Monday 30 September 2013

[wanabidii] Al Shaabab Na Chimbuko la Ugaidi ( II)

Tumeshajadili maana ya ugaidi na aina  za ugaidi kwa kuzitolea

mifano.  Hapa tutajadili juu ya chimbuko la ugaidi na kwa kutoa mifano. Na kama nilivyobainisha huko nyuma, tutaanza pia kuona mahusiano ya mwezi Septemba na vitendo vya kigaidi.

 

Wa- Salote

Kwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita kikundi cha Wayahudi kilipambana vikali
dhidi ya himaya ya Waroma katika iliyokuwa Palestina ya zamani.  Kikundi
hiki kiliitwa Salote. Ni  wenye hasira kali ikiwa na maana pia kuwa  kilikuwa ni
kikundi cha kisiasa na kidini chenye imani kali.  Kikundi hiki kilitaka
Wayahudi wote wazingatie yote kulingana na maagizo ya dini yao.

Wasalote walipambana kisiasa dhidi ya dola ya wavamizi ya Waroma.
Wasalote waliongozwa  na Myahudi Galileo, ambaye amri yake ya kuwataka
wafuasi wake  kugoma kulipa kodi ndio ilikuwa chachu ya  kuanzisha mapambano
ya kigaidi dhidi ya wavamizi wa Kiroma. Jambo hili linashuhudiwa pia katika
maandiko matakatifu ya  Biblia juu ya kodi  katika Agano Jipya.

Hatma ya Wayahudi haikujulikana , lakini, kiongozi mpya  alijitokeza
na kuwaahidi Wayahudi  ukombozi kutoka kwenye  mikono ya wavamizi. Hatimaye,
baada ya  machafuko yaliyodumu kwa miaka sabini, Wasolote waliangamizwa 
baada ya Jerusalem kutekwa na hekalu kuangamizwa. Wasalote walirudi nyuma
hadi  kwenye vilima vya Masada.

Baada ya kushindwa huko kwa Wasalote, Wasalote wapatao elfu moja 
walijiua kwa pamoja. Wasalote waliwaua kwanza wanawake  , watoto na wazee,
baadae wanaume nao walijiua kabla ya Waroma hawajavitwaa vilima hivyo.
Inasadikiwa tukio hili lilitokea mwaka 73 baada ya Yesu Kristo.

Wa-Assassine

Miaka elfu moja baadae lilijitokeza kundi jingine la kigaidi, hawa waliitwa 
Assassine. Hawa walikuwa wafuasi wa dhehebu la dini ya Kiisamu  lililokuwa
na makao yake makuu katika  Iran ya leo. Kutoka huko Iran walimtuma kiongozi
wao aliyeitwa  Hassan Ibn Sabah, aende  katika Mashariki ya Kati yote. Huko
akafanye  mauaji ya kulipwa.

Wafuasi wa dhehebu hili walifahamika pia kwa  kuvuta bangi  kabla
hawajafanya tendo la kigaidi  kwa jina la Allah. Hapa tunaona neno
"Assassin" kwa Kiingereza na hata kwa Kifaransa,  lina maana ya "kuua."
"Assasination" kwa Kiingereza, na kwa lugha ya kiarabu linamaanisha "
Mla-bangi". Wa-assassin walikuwa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.  Vitendo
vyao vya kigaidi viliwalenga zaidi Wasuni waliochukua sehemu kubwa ya
Persia.

Kunako mwaka 1200  vitendo vya kigaidi vya Wa-assasasine  vilikoma
baada ya mjuukuu wa Djingis Khan kuangamiza ngome na makao  makuu ya
Wa-assassine.


Utawala wa hofu  1773-94

Kwa kawaida Mapinduzi ya Ufaransa uangaliwa kwa kutazama tarehe ile 
Wafaransa walipovuka mstari  wa Basti. Ni  tarehe 14 Julai 1789. Kuna historia
yenye kuelezea tukio lile la kuvamia na kuvuka mstari ule. Kiuchumi taifa la
Ufaransa lilikuwa katika wakati mgumu baada ya kushiriki vita kadhaa vyenye
gharama nyingi na pia hali ya ufalme wa nchi kutokulipa kodi ikiwemo kufanya
anasa ya kupindukia. Hali ya uchumi mbaya na mlipuko wa bei za bidhaa baada
ya vita vya gharama nyingi ndio iliyopelekea wananchi kuanzisha mapinduzi
yale.

Mfalme alikamatwa  na kufungwa gerezani baada ya jaribio lake la
kutoroka nchi kushindwa. Kati ya mwaka 1792 na Julai  1774 Ufaransa ilikuwa
chini ya  himaya ya Maximilien Robespierre. Ulikuwa ni utawala dhalimu na
uliosambaza hofu kuu kwa watu wake, " La Grande terreur" kwa lugha ya
Kifaransa. Lengo hasa la kusambaza hofu ile ilikuwa kuhakikisha madaraka ya
Serikali ile ya kimapinduzi  yanabaki chini ya walioshika himaya ya dola.

Kilikuwa ni kipindi ambacho watu walikuwa na hofu hata ya kunong'ona
kuishutumu serikali. Watoa habari walikuwepo kila kona na hata ndani ya
familia.  Inasadikiwa, kuwa Wafaransa takribani 40 000 walinyongwa  bila hata
kufikishwa mahakamani. Kosa kubwa wakati huo ambalo mtu alihukumiwa
kunyongwa ni  vitendo vyenye mwelekeo wa kupinga mapinduzi.


Magaidi  wa Kiyahudi

Mwanzoni mwa miaka ya 1900,  Mazayuni wa Kiyaudi walianzisha ujenzi wa
makazi ya Wayahaudi katika iliyokuwa Palestina ya zamani. Ni Palestina 
iliyokuwa chini ya himaya ya Ottoman. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza,  Palestina
ilikuwa chini ya udhamini wa Waingereza.

 Baada ya kampeni ya vikundi vya kishawishi vya Wayahudi , Serikali ya
Uingereza ilitangaza kuwepo kwa taifa la Kiyahudi. Lakini,   Serikali ya Uingereza ilionesha pia kutopendelea mradi ule wa ujenzi wa makazi ya Wayahudi.

Hali ile ilipelekea kuanzishwa kwa vikundi kadhaa vya kigaidi vya Wayahudi vilivyopambana na Waingereza. Wakati  wa Vita Kuu ya pili ya dunia , vingi ya vikundi hivi vilisimamisha harakati zao za kigaidi.

Baada ya Vita Kuu ya pili ya Dunia , vikundi hivyo vilianzisha tena
mashambulizi ya kigaidi kutetea kuwapo kwa taifa la Wayahudi . Moja ya
shambulizi la kigaidi la Wayahudi ni dhidi ya Hoteli ya Waingereza
iliyojulikana kama King David Hotel katika mji wa Jerusalem. Jengo la hoteli
liliangamizwa na watu 89 waliuawa.


Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia  wahamiaji wengi zaidi wa Kiyahudi
waliendelea kuingia katika  Palestina iliyokuwa katika udhamini wa
Waingereza. Lengo  la kisiasa la Wayahudi la kuanzishwa kwa taifa la Uyahudi
  lilipelekea kuanzishwa kwa vikundi zaidi vya kigaidi vyenye  mitazamo ya
kitaifa. Viwili kati ya vikundi hivyo ni Irgun na Stern. Vikundi  ambavyo vilitumia
mbinu za kigaidi katika kuendesha harakati zao. Miongoni mwa mbinu hizo ni
matumizi ya mabomu ya barua.

Tangu mwezi Septemba  1947 hadi kutangazwa kwa taifa la Israel ,
mwezi Mei 1948, vikundi vya Irgun na Stern vilijulikana sana kwa matumizi
yake ya mabomu ya barua.

Kabla na hata baada ya kutangazwa kwa taifa la Israel, vikundi vya Irgun na
Stern,  na baadae  taifa la Israel, vimekuwa vikiendesha mashambulizi ya
kijeshi dhidi ya Wapalestina. Vitendo hivi viangaliwe kama matendo ya
kigaidi dhidi ya watu wa Palestina , ambapo, lengo kuu ni kuwafukuza wale
wote wasio –Wayahudi.

 

 Katika kufankisha malengo haya,  Israel imeendesha mashambulizi mengi
ya kigaidi katika vijiji na maeneo ya Waarabu. Takribani watu laki saba
walikimbia  makazi yao katika vita vya awali kati ya Waarabu na Waisrael. 
Watu hawa hawakuruhusiwa kurudi makwao. Hii ndio sababu Wapalestina wengi
wanaishi kwenye makambi ya wakimbizi ndani ya ardhi yao na hata katika nchi
jirani kama vile Lebanon. Itaendelea...

 

Maggid.

0754 678 252

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment