Tuesday 26 March 2013

[wanabidii] UTARATIBU WA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI KUSHIRIKI KUTOA MAONI YAO KUHUSU KATIBA MPYA

MWONGOZO KUHUSU UTARATIBU WA WATANZANIA

WANAOISHI UGHAIBUNI KUSHIRIKI KUTOA MAONI

YAO KUHUSU UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA

_________________________

Kwa kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote wanaotaka kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana katika tovuti ya Tume ambayo ni www.katiba.go.tz

Kusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa ubora na upungufu wake na kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa kisheria kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.

  1. 1.   MAMBO YA KUZINGATIA

Kwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa na Sheria, Tume inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:

(a)Nani Mwenye Haki ya Kushiriki:

Mtu yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki ya kushiriki katika mchakato huu.   Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania, lakini amepoteza uraia wa Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria.

(b)Utaratibu wa Utoaji Maoni:

Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika.  Njia hizo ni kama zifuatazo:

(i) Utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti (www.katiba.go.tz) barua pepe ya Tume, ( katibu@katiba.go.tz), nukushi + 255-22-2133442 na +255-224-2230769

(ii)Utoaji wa maoni kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani ya Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681 DSM au Ofisi ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.

Endapo Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama Watanzania wengine walioko nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Tume.

(c)      Utambulisho wa Mtoa Maoni:

Kila mtu atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-

(i)           majina yake matatu;

(ii)          namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;

(iii)        nchi na mji anaoishi;

(iv)        endapo atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi yake (ukurasa unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).

Tume inapenda kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji wa maoni ni jambo la uhuru na hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unawahusu raia wa Tanzania pekee.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment