Monday 29 April 2013

Re: [wanabidii] MEI 3 ,TAALUMA YA HABARI ILIVYOPATA KILEMA

hakika maneno yako yamenigusa

On 4/28/13, mobini sarya <mobinsons@yahoo.com> wrote:
> Katuni ya Kibanda ilivyomaliza Taaluma
> ya habari
>
> Na TANpress
> MEI 3 YA KILA MWAKA ni siku ya uhuru wa habari,hivyo wadau wa habari
> hukutana mahali fulani kutathimini mwenendo wa uhuru wa kutoa maoni katika
> nchi husika.
> hivyo kwa kuwa ni wiki ijayo nimeona nitoe maoni yangu mapema kabisa ili
> kutoa nafasi ya mjadala.
>
> MARA nyingi huwa navutiwa na michoro ya
> katuni kwenye magazeti, ingawa mimi sina kipaji cha kuchora lakini huwa
> nasema
> pengine ningewa kipaji hicho ingekuwaje?
> Huwa najisifu kuwa pengine ningekuwa
> mchora katuni ningeifanya kazi hiyo kwa ubora na umakini mkubwa zaidi
> kuliko
> hii ya kuandika.
> Katuni ni kitu nachokipenda kwa kweli
> jinsi ambavyo kinawasilisha ujumbe mzito kwa njia ya michoro, ndio maana
> hata
> nikichukua gazeti liwe la kiingereza au Kiswahili huwa nakimbilia kwanza
> kwenye
> kibonzo baada ya hapo ndipo nitasoma habari zinazonivutia.
> Kutokana na mapenzi makubwa niliyonayo
> kwenye katuni au vibonzo ndipo yakanijia mawazo  wakati nikifikilia juu ya
> kutekwa na kuteswa kwa mwenyekiti wa jukwaa la
> wahariri Absalom Kibanda, siku ya Machi 5 Mwaka 2013.
> Nilifikiria mateso aliyoyapata mhariri
> huyo, nikasikitika jinsi ambavyo taaluma ya habari imetendewa ukatili
> mkubwa.
> Nikakumbuka kuwa aliyefanyiwa hivyo, ni
> mwandishi wa habari,mhariri, mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, hivyo
> kibanda
> alikuwa taswira ya habari hapa nchini.
> Nikafikiria kuwa jinsi ambavyo
> ningechora katuni kuhusiana na tukio hilo,mchoro wangu ungesimamaje
> kuwakilisha
> taswira ya tukio hilo.
> Nikajiuliza kuwa ikiwa mtu huyu mhimu
> kwenye taaluma ya habari ameng'olewa meno ya mbele bila ganzi maanake ni
> kwamba
> taaluma ya habari nchini imekuwa kibogoyo.
> Kwamba sasa waandishi na watangazaji
> hawataweza kusema na kutangaza wazi wazi habari,  wakasikika kwani ni
> vibogoyo hawana meno
> tena.
> Kwamba mchoro wa katuni yangu ungeelekea
> kwenye macho, ili mwandishi  wa habari
> aweze kufanya kazi yake kwa makini anatakiwa awe na jicho kali, ndio maana
> wanaitwa jicho la jamii, sasa wametobolewa.
> Kwa hiyo ukiitazama katuni hiyo kwa
> makini unaona kwamba taaluma ya habari nchini imeingia gizani, wandishi
> hawataweza kuona kwa ufasaha yale yanayofanywa na jamii au dola.ni vipofu
> sasa.
>
>
> Ndio maana wananchi wanashangaa kuona
> wabunge wanaochafua bunge kwa kumdharau Spika lakini anayelalamikiwa ni
> Spika
> badala ya walengwa ambao ni wabunge wanaotaka  kumuonyesha mafunzo
> waliyopata JKT.
> Hakuna anayewakemea wazi wazi bila
> kutaja cheo au kiti cha Spika hii inadhibitisha jinsi ambavyo tumetobolewa
> macho hakuna anayeona ukweli tena.
> Mchoro wa katuni hiyo unaelekea chini ya
> Mabega na kukutana na mikono ya Mwandishi wa habari, itakumbuka kuwa bila
> mikono mwandishi hawezi kukaa kwenye kompyuta na kuandika habari kwenye
> mitandao zinazoitwa za uchochezi.
> Mhariri Kibanda licha ya kutobolewa
> jicho ili awe kipofu pia amekang'olewa na kucha na kukatwa kidole kama njia
> ya
> kuwanyanganya wandishi haki ya kuandika chochote.
>  Ili
> kuhakikisha wandishi wa habari za mitandao hawaendelei na shughuli zao
> ikabidi
> kibanda akatwe kidole ,sawa na mkono hivyo kuwafanya wandishi wa habari
> washindwe kuandika habari.
> Taaluma ya habari sio tu imekatwa mikono
> bali imenyofolewa kucha na kuachiwa maumivu makali yatakayowafanya wandishi
> wachanganyikiwe washindwe kuandika habari za uchunguzi.
> Mwandishi mwenye maumivu ya kucha kisha
> amekatwa mkono hawezi kuwa makini kuandika habari zitakazolikomboa taifa
> badala
> yake atabaki analilia kidole chake.
> Ukifuatilia mchoro wa katuni bila kujali
> nani amehusika na uovu huo unagundua kuwa taaluma hiyo kwa miaka ya hivi
> karibuni imefanyiwa ukatili mkubwa unaweza kupelekea uhuru wa maoni
> ukapungua
> kama sio kutoweka kabisa.
> Kosa kubwa la kuuwa uhuru wa habari
> lilianzia pale mwandishi wa kituo cha Chaniel 10 alipouwawa mchana kweupe na
> hatua
> stahiki hazikuweza kuchuliwa.
> Chanzo cha mwanahabari huyo Daudi Mwangosi
> kuuwawa septemba Mwaka 2012kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari
> wa
> gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi.
> Hivyo  mwanahabari huyo akataka kuhoji polisi sababu
> ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia
> kwa
> kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo
> na
> askari mmoja waliaguka chini ikawa ndio mwisho wake.
> Licha ya wandishi kujitokeza kuandamana
> kwa kulaani dola  lakini laana zao
> hazikuwa na nguvu wala hazikuathiri serikali kwasababu wandishi waliendelea
> kushirikiana nayo kama kawaida, hata pale Rais wa Nchi alipogoma kutoa
> rambi
> rambi ya kifo hicho.
> Ni katika kipindi hicho ndio maadui wa
> uhuru wa habari walidhani wameshinda na taaluma ya habari imekufa kutokana
> na
> jamii kushindwa kujitokeza hadharani kupambana na uovu huo kama ilivyotokea
> Tunisia
> mara baada ya mmachinga kujilipua akiipinga dola.
> Tangu afariki mwandishi huyo na hatua
> madhubuti zikashindwa kuchukuliwa ndio sababu ya kuzaa haya ya Kibanda na
> sasa
> uhuru wa habari unaelekea kuto weka kwa mbali wandishi wanakuwa vibogoyo na
> vipofu.
> Kama jamii ya watanzania ingeungana
> kipindi kile na kujitokeza kwa pamoja kulaani tukio lile kwa kuitia dola
> misuko
> suko ya hatari ambayo ingelazimisha wakuu wa usalama kukutana kwa dharura
> kujadili hali hiyo kisha kuja na majibu kuwa jambo baya kama hilo
> halitawakuta
> tena wanahabari wala kwenye jamii.
> Kwa kuwa hakuna misuko suko iliyotokea
> na kwa kuwa laana za wandishi hazikuwashika ,walengwa ndio maana leo
> anapotokea
> kiongozi mhimu kwenye taaluma ya habari anaumizwa vibaya wenyengine
> wanatumia
> bunge kudhihaki kwamba Kibanda ni nani hata atekwe.
> Dhihaka za namna hiyo hutolewa na watu
> walioshiba amani lakini nchi ambazo zimeonja machafuko yaliyoletwa na
> dharau
> kama hizo, tayari kiongozi huyo alipaswa kufukuzwa kazi kama sio kujiuzulu
> kwani anaweza kuletea dola balaaa.
> Kinachoshangaza zaidi ni kuona miezi
> miwili inamalizika tangu mwenyekiti wa jukwaa la wahariri ,(TEF)atekwe na
> kuumizwa lakini hakuna aliyekamatwa, wakati aliyekuwa RPC wa mkoa wa Mwanza
> aliuwawa usiku wa manane lakini wauwaji walikamatwa mapema.
> Hali hiyo ndio inaifanya jamii kukosa
> uaminifu na vyombo vya usalama ikiaminika kwamba pengine nchi hii hutoa haki
> ya
> kulinda raia wake kwa upendeleo, hivyo wapo raia wa daraja la kwanza ambao
> wakiumizwa tu serikali inafanya haraka kuwatafuta wahusika.
> Hali hii ikiachwa iendelee tunaweza
> tukazika uhuru wa habari tukidhani tunajipa ahueni ,kumbe baada ya muda
> sisi
> tunaoshikilia dola tutakuwa nje ya ulingo na wengine watakuwa ndani ya dola
> ,kwakuwa tulisha haribu mfumo huo ,tutakosa sehemu ya kutolea maoni.
> Kuna watu tunawafahamu zamani walikuwa
> kwenye mfumo wa dola na walikuwa sehemu ya kukandamiza uhuru wa habari
> lakini
> leo hii wapo nje ya mfumo huo wanajaribu kutumia vyombo vya habari kama
> sauti
> ya kudai haki zao.
> Hatuwezi kushiriki kukandamiza uhuru wa
> habari, tukadhani kuwa kuna kitu tutafaidika nacho katika siku za baadaye ,
> kwani muda utakapohitajika kwa kuvitumia vyombo hivyo ,vitakuwa vimepoteza
> meno
> na macho ya kuona.
> ni malize kwa kusema kuwa ni kweli dola imeshindwa kuwakamata waliomjeruhi
> Mhariri Kibanda ili tuombe msaada katika shirika la upelelezi la marekani
> FBI,
> litusaidie kama lilivyofanikisha kumkamata kijana aliyelipua bomu mitaa ya
> Bostoni?
>    Kama jibu ni ndio tuvunje kwanza ofisi ya mkurugenzi
> wa upepelelezi wa makosaji ya jinai ndipo tuombe msaada nje, ile ofisi
> haitusaidii kitu zaidi la kula kodi zetu.
> SIR MOBNI  SARYA
> TANZANIA NEWS FORUMS
> DIRECTOR
> www.mobinday.blogspot.com 0753399579
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment