Monday 30 September 2013

[wanabidii] Si kweli kuwa flagyl inaathiri ujauzito, inaunga au kulemaza watoto

Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Semwanza, akizungumza na gazeti la Tanzania Daima jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki amesema dawa aina Metronidazole 'Flagyl' haina madhara yoyote kwa wanawake kama inavyodaiwa katika taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kuwa mwanamke akitumia dawa hizo anajihatarisha kuzaa watoto wenye ulemavu au walioungana.

Hata hivyo, Semwanza alisema mwanamke anapokuwa mjamzito haruhusiwi kutumia dawa yoyote bila ushauri wa daktari kwa ajili ya usalama wa afya yake na ya mtoto aliyeko tumboni, "Ndiyo maana hata watu wanapokwenda kwenye maduka ya dawa za binadamu wanapaswa kuwa na cheti cha daktari, lakini nasisitiza matumizi ya metronidazole kwa wanawake hayana madhara, isipokuwa kwa mjamzito si vizuri kutumia dawa bila kuandikiwa na mtaalamu," alisisitiza.

Mtaalamu wa dawa kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya, Oswald Mwihava, alisisitiza hilo la matumizi sahihi ya dawa kwa wanawake wajawazito kwa kusema, "Dawa zote ni hatari kwa kinamama wajawazito, lakini pale ambapo atazitumia bila kushauriwa au kuidhinishiwa na daktari."

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

1 comments:

  1. Naomba msaada wenu, nilitumia metronidozole baada ya wiki 2 badae nikagundua nina ujauzito wa wiki 3, je haitaleta shida?

    ReplyDelete