Monday 30 September 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Al Shaabab Na Chimbuko La Ugaidi ( III)

Maggid,

Meles Zenawi ni marehemu Waziri Mkuu wa Ethiopia, hakuwahi kuw Rais.

wa Simbeye





From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, October 1, 2013 7:38 AM
Subject: [Mabadiliko] Al Shaabab Na Chimbuko La Ugaidi ( III)


Tunapotafakari harakati za kigaidi za kikundi cha Harakaat Al Shaabab Mujaheedin maarufu kama Al Shaabab, hatuna budi pia kuipitia historia.
Kuna taarifa ambazo hazichambuliwi zikawekwa mezani, kuwa nafasi ya Ethiopia katika kuingilia kati na kupambana na Al Shabaab nchini Somalia inatokana pia na ukweli wa kihistoria, kuwa Ethiopia na Somalia kwenye miaka ya 70 wamekuwa kwenye mgogoro wa mipaka  na hususan kwenye jimbo la Ogaden. Ni mgogoro uliopelekea vita pia.
Na ni Ethiopia iliyowahi kuingia Somalia na kupambana na Al Shaabab na hivyo kuvunja taratibu za utawala wa Sharia na uwepo wa Mahakama za Sharia. Ethiopia imekuwa mstari wa mbele katika kuisadia Serikali ya Shirikisho ya Somalia. Ndio, Ethiopia ina maslahi ya moja kwa moja katika Somalia.
Hivyo basi, yumkini adui namba moja wa Al Shabaab ni Ethiopia na si Kenya. Na kwa kuangalia nadharia ya adui wa adui yako ni rafiki yako, tunaona uwepo wa mahusiano ya ajabu. Kwamba kuna taarifa ya uwepo wa mahusiano kati ya Eritrea na Al Shaabab. Maana, kwa miaka mingi sasa, Merek Zenawi, Rais wa Ethiopia, amekuwa adui na Isaias Efeworki, Rais wa Eritrea. Hizi ni nchi jirani, na Marais wawili hawa inasemekana wana undugu pia.
 
Lakini leo tuliangalie kwa karibu tukio la kigaidi lililoushtua ulimwengu  na hata kuigizwa kama filamu ya Hollywood.  
Ni tukio  la utekaji wa ndege  ya abiria ya Ufaransa iliyokuwa na abiria wengi wa Kiyahudi.  Na mmoja wa wahusika wakuu katika tukio hili la kigaidi alikuwa Jenerali Idd Amin Dadah wa Uganda.
Ndio, licha ya kuwa Jenerali Idd Amin kuendesha ugaidi wa dola kwa maana ya State Terrorism, kwenye tukio hili, Jenerali Idd Amin alishiriki rasmi kwenye Ugaidi wa Kimataifa. Maana, tukio lile la utekaji ndege lilianzia Ulaya, likaambaa Mashariki ya Kati na kumalizikia kwenye ardhi ya Uganda. Ni kwenye  uwanja wa ndege wa Entebbe huku Idd Amin mwenyewe akishiriki kuratibu harakati za kigaidi.
 
Maelezo marefu juu ya sakata ya Entebbe yanasimuliwa kwa umahiri
mkubwa na mwandishi  William Stevensson katika kitabu chake cha (90 Minutes At Entebbe), Yaani Dakika 90 katika Entebbe.

Ndege hiyo ilitekwa nyara Juni 27, 1976  mara ilipoanza kuruka
kutoka uwanja wa ndege wa Athens nchini Ugiriki kuelekea Tel Aviv. Miongoni
mwa watekaji nyara,  walikuwemo Wapalestina, lakini raia mmoja wa Ujerumani naye alishiriki utekaji  huo.  Mjerumani huyo alikuwa ni mfuasi wa kikundi cha kigaidi cha Ujerumani kulichojulikana kama  "Baader-Meinhof."
Inasadikiwa, kuwa  Dr. Wadi Hadad, mwanaharakati na Kiongozi wa chama
cha ukombozi wa Wapalestina cha PFLP (Popular front For Liberation of
Palestene) alishiriki kwenye kupanga kazi hii ya kigaidi. Bila shaka,
inaaminiwa pia, kuwa  aliyekuwa gaidi nambari moja wakati huo, Ramirez
Carlos, ambaye pia alijulikana kama  "The Jackal", alikuwa na mkono wake
kwenye kazi hiyo.

Baada ya kutua na kujaza mafuta Tripoli , Libya, ndege hiyo iliendelea hadi Uganda na kutua Entebbe. Wakati huo Idd Amin alishakorofishana na maswahiba wake Waisrael na kutangaza kuunga mkono  harakati za Wapalestina kuikomboa nchi yao. Kuna wakati, Idd Amin alishawahi  kutamka,  kuwa anawaandaa askari wake kwenda kushiriki mapambano ya kuwandoa Wayahudi kwenye milima ya Golan waliyoiteka toka kwa Wapalestina. Na Idd Amin alishaviamrisha vikosi vyake kufanya mazoezi ya kivita kujiandaa na operesheni ya kuikomboa milima ya Golan.

Naam, ndege ilipotua Entebbe, abiria wote walikaribishwa na Idd Amin mwenyewe. Siku mbili baadae, watekaji nyara walianza kutoa madai yao; walidai  mateka wangeachiwa huru kama idadi kubwa ya wafuasi wa vikundi kadhaa vya kigaidi wangeachiwa huru kutoka kwenye magereza ya Ulaya na hata Afrika.

Ni katika tukio hili la utekaji nyara ndege ambapo kwa kiasi fulani mateka walihisi kuwepo kwa tumaini la kukombolewa. Ni  kwa vile maofisa  wengi wa jeshi la Israel wamefanya kazi Uganda ikiwemo kutoa mafunzo ya  kijeshi. Na kama kuna watu duniani waliokuwa wakimjua vema Idd Amin ikiwemo uwezo wa jeshi lake, basi, watu hao ni Waisrael. Maofisa wengi katika jeshi  la Idd Amin walipata mafunzo yao ya kijeshi Israel.
Kabla ya operesheni hiyo iliyopewa jina la Thunderbolt kuanza, Mossad, Shirika la Ujasusi la Israel, liliamua kumtumia Jenerali wake mstaafu aliyeitwa Chaim Bal  Lev.  Bwana  huyu alikuwa ni rafiki mkubwa na wa siku nyingi wa Jenerali Idd Amin. Wawili hawa walifanya mazungumzo ya muda mrefu na ya kirafiki kwa kutumia simu. Waliongea  karibu siku zote kabla ya mateka kuokolewa.
Kwa kumtumia Jenerali huyu  rafiki wa Amin, Waisrael walikuwa wanaiba muda ili kujiandaa zaidi,  na vile vile kujaribu  kumshawishi Amin asiwadhuru mateka hao na pengine kuwaachia huru.

Hata kama majasusi ya Kiyahudi walikuwa na michoro yote ya uwanja wa Entebbe ambao waliuchora wenyewe na kuujenga, lakini, kazi ya vikosi vya Israel kutua Entebbe haikuwa rahisi sana. 
Hawakuwa na hakika ya ukubwa wa vikosi vya Amin uwanjani hapo. Walitegemea zaidi , ufahamu wao wa  uwanja wa ndege wa Entebbe. Maana, ni Waisrael  waliojenga uwanja huo. Kutoka Tel- Aviv hadi Entebbe ni mwendo wa takribani  saa nne kwa ndege.
Uganda na Israel wamekuwa na mahusiano mazuri ya muda mrefu.
Mahusiano hayo yangalipo hadi hii leo. Ni kutokana na sababu za kihistoria. 
Kabla ya Jumuiya ya Kimataifa kupendekeza  makazi ya Wayahudi waliokuwa
wametapakaa dunia nzima yawe  katika Israel ya sasa, nchi ya Wapalestina,
kulikuwepo na wazo la Wayahudi kutafutiwa makazi mapya katika nchi ya
Uganda. Mpaka miaka ya karibuni, nchi pekee ya Kiafrika ambapo raia wa Israel hakuhitaji kuomba viza  ni Uganda. Raia wa Uganda pia hawakuhitaji pia kuomba viza ya kuingia Israel.

Tukirudi kwenye tukio lile la utekaji ndege. Kwa haraka,  Waisrael  waliendesha operesheni ambayo si rahisi kusadikika. Makomandoo wa  Israel waliruka kwa ndege kubwa kutoka Tel-Aviv kuelekea Entebbe. Ndege yao   ilitua saa sita na dakika moja usiku kwenye pembe ya mbali ya Uwanja wa Entebbe. Taa za ndani na nje ya dege lile kubwa zilizimwa wakati ndege ilipoukaribia uwanja wa Entebbe ikiwa na mwungurumo dhaifu. Mwungurumo
usiosikika kwa mbali.

Waisarel  walikuja na ndege mbili, moja ilibaki Nairobi ikiwa na
vifaa vya tiba na vingine muhimu. Iliyotua Entebbe ilibeba gari mbili,
Landrover na Mercedes Benz nyeusi.
Gari hizo zilitumiwa na makomandoo wa Kiyahudi kufika kwenye jengo walilokuwamo mateka. Waliwakuta mateka wote na wateka nyara wakiwa katika ukumbi wa mapunziko kwa abiria.
 Amri ilitolewa kwa lugha ya Ki-hebrenia ikiwataka Wayahudi wote wajilaze chini mara moja.  Wote waliobaki wamesimama au kuinama kwa kusitasita, hawakupata sekunde zaidi za kutafakari. Risasi za makomandoo wale ziliwamiminikia miilini mwao.

Operesheni ya kikomandoo iliyochukua takribani dakika tisini
pale Entebbe iliwaacha  watekaji nyara saba bila uhai. Idadi ya askari wa
Amin takribani ishirini nao waliuawa pale Entebbe. Mateka wote walikombolewa isipokuwa mama wa miaka 75 Dora Bloch aliyekuwa hospitalini Mulago, Kampala.
Inasemekana, kuwa  mateka huyo akaja kuuawa na Idd Amin mwenyewe. Habari hiyo haijathibitishwa .

 Kwa upande wao,  Makomandoo wale wa Kiisrael walimpoteza  Kanali
Yoni Netanyahu. Komandoo yule aliuawa kwa kupigwa risasi ya usoni na askari
mmoja wa Idd Amin. Miaka ishirini baadae, kaka wa Yoni Netanyahu  akaja kuwa Waziri Mkuu wa Israel, jina lake ni Benjamin Netanyahu, na hadi hii leo, Benjamin Netanyahu ni kiongozi katika Israel. Itaendelea....
Maggid.

0754 678 252
 
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment