Wednesday 26 June 2013

[wanabidii] Historia Ya Kombe La Dunia ( IV); Italia 1934, Mcheza Kwao Hutuzwa....


Na Maggid Mjengwa,

Jana tulianza kwa kuzingalia fainali za pili za Kombe la Dunia
zilizofanyika nchini Italia maka 1934. Tulisema,  kama fainali za kwanza za
mwaka 1930 kule Uruguay zilionekana ni za majaribio, basi, fainali za pili
za  Kombe la Dunia  zilikuwa ni fainali za "kweli kweli".

Naam, enyi wapenzi wa soka, tutakumbushana , kuwa nchi ya Misri
ilikuwa ni taifa la kwanza barani Afrika kututoa mchanga wa macho kwa
kushiriki fainali hizi za Italia.

Katika fainali hizo, ingawa Misri  ilitolewa raundi ya kwanza ya mechi za mtoano,  ilifanikiwa kupachika  nyavuni magoli mawili ya kihistoria yaliyofungua mlango kwa bara hili kwenye kandanda ya dunia. Ilikuwa ni katika mechi kati ya Misri na Hungary ambapo  Misri ilibugizwa magoli 4-2 mjini Naples.

Magoli hayo mawili ya Misri yalifungwa na mshambuliaji aliyeitwa  Fawzi. Misri hawakuwa peke yao katika kutolewa kwenye raundi hiyo ya kwanza.  Walisindikizwa na nchi kama Brazil na Argentina, nchi zilizokuwa na majina makubwa katika kandanda hata wakati huo.
 

Ajabu katika fainali hizo za Italia ni kwa bingwa mtetezi, Uruguay
kususia kushiriki na kutetea taji lake..... Soma zaidi...http://www.mjengwablog.com/michezo/item/3534-hstoria-ya-kombe-la-dunia-iv-italia-1934-mcheza-kwao-hutuzwa.html#.UcsdNpyNCAg

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment