Wednesday 26 June 2013

[wanabidii] Msimamo Mkali Wa Vijana Wa Mlimani ( III)- Julius Nyerere Alikoshwa Na Michango Ya Wasomi Wa Enzi Hizo...



Na Born Again Pagan



Makala haya kwanza yaliandikwa kwenye "Kijiji" chetu (mjengwablog.com) mwezi Mei, 2007, chini ya kichwa cha habari, "BAP Anavyomwelezea Yoweri Museveni". Madhumuni yake yalikidhi ombi la "Mwenyekiti wa Kijiji" kunitaka nitoe maelezo kidogo juu ya wanafunzi wenzangu Darasa la 1970 hapo Mlimani: Yoweri Kaguta Museveni na Hirji.

Nilianza kwa kutoa hoja kwamba haiwezekani kabisa kuweza kusimulia ya Yoweri Kaguta Museveni na Hirji bila kutoa, pengine, "background" ya miaka kumi ya kuanzia 1960 na jinsi matukio hayo yalivyojenga mikitadha iliyozalisha wanafunzi wenye msimamo mkali, kama akina Yoweri Kaguta Museveni na Hirji.... Endelea....

 

Katika makala yaliyopita, tuliona matukio kumi na moja yaliyochangia kikamilifu katika kujenga mkitadha wa msimamo mkali wa baadhi ya vijana waliokuwa wakisoma hapo Mlimani (1960 hadi 1970). Hii haina maana ya kwamba hao ndio walikuwa vijana tu wa msimamo mkali waliopata kuelemishwa hapo Mlimani. La, hasha!

Na wala haina maana ya kutamati kuwa matukio hayo yalitokea kuwafanya wawe na msimamo kama huo. Ilikuwa ni dhamira au busara (prudence) ya vijana hao wachache kuyaona matukio hayo yakitoa changamoto; wakapata fursa (opportune) kuyatafsiri ili yawe na maana maishani.

Makala haya yanaendelea kuelezea matukio mengineyo sawa na yaliyopita, kama ifuatavyo:

Kumi na nne, Tanzania Bara: Kushindwa kwa siasa na sera za ki-Bepari, chini ya Mpango wa Taifa ya Maendeleo wa Miaka Mitatu-Mitatu (ulioishia mwaka 1965). Mipango hii ilizalisha matabaka ya akina "ma-naiza" na "ma-kabwela" (mithili ya hali ilivyo sasa nchini kwetu) Ikumbukwe kwamba mfumo wa mipango hiyo ulitungwa na Mashirika ya Kimataifa ya Fedha (Benki Kuu ya Dunia na Mfuko wa Fedha).

Kujengeka kwa matabaka hayo ya "ma-naiza" na "ma-kabwela" kulichangia sana kuelekea kwenye wimbi la Ujamaa wa ki-Afrika. Wimbi hili lilitingisha sana, eti, maslahi ya wakubwa wengine kwa kuogopa kile Waziri Mkuu wa u-China Chou-en-Lai alichokiita "Afrika imeiva tayari kwa mapinduzi" (Africa is ripe for a revolution) – kufuatia safari yake katika nchi kadhaa za ki-Afrika, ikiwemo Tanzania.

Kumi na tano, kupinduliwa kwa Rais wa Ghana Kwame Nkrumah, ikiwa ni pamoja na nchi nyingi za.... Soma zaidi...http://www.mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/3535-msimamo-mkali-wa-vijana-wa-mlimani-iii-julius-nyerere-alikoshwa-na-michango-ya-wasomi-wa-enzi-hizo.html#.Ucsxa5yNCAg

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment