Thursday 28 March 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Neno La Leo: “ E bwana, Tutakula Wapi Pasaka?”

Amen, Mtumishi Mjengwa

Sent from my iPad

On 28 Mac 2013, at 11:47 alasiri, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

Ndugu zangu,

Na ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza; `` E nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka."

Nao wakamwuliza; ``Tukaandae wapi?''

Yesu akawajibu; ``Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni huyo huyo, mpaka kwenye nyumba atakayoingia."

"Kisha mwambieni mwenye nyumba; Mwalimu anauliza, kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka? Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani. Chumba kilicho na fanicha zote. Fanyeni maandalizi humo.''

Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Hivyo, wakaandaa chakula cha Pasaka. Wakati ulipofika, Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. Kisha akawaambia;


``Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.''

Hapo Yesu akapokea kikombe cha divai, akashukuru akisema, ``Chukueni mnywe wote. Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.'' Alitamka Yesu.

Ni Neno La Leo.

Nawatakia nyote Pasaka Njema!
Maggid,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment