Monday 30 September 2013

Re: [wanabidii] KUFUNGIWA MAGAZETI - WAHAFIDHINA SASA WANAONGOZA

bandugu,
msipopoe macho huyo bwana kunyanyara kwa sababu kila msafara wa mamba kengo nao wamo. kwa hiyo katika safari na harakati za kudai haki ya kupata na kupasha habari ambayo imehakikishwa kwa watanzania na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania mamba wamo akiwamo kunyanyara. msipagawe kukuta mtu anapinga lisilotarajiwa kupingika.
kunyanyara anashangaa na kudai eti zito anatoa povu kwa sababu tu kasema kuwa atatangaza mishahara ya wakubwa! kwani kuna ubaya gani kutangaza mishahara ya wakubwa? kwani mwajiri wa hao wakubwa ni nani? leo hii mwajiri wa mtu kutangaziwa mshahara wa mtumishi wake kunyanyara anaona nongwa? hili ni tatizo la kila mtu kutoa maoni hata juu ya somo ambalo ni geni kwake. kwani lazima tutoe maoni hata kuhusu jambo tusilolijua?
kuhusu sheria ya magazeti ya mwaka 1976 nambari 3 sina la kuongeza, mdogo wangu jesse kamaliza yote? bravo jesse, tuko pamoja. lakini usishangae watu kupinga sheria hiyo kuondolewa kwenye statute books, hii ni kwa sababu wananufaika nayo kwa njia moja au nyingine. muulize kunyanyara kwa nini vifungu vingine vya sheria hiyo havitekelezwi huku havijafutwa? mfano kifungu kinachoruhusu polisi mwenye cheo cha inspekta kwenda juu kukagua magazeti nyumba hadi nyumba kuhakikisha yamechapwa kwenye mitambo halali au vifungu vya sheria hiyo vinavyotaka magazeti na vitabu vyote kutoka nje vihakikiwe; au vifungu vya sheria hiyo vinavyotaka kuwekwa bond kila gazeti linalochapishwa nchini au vifungu vinavyotaka polisi kuingia na kunyofoa vipuri vya mtambo ambao kwa mawazo ya polisi hao unatumika au wanadhani utatumika kuchapa gazeti lisilotakiwa! hii si sheria ni zimwi. nchi yetu tanganyika haitaruhusu sheria hii kufanya kazi.
kicheere, tungi, kigamboni, tanganyika territory



From: ananilea nkya <ananilea_nkya@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, September 30, 2013 7:29 PM
Subject: Re: [wanabidii] KUFUNGIWA MAGAZETI - WAHAFIDHINA SASA WANAONGOZA

Jesse Mhariri wangu,
Nakuunga mguu, kichwa na mikono kwa hoja uliyotoa. Niongeze  ufafanuzi kidogo tu,  vyombo vya habari haviwezi kuchangia maendeleo effectively kama  vinaendesha shughuli zake kwa kutumia sera na sharia za miaka 40 iliyopita. Kama nchi, TUNAJIDANGANYA, basi. Na maumivu ni lukuki leo na kesho hadi sisi wananchi  wote tutakapopata ujasiri wa kutosha na kusimama kusema sharia hizi  za KIKOLONI  basi, tunataka uhuru wetu. 
 

From: Jesse Kwayu <jesse.kwayu@guardian.co.tz>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, September 30, 2013 4:19 PM
Subject: RE: [wanabidii] KUFUNGIWA MAGAZETI - WAHAFIDHINA SASA WANAONGOZA

Watu aina ya ezekiel kunyaranyara ni wa kuombea tu labda kuna siku Mungu
atawafungua macho ili waone au labda masikio yatafunguka ili wasikie. Hana
ufahamu na hayo asemayo. Laiti midomo ingelikuwa inalipiwa kodi kwa kila
neno litokalo labda angekuwa makini, au angelikuwa ana subira hata kama ya
mtoto angerudia kusoma alichosema Zitto kwa hakika angelijua kuwa yeye ndiye
anatoka povu tena jepesi mno.
-Kama hajui hayo aseme kama sheria ya Magazeti namba 3 ya mwaka 1976 siyo
kandamizi; aseme kama serikali haijawa mlalamikaji na hakimu kwa wakati
mmoja; aseme kama utawala wa sheria unaruhusu mtu kuhukumu kesi yake
mwenyewe; lakini mwisho ajiulize nchi hii ni mali ya serikali au mali ya
Watanzania? Nani mwenye uamuzi wa kupora haki ya Watanzania? Siyo serikali,
siyo Bunge, siyo mahakama, haki ni haki. Kufungia magazeti tena kiimla kama
ambavyo serikali imekuwa ikifanya miaka yote ni kuendeleza utendaji wa
kiimla.
-Mwisho ezekiel kunyaranyara ujue kuwa hakuna marefu yasiyo na mwisho, ni
bora kujiandaa kwa mwisho mzuri/mwema kuliko mbaya. Walikuwako watu hodari
na shupavu, lakini leo wako wapi. Tenda wema nenda zako; sikia ushauri mzuri
ili kuishi maisha ya amani kesho.
- serikali inayojiweka kwenye mgogoro kila uchao ina walakini, kuna shida
mahali, kuna tatizo la kutafakari. Kuna uduni wa kuelewa mambo na
kuyapambanua kwamba jana asilani haiwezi kuwa leo. Mwaka 1976 siyo leo, hata
mwaka 2005 siyo 2010 ndiyo maana hata kura zinasema hivyo, na hata jana
haiwezi kuwa leo. Sheria mbaya zina asili ya kusaidia tawala mbovu kwa
kitambo tu, lakini mwisho na zenyewe hulizwa na sheria hizo hizo. Haya
yalipata kutokea Zambia, Malawi na hata hapa Tanzania. Ukibisha muulize
Agostino Mrema akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alitumia polisi na mabomu ya
machozi kuwashughulikia kina Nesamburo kule Moshi kisa wapinzani, lakini
naye baada ya kitambo tu naye akapitia tanuru hilo hilo. Ni wakati tu.
ezekiel kunyaranyara fikiri, fikiri zaidi na fikiri tena.
Jesse

-----Original Message-----
From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On
Behalf Of Joseph Ludovick
Sent: Monday, September 30, 2013 5:28 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] KUFUNGIWA MAGAZETI - WAHAFIDHINA SASA WANAONGOZA

jueni kwanza maana ya kunyaranyara: ni kuogopaogopa. sasa endeleeni. mwoga
huyu!

On 9/30/13, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
> Kunyaranyara
>
> Jifunze kusoma au kusikia habari isiyo na mwelekeo wako, nimesoma hoja za
> zito mara mbili mbili sijaona ni wapi katoa "povu" kama ulivyoita wewe.
> Zitto ana hoja za msingi na zinajadilika sioni ni kwa nini Kunyaranyara
> huzioni kama hoja bali povu. Unapomnyooshea mtu kidole kumbuka vinne
> vinakupoint wewe katika hili umechemka babu. Hivi tatizo liko wapi Zitto
> anaposema sheria iliyotumika kuyafungia magazeti ni mwaka 1976. Swali ni
je
> wewe hiyo sheria umeisoma na kujua siyo kandamizi?
>
> Pengine ungemuuliza Zitto atwambie sheria hiyo inasemaje au ukapekua
> mwenyewe na kutueleza strengths za sheria hiyo kama utagundua haina
> mapungufu. Mambo ya sheria wakati mwingine yanakuwa kinyume na
> tunavyofikiri sisi tusiokuwa na taaluma hiyo. Nakumbuka Kesi ya Zombe
> ambapo wengi tulijua lazima angetiwa hatiani lakini Jaji alisema
> haiwezekani kumtia hatiani mtu anayethaniwa kuwa msaidizi wa muuaji kabla
> ujamtia hatiani muuaji mwenyewe.
>
> Zitto anapendekeza kwamba magazeti yangeshitakiwa badala ya kufungiwa ana
> hoja kwa wenye ujuzi kwenye mambo kama hayo tunaomba muijadili hoja ya
> Zitto kwa mapana yake badala ya kuipuuza. Ni wakati gani habari fulani
> inaitwa ya uchochezi au siyo ya uchochezi? Pengine ni pale
isipolifurahisha
> kundi fulani hata kama habari hiyo ni muhimu kwa tulio wengi kuijua .
> Tujadili kwa mapana kidogo kuhusu jambo hili, tutafika mahali kila gazeti
> litapangiwa liandike vichwa gani vya habari mfano " Serikali kumuwezesha
> kila mtanzania kuishi maisha ya kifalme ifikapo 2015'
>
>
> 2013/9/30 ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
>
>> Zitto
>>
>> Wakati mwingine inaonekana unapoteza kabisa hekima ambayo wakati mwingi
>> ninakuona unayo. Watu wengi wamekuwa wakinikanya kuhusu kukuamini sana
>> nawabishia lakini kwa mbali sasa naaanza kuona kama wanakuwa wako sahihi.
>>
>> Utamtishiaje mtu mzima kwamba sijui eh, oh ... tutataja mshahara wake ...
>> oh sijui itakuwaje... Hivi uko sawa wewe? Au umepagawa kaka, au kaguswa
>> nduguyo???? au ulikuwa na article ambayo ulipanga kuitoa katika magazeti
>> hayo sasa dili limekufa...
>>
>> Usitoe povu, usije ukaonesha kupwaya kwa hoja. Jadili kwa umakini
>> wasomaji
>> tutasoma tutapima. Acha siasa hizi ndizo sheria zinazotuongoza kwa sasa.
>> Onesha the way forward siyo kutishia nyau watu wazima.
>>
>> Umenisikitisha sana.
>>
>> K.E.M.S.
>>
>>  *From:* Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
>> *To:* Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
>> *Sent:* Monday, 30 September 2013, 14:59
>> *Subject:* [wanabidii] KUFUNGIWA MAGAZETI - WAHAFIDHINA SASA WANAONGOZA
>>
>>  *Zitto Kabwe, Mb*
>> Kwa mshtuko na masikitiko makubwa kuanzia jana jioni tumepokea taarifa za
>> kufungiwa kwa magazeti mawili ya kila siku hapa nchini ya Mwananchi na
>> Mtanzania. Serikali imechukua uamuzi huo kwa kutumia sheria ya kidikteta
>> ya
>> magazeti ya mwaka 1976 ambayo Tume ya Jaji Francis Nyalali iliiorodhesha
>> kama sheria kandamizi. Sababu zilizotolewa kuhalalisha uamuzi huu ni
>> sababu
>> zisizo na maana na ambazo Serikali ingeweza kufungua mashtaka ya kawaida
>> kabisa mahakamani kushtaki magazeti hayo iwapo haikupendezwa na habari
>> walizochapisha.
>> Moja ya sababu ya kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi ni kuchapisha taarifa
>> kuhusu mishahara ya Serikali. Serikali inasema habari hii ni siri.
>> Serikali
>> hii hii ambayo imesaini makubaliano ya kuendesha serikali kwa uwazi (Open
>> Government Initiative) na kumwagiwa sifa na Rais Barack Obama wa Marekani
>> inalifungia gazeti kwa kuandika habari za mishahara ya watumishi wa
>> Serikali. Mishahara kuanzia mshahara wa Rais mpaka wa mtendaji wa Kijiji
>> haipaswi kuwa jambo la siri. Kuonyesha kuwa jambo hili linapaswa kuwa
>> wazi
>> mkutano ujao wa Bunge tutatafuta kila namna kutaja mshahara wa Rais,
>> Makamu
>> wa Rais, Waziri Mkuu na baadhi ya Watendaji wa Mashirika makubwa ya Umma
>> kama njia ya kuwaunga mkono gazeti la Mwananchi kwa habari yao hiyo.
>> Mapato
>> ya Mbunge yanajulikana sasa kuwa ni shilingi milioni 11.2 kwa mwezi kabla
>> ya kuongeza posho za vikao za shilingi laki 200,000 kwa siku na posho ya
>> kujikimu ya shilingi 130,000 kwa siku. Watanzania wana haki ya kujua
>> wanawalipa kiasi gani watumishi wao. Tutaanza na mshahara wa Rais!
>> Gazeti la Mtanzania limefungiwa pamoja na mambo mengine kwa kuandika
>> 'mapinduzi ni lazima'. Inashangaza Serikali ya Chama cha Mapinduzi
>> inaogopa
>> neno mapinduzi. Marehemu Mzee Steven Salum Nandonde, aliyekuwa mbunge wa
>> Jimbo la Tandahimba alipata kusema bungeni kuwa 'lazima nchi ipinduliwe'.
>> Ni matumizi ya lugha tu. Mzee Nandonde yeye alikuwa analalamikia
>> maendeleo
>> duni ya mikoa ya kusini na kutaka Kaskazini iwe Kusini na Kusini iwe
>> Kaskazini. Serikali inafungia gazeti kwa sababu ya kuandika Mapinduzi ni
>> lazima ilhali kila siku Zanzibar wanasema Mapinduzi daima!
>> Gazeti la Mtanzania linahaririwa na Absalom Kibanda, mwandishi wa habari
>> ambaye bado anaponya majeraha ya mwili na kisaikolojia ya kuteswa na watu
>> ambao mpaka leo hawajakamatwa. Badala ya Serikali kuwakamata watesaji wa
>> Kibanda, inamnyima kazi Kibanda ili ateseke kwa njaa kwa kukaa miezi
>> mitatu
>> bila kazi. Pia wanatutesa Watanzania kwa njaa ya kupata habari ambayo ni
>> haki ya msingi ya kikatiba. Hii ndio zawadi Serikali inampa Kibanda baada
>> ya kung'olewa kucha, kunyofolewa jicho, kukatwa vidole na kuteswa kwa
>> namna
>> isiyoelezeka.
>> Matukio ya hivi karibuni na namna Serikali inavyoyachukulia yanaonyesha
>> dhahiri kwamba Rais Kikwete kazidiwa nguvu na kundi la wahafidhina ndani
>> ya
>> chama na Serikali yake. Rais ambaye alianza kwa kuhubiri uvumilivu wa
>> hali
>> ya juu na hata yeye mwenyewe kupata kusema uvumilivu huu wengine wanauona
>> kama udhaifu lakini ameamua kujenga Taifa la kuvumiliana. Rais alipata
>> kulalamika hadharani kwamba kuna wenzake wanataka aongeze ukali. Ni
>> dhahiri
>> kundi hili la wahafidhina sasa ndio linalomwongoza Rais Jakaya Kikwete.
>> Kitu kimoja tu Rais azingatie, kundi hili linaongozwa na maslahi binafsi
>> ya
>> kubakia kwenye utawala wakati yeye anapaswa kuacha 'legacy'. Rais Kikwete
>> asipokuwa makini atakuwa Rais karatasi (lame duck) tu tunapoelekea mwisho
>> wa utawala wake. Maamuzi ya hovyo na ya kidikteta ya kufungia magazeti
>> yanamchora vibaya mbele ya wananchi na jamii ya kimataifa. Wahafidhina
>> kuwa
>> nguvu zaidi ya kiutawala ni makosa ambayo watanzania hawapaswi kuyakubali
>> kamwe.
>> Wananchi sasa waifanye Serikali kujutia uamuzi wake wa kufungia magazeti.
>> Nimeamua mimi binafsi kama mbunge kesho Jumatatu tarehe 30 Septemba, 2013
>> kupeleka taarifa rasmi kwa Katibu wa Bunge ya kupeleka muswada Bungeni wa
>> kuifuta kabisa Sheria kandamizi ya magazeti ya mwaka 1976. Sasa tupambane
>> na kundi dogo la wahafidhina ndani ya Serikali na CCM wasiopenda
>> mabadiliko
>> na iwe fundisho kwa wahafidhina wengine wowote waliopo ndani ya Serikali
>> au
>> nje ya Serikali kwamba Uhuru wa habari sio jambo la kuchezea kama golori.
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>  --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment