Thursday 28 March 2013

RE: [wanabidii] HADITHI YA PANYA!

Hii hadithi nimeisoma mara nyingi sana. Ingawa inatofautiana kidogo na hadithi niliyoisoma, mantiki inabaki pale pale kuwa, MTEGO WA PANYA HUINGIA NA WASIOKUWAMO.

Panya alianza kumwomba msaada nyoka kwa kuwa anatambaa akamtolee mtego uvunguni. Nyoka akakataa.

Panya akamwomba msaada jogoo. Jogoo akakataa.

Panya akamwomba msaada mbuzi. Mbuzi akakataa. Vivyo hivyo kwa ng'ombe.

Wote, nyoka, jogoo, mbuzi na ng'ombe walikataa kwa kudai huo ni mtego wa panya tu wao wala hauwahusu hata kidogo. Panya alikuwa akiwajibu kuwa, mtego wa panya huingia na wasiokuwamo.

Akaanza nyoka katika pitapita zake akanaswa. Binadamu akivyosikia kukurukakara akajua panya kanaswa. Kwenda kuangalia nyoka akamuwahi kumgonga katika kujihami.

Binadamu akakimbilia kwa mganga. Mganga akasema ili upone lete jogoo tumchinje. Jogoo akakamatwa akachinjwa. Mtego wa panya huingia na wasio kuwamo.

Hali ikawa mbaya. Binadamu akafariki. Siku ya kwanza wakaja wageni wachache. Akakamatwa mbuzi akachinjwa.

Siku ya pili watu wakaongezeka. Ng'ombe akachinjwa.

Kila aliyekuwa akipatwa masahibu hayo kuanzia nyoka hadi ng'ombe, panya alikuwa kando akiwacheka kwa kuwaambia kuwa, mtego wa panya huingia na wasiokuwamo.

Ni hadithi yenye falsafa ya juu sana. Viongozi hudharau matatizo ya watu wakisahau na wao huingia.

Kuna afisa mwajiri kwenye sshirika moja la umma alikuwa hapeleki michango NSSF. Wastaafu wanahangaika kweli kweli. Akasahau kuwa mtego wa panya, huingia na wasiokuwamo. Naye siku moja akastaafu. Akateseka vile vile.

Sent from my Nokia phone
-----Original Message-----
From: Hildegarda Kiwasila
Sent: 29-03-2013 05:36:24
Subject: Re: [wanabidii] HADITHI YA PANYA!


Hii Kali!! Inafundisha. tatizo ni uafrika wetu.

Na ndio maana unaona katika jamii-baba amebaka mwanae na imethibitishwa kutokana na maeleo ya mtoto, matukio na hata akaweza umwelezea maumbile yale ya siri (sio hiyo DNA tu maana haitopimwa si hakuna wa kugharimia!)-ukoo wa mume/baba mbakaji pamoja na mke wa mbakaji (i.e. mama mzazi wa mtoto) wakamtoa baba kwa dhamana kisingizio-lishe. nani atalisha familia ya baba mbakaji kama atakaa rumande kisha kufunga miaka 30 au 35. Hawajali sheria, haki za binadamu na za watoto. Katoto kamelawitiwa na jirani-wanaficha siri na kuchukua hela. Siri ni kulinda hadhi ya familia. katoto kamechukuliwa kwao na kuletwa mjini DSM katika danguro, kameonyesha na danguro, kametoa na matukio ya waliomfanyia uchafu hadi polisi alikopelekwa na kutendewa uchafu-hawakamatwi na kulazwa ndani, danguro chumba kimefungwa polisi walipofika mwenye nyumba kagoma kufungua kumbe ndani huko kafungia visichana-tunasoma mlango haukufungwa baada ya muda tunasoma magazetini danguro linaendelea.

-Tunaona ktk TV DSM Mifugo ilivyozagaa barabarani na kusababisha ajali. Ming'ombe mikubwa unapishana nayo mjini inachungwa kando ya njia na wahusika wa vyombo vya usalama na sheria wanapita wanaona-wanakula jiwe. Wanakula jiwe hivyo hata wanapowaona wazezagaa katika state and donor financed irrigation schemes za kuondoa njaa na hata kwenye catchment areas ambazo ndio tegemezi la maji vijijini na mijini. Wanakula jiwe. Misitu inaharibiwa kwa ukataji miti, ufugaji na uchimbaji madini. Kisingizio-wanaganga njaa kwani viongozi wa CCM mafisadi. ila madhara ni ya kitaifa au makubwa kama hivyo sumu ikamuua mweyenyumba, ikabidi hao wengine wote waliokataa kumsaidia panya wachinjwe. Ndivyo tunavyocjinja maji for hydropowe, umeme tatizo, tunachinja viwanda, hoteli na uzalishaji mwingine hata elimu na kazi madarasani kwani bila umeme na alternative power vyuoni, hospitali, mashule hakuna elimu wala kazi ya maana. Kwa nini tusihamasishe ufugaji na kilimo endelevu na
kuondoa kuzagaa mifugo mijini na vijijini bali tuzingatie uchumi kwa carrying capacity?-Utapataje KURA usipowaachia huru wafanye watakavyo? Lakini hivyo sumu inayotokea ktk uharibifu wa mazingira na sumu hasa za mecury na cynaide twanywa wote hadi mijini tu mazombi watarajiwa.

-Wapo mabondeni, wanajenga, wanazuia mapito natural ya mto-tunawaangalia. Kila mmoja anazungusha kuta atakavyo hajengi kuwacha uwazi wa kupita maji. Mvua ikija maji hayana mapito yanatengeneza mapito yake yenyewe, kujaa barabarani na kupita ndani ya majumba kuua na kuharibu mali. Tunamwona anavyojenga, tunamwacha tuje kumkomoa kubomoa baadae. Ukienda kubomoa-anakwenda mahakamani kupata kizuizi na case haiishi miaka na ni gharama kwa taifa. Wanakindua mawe ya barabarani yanayoonyesha mita 30 au 60 za mwisho wa barabara na ujenzi-twaangalia. maghorofa makubwa yanajengwa hata mijini yanachukua road reserve. Kwa nini unaachia linaendelea kujengwa uje uingie gharama ya kubomoa? Wanabomoa DSM Kawawa Road lakini yapo maghorofa yaliyochomoza barabarani na ni mapya. Twaogopana. Watajiju. Matokeo yake ni vita-wananchi wanaonewa na serikali. Usitetee uovu kwa visingizio. Tuzingatie sheria kwa kuuzuia kama vile unahakikisha nyumba yako imejengwa vizuri ili panya na
nyoka wasiingie kuleta matatizo.

-Kwani-wanapofanya maandamano na wali waliokeketwa na SARRO ikaendelea kila kipindi chake kinapofika na baadhi ya watoto wakakamatwa kwa nguvu (eti mzazi hakupenda lakini mkeketaji hakumfikisha mahakamani) picha za wali wenye mpako wa unga usoni twaziona mitandaoni na magazetini-wanasheria, police, Diwani, Mbunge wao yupo wapi?-Hiyo ni mila yao au yetu tuachieni wenyewe. hayo yao-watajiju.
 
-Mabango ya waganga kutoka Nigeria, Congo etc yapo barabarani; yapo magazetini tunayatoa. Kweli gazeti linadiriki kutangaza Imani za Kishirikina, gazeti la wasomi na watu wa dini, kupoteza jamii-Mganga Kiboko kutoka Nigeria (kafikaje TZ ana kibali cha uhamiaji?) Pesa za majini, ndoa ya haraka kumvuta mchumba aliyembali/hakutaki utampata kwa masaa matatu (3hrs-hata awe London?); Pete ya bahati na mali, cheo, akili darasani na kupasi mitihani; kukuza biashara; kutengeneza shape kupunguza matiti, kitambi, uzito, mafuta mwilini (bila ya mazoezi ya kukimbia na kuacha kula hovyo!); kuongeza (nanihii) ili urudie mara...; pesa za kuzimu. Anatibu kwa simu. Namba ya simu imewekwa. Hili ni gazeti la msomi/wasomi watanzania, wazawa. ambao wao huangalia kuganga njaa tu sio maadili, utu na utaifa. Kisha ndio haya haya magazeti yanayolaumu kuporomoka kwa maadili, kufeli wanafunzi, umasikini kukithiri, kutoa taarifa za kizee kuuawa kwa kushukiwa uchawi na mtu kukutwa na
fuvu la kicha na maboksi matupu kadhaa aliyoambiwa na mganga aweke ili yajae fedha kutoka kuzimu au majini. Baraza la Utamaduni lipo wapi? Chama cha Waganga Tabibu kipo wapi? Chama cha Waandishi wa habari na waziri wake wapo wapi magazeti yafanye hivyi? au ndio ile ya kututangazia Digitali tukaenda mkiki mkiki sasa hela imegota haiingii tunatakiwa turudi analogi? na haya matangazo ya hela za majini na za mizimu yataongezeka ili kuganga njaa.

Kundi hili la panya, paka, ng'ombe, mbuzi etc ni sisi Watanzania wa makabila mbali mbali, dini mbalimbali, mila na elimu tofauti, uchumi tegemezi tofauti ambapo tunatakiwa kuweka mwelekeo mmoja wa maendeleo, kupendana, kusaidiana ili kuishi kiendelevu kama Taifa moja.Mmoja si bora kuliko mwingine.

Labda, hizi si hadithi ya panya iwe pia hadithi kama ya yule Samaki yule mwenye mdomo mrefu kama mkuki (Nduaro) aliyewekwa kwenye hela yetu senti 5 zamani ambaye huruka na kuchoma kitu kwa mdomo wake ulio kama mkuki kisha akanasa huko yeye mwenyewe akakamatwa, akachinjwa, akaliwa. TUNAJIMALIZA wenyewe kwa baadhi ya matendo yetu yasiyo mema. Tunajikaanga kwa kutokuchukua hatua husika kutegemea kujenga sio kuziba ufa. Na huu udini na mauaji yanayopikwa kwa nia fulani-ndio sumu kubwa kama ile ya nyoka.

From: Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] HADITHI YA PANYA!
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 28 March, 2013, 18:34

Siku moja Panya aliona mtego wa Panya uvunguni mwa kitanda cha Mwanadamu. Akahisi hatari. Panya akamwendea rafikie Kuku/Jogoo na kumwambie. Rafiki maisha yangu ya hatarini maana kuna mtego. Tafadhali nisaidie kuutegua. Jogoo akasema hiyo ni hatari yako mwenyewe. Utajiju. Pole sina nafasi.

Panya akamwendea rafikie mwingine Mbuzi. Mbuzi akasema we, tangu lini nikaingia uvunguni? Panya akasema wewe ni mkubwa unaweza tumia hata fimbo ukategua?
Mbuzi akasema nenda zako Bwana. Sina muda huo.

Panya akamwendea Ng'ombe kwa shida yake. Ng'ombe akamcheka akasema mie naweza ponda pomba kitanda na hata hako kamtego. Lakini sitaki. Hatari ni kwako tu. Omba Mungu uwe na umbo kubwa kama mimi. Ndipo utasalimika. Sisi wakubwa hakuna hatari kama yako.

Panya akakwama kila upande.

Katika hali hiyo; nyoka mwenye simu akaingia ndani mwa Mwanadamu akiwinda panya yule yule. Kwa bahati mbaya, akanaswa mkiani kwenye mtego. Akawa anatapatapa. Mwenye nyumba akaja bila kujua akaketi kitandani. Katika kujihami Nyoka akamgonga Mwanadamu. Kwa vile alikuwa na sumu kali mwanadamu akafa pale pale.

Mipango ya maziko ikaanza. Siku ya kwanza walikuja watu wachache. Jogoo akachinjwa. siku ya maziko wakaja watu wengi; Mbuzi akachinjwa. Na siku ya kuondoa Matanga wakaja watu wengi zaidi. Ng'ombe akachinjwa.

Kumbe Panya akaishi na waliokataa kumsaidia wote wakafa.

Swali la kujiuliza, je Jogoo au mbuzi au ng'ombe wangemsaidia rafiki yao Panya wangefikwa na Mauti? Jibu unalo.

Serikali imeambiwa na kila mpenda amani kuwa ifanye kitu. Ina uwezo wa kuondoa matatizo yanayokabili wananchi wake, hususani suala la usalama. Kuna
wakorofi wachache na ina uwezo wa kuwathibiti. Serikali aidha inakaa kimya au inadharau. 

Nadhani sasa wanangoja nyoka wa sumu. Atawaletea madhara makubwa.

Mwisho wa hadithi.


Kessy




--

Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com

International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

 

 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment