Hallo selemani
katika kudhani unafanya jambo zuri tusitake mifano ya nani anafanya kuwa ndio uthibitisho wa ubora wa jambo ,kwani hata mfumo wa serikali mbili tulizonazo hakuna mfano wake popote duniani,sisi watanzania ndio wakwanza na tunang'ang'ania kuwa ni mzuri
pili suala la kuwa na zamu katika uongozi kwa mazingira yetu ni sahihi kabisa hatuwezi kuweka mazingira ya ushindani kwa Tanganyika na Zanzibar kama tulivyoona kuwa haiwezekani kuwa na ushindani kwa mwanamke na mwanamme katika nafasi za uchaguzi kwani mazingira yetu na mifumo yetu ingehakikisha mwanmme anashinda kila wakati,hivyo ni bora kukawa na zamu ya uraisi wa muungano ilikutoa nafasi kwa pande zote za muungano kuongoza serikali ya muungano kuliko kushindanisha mtanganyika na mzanzibar kwa uwiano gani wa kura milioni 40 na milioni 1.
lakini tatu na muhimu kabla ya kuendelea au kuvunja muungano ni lazima tuwe na kura ya maoni kuona je tunauhitaji muungano au la ili kuona sababu zilizo wafanya waasisi wetu kuwa na muungano bado zinaishi na tunazihitaji
--------------------------------------------
On Thu, 25/7/13, Selemani Rehani <srehani@hotmail.com> wrote:
Subject: RE: [wanabidii] KUTOKUBALIKA KWA MUUNGANO WENYE SERIKALI MBILI NA TATU
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 25 July, 2013, 12:29
Asante Fakhi kwa maelezo yako mazuri.
Nataka tu ku-engage na wewe katika majadiliano haya ili
niweze kukuelewa vizuri zaidi.
Kwanza, utaratibu wa kupokezana. Nadhani
umejenga hoja zako kuhusu utaratibu huu, lakini mwishoni
wewe mwenyewe unajichanganya na kujikanganya na kujipinga
mwenyewe. Umeeleza kwa kirefu uzuri wa kupokezana mwishoni
unasema "utaratibu huo kwa kutumia mfumo wa serikali
mbili zilizopo au shirikisho la serikali tatu
zilizopendekezwa na Tume ya Warioba hautekelezeki kwa
kuzingatia utaratibu wa kiuchaguzi na misingi ya
demokrasia."
Baada ya kuwa
umejipinga mwenyewe sidhani kama kuna haja ya kujadili wazo
hili la kupokezana tena. Ila nadhani utakubalina na mimi
kuwa mwenye sifa ndio anafaa kuwa Rais, haijalishi anatoka
Bara au visiwani. Kama wapo wenye sifa Zanzibar, mimi sina
tatizo, hata wakiwa Marais mfululizo kwa miaka chungu nzima,
kwangu hilo ni sawa, almuradi wana sifa na wanaipeleka nchi
kule tunakotaka. Kwangu mimi, kiongozi ni yule atakayekuwa
na mikakati ya kuboresha huduma za jamii, ziwe nzuri. Elimu
bora, afya bora, makazi bora, maji safi na salama, miundo
mbinu n.k. Kwangu hivi ndio vya msingi na wala si eti
anatoka Zanzibar au Bara, kwangu mimi hii si hoja ya msingi.
Kama hawezi kutupa huduma za jamii na kuondoa umaskini na
rushwa, hata niwe nimezaliwa naye hafai au hata tuwe
mapacha, hafai.
Kama wewe
unaamini Wazanzibari wana sifa basi let them put their names
forward kupitia vyama vyao na kama vyama vitaona
wanachagulika na wana sifa basi vitawasimamisha. Kama una
amini wana sifa kwa nini unataka iwe zamu zamu?! kwa
nini usiache ushindani kuchukua mkondo wake? Kwa mfano, CCM
wakiamua kumsimamisha Juma Shamhuna, au Raza sawa
tu kama wanaona anachagulika. Ndugu yangu cha msingi ni sifa
za kuchagulika tu.
Utaratibu wa Rais za Zanzibar kuwa
Makamu wa Rais: Sababu ninayoijua mimi iliyopelekea
kubadili utaratibu huu ni tahadhari ya msingi kabisa, kuwa
kulikuwa na uwezekano kabisa wa chama A kushinda Zanzibar na
chama B kushinda Bara. Sasa kama ingetokea hivyo, maana yake
ni kuwa Rais wa Zanzibar mathalani akatoka CUF na Rais wa
Tanzania akatoka CCM, sasa iwepo anakuwa moja kwa moja ni
Makamu wa Rais, wataweza vipi kuendesha serikali wakati
wanatoka vyama tofauti wakiwa na sera tofauti? kumbuka kuwa
dhana za coalition government kwa nchi nyingi za Afrika bado
ni ngeni na changa sana. Kwa hiyo mabadiliko hayo
hayamkumlenga Seif bali hali halisi ambayo ipo wazi CUF na
CCM wamekuwa wakipisha kidogo sana katika kura za uchaguzi
Zanzibar. Hivyo upo uwezekano wa CUF kushinda uchaguzi
visiwani na wengine wanaamini kuwa ni CUF ndio wamekuwa
wakishinda ila wanaporwa ushindi.
Lakini pia
haikuwa sahihi kwa Rais wa Zaznbar automatically kuwa Makamu
wa Rais, kwani hakuwa amechaguliwa na wananchi huku Bara. Na
kumbuka kuwa iwapo Rais angefariki basi yeye angekuwa Rais.
Hivyo kulikuwa na hatari ya kuwa na Rais ambaye
hatukumchagua sisi wa Bara ilia alichaguliwa na wananchi wa
visiwani. Utaratibu huo haukuwa mzuri kwa sababu
hizo.
Binafsi yangu
wakati wa utawala wa Mwinyi, sijawahi kusikia
malalamiko ya eti Zanzibar wametoa Rais na makamu wa Rais.
Inawezekana unachosema ni kweli lakini pia you need to bear
in mind kuwa tupo katika mfumo wa vyama vingi na kila chama
ni lazima kisimamishe mgombea ambaye ana sifa , ataleta
ushindi na anachagulika, kigezo cha mahali anapotoka si cha
msingi sana. Yale yaliowezekana wakati wa mfumo wa chama
kimoja yanaweza yasiwezekane katika mfumo wa vyama
vingi.
Muungano wa mkataba: Pia
umelizungumzia hili. Umesema iwepo tume au kamisheni ya
muungano. Hebu fafanua zaidi na tupe mifano ya nchi nyingine
ambazo zina muundo huu. Tueleze unafanya kazi vipi?
unaundwaje? na masuala ya muungano yanakuwaje katika
mazingira ambayo kila nchi ina mamlaka yake? Je muungano
unakuwa katika mambo gani? na unaendeshwaje? una mifano
katika nchi nyingine? huoni kama hilo litavunja muungano? au
nia ni kuvunja muungano ila mnazunguka kwa mlango wa nyuma?
itakuwa vizuri u/mkiwa wazi na kusema je muungano mnautaka?
au hamuutaki?
Asante
Selemani
Date: Thu, 25 Jul 2013 13:26:20 +0300
Subject: [wanabidii] KUTOKUBALIKA KWA MUUNGANO WENYE
SERIKALI MBILI NA TATU
From: fkarume@gmail.com
To: wanaBidii@googlegroups.com
KUTOKUBALIKA
KWA MUUNGANO WENYE MIUNDO WA SERIKALI MBILI NA
TATU
Kwanza
ifahamike kwamba zilizoungana ni nchi mbili tofauti,
Tanganyika na Zanzibar na hivyo kabla ya muungano zilikuwa
na heshma na hadhi sawa kama mataifa huru na bila shaka
ndani ya muungnao inapaswa kuwa hivyo.
Kwa mtazamo
huo basi ndani ya muungano wa serikali 2 na hata shirikisho
la serikali tatu zilizopendekezwa katika rasimu utaratibu wa
upatikanaji wa Rais wa muungano hauna budi kuwa ni kwa
msingi wa kupokezana zamu ili kujenga sura ya usama na
heshima kwa nchi mbili zilizoungana katika suala la uongozi
wa juu wa nchi.
Wapo baadhi
ya viongozi kutoka Bara wanabeza utaratibu wa urais kwa
kupokezana zamu kwa kuweka hoja kwamba eti tusilazimishe
utaratibu huo kwani itapelekea kupata Rais asie makini na
mwenye sifa kutoka uopande wenye zamu kwa kumzuia mwenye
sifa kutoka upande wa pili usio na zamu. Hoja hii si ya
msingi na pia ni hoja ya uongo.
1. Ni hoja
ya isiyo ya msingi kwa sababu hakuna taifa kati ya mataifa
haya mawili ya Tanganyika na Zanzibar yenye historia ndefu
kutokea uhuru. Hakuna nchi hata moja kati ya mbili hizi
yenye ukosefu wa wasomi na wanasiasa wenye uzoefu na maarifa
ya kutosha kuwa viongozi wakuu wa nchi wenye sifa. Mimi
nadhani watoaji wa hoja hiyo wanakusudia kwamba inaweza
ikafika zamu ya Zanzibar lakini Zanzibar huko kusiwe na
Mgombea wa Urais mwenye sifa lakini upande wa Tanganyika
ambao haupo katika zamu yupo mwenye sifa ila amekwazwa na
kigezo cha zamu. Hii ni kwa kuwa siku zote watanganyika
wasioipenda muungano wa haki na usawa wamekuwa
wakiwazingatia wazanzibari kama ni watu wasijuwa kitu au
wasaidizi tu katika utaratibu wa uongozi katika masuala ya
Muungano pamoja na serikali yenyewe ya muungano.
2. Pia nii
hoya ya kujifichia kwani utaratibu wa mwanzo wa muungano
uliosema makamo wa Rais atakuwa Rais wa Zanzibar unafichua
unafiki wa hoja hii. Ilipofika kipindi cha awamu ya pili,
Rais wa Muungano alipokuwa Mzee Ali Hassan (anaedaiwa kuwa
ni mzanzibari), Rais wa Zanzibar Mzee Idris Abdulwakil
alikuwa Makamo wa Rais wa muungao pia mzanzibari. Msingi wa
malalamiko ya upande wa bara hapa ilikuwa eti Zanzibar
imetoa Rais wa muungano pamoja na Makamo wake. Hilo
liliendelea kuwa halipendwi upande wa Bara mpaka pale katiba
ilipobadilishwa mwaka 1994 ili isije ikatokea tena kama
kipindi cha Mwinyi Zanzibar kutoa Rais na Makamo wake na
badala yake kuwekwa mgombea mwenza ndio awe Makamo wa
Rais.
Ili kuwaziba
macho wana CCM wa Zanzibar walikubali hilo upande wa bara
ulitumia kisingizio kwamba ni kumzuia Maalim Seif asiwe
Makamo wa Rais wa Muungano pale atakaposhinda Urais wa
Zanzibar kwani utalifanya baraza la mawaziri kuwa na
mpinzani na hata Rais wa Muungano kuwa mpinzani pale Rais
atakapopata dharura ya kuondoka katika kiti chake. Upande wa
bara walipata kichaka hicho na wauza nchi wa Zanzibar
wakaridhia kubadilishwa kwa utaratibu wa Rais wa Zanzibar
kuwa Makamo wa Rais. Hoja hapa ni kwamba hata watanganyika
wenyewe hawapendi kuona Zanzibar inatoa viongozi wengi kwa
wakati mmoja au kwa mfululizo wa vipindi, hivi inakuaje leo
walete hoja ya kutokuwepo ulazima wa kubadilishana Urais kwa
kuchelea Rais asiye na sifa?
Tukirejea
katika mchakato wa maoni hata CCM wauza nchi waliopo
Zanzibar wanasisitiza Urais wa muungano uwe ni kwa utaratibu
wa zamu baina ya Tanganyika na Zanzibar, hivi ndivyo maoni
yao yalivyokuwa na kwa hili tunawaunga mkono, wako juu ya
mstari.
Sasa tuje
katika msingi wa hoja hii, pamoja na kwamba upo ulazima wa
kubadilishana Urais wa muungano baina ya Tanganyika na
Zanzibar, suala hilo linajidhihirisha kuwa ni gumu na
lisilowezekana kwa kutumia mfumo wa muungano wa kijamhuri
uwe wa serikali 2 zilizopo au shirikisho la serikali 3
zilizopendekezwa na Jaji Warioba.
Kwa
utaratibu wa chaguzi, ili kumpata Rais ambae atatoka upande
mmoja wenye zamu ni lazima upande wa pili usiweke mgombea,
na hili liwe ni kwa vyama vyote. Hii ni kwa sababu mgombea
akisimama kutoka pande zote mbili uwezekano sawa wa kila
mgombea kutoka pande mbili za muungano kuwa Rais upo . Kwa
mujibu wa tofauti za kimitazamo za vyama vingi vya siasa za
Tanzania vlivyopo si jambo la rahisi baadhi ya vyama
kukubali utaratibu chama chao Fulani kisisimamishe mgombea
wa Urais.
Hata hivyo
tuseme hilo la upande mmoja kutoweka mgombea limekubaliwa na
vyma vyote, basi sasa kutakuwa na kikwazo cha uhalai wa Rais
huyo kwani upande ambao hauna zamu utalazimika kutokumpigia
kura mgombea, kwa msingi kwamba zamu ya Urais ni kutoka
upande mmoja na hivyo anapaswa kupata ridhaa ya nupande huo
wenye zamu tu, upande wa pili haupaswi kuwa na ridhaa ya
mgombea huyo ili kutoingilia matashi ya upande wenye zamu
juu ya ni nani wanamtaka awe Rais wao. Hakadhalika Suala la
upande usio na zamu kulazimika kutokupiga kura ya kumchagua
Rais ambae ndie Mkuu wa nchi yao kunaondosha uhalali wa Rais
huyo kwani bila shaka atakuwa hana ridhaa ya wananchi kutoka
katika nchi ya pili inayounda muungano.
Hivyo basi
utaratibu wa kupokezana Urais pamoja na ukweli kwamba
hauepukiki baina ya pande mbili za muungano, utaratibu huo
kwa kutumia mfumo wa serikali mbili zilizopo au shirikisho
la serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Warioba
hautekelezeki kwa kuzingatia utaratibu wa kiuchaguzi na
misingi ya demokrasia.
Hivy basi
mfumo pekee ni kutokua na serikali ya Muungano badala yake
kuwe na chombo tu kinachounganisha nchi mbili kwa mfano tume
ya Muungano au kamisheni ya muungano. Huu ndo muungano wa
MKATABA. Nchi mbili zinabaki zikiwa na mamlaka yake na
marais wake bila ya kuingiliana na mwenzake huku masuala
machache ya muungano yakitaribiwa na chombo hicho.
"MBILI",
"TATU" NO!, MUUNGANO WA "MKATABA"
HAUEPUKIKI
JAMHURI YA
WATU WA ZANZIBAR KWANZA!!
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment