Friday 29 March 2013

[wanabidii] 'Njiani Kwenda Kwa Rais!'-3

' Njiani Kwenda Kwa Rais!'- 3

Ndugu zangu,

Jana nilimalizia kwa kuandika haya; "miezi michache tu baada ya tukio lile Ubalozini, marafiki wawili; Julius na Oscar walifunga safari ya kwenda China. Ilikuwa ni mara yao ya kwanza kwa wote wawili kwenda China.

Huko China Julius na Oscar waliiona China kwa ' miwani tofauti'. Ni nini kilitokea kwa marafiki wawili hawa, Oscar na Julius, waliporudi nyumbani?" – Endelea na simulizi hii.

Ndugu zangu,

Hakika, sikufikiri kuwa simulizi hii ingewavutia wengi hivi. Nami nimehamasika kusimulia zaidi. Na hapa ieleweke, kuwa ninapomsoma Mwandishi Stig Holmqvist nalinganisha pia anachokiandika na yale yaliyopatwa kuandikwa na kusimuliwa na wengine. Yale ambayo hata mimi utotoni nimepata kusimuliwa na hata kuyaona. Hivyo, nafanya uchambuzi wa jumla. Msije basi mkashangaa nitakapowarejea waandishi wengine hata yale ambayo mimi mwenyewe nimepata kuyaandika huko nyuma.

Mathalan, wale waliotaka kujua kama kitabu cha Holmqvist kinapatikana kwa lugha ya Kiingereza, jibu lake ni hapana. Lakini, mengine anayosimulia Holmqvist unaweza pia kuyapata kwa lugha ya Kiingereza kwenye vitabu vya waandishi kama ( The Critical Phase in Tanzania 1945-68:Nyerere and the Emergence of a Socialist Society, Cranford Pratt ) , ( Nyerere of Tanzania, William Edgett Smith) na hata( The Dark Side Of Nyerere's Legacy, Ludovick Mwijage) Hiki kimepigwa marufuku.

(Ninanavyo vitabu hivyo na vinginevyo kwenye maktaba yangu kwa anayetaka kuniazima)

Tuje basi kwenye mwendelezo wa simulizi hii;

Kama inavyoonekana kwenye maandiko ya Stig Holmqvist, kuwa Oscar na Julius waliiona China kwa miwani tofauti.

Julius aliona nini China?

Julius alivyutiwa sana na ... Soma zaidi..http://mjengwablog.co.tz/siasa/item/1905-njiani-kwenda-kwa-rais-3.html#.UVVoUTdafx0

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment