Sunday 28 April 2013

Re: [wanabidii] Taarifa ya Godbless Lema kwa vyombo vya habari Kuhusu Chuo cha Uhasibu Arushao

Nimewahi kukutana na wakuu wengi wa mikoa enzi za utawala wa Mkapa na hawa wa sasa. Kuna tofauti kubwa sana ya utendaji wao.

Wakuu wengi wa mikoa na wilaya wa sasa ni wa namna ya Mulongo. Ukiwatazama na ukiwasikiliza unashindwa kuelewa wamepata nafasi kwa kuangalia vigezo gani. Hali hiyo ipo pia kwa baadhi ya Mawaziri.

Tunamwomba Rais awatendee haki Watanzania. Watanzania wana haki na wanastahili kuongozwa na Watanzania wenye uwezo wa kuongoza, wenye akili, upeo na hekima.

Viongozi kama akina Mulongo watakuja kusababisha maafa. CCM inaweza kuheshimika, kuaminiwa na kuungwa mkono kwa kuwa na watendaji wazuri wa serikali siyo kwa kuwa na viongozi wanaotumia nguvu bila hekima wala busara. Viongozi wa namna hii ndiyo wanaoifanya CCM, serikali na viongozi wachukiwe na wananchi. Ikumbukwe hakuna binadamu anayependa kuonewa au kudhulumiwa.

Hatuna uhakika, lakini kwa tukio hili tu, kuna wengi watatoka na hisia hasi dhidi ya CCM, serikali na Rais pia maana ndiye anayewateua, wengi wakiamini kuwa yanayofanywa na hawa wasaidizi wake ni maeekezo yake.

Rais inabidi awe anafanya utafiti wa hali ya juu kwenye uteuzi wa viongozi, na hasa hawa UVCCM. Uzoefu unaonesha uteuzi wa Rais wa viongozi vijana haujaweza kulisaidia Taifa. Katika orodha ya Mawaziri watendaji wazuri, hakuna waziri kijana. Na wengine mpaka wameondolewa bila kutoa mchango wowote wa kuonekana. Wapo pia Wakuu wa Wilaya na mikoa vijana ambao utendaji wao wa kazi ni wa dosari kubwa. Wengine ni kama hakuna wanachojua zaidi ya majigambo, majivuno, lugha za kejeli na matusi.

Hivi nchi hii kwa sasa, tuna kiongozi yeyote kijana katika serikali, iwe ni waziri, mkuu wa mkoa au wilaya, ambaye tunaweza kusema umeonesha uwezo unaostahili na tunaoutegemea. Tunawlalamikia sana wazee kwa kuendesha nchi vibaya lakini kwa vijana ndiyo kuna giza totoro, baadhi ndiyo hawa akina Mulongo.

Wako wapi akina Kaisi, Balele, Kiwelu, n.k. Wa sasa?

Wakuu wa Mikoa na Wilaya wengi kwa sasa wameacha kazi yao ya msingi ya kusimamia sheria katika maeneo yao na kufanya kazi za propaganda za kisiasa/kichama. Wakuu hawa tangu walipoacha kazi zao za msingi na kujitwika jukumu la propaganda za siasa za CCM kwa kutumia vyombo vya dola katika maeneo yao, wamekosa credibility ya kuwa viongozi wa watu wote, wanaonekana kuwa ni viongozi waliopo kwaajili ya maslahi ya wanaCCM. Falsafa hii mpya ya kuwafanya viongozi wa serikali kusimamia maslahi ya chama badala ya umma, yanaondoa uungwaji mkono wa wananchi wote hata katika shughuli zenye manufaa kwa watu wote.

Bart
Sent from Yahoo! Mail on Android



From: Ephata Nanyaro <nanyaro04@gmail.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] Taarifa ya Godbless Lema kwa vyombo vya habari Kuhusu Chuo cha Uhasibu Arusha
Sent: Sun, Apr 28, 2013 9:24:22 AM

Wanabidii
Hii sms imetoka kwa Mkuu wa mkoa,hilo halina shaka wala ubishi,binafsi
namfahamu vizuri huyu RC ni mtu mwenye Jazba,majigambo,majivuno,na
kiburi cha hali ya juu.Tangu amekuja Arusha amekuwa na vituko kila
uchwao,hata hivyo aliwahi kunitamkia zaidi ya mara tatu kuwa yey ana
jukumu moja tu,kushughulikia CHADEMA
Sakata hili lilikuwa dogo sana kwa RC kuwapa pole wanachuo,na
kutekeleza mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa serikali ya mtaa
husika,wala sio mkoa,kwa kuwa nia yake ni OVU na dhamira yake ni mbaya
ameamua kuacha kufikiri na kutumia msiba kama namna yake ya
kuishughulikia CHADEMA,tayari kuna watu wanaandaliwa ili kutoa
ushahidi wa uongo dhidi ya Mh Lema na CHADEMA kwa ujumla,pia walidhni
tungereact ili wakamate viongozi mbalimbali wa CHADEMA wa mkoa nNa
kuwaweka ndani ili kuadhiri  uchaguzi wa kata nne utakaofanyika June
16

On 4/28/13, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
> Anachoshangaa Ngetti ni kipi? Tunaujua uwezo wa viongozi wetu, waliowengi
> wamekuwa ni manyapala wa kutoa amri na kuonyesha wana nguvu kiasi gani bila
> ya kuwa hata na dalili moja ya uwezo wa kiuongozi (influencing leadership).
> Kama huyo Mulongo alifika na akashindwa kutuliza ghasia kwa kutumia busara
> nani angeendelea kuhoji uwezo wake kiuongozi? Historia ya uongozi wa huyo
> mtu imeelezwa na wenyekumbukumbu kuhusu yeye, je ni wapi amesingiziwa?
>
> Niliona kipande kidogo katika TV kuhusu sakata hilo, nilichokiona na
> kusikia huyo Mkuu wa Mkoa akisema hakina tofauti yoyote kimantiki na
> alichoeleza Lema. Nafikiri tatizo la msingi hapa ni kifo cha mwanafunzi
> ikifuatiwa na vurugu za wanafunzi. Hivi kumkamata Lema kumehusishwaje na
> kifo cha mwanafunzi?
>
> Kuna utafititi wowote uliofanywa na intelijensia yetu tukufu isiyoegemea
> upande wowote wa kisiasa kuonyesha kwamba Lema ndiye mwanzilishi wa vurugu?
> Haya ya maneno ya Lema aliwahi kuwa mwizi wa magari yanatoka wapi? Lema
> kama mbunge ni kiongozi wa eneo hilo anayo haki na wajibu wa kujua
> yanayojiri jimboni na kutumia busara zake kutatua matatizo hayo. Si lazima
> kusubiri mkuu wa mkoa au RPC. Kuangalia kila kitu kwa ushabiki wa siasa
> tunalibomoa taifa letu kwa mikono yetu wenyewe. Siku zote watu wenye uwezo
> kiuongozi ujitokeza namna hiyo hata bila kuitwa iwe wanajipendekeza au la
> lakini cha msingi ni kutatua tatizo lilio mbele yake na hiyo ndo nafasi ya
> sisi wapiga kura kuwaona na kuwapima
>
> Hivi katika hali ya kawaida nani hakutegemea wanafunzi walete rabusha pale
> ambapo mwenzao kauawa? Haya yalikuwa yakitokea tangu enzi ya chama kimoja,
> iweje leo tujifanye wanafunzi kuleta fujo kwenye tukio kama hilo ni sababu
> ya vyama vya upinzani? Upuuzi na ubabe umekuwa ukitumiwa na viongozi wengi
> wakati wa kumaliza migogoro ya wanafunzi tangu enzi ya Nyerere ni kwa
> sababu ukweli na uwazi havikuwepo kama leo. Siku zote wanafunzi walikuwa
> wanasingiziwa lolote baya na kuonekana hawana haki. Dunia ya leo mwanafunzi
> hasomi ili apewe ajira na serikali na wala hazibwi mdomo kwa namna yoyote
> (education for silence). Naamini watu wote waliosoma miaka ya nyuma
> wakiwemo akina Mulongo wanaweza kutofautisha haya. Japo inashangaza hao hao
> ndo wanaojifanya hawaoni tofauti hizi .
>
> Tubadilike twende na wakati, dunia ya leo si ya kufichaficha matatizo na
> wala si ya kutumia mabavu kama wanavyofanya viongozi wetu. Tumieni busara
> na hekima ili kuliepusha taifa letu katika machafuko ya wenyewe kwa wenyewe
>
>
>
>
> 2013/4/28 <saidmdee@gmail.com>
>
>> **
>> Nini sababu ya mwanafunzi kuchomwa kisu!?
>>
>> Ila kwa ujumla, ninachokiona na "MAFAHARI WAWILI WAPIGANAPO, ZIUMIAZO NI
>> NYASI"....
>>
>> Yaani, hapo ipo dhahiri kuna UGOMVI BINAFSI BAINA YA LEMA NA RC MULOGO
>> ambao ugomvi huo haukusababishwa na ishu ya mwanafunzi bali ni UGOMVI WA
>> SIKU NYINGI kwa sababu zao wazijuazo wao ambazo hazikuwekwa wazi
>>
>> USHAURI: viongozi wote wa kisiasa (CCM, CHADEMA) acheni kutumia shida au
>> majonzi ya wananchi kwa ajili ya kujijengea umaarufu! Mbona vipengele vya
>> kujijengea umaarufu vipo kibao hii tanzania jamani!??????? Mavitu kibao
>> yapo, mabarabara, mahospitaki, maji nk
>>
>> ANGALIZO: mmeachana na tatizo kamili (mwanafunzi kuchomwa kisu)
>> mmeshikana
>> ninyi wenyewe badala ya nguvu nyingi kuzipeleka kule palipohitajika
>> ambapo
>> ni KUWABANANISHA WALIOMCHOMA KISU MWANAFUNZI NA KUJUA CHANZO CHA KUCHOMWA
>> KISU PAMOJA NA KUWEKA MIKAKATI YA KUHAKIKISHA JAMBO HILI LA KUCHOMANA
>> VISU
>> LINAKWISHA. Ninyi mnachukua nafasi hii kutuonyesha ubabe wenu, ugomvi
>> wenu,
>> ushindani wenu, uzembe wenu nk.... Hatuvihitaji hapa.... Wanafunzi
>> walikua
>> na nia moja tu nayo ni KWANINI VITENDO VIMEKUA ENDELEVU NA HAKUNA
>> WANAOCHUKULIWA HATUA!?? Nilitaraji magazeti na vyombo vya habari vingine
>> vijae taarifa kua: fulani bin fulani akamatwa na kufikishwa mahakama
>> kujibu
>> kesi ya kuchoma visu au wanafunzi waaswa kutofanya vitendo ambavyo ni
>> chochezi kwa wao kufanyiwa uhalifu
>>
>> ANGALIZO 2: wananchi, watanzania tuacheni ushabiki bwege wa kisiasa!
>> Tuangalie mantiki, tusipigwe/tusilambwe chenga za kizembe za kisiasa na
>> hawa wanasiasa kupitia mipasho yao! Tunahamishwa "focus" zetu kijinga
>> mno,
>> tunaacha yaliyo ya msingi tunajadili "mipasho ya wanasiasa badala ya
>> maendeleo yetu"
>>
>> Napenda niseme moja, mwanasiasa yeyote aliyepo madarakani (rais, mbunge,
>> waziri, diwani, DC, RC, mwenyekiti, balozi nk) awe "mpinzani au tawala"
>> hatakiwi kamwe kuwa "mtetezi wako kimaneno" bali awe mtetezi wako
>> kivitendo
>> vya kimaendeleo na sio blah blah kwani ukae ukifahamu, mwanasiasa yeyote
>> yule ni bigwa wa BLAH BLAH!
>>
>>
>>
>>
>>
>> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom
>> ------------------------------
>> *From: * Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
>> *Sender: * wanabidii@googlegroups.com
>> *Date: *Fri, 26 Apr 2013 16:50:09 +0300
>> *To: *Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
>> *ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com
>> *Subject: *[wanabidii] Taarifa ya Godbless Lema kwa vyombo vya habari
>> Kuhusu Chuo cha Uhasibu Arusha
>>
>> Jana majira ya saa nne asubuhi nilipokea taarifa kutoka Chuo cha Uhasibu
>> juu ya tukio la mauaji ya mwanafunzi yaliyotokea jana usiku kwa kuchomwa
>> kisu eneo karibu na chuo , nilipita Chuoni hapo baada ya kusikia taarifa
>> hiyo, nilikuta Wanafunzi wengi sana wakiwa wamekusanyika pamoja wakiwa na
>> jazba huku Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilaya akijaribu kuwasihi watulie
>> wakati walipokuwa wanatafuta muafaka wa kuzuia jazba ambayo ilikuwa ina
>>  lengo la kuandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa.
>>
>> Nilipata faragha ya kuongea na Mwalimu aliyekuwa pale ( Dean of Student )
>> pamoja na OCD na wote walinieleza tatizo lilivyoanza na kuomba nitumie
>> busara kuzuia jazba na maandamano hayo yaliyokuwa yamepangwa kuelekea kwa
>> Mkuu wa Mkoa niliongea na wanafunzi na niliwasihi watulie na nilifanya
>> jitihada za kumtafuta Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa na kwa bahati nzuri
>> nilimpata Mkuu wa Mkoa na kumweleza juu ya kifo hicho na kile ambacho
>> wanafunzi wanakusudia kufanya kuandamana kwenda ofisini kwake. Nilimuomba
>> afike ili aweze kutuliza hali hile na pia atoe kauli juu ya tukio hilo
>> baya
>> la kuhuzunisha kwani ikizingatiwa kuwa ni zaidi ya mara moja matendo kama
>> haya yamekuwa yakitokea na hakuna hatua zozote zimekuwa zikichukuliwa
>> kuwahakikishia Wanafunzi Usalama wao na mali zao.
>>
>> Mkuu wa Mkoa pamoja na mimi kumpa taarifa mapema aliahidi kufika mapema
>> jambo ambalo halikufanyika na wanafunzi walianza kuwa wakali na nilifanya
>> jitihada na hekima za hali ya juu kuvuta subira za wanafunzi hao ili Mkuu
>> wa Mkoa afike . Baada ya Mkuu wa Mkoa kufika Makamu wa Chuo aliniomba
>> niwaandae wanafunzi kumsikiliza Mkuu wa Mkoa na yeye alikwenda kumchukua
>> Mkuu wa Mkoa na kumpa mukutasari wa tukio zima na hali halisi ya
>> kilichokuwa kinaendelea na kimsingi Mkuu wa Mkoa alipofika Wanafunzi
>> walitaka apande juu kuongea mahali ambako tulitumia kama jukwaa kwa
>> maongezi wakati wote lakini badala yake mambo yafuatayo yalianza kutokea
>>
>> 1) Mkuu wa Mkoa alikataa na kunitaka nishuke chini mahali alipokuwa yeye
>> na timu yake ya ulinzi na usalama Mkoa kwa kweli nilitii na nilipotaka
>> kuongea nae alinidharau na kuniambia hawezi kuongea na wanafunzi wahuni
>> wasiokuwa na nidhamu maneno ambayo yaliwatia wanafunzi hasira zaidi na
>> nilimsihi na kumuomba Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa (RSO) kumshawishi
>> Mkuu
>> wa Mkoa kukubali kuongea nao kwani hali ilivyokuwa ni dhahiri kwamba
>> wanafunzi wale walikuwa na jazba ya hali ya juu na hivyo hekima na
>> unyenyekevu ndio ilikuwa njia pekee ya kutuliza hali hile.
>>
>> 2) Mkuu wa Mkoa alitoa masharti kwamba asingeweza kuongea nao bila kipaza
>> sauti na wanafunzi wote waende jengo lililokuwa karibu na Utawala na
>> wakisha kaa atakuja kuongea nao jambo ambalo wanafunzi waligoma kwa imani
>> kwamba jengo hilo lisengeweza kuchukua wanafunzi wengi na mimi niliaga
>> naondoka kwenda msibani na wanafunzi waligoma nisiondoke mpaka watakapo
>> sikilizwa na kwa kweli nilitii maombi baada ya kunizuia na kukaa mbele ya
>> gari yangu.
>>
>> 3) Tulipokwenda eneo la kukutania na mara hii ilikuwa ni nje jirani ya
>> jengo la utawala wanafunzi walikusanyika wakimsubiri Mkuu wa Mkoa na
>> kabla
>> hajafika nilitwa na yeye mwenyewe ili tuweke msimamo wa pamoja kama
>> viongozi lakini badala yake alitumia Polisi kunitisha na kuhaidi kuwa
>> nitamtambua kuwa yeye ni Serikali ,tulitofautiana tena nilipokataa hofu
>> hiyo na ghafla tuliamua kwenda eneo la kuongea na wanafunzi na ndipo
>> yafuatyo yalitokea "
>>
>> Mkuu wa Mkoa wakati anaanza kuongea alianza kusema maneno yafuatayo "
>> Mnaona hiki Kifua na huu mwili wangu , na hapo ndipo hali ilipochafuka na
>> kuamsha vurugu kubwa kutoka kwa Wanafunzi waliokerwa na kauli yake na
>> Polisi wa walimchukua na tafrani kati ya Polisi na Wanafunzi ikapamba
>> moto
>> hali iliyosababisha mabomu ya machozi kulipuliwa kwa wingi kila kona ya
>> chuo na kila mtu kuanza kukimbia kuangalia usalama wake nikiwemo mimi.
>>
>> Nimesikiliza Mkutano wake na Waandishi wa Habari na leo nimesoma
>> nakusikiliza vyombo mbali mbali vya habari kwamba ninatafutwa na Polisi
>> kwa
>> amri ya Mkuu wa Mkoa , nimeshangaa sana japo sio kumshangaa Mkuu huyu wa
>> Mkoa kwani ufahamu na uwezo wake naujua ulivyo katika kufikiri na kutatua
>> mambo ya msingi na muhimu , kwa jinsi nilivyomsikia na kumuona alivyokuwa
>> anashughulikia tatizo lile lililotukutanisha jana pale Chuoni , kwa kweli
>> nilishangazwa sana na kuogopa kama hekima ya Mkiti wa Kamati ya Ulinzi na
>> Usalama ya Mkoa angeweza kushughulikia tatizo lile kwa namna ile ya
>> Kiburi
>> , Dharau na Majivuno ambayo hakika ilikuwa ni chanzo cha wanafunzi
>> kukataa
>> kumsikiliza na ndipo alipoamua kuondoka huku zomea zomea ikiendelea
>> kushamiri vizuri.
>>
>> Mabomu yalianza kupigwa , wanafunzi walipigwa na kunyang'anywa pesa ,
>> simu
>> , na lap top na vitu mbali mbali ambavyo Polisi walikuwa wanaona vina
>> thamani kwao , nilikuwa ninatazama mambo haya huku roho yangu ikiwa
>> inauma
>> sana kwamba wanaopaswa kulinda usalama wa raia na mali zao ghafla
>> waligeuka
>> kuwa vibaka wa kuumiza raia na kupora mali zao .
>>
>> Ninawapa pole wanafunzi kwa msiba wa rafiki yao na siku ya jana ilikuwa
>> ni
>> siku ya Serikali kutumia busara kurudisha matumaini kwa wanafunzi wale
>> pamoja na raia , lakini badala yake wafiwa walipotaka kudai haki zao za
>> kulindwa , walipigwa , walidhalilishwa na Chuo chao kufungwa bila sababu
>> ya
>> msingi wala kuzingatia mambo muhimu .
>>
>> Ifahamike kuwa Chuo cha Uhasibu Arusha kina wanafunzi kutoka sehemu
>> mbalimbali za nchi hii, na amri ya mkuu wa mkoa kufunga chuo na kuamuru
>> wanafunzi watawanyike ifikapo saa kumi na mbili jioni , huu ni ukosefu wa
>> upendo , hekima , busara na utu ikizingatiwa kuwa sababu na mchochezi wa
>> vurugu hizi ni Mkuu wa Mkoa kukosa maarifa na hekima.
>>
>> Nimepokea ujumbe katika simu yangu kutoka kwenye simu yangu ya kiganjani
>> kutoka kwa Mkuu wa Mkoa inayonitishia na kuweka maisha yangu kwenye hali
>> ya
>> hatari na ujumbe huo unasema "*UMERUKA KIHUNZI CHA KWANZA , NITAKUONYESHA
>> KUWA MIMI NI SERIKALI ULIKOJIFICHA NITAKUPATA NA NITAKUPA KESI NINAYOTAKA
>> MIMI* " Mwisho wa kunukuu.
>>
>> Mwisho, Ninamshukuru kijana aliyerekodi tukio lote kuanzia mwanzo mpaka
>> mwisho na hivi tutanza kusambaza video cd hizo Nchi ili watanzania wajue
>> ukweli na Mh Rais aone utendaji mbovu wa wateule wake na vile nilitake
>> Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, maadili ,taratibu na
>> kanuni za kazi na sio kuendesha Jeshi kwa matakwa ya kisiasa , kufanya
>> hivi
>> ni kuhatarisha usalama na utulivu wa Nchi yetu.
>>
>> Che Guavera alisema "if you tremble indignation at every injustice then
>> you are a comrade of mine."
>>
>> Wanafunzi jipeni moyo bado kitambo kidogo Taifa hili litabadilika.
>>
>>
>> Godbless J Lema (MP)
>> 25/4/2013
>>
>>  --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>


--
Ephata Nanyaro
P.o.box 15359
Arusha
+255 754 834152
Skype.nanyaro.ephata

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment