Wednesday 27 March 2013

RE: [wanabidii] Katiba Mpya: Maoni ya CUF

maoni ya katiba yakiwa na sura hii ni poa,kwan hakutakuwa na misuguano isiyo ya lazima..mambo ya ajabu ajabu yenye kuzingatia maslah ya makundi fulani iwe ni marufuku ktk katiba mpya hata kama yametolewa na wengi.ngupula



------------------------------
On Wed, Mar 27, 2013 15:05 EET Mobhare Matinyi wrote:

>
>Kwa kuipitia haraka haraka ina maono mazuri kwa nchi yetu.
>
>
>
>
>> Date: Wed, 27 Mar 2013 04:57:18 -0700
>> Subject: [wanabidii] Katiba Mpya: Maoni ya CUF
>> From: fkarume@gmail.com
>> To: wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Chama cha CUF kipo tayari kutoa ushirikiano unaostahiki kwa Tume
>> katika kipindi chote cha mchakato huu pamoja na kushirikiana na
>> Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa na tofauti nyinginezo,
>> kuhakikisha kuwa kwa pamoja nchi yetu inakuwa na katiba bora yenye
>> kukidhi haja na matakwa ya hali ya kisiasa, kiuchumi na ustawi mwema
>> wa jamii ya Watanzania.
>>
>> UTANGULIZI
>>
>> Kwa niaba ya The Civic United Fronf (CUF-Chama Cha wananchi), na kwa
>> niaba yangu binafsi napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe
>> Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
>> Tanzania pamoja na wajumbe wako kwa kutualika rasmi Chama Cha CUF
>> mbele ya Tume yako kutusikiliza na kupata maoni ya chama chetu juu ya
>> mchakato huu muhimu kwa mustakbali mwema wa Taifa letu la Tanzania
>> pamoja na watu wake.
>>
>> Aidha, tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya
>> Mrisho Kikwete kwa kuanzisha mchakato huu wa mapitio makubwa na
>> kukusanya maoni ya katiba ya nchi yetu ili ikidhi matakwa ya wakati wa
>> sasa na kutupeleka mbele zaidi kwa ustawi wa Taifa letu na watu wake.
>> Madai haya ya kuandaa mchakato wa kuwa na katiba mpya inayokidhi
>> matakwa ya wakati tulionao ni madai ya msingi ambayo chama chetu cha
>> CUF kimekuwa kikiyasisitiza tangu kurejeshwa tena kwa mfumo wa
>> demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini mwaka 1992 na mara zote
>> kuainisha suala hili katika manifesto zake za uchaguzi.
>>
>> Kutokana na muongozo wa Tume ya Mabadiliko ya katiba maoni yetu
>> yamejikita katika maeneo yafuatayo; Misingi na Maadili ya Kitaifa,
>> Madaraka ya Wananchi, Muundo wa Nchi na Taifa ndani ya Jamhuri ya
>> Muungano wa Tanzania, Haki za Binadamu na Wajibu wa Wananchi, Ardhi,
>> Maliasili na Mazingira, Mihimili ya Nchi (Ardhi, Watu na Utawala),
>> Mihimili ya Utawala (Serikali, Bunge na Mahakama), Muundo na Mamlaka
>> ya Serikali za Mitaa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
>>
>> Kwa muhtasari maudhui haya Chama Cha Wananchi CUF kinapendekeza
>> yafuatayo katika mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
>> Tanzania:
>> 1. Muundo wa serikali tatu za muungano yaani serikali ya Zanzibar,
>> serikali ya Tanganyika na serikali ya Mungano.
>>
>> 2. Uanzishwaji wa Tume huru za uchaguzi mapema iwezekanavyo. Kwa kuwa
>> Tume ya uchaguzi inapaswa kuanza kazi zake mapema ili kufanikisha
>> uchaguzi wa mwaka 2014/15, Tume haiwezi kusubiri mabadiliko ya katiba
>> yakamilike ndio ianze kazi zake kwa Muundo mpya utakaopendekezwa.
>>
>> 3. Katiba yenye misingi ya mfumo wa uwajibikaji kwa watendaji wote wa
>> umma na uainishwaji wa wazi wa Dira ya Taifa.
>>
>> 4. Katiba itakayotoa haki kwa wagombea binafsi kushiriki katika
>> uchaguzi.
>>
>> 5. Katiba itakayotoa uhuru wa vyama vya siasa kuungana muda wowote
>> vitakapoona inafaa bila kupoteza usajili wa kawaida wa vyama hivyo.
>>
>> 6. Katiba itakayoweka muundo wa kuwa na Rais mtendaji "Executive
>> President" mwenye madaraka yanayopimika na kukubalika yasiyobana wala
>> kuingilia au kuondoa uhuru wa utendaji kazi wa mihimili mingine ya
>> dola. Rais achaguliwe kwa kupata asilimia 50+1 au zaidi ya kura
>> zilizopigwa.
>>
>> 7. Katiba yenye kuweka mfumo sahihi wa kulinda rasilimali za Taifa na
>> kuhakikisha zinawanufaisha Watanzania wote kwa haki na usawa.
>>
>> 8. Katiba itakayompa kila Mtanzania kwa nafasi yake kushiriki katika
>> maendeleo ya nchi yake kwa kuwa na muundo wa serikali
>> itakayoshirikisha kila Mtanzania mwenye uzalendo wa kweli na uwezo wa
>> kutoa mchango wake kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa taifa.
>>
>> 9. Katiba itakayoweka muundo wa uwakilishi wa uwiano (propotional
>> representation) ili kila kura itakayopigwa kuwa na thamani tofauti na
>> utaratibu wa sasa wa mshindi kuchukua vyote (winner takes all) hata
>> kama ameshinda kwa kura moja.
>>
>> 10. Katiba itakayo hakikisha uwepo wa mgawanyo wa madaraka kati ya
>> serikali kuu na serikali za mitaa kwa kuondoa mfumo wa kuziburuza
>> serikali hizo zilizokaribu na wananchi. Wilaya zisianzishwe kiholela.
>> Vigezo vya halmashauri ya wilaya, miji, manispaa na majiji vitawekwa
>> na sheria. Utawala wa mikoa uondolewe.
>>
>> 11. Katiba itakayoweka msingi wa kuzuia ufisadi mkubwa wa rasilimali
>> za nchi hasa kwa njia ya uingiaji wa mikataba, Bunge likiwa ni chombo
>> cha uwakilishi wa wananchi lazima lishirikishwe.
>>
>> 12. Katiba itakayoweka Muundo wa Tume huru za Taifa za uchaguzi tangu
>> ngazi ya uteuzi wake kuanzia ngazi ya Taifa hadi ngazi ya chini.
>> Katiba itakayotoa fursa matokeo ya uchaguzi kwa ngazi zote kuhojiwa
>> mahakamani ikiwemo matokeo ya uchaguzi wa Rais.
>>
>> 13. Katiba itakayopambanua mgawanyo wa madaraka na mamlaka ya mihimili
>> yote mikuu katika nchi kwa maana ya Bunge, Serikali na Mahakama.
>>
>> 14. Katiba itakayoeleza wazi kuhusu haki na wajibu wa dola kuhakikisha
>> elimu ya watoto wetu, matumizi ya rasilimali za taifa, huduma za
>> msingi za afya, ulinzi wa nchi yetu na sera za ardhi na kilimo
>> zinasimamiwa na kutekelezwa kwa manufaa ya wananchi wote. Katiba ndiyo
>> yenye nafasi ya kulinda haki hizi za mwananchi na si huruma ya mtawala
>> atakaye kuwepo kwa wakati huo au chama cha siasa. Sera za kitaifa
>> lazima zifuate na kuheshimu haki zilizoainishwa ndani ya katiba.
>> 15. Kuhakikisha kwamba wananchi wana madaraka ya kujiamulia wenyewe
>> masuala ya maendeleo yao kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
>>
>> 16. Katiba yenye kulinda haki za binaadamu, na kupinga aina zote za
>> ubadhilifu, ukandamizaji, ubaguzi wa aina yeyote iwe wa kidini,
>> kikabila, kijinsia au kikanda.
>>
>> 17. Katiba yenye kuweka misingi endelevu ya kulinda amani ya nchi
>> yetu.
>>
>> 18. Masuala ya Ardhi yawe na sura kamili katika katiba mpya. Ardhi ni
>> mali ya Watanzania wote. Mtanzania peke yake ndiye anayeweza kumiliki
>> ardhi moja kwa moja.
>>
>> 19. Katiba inayohakikisha kuwa haki za msingi za makundi maalum,
>> wanawake, watoto, wazee wasiojiweza na walemavu zinalindwa kwa
>> kuainshwa ndani ya katiba.
>>
>> Chama cha CUF kipo tayari kutoa ushirikiano unaostahiki kwa Tume
>> katika kipindi chote cha mchakato huu pamoja na kushirikiana na
>> Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa na tofauti nyinginezo,
>> kuhakikisha kuwa kwa pamoja nchi yetu inakuwa na katiba bora yenye
>> kukidhi haja na matakwa ya hali ya kisiasa, kiuchumi na ustawi mwema
>> wa jamii ya Watanzania.
>>
>> Ni matarajio ya Chama Cha Wananchi CUF kuwa maoni haya yatazingatiwa
>> na kuingizwa katika rasimu ya mabadiliko ya katiba kwa mjadala na
>> hatimaye kufanyiwa maamuzi yanayofaa kwa mustakbali mwema wa Taifa
>> letu la Tanzania.
>>
>> Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
>>
>> HAKI SAWA KWA WOTE
>>
>> Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
>> Mwenyekiti wa CUF Taifa
>>
>> --
>> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
>> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>
>
>--
>Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
>International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to t

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment