Sunday 31 March 2013

Re: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA

Madam Kiwasila,
Umeeleza mambo mengi sana hapa chini na daima umekua ukieleza. What is the root cause ya haya mambo haya yote? Kwanini madam leo tusikubaliane kua gvt imeshindwa jukumu la kuongoza hii nchi?? Kumbuka ni serikali ndio imetunda hizo sheria na ina machinery mbalimbali za ku-enforce hizo sheria. Lakini nchi imekua kama haina mwenyewe. Sina hakika kama ulisikia kisa cha Tegeta cha wananchi kubomolewa nyumba na mfanya biashara wa mafuta. 

Mfanyabiashara alikua anajenga petrol station akaona nafasi yake ni ndogo. Alichokifanya alianza kuwalazimisha majirani wamuuzie nyumba iliapanue eneo. Wenye nyumba wakakataa, alitaka kununua nyumba kumi akajipangia bei kua kila moja atalipa 10 mill. Wenye nyumba wakakataa. Walipokataa akakodisha mabaunsa na kwenda kuzivunja zile nyumba kwa nguvu, ilitokea tafulani kubwa. Madam tukio kama hilo  maaana yake nini? Lina ashiria nini? Kwangu naona niishara kua anajua nguvu ya seriakali na udhaifu wa vyombo vya usalama ndio maana hakuona shida kutenda ule unyama. Shida ya nchi hii ni uongozi. 
Alexander


From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, March 31, 2013 10:33 PM
Subject: Re: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA

Daima husema 'Mtanzania anahitaji kitu fulani kimsaidie kuwapa Mental Revolution ili aweze kubadilika.' Tuna macho ila tu vipofu, tuna masikio ila tu viziwi, tuna viuongo vyote vya mwili lakini tu vilema tumepooza.

Katika jengo lililoanguka aliyekuwa akichakachua ratios naye huenda kafukiwa na innocent others. Mifano ya kuanguka maghorofa nchini na nchi jirani (kenta) ipo tunaona na kosa linajadiliwa lakini bado inaendelea. Tunachakachua uhai wetu kwa kupitisha vibali vya kujenga aina hii ya mbanano inayoonekana leo mjiji dar ya maghorofa kuzuka hovyo ahta squatter areas.
Waliporuhusu wajenge ghorofa 10 tu, hawakuona hao wasimamizi na wakaguzi hata walipopita njia tu kama 10 zinaongezeka na kuendelea kupanda kufika 16? Monitoring yao inakuwaje?

Wanapita njia mawaziri, viongozi wakurugeni wanaona jengo mfano eneo la victoria linajengwa lakini linachukua eneo la road reserve. Wananliona mpaka linakamilika. Njia yao kuu ni hiyo. Nawayaona maghorofa uchwara yanavyozuka mwenge bus stand-wanaangalia. Unaambiwa wanajenga eneo la ofisi ya CCM. Hivyo hao wote wapo plot ya CCM wapangaji wanatoa ushuru. haribu mradi tu unatoa ushuru. Hii ni sera mbaya. Vipofu. Baadae-waje kuwabomolea izuke zahama.

Wahusika na sheria wanaona kabisa kuwa baadhi ya wapangaji wa nyumba za NHC Jangwani, Upanga, Kariakoo, Oysterbay, Posta etc Mjini hapa wamefanya extension katika hizo nyumba za maghorofa na kufungia maduka, migahawa. Kwingine wazeziba kuta wamefunga mapito na kuweka viduka. Jee, sheria inaruhusu mpangaji kubadili design ya nyumba aliyopanga? Wanaona bali tu vipofu

Ukimlaumu kiongozi ni lawama upande mmoja haisaidii kitu kwani anapojenga na kubananisha njia, kuziba mapito; kuongeza vyumba na kubana nafasi zilizowekwa kati ya maghorofa za kucheza watoto wote wakazi si tupo hapo? Mbona hatuandamani kama tunavyotaka kuandamana kwa wanafunzi kufeli mtihani wa form four wakati wakitoka nyumbani ni sisi wazazi tuwanunuliao simu za kuongea nao nao wanakesha ktk facebook darasani, nyumbani TV hadi manane sio kusoma kwa bidii.Walimu wakiwachapa fimbo-tunavamia shule na kutandika viboko wazazi eti wanawaonea watoto. Inafika hata wanafunzi kuvamia nyumba za walimu na kuwabaka na mzazi kutolea mtoto huyo mbakaji dhamana. Maadili hayo?

Kama ni kuzama meli au boti baharini iwe kosa za kiongozi-jaribu kusafiri majini kwa boat au meli uone tulivyo wabishi kuacha kupanda kuwa meli au mtumbwi umeshajaa. hakuna anayetaka kuacha kupanda hawezi kusubiri mtumbwi uende urudi. Boat inalala upande mmoja na watu kukupa maji na kuisaidia kwa miguu. Meli inajaa mpaka hata pa kukaa hakuna hataki wa kusubiri ya baadae. Tunaona hatari hizi bali wabishi kufikia hata kujificha uvungu wa mizigo wakaguzi wasiwaone wakisha kukagua ndio wanatoka. Kufa tunakuona na kusikia lakini tu viziwi. Panda meli, boat uone haya yasemwayo. Hata ndege wakibananisha abiria na watoto wakubwa kupakatwa na wanajua huko juu agani ni hatari kuwa overloaded. Unabambikiziwa mzigo si wako kwenye ticket yako. atoae mzigo nna apokeae mzigo na huyo anayeogopa kusema kuwa anabambikiziwa mzigo si wake wote wakosa.

Danganya toto nchini ni nyingi. tunalia ajira na makampuni ya nje kuchukua kazi za kuweza kufanywa na wananchi. lakini kampuni ya kibongo ikipewa majengo ya shule ya msingi, chuo kujenga-yanabomoka kabla haya ya kukabidhiwa. Barabara ni hivyo hivyo mwisho kampuni kufungiwa. mamilioni kutolewa tena mkopo toka nchi za nje, lami kuwekwa vumbi na barabara mpya kusombwa na mvua. Kisha-lawama eti makampuni ya Kichina, Japan etc kuchukua kazi za wabongo ambao kuchakachua ndio jadi na mental happiness. Awe bilionea muda mfupi kwa kufanya ujenzi chini ya kiwango, mihela akajenge mahoteli na kuwa na magari ya kifahari. Anawapa rushwa wahusika kazi anachakachua. Watamfanya nini na wakithubutu atatoa SIRI nao wataipata? Hivyo kunakuwa hakuna kuchukua hatua maana wamelamba fweza wataadhirika.

Hebu angalia ujenzi wa Mlimani City DSM-kampuni ya NOREMCO ilivyojenga mjengo wa kutokuharibu ardhi kwa kuchimba chini kuondoa udogo bali kujenga ntumba bila kuharibu mazingira kwa kuiweka nyumba kwa kuishonelea kuu ya ardhi. Nyumba za hapo zina nyufa? Mbona madhubuti jengo za supermarket na nyumba za kupangisha kuishi watu.

Mtu unajiuliza-mafuriko yamemtia hasara miaka yote, kapewa kiwanja mabwepande kakiuza; sasa wamepewa mabati na simenti-watauza. Kutokana na tabia hii inayojulikana, kwa nini serikali  isimpe mkandarasi aliyejenga nyumba za NHC za bei ya chini akawajengwa kule mambwepande akaipa kila familia nyumba yake kisha familia ilipe kiasi kilichobaki kidogo kidogo baada ya kutoa hayo mabati na mifuko ya simenti mia kila familia. Maana cement itaolowa mvua, itauzwa pamoja na vifaa vingine watasema-kuganga njaa? Mpe hiyo low cost house sio vifaa? hatuoni akili na tabia za mbongo?

Wakati mwingine issue ni kusimamisha ujenzi mara unapoonekana kuendelea mahala sipo au kuonekana una mashaka, sio kungojea uishe kuja kubomoa au libomoke ila mhusika akomoke kuingia ile gharama. Gharama ya kuuua na kukoza nyumba iliyobomoka ni ya mwenye nyumba au mkandarasi pekee. Na inapokuwa mmoja wa wamiliki washiriki  ni NHC-inakuwa ni aibu ilioje. Hata wewe NHC kukuwa mwangalifu. Ghorofa 10 inakuwa 16 nawe umo?

Tunategemea wenzetu toka nje kutusaidia kuokoa, lakini tunaona maafa yanavyotushinda kuyakamili itokeapo dharura kama kuokoa majini na kufukua waliopata ajali ya kuangukiwa jengo. Lakini tukimaliza kufukua-tunasahau. unapata mental fatigue. Hatuchangishi mamilioni toka akina wema wala Sabodo kuwreza kununua vifaa vya kuokolea. Ukichangisha vya kisiasa utapata. Lakini cha kuokolea-tabu kidogo. Mungu atusaidie na kutufunua macho.

--- On Sun, 31/3/13, Mwahija Juma <mwahija_juma@yahoo.com> wrote:

From: Mwahija Juma <mwahija_juma@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 31 March, 2013, 11:27

Akifanya majumuisho katika hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwamwaka 2008/09. Waziri Mkuu alizungumzia jinsi tume ya Lowassa ilivyofanya kazikatika sakata la ghorofa kuanguka jijini Dar es Salaam.

Pinda alilithibitishia Bunge kuwa zaidi ya maghorofa 100jijini Dar es Salaam yalibainika kuwa yalijengwa kinyume cha taratibu za ujenzi.Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa,kati ya maghorofa 505 ambayo waliyakagua, 147 yalikutwa hayana nyaraka zaujenzi.

Lowassa aliunda tume baada ya jengo la Hoteli ya Chang'ombe Village Inn, Keko,Dar es Salaam kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.Ilidaiwa kwamba ulikuwapo ukiukwaji katika ujenzi wake.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa, ilibainikuwa ukaguzi huo, pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi hukumaghorofa mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bilakuzingatia sheria za ujenzi pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji wakiwamowahandisi wa manispaa husika.


1.Pinda asemebaada ya kukabidhiwa ripoti hii alimwajibisha nani tangu 2008 hadi sasa?
2.Watanzaniatupo tayari kuletewa danganya toto ya Tume nyingine ikalete majibu yaliyoko kwaPinda mezani?
3.Kwa Uzembehuu, Pinda ameshiriki kwa kuwa hawakuwawajibisha waliojenga kinyume nautaratibu hadi watanzania wengine wakafa. Zamu hii hata akilia anahusika!
4.Tangu tumezianze kuundwa kuhusu maafa ni akina nani walichukuliwa hatua. – Tangu MVBukoba hadi Tume ya matokeo ya Kidato cha Nne.
5.Watanzania Tumechokakuneemesha mifuko ya wajumbe wa Tume, na kufilisi rasilimali zetu. PINDAAJIUZULU.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment