Ombi lako Ezekiel la 'Punda haendi mpaka kwa viboko':
Ulichosema ndugu yangu cha kiboko ndicho alichosema Mh Mangufuli jana kuhusu barabara ya Kigamboni. kasema kesi ya wananchi mahakamani sasa ni 2 years haiendi na nyumba zao zipo katika mapito ya barabara right-of-way ya barabara iliyopo. Sasa mkandarasi aendelee na kazi na apitishe barabara mbele ya majengo yao. Anaombea kuwa siku moja hao waliopo katika pembe za barabara ktk right-of-way lori likosee njia au liwe na mapungufu liingie ndani ya nyumba halafu tuone itakuwaje maana hawataki kuondoka. RC wa DSM Nd Meck Sadick naye alisema-hao waliopewa viwanja Mabwepande ambao walijenga mabondeni kwa hiyari yao, maji nyakajaa mpaka juu ya paa na kupata madhara ambao wamegoma kuondoka-wasitegemee kama kukitokea mafuriko tena wataiona serikali ikienda na mitumbwi kuwaopoa.
Sijui na wale waliotandaza biashara barabarani huku katapila na lori zinapita zinatimua vumbi kila kona wao wamenyoosha miguu kuuza nguo, mbogamboga na vyakula vingine. Na yule ombaomba kilema aliyekaa mbembeni na katikati ya njia mbili kama gari ikikosea ikiwapanda itakuwaje. Kutwa nzia anasita kona hadi kona na mwingine unamuona ana athari ya pombe kalewa. angetumia muda huo ktk kambi ya vilema kushona mazuria-kama social welfare ingewezeshwa si angekuwa na afya nzuri kuliko kubwia unga wa vumbi la TB kutwa barabarani? Tufutue taasisi wa malezi ya wazee na vilema, ziwe za kutoa huduma nzuri kisha tuwazoe tuwafungie huko wawe wajasiriamali.
Ukimuona mtoto na mama na vitoto anazurura kando ya magari kuomba-kamata kafungie huko mtoto asome na mama, babu ombaomba wazalishe mali. Wanaume vifua miraba mine anatembeza vitu wamejaa barabara zote-zoa kwa lori peleka mashamba ya vijana ya kingorwira, Mufindi, Sumbawanga, mipakani wale gwaride la kijeshi, piga siasa ya kitaifa na kimataifa, fundisha ujuzi, weka viwanda huko wachakachue na kufunga bidhaa, uza nchi za nje na nchini bidhaa hizo. Ikitokea vita-peleka ktk mikakati ya kulinda amani. Weka kambi hizo mipakani maana iko wapi wanyarwanda wanatumia kukata mbao, kuchunga mifugo, kufanya ujambazi na kuwinda wanyama wetu wakati tuna vijana wanazurura mijini!! Viboko na maarifa ndio haya Mheshimiwa Kunyaranyara. Ikiwa viboko na mipango ndio hii-wataacha kunyaranyara mijini kuongeza idadi ya wazururaji, vibaka na wezi wa pikipiki,bajaji na wakabaji watu wavushaji wahamiaji haramu-wapenda maandamano ya vurugu ili wavunje na kuiba madukani na mali za watu.
From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups com" <wanabidii@googlegroups.com>; "khildegarda@yahoo co. uk" <khildegarda@yahoo.co.uk>
Sent: Friday, 5 July 2013, 9:31
Subject: Re: [wanabidii] Tujifunze uzalendo, uchapaji kazi wa Wamarekani
Hilda Hoja yangu kubwa ni kwamba, kwa kuwa tumeshindwa kubadilika wenyewe kwa hiyari yetu, pamoja na ushawishi wote unaotolewa na watu wengi kama wewe, viongozi, wahisani basi kuwe na nguvu ya kusukuma - I mean cohessive force, kiboko kwa jina lingine yaani tumekuwa kama punda, haendi ila kwa mjeledi. There after watu watajua kwa nini walilazimishwa kuwa hapo watakapokuwa wamefika. That is what I meant my dear. KEMS Sent from Yahoo! Mail on Android |
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] Tujifunze uzalendo, uchapaji kazi wa Wamarekani
Sent: Fri, Jul 5, 2013 6:16:34 AM
Usiniambie habari za Bunda nilikaa huko miaka miwili nikisimamia mradi donor funded Bunda, Musoma Rural, Serengeti. Ni kwamba, baada ya ujenzi wa boreholes zenye handpumps, shallow wells with pumps kwa kazi ngumu ya kupambana na rushwa na wizi wa vifaa na hela za mradi (maofisa wasio waaidilifu);kuhamasisha ushirikishaji, O&M kukajengwa visima na kuboresha vile vya jadi kwa kuvijenda kwa mawe. Mradi ukakamilika na kukabidhiwa. Baada ya kukabidhi tu mradi mwaka huo kikazuka kitu 'dhahabu' kuonekana kijiji cha Kamkenga huko Kata ya Kabasa. Walichimba dhahabu mpaka kufukua visima vya pampu. Wakabomoa handpump wells kukosha dhahabu zao na kuchafua maji kwa mercury. walichimba mpaka barabarani na kuharibu barabara. Mabanda ya pombe, mama ntilie yakazuka, zinaa na vituko vyake. Baada ya muda dhahabu ukayeyuka lakini uharibifu ulikuwa mkubwa. Wamebaki na umasikini, maji ya kuchangia na mifugo ktk vibwawa vyao, HIV/AIDS. Mabomba wamekongoa na kuweka nati ktk virungu au gari la kukukotwa kwa ng'ombe. Baadhi ya miradi mizuri inayoanzishwa kwa ajiri ya shule, out-of-school village youths unakuta inafanyakazi donor au NGO zimamizi ikiwepo. Ikikabidhiwa-haidumu. Daima kutegemea mikutano na posho. Ukiwaalika waje mafunzo wajigharimie ina utalipia training na chakula wakati wa mafunzo na kulipa wafundishaji-hawapendi hadi utaje neno allowance (posho). Pia, uangalie hao trainees na uwathibitishe kuwa wanawakilisha vikundi halisi ama sivyo-utakuta ni watoto wa viongozi wa kijiji, vitongoji, balozi, mzee wa mila kujichagulia watu wao na akichaguliwa mwinginewe-atoe mgao wa hela ya posho nusu akirudi. Mashamba ya shule yakilimwa-waibaji ni wazee na vijana kijijini. Ilinisikitisha sana kijiji kimoja mbali na Mara/Bunda ni cha Same Kusini Upareni (Mkonga Ijinyu) kulikuwa na dada umri wa kati ana ugonjwa wa UKOMA. Lakini akijitahidi kulima mihogo ili auze na kupata chakula chake. Huyu mkoma akilima lakini wasima baadhi wakifanya vyao na kumuonea walikuwa wakiiba mihogo yake (dada mwenye ukoma)daima hapo kijijini. uonevu wa kuonea kilema na kumporea hela alizoomba kutwa ni laana inayoendelea nchini, kuvamia vizee na kuvibaka na kubaka vilema wakike, kuonea yatima na kuoneana katima masuala mengi kifamilia na hata maofisini. Hata yanapoonekana yanakwenda hovyo majumbani, mtaani-tunaogopa kutajana maana utakayemwambia atatoa siri kaambiwa na nani naye ataadhibiwa-Kisasi. Hivyo, yetu mengi hayafanikiwi kutokana na undumakuwili, kisasi na kuoneana kutokuwa wakweli bali kulaumu tu wengine. Ujiangalie pia kama unasimamia au mmegharimia miradi, unapokagua kuonyeshwa miradi hiyo-fanya upelelezi kisiri amasivyo-utaonyeshwa kanyaboya. Mtu analipwa ili wageni wakija ile miradi ionyeshwe kuwa ndio ya hicho kikundi. Lakini kama ni mbuzi, nguruwe au kuku wa kienyeji-walishakufa kutokana na matunzo duni ya kushindana. Hela za kukopeshana-mzunguko haukwenda wengine walitoroka baada ya kukopa hawana cha kuonyesha. Wengine wanatoroka wanaacha mume au mke peke na familia kutokana kuwa hela ya kikundi aliyokopa au ya vikoba hakumueleza mwenzake na kaitumia kianasa. Ndio maana ktk miradi ya vikundi vinavyoendelea ni vichache na ugomvi wa uongozi mwingi. Kila mtu anataka kuongoza ili apate mafao bila kutoka jasho. Ndio inakuwa kama Misri wanategemea Rais ajae atateremsha kama mana jangwani awaachie wafanye watakavyo. Ndio sera za bongoland za vyama vyetu na watu wetu kudhania uhuru wa kila kitu kufanya utakavyo kama machinga barabarani ndio maendeleo. Maendeleo yatakuja kwa kulalamika sio nawe kuwa mfano ukatenda na kujitendea haki? Fikiria kijana kaondoka kwenye good land kilosa hawezi kulima bibi na babu ndio wanalima. kazi mjini hapati. shamba lao lipo km 5 toka nyumbani kwao na mengine around the house-hawezi kulima. Hapa Dar au district town yao kutwa anatembea kilometa 50 kutembeza (kariakoo-buguruni-ubungo-mwenge-kinondoni-kariakoo) na zigo la mavitu kabeba na akiuza kutwa moja shs elfu 10 na sio kila siku na kulala, kula tabu. Mateso ya nini? Anapunguza uchovu kwa kunywa kiroba maana siku hizi viroba vinauzwa kama vocha za simu. Lakini kijijini angetembea km 10 tu au pungufu na angeuza mazao gulioni akamtunza bibi na babu na akala ugali wa muhogo/mtama/mahindi kwa mboga za majani kwa afya yake. hatuna uwezo wa kulinganisha zuri na baya-lawama tu. Mbona mifano tunayo!! Tubadilike. From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com> Sent: Thursday, 4 July 2013, 10:51 Subject: Re: [wanabidii] Tujifunze uzalendo, uchapaji kazi wa Wamarekani Hilda Naungana na wewe na Manyerere kwa mtizamo chanya kuhusu hali yetu kama tunataka kuendelea. Kimsingi hoja kama hii inawezekana isiungwe sana mkono kwa kile ulichosema kuwa watu wanasubiri waletewe maendeleo. Mchango wangu katika hoja hii ni kwamba inaonekana ndani ya vichwa vya watu (hasa vijana) kwa sasa kumejaa utegemezi basi itokee basi siku moja mtu alazimishe.. yaani watu walazimishwe kufanya kazi. Nina mfano katika hili: Wakati Fulani nikiwa Wilaya ya Bunda alikuwepo DC mmoja ambaye aliwaita wananchi akakaa nao siku mbili wakakubaliana kujenga shule za Sekondari kila Kata kabla hata ya maelekezo ya Waziri Mkuu wa wakati huo. Walipangiana siku kwa kila hatua ya ujenzi, waliokaidi walikuwekwa rumande na faini zilipigwa zilizolenga kukamilisha ujenzi wa shule hizo DC huyu akisimamia maamuzi waliyokubaliana. Mfano mtu alipigwa faini mbele ya watu wote kuleta bati moja au mfuko wa simenti pale shule na alipokosa aliwekwa ndani na kasha kesho yake nduguze au watoto wakavileta vitu hivyo na kazi ikaendelea. Katika Wilaya hiyo ndani ya miezi mitatu shule kumi na saba za Sekondari zikafunguliwa na ilikuwa ni wilaya ya kwanza nchini kukamilisha ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata hata kabla ya maelekezo ya wakubwa huko juu serikalini, chini ya msukumo wa DC huyu. Waulize leo wananchio wa Bunda kuwa ni nani aliyewaletea maendeleo ya kweli watakawambia huyo DC (Simtaji jina tusije anza kujadili majina ya watu). Hoja yangu tunahitaji nguvu kidogo ili kutoka pale tulipo. Newton third Law of Motion inasema " If a body is at rest it will continue to rest unless there is a force acting on it...." Tunahitaji nguvu kidogo tu ili tusonge mbele. Vichwa vya watanzania kwa sasa vimejaa kutu, za kulalamika tu, Kila mtu anaota kupata fedha bila kufanya kazi, au anataka kazi kidogo fedha nyingi. Jaribu kupita vijiweni kwa wanaokufahamu utasikia "....sasa unatuachaachaje bro.. au sister..." Hii ni hatari. lakini kwa positive thinking kama hii nafikiri tunaweza sasa kuondoka hapa tulipo na kusonga mbele kama taifa. Asante kwa mtizamo mzuri kama huu Manyerere na Hilda. K.E.M.S. From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com> Sent: Thursday, 4 July 2013, 3:53 Subject: Re: [wanabidii] Tujifunze uzalendo, uchapaji kazi wa Wamarekani Ahsante sana Manyerere. Tunahitaji watu kama wewe. Umeandika na kutuasa kwa kirefu. Wengine urefu huu wenye maadili na maonyo ya maana hawaupendi. Wanaona kero kusoma. labda uongee jinsi CCM ilivyombaya na Chadema kuwa mkombozi-hapo ndio umefika. Lakini kujitezama kwa kioo cha matendo na mitazamo yetu kinyume na maendeleo yatakavyo-hapana. Wanataka mistari 2 tu. Kweli baadhi na tuliowengi tupo kuwaza kuletewa maendeleo si kujitafutia, vianguke kama mkate waliopewa waislaeli jangwani. Kukusanya kodi kuzila sio kuwakilisha serikalini au kutokutoa kodi kwa kutumia mbinu nyingi. Halafu bei ya petroli na mazao ikipanda ili GVT ipate hela-Kulalama. Tunahitaji kufanyakazi, kuzingatia sheria za kila sekta. Tanzania ni nchi kama USA ya watu wa kila race na makabila kutoka nchi za mbali North, South, East, West wakakutana hapa. Wapo waliokuja kutokana na climate change effects huko kwao wakaunda makabila makubwa na madogo hapa; wapo walikuja kutokana na vita huku kwao kutoka S. Africa, Chad, Congo etc. Wapo walioingia kutokana biashara ya utumwa na wapo waliokuja kupita na majahazi wakiwa ktk safari za maraha ila wakaona coastal area na visiwa vizuri wakanunua ardhi kwa chiefs au wakahamia kwa nguvu na kututumikisha. Ni kama USA tu hii bongoland-infact Obama kaja kwenye historia kama yao USA. Taifa letu likiwa na watu tofauti tumechanganyika kama USA-a country in a melting pot kuna matajiri na masikini kama kwao. Wapo wahindi, waarabu, washigiri, Goa, Bohora waliokuwa matajiri zamani, sasa masikini wa kutupa. wapo waswahili hivyo pia na wapo walioibikia. Utakuta USA mtu toka nchi za latin america yupo hata engish hajui, china town wachina wamejaa na sasa mchina anajaa nchi nyingi duniani anafanya kazi zote za kipuuzi. Lakini wapo matajiri USA na masikini pia. Tena masikini hasa (Mississipi, South Carolina vijijini huko wapo) hata choo hana labda ana bucket latrine mbovu.Hiyo nyumba kama mobile home ya mbaoakaayo ni hatari. Akitaka asaidiwe akae nyumba za GVT-awakilishe ardhi yake serikalini maana ina value. Hapa petu unayo maekari na bado unavamia protected areas na mashamba, machongo ya wengine na inashindikana kukutoa bila mipambano ya kuuana. Na masikini wazungu wapo wengi sana ila system yao ya Social Security -kima cha chini cha mshahara na kupewa food stamps asiye ajira inawasitiri (kuliko sisi hatuna). Bangi bangi, walevi, wavivu, pombe kutwa USA na nchi nyingine ulaya wapo. Ila, jeshi limesaidia kuchukua hao wa elimu ya chini, wasioajira. Nasi tuingize hawa vijana wasioajira JKT kufungua mashamba na viwanda vya ufundi huko wakazalishe na visafirishwe masoko ya nje. Hapa kwetu ardhi na mali ya umma. Wapi ulaya utapata ardhi yaani uhamie tu uanze kukata miti, kuchoma mkaa, kuhamahama na mifugo upendavyo na kulishia mashamba ya watu hutaki kubadilika mkulima au mfugaji au mvuvi kutumia sumu use dilution ndogo ktk kuvua au kutumia mabomu. Watu wanaona ardhi mali ya umma. Wakutoka ZNZ wanahamia huku na wana mashamba na biashara bara kwenye soko lakini bado wanataka muungano uvunjike. Mtu wa bara anahamia toka mkoa wake wa uzawa kwenda kwingine unamkuta msituni tu na kumtoa inakuta tatizo. UK, USA wanachoma mabada ya Gypsies au kuyabomoa. Hapa kumuondoa mharibifu msituni, aliyejenga pasipotakiwa ni balaa. Hatuoni mbali. Na sijui kama ndugu zetu ZNZ wanaelewa pia kuwa kama watajitenga kama watakavyo itabidi nao wahame waachie ardhi yetu au vipi. Tunajisahaulisha historia. Aliye ZNZ ana ndugu bara kama si nchi jirani -congo, burundi au kenya-mombas kama hawajafa na kama alifuatilia roots zake. Shinikizo la kujitoa, lawama za kuonewa wao tu sio sisi huku bara inaleta jazba kubwa bila mtazamo chanya wa utatuzi. yaani kuonewa pandew moja daima hatari. Zaidi kukazania lawama kuliko kujikanya na kujituma kwa mipango na mitazamo ya mafao zaidi kuliko ya kubomoa. Tunajisahau kama anayekupa dezo ukimkosea au kukataa kukabiliana na matakwa yake-anaweza kukufanyizia kama ulivyoonyesha hapa mifano ya Rais wa Iraq, Libya etc na Osama aliyekuwa wao, Savimbi, Mobutu-walipoona wamefaidika nao sasa 'yatosha' wakawafanyizia. tujitume. Wealthy people wa Tanzania wachukue nafasi hizi waanzishe viwanda na shughuli waajiri vijana. Jeshi liwabebe wakazalishe huko kwa kutumia hizo power tiller wauzazo na vifaa vingine. Vyuo mfano vya kilimo, Mifugo-wafunguo mashamba makubwa ya kilimo na ufugaji wa mifano processing industries ambako hawa vijana watakwenda kuho kuajiriwa na wanafunzi watajifunza kwa mifano ili tusitegemee kuokota chupa na kuuza madawa ya kulevya, kupata bangi kujipatia hela za haraka lakini kuharibu taifa. Iweje chuo cha Kilimo kinunue chakula dukani na magereza iwe hivyo na serikali kugharibia kukinunua kuwalisha wafungwa kwa kukinunua badala ya wafungwa kulima wenyewe na kujaza maghala? gereza lipo kwa Mfano Ruvu kwenye wetland na irrigation au kingolwira wasilime kujilisha? Chuo cha mifugo kinunue maziwa na nyama na kiko nje ya mji au mikoani? Tuangalie haya tujirekebishe. From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> Sent: Wednesday, 3 July 2013, 15:53 Subject: Re: [wanabidii] Tujifunze uzalendo, uchapaji kazi wa Wamarekani 2013/7/3 Adam Mwambapa <adammwambapa@ymail.com>
Find Jobs in Africa Jobs in Africa International Job Opportunities International Job Opportunities Jobs in Kenya Jobs in Uganda Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out. Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out. Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out. |
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment