Sunday 31 March 2013

[wanabidii] RWAKATALE: Kesi au Mbinu za Kuzima Mjadala wa Elimu na Udini?

Bandugu,

Kwa uzoefu wangu, mara nyingi likuwepo jambo kubwa linalozua mjadala wa kitaifa kiasi cha kuitetemesha Serikali; katika mazingira ya kutatanisha; huwa linajitokeza jambo jipya kubwa na kwa kasi kiasi cha kufunika lile lililopo kwa wakati huo.
Taratibu akili na mawazo ya watu uhamishwa moja kwa moja katika suala jipya.

Tuliona kasi ya EPA, Richmond na hata namna alivyozuka Baabu wa Loliondo..ni kama mchezo fulani ambao unabuniwa kwa umakini ili kupunguza kasi kama sio kabisa kuzuia mijadala muhimu ya kitaifa.

Ndivyo ninavyolitazama pia hili katika jicho la pili kuanzia kwa tukio la kujeruhiwa AK na hadi keso ya Rwakatale.

Haya masuala ambayo kimsingi yamefanikiwa kuzima vuguvugu la mijadala iliyopamba moto ya kidini na tatizo zima la elimu linaloikumba nchi.

Kimsingi yote haya ni muhimu katika mstakabali mzima wa ustawi wa nchi na sisi tuna haki ya kujua linaloendelea.

Yanapojitokeza matukio mapya na kuyafunika yale mengine tunalazimika kufikiria katika mtazamo kama huu. Tunahitaji kupata taarifa ama mrejesho kamili wa masuala tete kama hayo yanayoendelea nyuma ya pazia baada ya kuwa yamefunikwa na matukio mapya.

Katika mjadala mmoja huku mtaani niliwahi kusikia kuwa hapa kwetu mara nyingi huwa tinataarifiwa juu ya kukamatwa madawa ya kulevya lakini huwa hatutaarifiwi matokeo ya kesi za wahusika hawa.

Tunaomba haya ya kitaaluma na udini yasifunikwe kwa stahili hii ya kutengeneza mambo mapya. Tupewe majibu ya nini kinaendelea.

Ni mtazamo wangu lakini..nina mashaka na kesi hii na matukio ya kabla yake na mkakati mzima wa kuzima mijadala muhimu ya kitaifa.

Hii inaweza kuwa hujuma ya Makusudi kwa Upinzani katika kuibua na kufuatilia mambo ama masuala mbali mbali ya kitaifa.

Tafakari

Ireneus

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment