Nimekupata Rashid Maalim lakini- Ila ninasema, tunayo mifano mizuri nchini-Tuige wachaga wanajituma!! Hawa, hawachagui kazi na wana ushindani. Usiniambie mzalisha kahawa (mchaga) anasomesha ila Mkusuma wa Mwanza mwenye ng'ombe 100, mbuzi 500, kondoo 50 na kuku kibao, samaki anavua kisha hasomeshi anaoza tu ili aongeze mifugo kuwa anaonewa. Vivyo hivyo kwa wafugaji wengine ambao wingi wa mifugo yao inatutesa wilaya mbali mbali wanasafiri huko na huko kulisha mashamba, watoto hawasomi kuwa-wanaonewa!! Msukuma amevuna dhahau toka ukoloni akija nazo DSM kabla ya Uhuru akijaza ktk Chupa kama vile anapeleka uji kwa mgonjwa muhimbili. Wahindi, Waarabu, Baniani, Goa, Bohora, Baluchi wametajirika kwa dhahabu crude ya kutoka Mkoa wa mwanza wakiwa na viwanda vya usonara mijini gold nzito ya ulaya imesingiziwa. Walioweka maduka ya dhahabu na waliokuwa na utajiri mkubwa wengi wameweza kuwa na maduka makubwa, viwanda kutokana na madini haya halafu vipusa pamoja na memo ya tembo. Operation Uhai ilirudisha nyuma matatiri wengi hasa Waarabu wa Tanga, Kilosa, Dar na Morogoro kwani vipusa viliwatajirisha sana malori ya mizigo na biashara zao zililala. Niambie msukuma kajenga viwanda vipi kwa dhahabu na almasi aliokuwa akiuza kwa mlango wa nyuma? Huyo kaongeza ng'ombe, wake na watoto. Goa, Mwarabu, Mhindi au Wajamii ya Asia wamepeleka kwao vito kupitia nduguzao huko wanauza dhahabu nzito makwao na wana maduka makubwa. Enzi hizo airport husachiwi sana mama wa kihindi anazivaa ndani na nje anapeta. Mmasai anashindwa nini kuendelea? Akichangia mbuzi mmoja tu ni mchango mkubwa wa kujenga madarasa lakini mkulima atauza mahindi magapi apate 50,000/= lakini unalimbikiza mifugo utajiri halafu watoto wanasoma chini ya mti? Donors wamejitolea sana kwao na unakuta wamehama na shule ipo tupu. Kusomea chini ya miti inakuwaje wakati mifugo kibao, udongo hauuzwi na mbao za miti unapata kibali halmashauri? Unamlaumu nani kama huna kipaumbele ktk elimu? Tembelea mazingira ya Pwani-coastal areas uone walivyobweteka. Kama elimu ilibagua wakati wa ukoloni-sasa ukoloni bado upo? Kama husomeshi na mtoto hapendi kusoma na humshauri au kumlazimisha-utabaki hivyo hivyo kulalama. Utawaona wa jirani yako wanapeta. Havidondoki kama mvua. Makabila yaliyopendelewa na Nyerere kwa vile ni madogo au traditionalists kubadilika wasome-akachukua watoto wao kupeleka kusoma ulaya-wamebaki huko huko hawakurudi. Waliorudi wamerudi na wake wazungu ambao bongo wameona tabu wamerudi nao tena ulaya. Sawa na kusomesha mtoto UDSM akaamua harudi kijijini akakuacha solemba unakufa pekee ktk poverty. Akija home-anauza mashamba na mali nyingine anarudi dar. Ona wivu hata ukiwa nyuma ili uige wale wa maendeleo nawe uendelee. Unajionea mwenyewe wa kutokuwa na malengo, mipango na juhudi halafu unakaa kutwa-tulionewa, bado tunaonewa, nchi mbaya etc kisha jani mpaka mlangoni hata kupalilia huoni ni cha maana. Mvua inanyesha tope limejaa, nyasi na makuti yapo-tunaonewa!! Ukuta upo wazi mtu anaweza kukuchungulia. Choo uwa upo wazi, kubanda cha choo kifupi ila nje miti mirefu kibao huezeki wala kukandika nyumba-Tunaonewa!! Unakula embe unatupa kokwa wala huipandi ila mwanzako akiipanda wewe kuvuna kwa mwenzako unakuwa wa kwanza-Tunaonewa. Hata kupanda mwembe na mpapai nje ya nyumba? Tuwaige hao wachaga na pia wapemba kibiashara na wakinga wamekuja juu kujituma. Waha nao na Wakurya wanakuja juu sana sasa. Elimu ndio ufunguo wa maisha. Tukiwa Ulaya masomoni kwa scholarship tukiwaona wenzetu wa huko wakiteseka kusaka hela wajilipie shule.Pilikapilika nyingi ktk kupata hela na scholarship wao kiduchu kulipiwa na mashirika. Anakuja shule lakini anaanza kazi kuanzia asubuhi, au akitoka shule na usiku. Kufagia barabara, kuosha vyombo hotelini, dreva wa taxi au bus, maktaba au mpishi cafeteria fulani, muuza beer bar. Sisi hapa university students wetu hawawezi haya. kuosha vyombo tu nyumbani tatizo. Kuchangia arusi si tatizo elimu tabu. Kulipa kiingilio cha mpira poa milioni 500 zinapatikana siku moja mpirani. Kuchangia hivyo secondari kwa mwaka kiwilaya zipatikane ili mabweni yajengwe-impossible. Ukitaka bure utapata-lakini Kodi lazima iwe kubwa-ipae juu hakuna kuepuka kama ilivyo ulaya. Kodi yao kwa kila kiuzwacho na bado hakuna free services. Jee tutaweza na sisi ni watu wa mission town? Maana hata hiyo Ulinzi shirikishi kuletwa kusaidia usalama wa jamii imekuwa balaa-rushwa tupu hao vijana. Kukwepa kodi ndio sala yetu. Dhuluma kibao mpaka ndani ya familia na mtu anaweka wakili anashinda kesi huku kadhulumu!! Ndio maana hatutoki hapa tulipo ktk umasikini. Bongoland kulalamika na shutuma ndio donda ndugu. Bure dunia nzima kwa sasa hakuna. Ajira directly ukimaliza shule hakuna. Soma, jenga uwezo, jiajiri uwe mkristu, mwislamu, Budha, Bohora, Ismailia whatever!! Ukitaka bure-uwe mtumwa wa anayekupa. Kuchangia maendeleo ndio sera ya sasa kidunia maana hakuna cha bure toka dunia ya nje. Kingine ni kufaidika na raslimali zilizopo hivyo budi tusitunze ili uwekezaji utufaidishe. Ukijenga-usibomoe eti umekasirishwa. Na ukisha kubomoa unapata nini hasira zikisha kuisha. Sheik Ponda (Mwanaume mzuri mwenye macho na lips nzuri-anapendeza) anasema NURU itakaribia!! lakini utaipata NURU tu ikiwa kama utahangaikia kujiendeleza sio kwa kukaa kitako ukisubiri kishuke. Cheap politics au mafunzo duni ndio unampa mtu kumwambia hivi, unampa mtu tamaa ya fisi kumbe-utoke jasho, uihangaike, ukihangaikie ukipate, ukitumie sustainably. Ninafunga sala. hii. Bye. --- On Tue, 4/6/13, Rashid Maalim <rashid.o.maalim@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment