Uswahili wetu watanzania, kudharau, kupenda rahisi rahisi, kutokukubali kuwa criticized, kupenda sifa-kusifiwa hata kama hustahili, majungu badala ya ushirikiano, ndio utufanyao tuwe nyuma.
Si ulisikia kesi au mashitaka ya matajiri wawili mmoja akimtaka mwenzie amlipe hela kama shs 100 hivi? Ni aibu kiasi gani? hatujitambui na hatujipendi na hatuna malengo na ndio maana unakuta watu wanapitisha wageni haramu, wanawapa ardhi, wanawaoza watoto zao na kuwapa makazi; wageni wanajaza mifugo, wanawaajiri kukata miti yao na kuchoma mkaa; kisha kuwadharau nao kulalamika kuomba msaada serikalinin kwamba wageni wanawaonea.
Kule ambako NGOs za Kisheria na za haki za wanawake walikofanya training for
capacity building kuhusu masuala ya ardhi-ndio magomvi ya ardhi yalikotawala na kuchomeana manyumba-Hanag ni mojawayo. LHRC, TAWLA, TAMWA, WAT, WLAC kwa hela za donors-Kabang!! Kuunda mabaraza ya sheria kata, kuuna kamati za ardhi na za usuluhishi masuala ya ardhi-hakuna kitu!! Yale mafunzo yote wametupilia mbali. Nenda Morogoro Rural, Mvomero-anachapwa fimbo na mmang'ati, maasai mpaka mwenyekiti wa kijiji. wapo wamelazwa muhimbili kwa fimbo za juzi Kidunda Moro rural kata ya Mkulazi. Kesi za kuchapwa na kuliwa mazao-haziishi miaka-RUSHWA. Usishangae kusikia polisi au hakimu hakubali assessment ya bwana kilimo eti anakwenda kuhesabu yeye mazao halafu anaandika-Hakukuta mazao ni bush. Hii huwafanya wananchi wakubali kumaliza kesi pembeni na nndipo mtuhumiwa halipi kabisa, anahama na au anapewa notice na kijiji ahame-ahami na anatamba hawamuwezi kaweka mkononi wakubwa? Mifugo inatia njaa, kiangazi inakula mboga za bustanini; kulishia mazao ya mzao wa pili au kuamua kulishia kabla ya mavuno; Kiangazi kikali wanaingia kuvua nyasi mpya zilizoezekwa katika nyumba kulishia mifugo yao na aliyendani kalala hutishiwa akitoka kichwa chao halali yao. Haya yanaendelea hakuna linalofanyika ila rushwa tuu. Wananchi wanaumia. Vita vinakuja na vitatokana na masuala ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima. Wawekezaji watavamiwa kwa makusudi ya visingizio maana wenyewe hatuwekezi. Ni kutumia excuses tu. Nenda ukaone machimbo ya madini kwa wachimbaji wadogo wadogo uone vichwa vyetu vilivyo pumba.Hela wanamalizia anasa, vileo n.k. wanachezea mercury na kuitia pia ndani ya maji ya mito na lake victoria. Usidhanie ukiwa DSM upo salama pia maana huko Mto Ruvu, Mgeta, Mkulazi maji yanachafuliwa na wachimbaji madini. Kuzaa watoto wasio vichwa, maumbile yasiyojulikana ni matokeo ya haya madawa. Bado mama ntilie anayechemsha ugali ndani ya mfuko wa plastiki na kuupikia hamira utune. Mainzi kibao na tambara afutialo meza ndio anafutia sahani (TB inashindana na malaria kwa sasa). Mwambie afunike chakula hapo nzi wasitue kama hajakutukana. Mwambie dreva asiovertake kilimani, mletemkoni na apunguze speed kama abiria wenzako hawajakutukana au kukuzomea na kukuambia ushuke wao wanataka kuwahi faster. Tunajijua na kujitambua sisi? Tungeusa nyumba Kariakoo, magomeni lengo ni kuonekana umeleta H.Kopa, na Mzee Yusuf mtoto katimiza arobaini toka azaliwe kisha-kuhamia bondeni jangwani. Pumba!! Mifugo mingi ufahari na kuoa wake wengi pamoja na vitoto vichanga
Semeni ya kusema-lakini kama hawa matajiri hawatajiunga kuweka kampuni kubwa ya kuwezesha vijana kulima na kuzalisha wao wanunue wasafirishe na kulisha viwanda nchini; kama hatutoondoa mijibaba barabarani ambayo inashainda kutwa kutembeza tochi, mipira, toys etc kila mtu yupo operating ktk level ya circulation ya mitumba, imported items sio uzalishaji; watu kuuza ardhi ya kilimo hovyo inajengwa majumba; mipango miji kuacha vijiji kuwa miji na kutokuruhusu miji hata midogo kuwa na mashamba na kupima mashamba kuwa plot za nyumba-tununuliwa hata na Rwanda.
Semeni ya kusema-lakini kama hawa matajiri hawatajiunga kuweka kampuni kubwa ya kuwezesha vijana kulima na kuzalisha wao wanunue wasafirishe na kulisha viwanda nchini; kama hatutoondoa mijibaba barabarani ambayo inashainda kutwa kutembeza tochi, mipira, toys etc kila mtu yupo operating ktk level ya circulation ya mitumba, imported items sio uzalishaji; watu kuuza ardhi ya kilimo hovyo inajengwa majumba; mipango miji kuacha vijiji kuwa miji na kutokuruhusu miji hata midogo kuwa na mashamba na kupima mashamba kuwa plot za nyumba-tununuliwa hata na Rwanda.
Maeneo mengine yamezungungwa na milima mashamba yapo mjini ndio wetlands-hutakiwi kulima mjini. Kwa nini nyumba zisijengwe milimani watu wakapanda miti wakalima bondeni? Matokeo bonde linajaa majumba na vyoo kuzalisha mbu wa ngirimaji. Na majumba hayo haswa mengi ni ya wageni toka mikoa mingine. Matokeo ya majumba bondeni watu wanapanda milina na kulima. Itakuja siku milima itaporomoka (land slides) na kufukia miji kama Morogoro, Mikumi. Kwani wenyeji hawana pa kulima, umbali wa mashamba aende kidoma, Kisanga etc unaleta matatizo (kuna ubakaji na uporaji). Na mashamba ya mbali-mifugo, wanyama pori inakula halafu mmesomea sekta mbali mbali lakini integration ya masuala kutatua matatizo kama haya ya mipango miji na mipango matumizi ardhi-tatizo. Ukikuta chuo cha Misitu-milima jirani haina miti. Cha kuzalisha mifugo-vijiji jirani hawana mifugo au hawafugi kisasa bado wanahama hama na kulimbikiza mifugo. Hizo livestock multiplication units na kuzalisha mitamba bora inakuwa kufaidisha wenye pesa watotao mbali sio adjacent communities. Tutafika? Tulalame tu ndio tumezoea. Hata kuiga mifano kilimo na ufugaji bora-hatutaki. Hata kuwe na mbunge mfugaji toka jamii ya wafugaji-hahusiki kubadili jamii yake anabadilika yeye tu kuwa na mitamba na majike bora na kufuga kisasa. wengineo ndio hao leo kilombero, Rufiji, Mtwara, Ruvu kulishia mashamba ya wenzao na kuwatesa
Inachosha ila kelele bungeni na maandamano ya kubomoa mali za watu-uharakati usio msingi maana hata mharakati pale alipo hana afanyacho cha maendeleo ya kusaidia watu. Takataka, mafuriko ya kinyesi, kubomoa mito kuichimba mchanga na maangamizo mengine-naye anaruka vihunzi hivyo anaingia kwake. Maneno pekee-hayatufai wala kujenga nchi kuleta mabadiliko.
Haya sasa ya Kagame huyo anapamba moto kujipendekeza nchi jirani na huku mnataka EAC irudishwe na kuboreshwa. Kinuksi kimeshaingia mtaivunja tena EAC Alexanda. sasa Bandari inashughulikiwa ikose mizigo. Tumezidi kudokoa vya watu badarini anyway. Kinachotakiwa sasa matajiri waungane tupae maana jirani wanaanza kututenga. Tukazane kuzalisha na kuuza mbali kwa kipato.
Hebu angalia kiambata!!
From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, 3 September 2013, 10:08
Subject: Re: [wanabidii] Hii ni dharau na fedheha kubwa kwa Taifa
Kiwasila,
Kwa jinsi ulivyoeleza kwenye andiko lako hapa chini kilamtu ataelewa. Maana umekosoa na kutoa njia mbadala ambayo wa-Tanzania wanaweza kuitumia kuwekeza hata katika miradi ya gas kwa kushirikiana. Kama kweli Mheshimiwa Mhongo kasema hayo amekosea.
Nionavyo mimi Kazi ya Waziri ni pamoja na kuwaelimisha watu wake na kutafuta namna ya kuboresha maisaha yao ikiwa ni pamoja na KUJITAMBUA huku uliko kuelezea kwa ufasaha kwenye andiko lako. Mhongo angesema hii miradi ya gas ni gharama hivyo akawahimiza matajiri kuungana kama ulivyofanya wewe hakuna ambae angehoji.
Alexander
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, September 3, 2013 5:00 AM
Subject: Re: [wanabidii] Hii ni dharau na fedheha kubwa kwa Taifa
Ifike wakati watanzania tukubali kujisema, kujipima na kuwa na dhamira ya kujifanyia vitu wenyewe. Tujiulize-tuna matajiri wangapi TZ ambao hela zao baadhi huzitoa kwa vyama vya siasa kwa mamilioni kujitafutia majina. Wachache sana husaidia development at grassoots level. Hawa matajiri waliopata hela kihalali au sio kihalali, baadhi yao badala ya kutoa misaada mikubwa kwa vyama, makanisa, misikiti na kuhonga watu wakaonekane mikutatoni au kufanya vurugu mikutatoni wangeungana na wale matajiri wa kupenda maendeleo wakaunda a multinational company wakafanya investment ndani na nje ya nchi. Utajisi sio kuonekana katika kumiliki malori, viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastiki au soda za rangi na maji-bali katika madini, kununua na kuuza pamba nje, kuchimba madini kusafisha hapa na kuuza nje, kulima mpunga, mahindi na mazao mengine ya biashara na ya chakula ili kujaza maghara ndani na kuuza nje ya nchi. haya yote pia yalenge kutoa ajira kwa vijana ambao saa kumi na 2 asubuhi huko vijijini unawakuta wanacheza pool chini ya miti hadi usiku kucheza kwa koroboi au taa za solar.
Ukipita vijijini unaona akili ya mwafrika ilivyofinyu. Udongo umejaa, misitu na miti imemzunguka lakini nyumba yake unamchungulia ndani anapolala unamwona. Chandarua alichopewa bure asiumwe malaria-kafunikia vifaranga au bustani ya mboga au kaning'iniza mlangoni kafanya pazia la mlango wa nje. Amekaa barazani na amelewa kuanzia saa moja asubuhi. haoni tatizo nyumba wazi na hawezi kujituma kukandina na hanunui udongo, maji wala fito. Ikitokea kiako cha kijijini kujadili maendeleo-atakacho ni posho tena watahimiza kikao kiishe mapema wanaharaka wapewe posho yao wanadharura waondoke. Mtumishi ugani-kukaa township kijijini hawezi. Na hata hapo kijijini-hajitumi na haelewi takwimu zozote za kijiji. Vyeti vyake anavyo na CV sifa kibao lakini hakieleweki kitu. Ila akiitwa semina anataka posho na nauli ya kutoka ktk Kata wakati yupo hapo hapo mjuini na ugomvi utaanzia hapo ktk posho ya kutoka mbali ambako hakai.
Mazingira bora gani utakayomtanzania ambapo mgeni akija katika mazingira yako anayatumia vizuri na anakulimisha kwa jembe hilo la mkono na unazalisha kulikoni na masimango juu unanyanyasika na upo upo tu. Kuibia wakandarasi ndio tina na ukishaiba la maana hakuna ufanyalo ni vileo na kutafuta magonjwa ambukizi.
Hata wachimbaji wadogo wadogo wakiambiwa kujiunga ktk vyama tabu-kila mtu anataka ubinafsi. hamudu kupata vifaa au mkopo mpaka wajiunge lakini hakuna kitu. wakijiunga kugombana ktk vikundi kugombania madaraka unakuta kikundi jina hawaelewani kila mtu anafanya vyake. Hata akipita wa kuwahurumia na kuwapa kuku bora wa kufuga, mbuzi wa kisasa na ng'ombe wa maziwa-kikundi hakidumu maana kila mtu anaona uvivu kupanda majani ya lishe, kuchanganya pumba za lishe na kuwalisha wanyama hao. Akijifanyia mmoja vizuri kwa kujituma-ugeni ukifika ndio watawaonyesha hao kama ndio wa kikundi kumbe kanyaboya. Vijijini tupo kukata miti na kuuza kuharibu mazingira, kulishia mifugo mashambani na kuhonga polisi na viongozi. Kila mmoja yupo petty trader wa vitumbua, mama au baba lishe kuuza vitu wazi mainzi tele na vumbi. Na hii ni kote mijini na vijijini. Kwa sasa pikipiki na bajaji ndio uwekezaji. Mijibaba vifua miraba minne ni pikie, bajaji, kupiga debe, mitumba kutwa kutembea kilometa 50 plus au kikimbizana na magari ili kuuza. Hata uwape mazingira bora ya kulima mazao, kuyafunga vizuri wasafirishe nchi jirani kama wajasiriamali-wachache utakaobaki nao-Serikali mbaya, haitujali ndio msemo wetu daima!! Kujitambua na kujituma ni tatizo la mtu mweusi wa Afrika na ndio maana vita haziishi daima na kugombania madaraka, kupenda rahisi rahisi vishuke kama mvua.
Sidhani kama kuna nchi Afrika yenye sera na miongozo kama TZ. tatizo letu ni utendaji wa kujituma kihaki na kuipenda kuitumikia nchi yetu kiuadilifu badala ya ubinafsi na kubweteka
Ushirikina tu unaongezeka kutawala. leo kikombe cha babu, kesho kibakuli cha bibi, keshokutwa tunguli Mtwara gas igeuke Maji isipatikane na kushabikia uharibifu-kubomoa madaraja, kuchoma nyumba za viongozi, mahakama, shule kupiga walimu; kutokumshitaki baba mbakaji binti na mlawiti mwanae kafikishwa polisi kasema eti atajirekebisha na bado anamrudisha mwanae kiujanja kutoka kwa ndugu anaendelea.wanaharakati wapo hawaandamani kumuweka polisi, ndugu walioizima kesi ya namna hii ndani washitakiwe na imeadikwa gazetini ila tupo kushabikia maandamano ya kisiasa.
Kama hatuna uwezo wa kulima na kuzingatia sustainable farming and livestock keeping, mifugo inazagaa nchi nzima kulishia mashamba kuingiza njaa; wananchi kuchapwa na wafugaji na serikali haina uwezo wa kurekebisha uvamizi mabonde, mito, wetlands, protected areas; tutakuwa na uwezo wa kuchimba na kulinda gas isiunguze misitu na majumba? Miji iliyopimwa tunashindwa control nyumba msongamano, fukwe kufamiwa na wenyewe kukataa kuchangia huduma na kuhujumu na kuingiza siasa-tutaweza kujiunga kuunda makampuni ya kufanya ukweli kiuchumi? Ona miji ya makorokoro, viwanda na mahoteli vinavyochafua mazingira, nyama maizi kibao inauzwa pa uwazi na hatufanyi kitu twanunua, twala-tutaweza ya uwekezaji?
tuondoe vibanzi vyetu wenyewe machoni kwetu kwa kujisema kama alivyoanza Sospeter Muhongo na wengineo kudiriki kutuchamba ili tutie akili kukichwa.
Naunga mkono alivyosema mheshimiwa, hana haja ya kuomba radhi, tunachekwa, kulalamika kwa vinavyoonekana vibovu ni desturi yetu bongo tusiopenda kujikanya tusonge mbele.
From: erick maro <rikmaro@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, 2 September 2013, 21:37
Subject: [wanabidii] Hii ni dharau na fedheha kubwa kwa Taifa
Sinahakika Nilichosikia kama ndicho waziri wa nishati na madini alichokisema akiwa timamu wa akili, huku akimaanisha alichosema. Kama alisema haya "Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye gesi na mafuta, bali waendelee na biashara ya matunda na juice, na pia hana muda wa kujadiliana chochote na Watanzania wale wanaofikiria kuwekeza katika mafuta na gesi ".
Hii ni kauli yake, ya serekali ilitoko madarakani au ya chama chake cha Ccm?
Kama alizungumza hayo akiwa timamu bila kutumia kilevi chochote wala kuagizwa na Serikali anayoitumikia au chama chake, hakika atakuwa ni mshenzi, mpuuzi na mpumbavu wa mwisho Duniani. Kama si kauli ya Serikali, wala chama chake basi nategemea awajibishwe ipasavyo na mabosi wake kwa kuutukana Umma wa Watanzania na Taifa letu kwa ujumla. Hata kama kweli hatuwezi si lugha ya kuitumia kwa Wananchi wenzako. Lakini siamini kama Serikali ikiweka mazingira rafiki, na sera bora zinazosimamiwa vyema tutashindwa kuwekeza katika gesi na mafuta. Hapa napata wasiwasi na uraia wa ndugu Sospeter Muhogo waziri wa nishati na madini, kwa kauli hii, pia serikali na chama chake.
Tujithamini, tujipende, tujikubali, tutumie kile tulichonacho kwa faida ya Taifa letu.
MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA .
-- Kama alizungumza hayo akiwa timamu bila kutumia kilevi chochote wala kuagizwa na Serikali anayoitumikia au chama chake, hakika atakuwa ni mshenzi, mpuuzi na mpumbavu wa mwisho Duniani. Kama si kauli ya Serikali, wala chama chake basi nategemea awajibishwe ipasavyo na mabosi wake kwa kuutukana Umma wa Watanzania na Taifa letu kwa ujumla. Hata kama kweli hatuwezi si lugha ya kuitumia kwa Wananchi wenzako. Lakini siamini kama Serikali ikiweka mazingira rafiki, na sera bora zinazosimamiwa vyema tutashindwa kuwekeza katika gesi na mafuta. Hapa napata wasiwasi na uraia wa ndugu Sospeter Muhogo waziri wa nishati na madini, kwa kauli hii, pia serikali na chama chake.
Tujithamini, tujipende, tujikubali, tutumie kile tulichonacho kwa faida ya Taifa letu.
MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment