Saturday 27 April 2013

RE: [wanabidii] MIAKA 49 YA MUUNGANO. MASWALI SITA

Juma Mzuri,
 
Majibu yako (au aliyekutuma au ulikotoa mada hii) kwenye rangi nyekundu:
 
¤Kwenye kuingia mkataba wa Muungano, kwa nini Nyerere alimshirikisha mwanasheria wake Roland Brown wakati Karume alimpa mwanasheria wake Wolfgang Dourado likizo ya muda kwenda nchini Uganda wakati Karume hakuwa msomi ukiachia uzoefu wa kazi ya ubaharia pamoja na umaarufu wa kucheza mpira?
 
Nyerere alimshirikisha mwanasheria wake huyu kwa sababu andiye aliyekuwa mwanasheria wake. Tanganyika haikuwa na wanasheria wa kabila ile wakati ule. Karume alikuwa Rais aliyemteua Dourado kuwa mwanasheria mkuu na alikuwa na mamlaka ya kumtoa cheo hicho au kumpeleka likizo. Aidha, kwa kuwa mwanasheria ni mtumishi wa mteja wake, hana maamuzi yoyote nje ya yale anayotaka mteja wake; hivyo kama Dourado hakukidhi mahitaji/matakwa ya Karume, alipaswa kuwekwa kando kwa mtindo wowote ule. Wanasheria ni matarishi tu wa wateja wao katika ufundi wa sharia.

¤Hati ya Muungano ilikuwa na mambo 11. Hivi sasa yamefikia 23 kutokana na kuongezwa na Nyerere taratibu kwa kupitia decree. Je, Karume alijua kuhusu uwepo wa decree kwenye katiba?
 
Ni kweli mambo ya Muungano yamefikia 23 kutoka 11 ya awali. Kuna sababu zake, mojawapo ikiwa kwamba hakukuwa na makubaliano ya kubakia na yale yale 11 bali kulikuwa na makubaliano ya kuuboresha Muungano. Pili, si kweli kwamba ni Nyerere pekee aliyeyaongeza, au tuseme kwamba yaliongezeka wakati wa Nyerere tu. Soma historia ya Muungano ujielimishe. Aidha, Karume alikuwa shuhuda wa kuongezwa mambo ya awali, mfano baada ya kuvunjwa kwa iliyokuwa sarafu ya Afrika Mashariki na kisha kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania. Mambo haya yameongezeka kutokana na ulazima wake, umuhimu wake, na yalifuatwa utaratibu kila yalipoongezwa. Kumbuka, mambo ya Muungano yanasimamiwa na serikali ya Muungano, Rais wa Muungano na Bunge la Muungano, si nje ya hapo. Ili kufahamu sababu za kila jambo liliongezwa, anzia na tovuti ya Makamu wa Rais, kisha ukikwama, uliza.

¤Mkataba wa Muungano uliridhiwa na Bunge la Tanganyika (tena weekend). Kwa nini Bunge la Zanzibar (Baraza la Mapinduzi) halikuwahi kukutana kuridhia? Je, Muungano ni halali?
 
Bunge lilikuwa na uwezo wa kukaa siku yoyote. Lingekaa Jumatatu ingebadili nini? Zanzibar haikuwa na Bunge halali. Hata hivyo, Baraza la Mapinduzi lilipitisha muswada wa Muungano ila kusichokuwepo ni rekodi. Muungano ni halali na nakala yake iko Umoja wa Mataifa, New York ambapo hawapokei mikataba magumashi.

¤Karume hakutaka muungano wa serikali mbili. Ilikuwaje Nyerere akakomaa?
 
Ukweli ni kwamba Karume alitaka serikali MOJA tu akisema, "Nyerere wewe kuwa rais, mimi Makamo". Walizungumza na wakakubaliana kuunda serikali mbili na Karume akawa Makamu na miaka yote ya uhai wake hakupinga uwepo wa serikali mbili. Kudai hivyo ulivyosema ni mzaha.

¤Kama lengo la Muungano ni regional integration (as opposed to Kwame Nkurumah's notion), kwa nini Muungano wetu haukuongezeka tena tokea 1964 (e.g. Kwa ku-include nchi za jirani e.g. Mozambique au Zambia? Je, ni kwa sababu waliona matatizo makubwa kwenye muungano wetu (kama Ethiopia/Eritrea, Sudan/South Sudan, Gambia/Senegal).
 
Lengo la Muungano halikuwa regional integration na wala haukufanyika ili kupingana na wazo la kidikteta la Nkrumah. Ili Muungano wa kikanda utokee ilipaswa kutimia ile ndoto ya Afrika Mashariki. Baada ya hoja hii swali linafia hapo hapo. Nenda kawaulize hao wengine sababu zao.

¤Kwa mazingira ya hivi sasa ambayo uwezekano wa kupata rais mzanzibar kuzidi kuwa mdogo, je, muungano unaweza kudumu miaka mingi mingine?
 
Rais wa Muungano kutoka Zanzibar ni jambo linalowezekana; si kweli kwamba haiwezekani. Mfano, kama Dkt. Salim Ahmed Salim asingepingwa na Wazanzibari kila anapojaribu, angekuwa Rais wa tatu (kama asingegoma kuweka jina lake) ama wa nne wa Muungano (kama angepata kura za kutosha). Aidha, muungano haupaswi kulindwa na zamu za urais. Urais ni taasisi nyeti, hatuwezi kupekezana kama njugu. Hii siyo kwenye Muungano tu, bali hata kwenye masuala mengine kama udini, ukabila, jinsia, umri, n.k.
 
Matinyi.

From: matinyi@hotmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] MIAKA 49 YA MUUNGANO. MASWALI SITA
Date: Fri, 26 Apr 2013 14:10:14 +0000

Safi Matanda.
 
Nitarejea hapa.
 
Date: Fri, 26 Apr 2013 10:53:03 +0000
Subject: Re: [wanabidii] MIAKA 49 YA MUUNGANO. MASWALI SITA
From: denis.matanda@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Juma,
 
> Swali lako namba moja linaonyesha ukosefu wa umakini kwa huyo unayemtuhumu kumpeleka mwanasheria wake likizo
> Kuna ushahidi kuwa hayo mambo yote 12 yaliongezwa na Nyerere? Kuhusu Karumne kujua kuhusu kuwepo kwa decree kwenye katiba; wewe unaamini kuna mtu anayeweza kumjibia marehemu mzee Karume hapa?
> Sijui jibu la swali la 3 na sitaki ku-speculate
> Hakuna ushahidi juu ya pointi yako namba 4. Mpaka Karume anauawa muungano ulikuwa ni wa serikali 2, kama hakuutaka si angeuvunja? Napata ugumu kuamini madai haya
> Point namba 5 naona jibu lake kwangu ni rahisi. Kupitia muungano huu watu wengi naamini hata Nyerere mwenyewe aligundua kuwa pengine furaha ya muungano inazidiwa na kero za muungano. Tayari tuna kero laki 6 na muungano huu, kuna haja ya kuongeza kero nyingine? Hii ndio imani yangu
> Pointi namba 6 naona haina nguvu kisiasa. Kitakachoudumisha muungano huu sio wazanzibar kuwa marais, kitakachoudumisha muungano huu ni mimi, wewe na yule kutaka udumu.
 
Happy union day kaka!

2013/4/26 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
¤Kwenye kuingia mkataba wa Muungano, kwa nini Nyerere alimshirikisha mwanasheria wake Roland Brown wakati Karume alimpa mwanasheria wake Wolfgang Dourado likizo ya muda kwenda nchini Uganda wakati Karume hakuwa msomi ukiachia uzoefu wa kazi ya ubaharia pamoja na umaarufu wa kucheza mpira?

¤Hati ya Muungano ilikuwa na mambo 11. Hivi sasa yamefikia 23 kutokana na kuongezwa na Nyerere taratibu kwa kupitia decree. Je, Karume alijua kuhusu uwepo wa decree kwenye katiba?

¤Mkataba wa Muungano uliridhiwa na Bunge la Tanganyika (tena weekend). Kwa nini Bunge la Zanzibar (Baraza la Mapinduzi) halikuwahi kukutana kuridhia? Je, Muungano ni halali?

¤Karume hakutaka muungano wa serikali mbili. Ilikuwaje Nyerere akakomaa?

¤Kama lengo la Muungano ni regional integration (as opposed to Kwame Nkurumah's notion), kwa nini Muungano wetu haukuongezeka tena tokea 1964 (e.g. Kwa ku-include nchi za jirani e.g. Mozambique au Zambia? Je, ni kwa sababu waliona matatizo makubwa kwenye muungano wetu (kama Ethiopia/Eritrea, Sudan/South Sudan, Gambia/Senegal).

¤Kwa mazingira ya hivi sasa ambayo uwezekano wa kupata rais mzanzibar kuzidi kuwa mdogo, je, muungano unaweza kudumu miaka mingi mingine?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
--
Wasalaam,
 
Denis Matanda,
Mine Planning Supt,
Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

0 comments:

Post a Comment