakini mbona tunajiharibia wenyewe? Ubungo Mataa-Kimara Temboni EIA study 1974 chini ya Renadet na IRA aerial photos nyumba ipi inaachwa ipi inaondolewa kwa fidia na wataalamu walipita kwa EIA/SIA. ikatokea  alama zilizowekwa za Bomoa-rangi na neno bomoa linafuta kisha kulalamika uongo kwa mbunge. Wameongeza mijengo na frame hawajaondoka toka zama hizo na baadhi waliolipwa wamewauzia wenzao plots kuwadanganya. Sasa anaingia mwanaume wa shoka mangufuli kubomoa bila malipo hata kama uliuziwa na tapeli, ulilipwa hukuhama-utajiju.

Tusichanganye SIASA na utendaji kisera na sheria yakazuka maandamano na kuwapiga/kuua polisi bomoa bomoa itakapoanza. Pia-matajiri wafanye challenge ya kujiunga na kuushika uchumi under PPP, kushika utalii. Wanasiasa kukemea maovu jimboni, wazee wa mila, dini kukemea ukiukaji sheria  za urban and rural planning and land use.siruke tu angani na chopa-waone pia chini yanavyoporomoka, kuwa over grazed and mined through extensive and intensive unsustaibale farming na mining without land recovery, kuharibu misitu maji na mito tutegemeayo. Malezi mazuri ni mzazi kulea familia na watoto kimaadili, kukemea adabu na uovu inapobidi sio kunana daima-mwanangu anaonewa. kama ni shule au majirani watakuachia uone matokeo yake.
Yanaporomoka-wanaona. Wanapanda milimani kulima, kufuga-wanaona. land slides zikitokea.....serikali haijali usalama wa wananchi wake!! Tunajikosesha wenyewe kisha kulalama.




On Wednesday, 19 November 2014, 10:05, Fakhi Karume <fkarume@gmail.com> wrote:


Jengo moja la gorofa laporomoka huko Zanzibar katika eneo la kihistoria Jaws Corner ndani ya manispaa ya mji mkongwe Zanzibar.
Taarifa zinasema wananchi wa karibu na eneo hilo wakishirikiana na vikosi maalumu vya serikali vinaendelea kufanya jitihada mbali mbali katika eneo hilo ikiwemo kuhakikisha hakuna athari zaidi zitakazoweza kutokea.
Baadhi ya shuhuda mmoja ameiambia mazrui media kuwa watu wana wasiwasi juu ya uwepo wa watu wawili waliokua wakipita njia hawana uhakika kama waliwahi kuvuka au laa.
Hadi sasa juhudi za kuondoa kifusi cha jengo hilo kimeanza ili kuweza kubaini kama kuna watu wowote wale waliojeruhiwa au kupoteza maisha.
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment