Sunday 28 April 2013

Re: [wanabidii] FASTJET – KASUKU MWENYE KUCHA ZA SIMBA?

Nakubaliana na wewe Matanda. Nafikiri Mwenzetu Musa usafiri wa PRECISION AIR haujui. Hakuna airline inaboa kama precision. They never tell the truth kwa wateja wao. Several times nimekuwa disappointed na shirika hili. Unaweza kuwa na ndege ya asubuhi let say unatoka Mwanza kuja Dar, unafika airport wanakwambia tulikutafuta jana kwenye simu siku nzima hupatikani kukuarifu kuwa ndege itakuwa saa moja usiku badala ya asubuhi hukupatikana. unashangaa inakuwaje wao tu ndio wakukose?

Tatizo umeishaingia gharama ya taxi, unatafuta pa kwenda kushinda upoteze muda inakuwa ngumu maana hotelini ulishatoka, yaani gharama juu ya gharama Shortly kama unatoka Mwanza unakuja Dar ana unategemea kuunganisha ndege nyingine labda unasafiri kwenda nje siku hiyo hiyo, nashauri usikate kabisa tiketi ya Precision utajuta. Nadhani mimi nina bahati mbaya na shirika hili, sijawahi kusafiri nalo kwa wakati ulioandikwa kwenye tiketi .

Ila na FASTJET nayo ina vituko vyake. Ukitaka burudani panda fastjet. Kwa upande wa nauli na gharama za mizigo inategemea wamekuangaliaje maana ni utata mtupu.
 
From: Sisty Basil <stiba7@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, April 27, 2013 2:47 PM
Subject: Re: [wanabidii] FASTJET – KASUKU MWENYE KUCHA ZA SIMBA?

Hapo ndo unapotambua kuwa nafuuu ni Gharama

2013/4/27 denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
POle sana Musa ila naomba nitofautiane na wewe kwenye kusema "nawapongeza sana PRECISION AIR kwa utaratibu wao mzuri  wa 'KIUTU' wa kuwajali wateja wao". Kama umekuwa frustrated na Fastjet kwa kukuweka uwanjani masaa 9 basi ni bora uachane kabisa na usafiri wa ndege bongo, rudi kwenye mabasi!!!! Ukikata zako Greenstar au Saibaba una uhakika saa 12 asubuhi limeondoka stand..............
 
Nikiangalia frequency za kuahirish a safari kati ya Precision na Fastjet basi ni kama kumlinganisha Mike Tyson na Francis Cheka. Labda tofauti na Fastjet ni kuwa Precision never tells it's apssengers the whole truth. Nina jamaa zangu ambao waliwekwa uwanjani kuanzia saa 7 mchana mpaka saa 5 usiku huku kila saa inayopita wakiahidiwa kuwa wataondoka muda mfupi ujao............
 
Tuna safari ndefu sana kabla ya kufika huko tunakotaka. Until then attempt yoyote ya kuoneysha eti kuwa Fastjet is so hopeless itakuwa ni kutoietendea haki na kujidanganya wewe mwenyewe.
 
Ni mtizamo tu.

2013/4/27 Mussa Mziya <mkmziya@yahoo.com>
Ndugu zangu;
Kwa mara ya kwanza wakati shirika la ndege binafsi la fastjet linaanza kazi hapa nchini, lilionekana kama ni mkombozi kwa wananchi wanyonge, wasio na uwezo mkubwa kusafiri na ndege! Kadri siku zinavyosogea shirika hili ndivyo linavyokunjua makucha yake na kuonyesha kwamba ni chui aliye ndani ya ngozi ya kondoo. FastJet imekuwa ikiwaimbisha wananchi wanyonge na nauli yake ya 32,000 tu! Ilhali ni wananchi wachache sana wanaopata nafasi katika daraja hili la chini.
Mbali na nauli zake zinazobadilika kama kinyonga wa jangwani, lakini sera zake (policy) zimejilenga kujineemesha zaidi na kuwadhulumu wananchi wanyonge. Mfano usiposafiri hata kwa dharura gani, huwezi kurejeshewa fedha zako. Pia huwezi kubadilisha tarehe ya kusafiri hata kama una dharura ya namna gani, bila kulipa fedha nyingi, wakati mwingine hata kukaribia bei ya tikiti mpya, inginevyo itabidi tiketi hiyo ipotee na uje ukate nyingine.  Moja ya sera zake unapotaka kubadili muda wa safari inasema  '' Fare difference may be substantial'' (tofauti ya nauli inaweza kuwa kubwa) bila kuonyesha kiasi cha ukubwa wenyewe mpaka pale watakapokuwa wamebadili, wakati ambapo ni lazima ulipe kwani tayari watakuwa wameshaiuza kwako.
Labda nieleze kisa kilichonipata jana na leo: 
Jana: Kuna ndugu yangu aliyekuwa asafiri kwa ndege FN 0161 kutoka Dar kuja Mwanza leo asubuhi (ambayo ndiyo ilifutwa) lakini kwa bahati alibadilisha muda na kusafiri jioni kutokana na dharura iliyompata. Ilibidi alipie kiasi cha Shs. 56,000 (ziada ya bei aliyonunulia tikiti ya Shs. 155,000/= one-way) kubadili tu huo muda wa safari. Lakini dharura ile iliendelea na ikabidi niombe tena kumbadilishia safari iwe kasho asubuhi. Hapo kwa mujibu wa utaratibu wao, system ika charge malipo ya 40,000/= kama adhabu (penalty) ya kubadili safari na malipo ya ziada ya Shs. 104,000/= kwa 'kosa' hilohilo la kubadili safari kwa dharura. Sasa ukijumlisha malipo tuliyolipa kwa safari ya one-way ni  155,000 + 56,000 + 40,000 + 104,000 =  355,000!!! Kwa safari moja tu (one-way Dar/Mwz) Sawa taratibu ni taratibu, lakini taratibu za hawa ndugu zetu ni za dhulma kubwa. Kumbe yule kasuku mzuri tunayemwona, ana kucha za Simba!.
Leo: Nilikuwa nisafiri na ndege hiyo ya fastJet flight No. FN 0162 kutoka Mwanza kwenda Dar-es-Salaam saa 2:50 asubuhi. Ndege hiyo ilifutwa (cancelled) kwa sababu tuliyoelezwa kuwa ni ya kiufundi. Tukaambiwa tutasafirishwa kwa ndege yao ya jioni saa 11. Lakini cha ajabu, tofauti na utaratibu unaotumika na mashirika mengi ya ndege ''serious''  duniani hakukuwa na msaada wowote (consideration) kwa wasafiri ukizingatia wasafiri hawa wametumia fedha kukodi taxi kuwaleta uwanja wa ndege. Tulifika airport kwa gharama zetu, tukaondoka kwa gharama zetu na kurudi tena jioni kwa gharama zetu. Sasa ilipokuwa ni dharura kwa upande wangu mimi mteja, wakanichaji fedha nyingi (355,000) eti kwa usumbufu walioupata kubadili safari. Sasa iweje na wao wanapokuwa na dharura za kuharibikiwa na ndege hawatujali hata kwa nauli ya taksi? Achilia mbali suala la wasafiri kupelekwa hotelini na kurudishwa wakati wa safari!
Nadhani wakati umefika sasa kwa Serikali kupitia mamlaka husika (nadhani ni mamlaka ya safari za anga) kuchukua hatua za makusudi kuangalia na kuridhia taratibu (policies) za mashirika haya ya ndege ili ziwe fair na zisiwadhulumu wananchi kiasi hiki. Nadhani hii itakuwa ni safari yangu ya kwanza na ya mwisho kusafiri na Kasuku huyu mwenye kucha za Simba (FastJet) na nawapongeza PRECISION AIR kwa utaratibu wao mzuri wa 'KIUTU' wa kuwajali wateja wao.
Mussa
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
--
Wasalaam,
 
Denis Matanda,
Mine Planning Supt,
Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
--
Africa Holds two fifths (2/5) of the world's Uranium and Gold, three quarters (3/4) of the world's platinum and 90% of the world's diamonds.....the world'd richest continent, Makes you Wonder WHY:-? 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment