Sunday 27 January 2013

[wanabidii] Ujumbe wa kuadhimisha leo Siku ya Ukoma Duniani

Jikabidhi kabisa kwa Mungu, atakutumia kutimiza mambo makuu kwa hali
ambayo utaamini zaidi kwamba ni Upendo wake dhidi ya Udhaifu wako.
– Mama Theresa
Siku ya Ukoma Duniani huadhimishwa Duniani kote kila Jumapili ya
mwisho ya mwezi Januari. Huadhimishwa ili kuongeza Ufahamu wa Ugonjwa
wa Ukoma (Leprosy/Hansen's Disease) .

Siku iliteuliwa ili kuwe ni Kumbukumbu ya Kifo cha Gandhi, Kiongozi wa
India aliyetambua umuhimu wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukoma.

Ukoma ni moja ya magonjwa ya zamani Duniani. Ni ugonjwa sugu
unaoambukizwa na vijidudu vya bakteria, unaathiri mfumo wa fahamu hasa
neva za mikono, miguu na uso.

Kwa zaidi ya Miaka 50, kila Jumapili ya mwisho ya mwezi Januari,
maelfu ya watu Duniani kote wameacha kuwakumbuka wale walioathiriwa na
Ukoma.

Mwaka 1953, M. Raoul Follereau wa Ufaransa alianzisha Siku ya Ukoma
Duniani kwa mara ya kwanza, ili kuleta hamasa kuwaangalia na kuwezesha
misaada kwa mamilioni ya watu waliothiriwa na Ukoma Duniani kote
katika zama hizi. Kwa miaka mingi, uangalifu umeongezeka na zaidi ya
nchi 100 hushiriki kwenye siku ya Ukoma Duniani, kila Jumapili ya
mwisho ya mwezi Januari.

Kwa karne nyingi katika nchi nyingi, Ukoma umefanya watu walioathiriwa
nao kutengwa na jamii zao kwakuwa haukuwa na dawa kwa ajili ya
matibabu. Watu walioathiriwa na Ukoma iliwabidi kuishi na ulemavu
unaosababishwa na Ukoma.

Siku ya Ukoma inasaidia kusimulia hadithi kwa watu wasiojua kuwa Ukoma
bado upo ila sasa unaweza kutibiwa. Siku hii husaidia pia kukusanya
pesa kwa ajili ya matibabu ya watu wenye Ukoma na utunzaji wao.

Tuungane kuadhimisha siku ya Ukoma Duniani, Jumapili ya Januari 27,
2013 na tusimame kwa ajili ya wale wanaoteswa na unyanyapaa kila siku.
Sisi ni ndugu, ni mwili mmoja, tusaidiane na kujaliana.

KUHUSU UKOMA
Ukoma ni ugonjwa ambao umekuwapo kwa karne nyingi sana tangu kipindi
cha biblia. Ni ugonjwa unasababisha majeraha katika ngozi, huharibu
mfumo wa neva na kudhoofisha mwili, matatizo huwa zaidi kadili muda
unavyokwenda.

VISABABISHI
Ukoma husababishwa na bakteria waitwao Mycobacterium leprae. Bakteria
hawa hukaa muda mrefu katika mwili kabla ya kutokeza dalili za
ugonjwa, kitu kinachosababisha ugonjwa ugumu wa kutojua ni wapi na ni
lini mtu alipopata maumbukizi. Watoto wako katika hatari zaidi ya
kupata ugonjwa huu.

MAMBO HATARISHI
Maeneo yenye ukoma sana huwa na hatari zaidi. Vitu vifuatavyo huongeza
hatari ya kuambukizwa mfano kulala kitanda kimoja na mgonjwa wa ukoma
asiyetibiwa, kutumia maji yaliyotumiwa na mgonjwa wa ukoma na ukosefu
wa lishe bora au ugonjwa wowote unaoshusha kinga ya mwili.

JINSI UNAVYOAMBUKIZWA
Wanasayansi bado hawajagundua jinsi hasa ukoma unavyoambikizwa. Wengi
wao husema bakteria wa ukoma husambaa kutoka kwa mtu mmoja mwenye
maambukizi hadi kwa mwingine kwa njia ya hewa. Haijagundulika kama
unaweza enea kwa njia ya ngono. Uchunguzi umebaini pia ukoma unaweza
kuambukizwa kwa binadamu na mnyama mdogo kama sungura anayejulikana
kitaalamu kama armadillos, anayepatikana sana Amerika ya kati na
Kusini.

DALILI:
-Kupasuka kwa ngozi au kuwa na mabaka kwenye ngozi. Mipasuko ya ngozi
huwa na rangi iliyofifia zaidi kuliko rangi ya kawaida ya ngozi ya
mwili wako. Mipasuko hupunguza nguvu ya kuhisi mguso, joto au maumivu.
Mipasuko haiponi haraka, inaweza kuchukua wiki kadhaa hadi miezi.
-Mwili kuishia nguvu.
-Mwili kufa ganzi hasa kwenye viganja, mikono na miguu.

VIPIMO:
Wataalamu wa afya hufanya uchunguzi kwenye maabara kwa kuchukua
mpasuko wa ngozi au kipande kidogo cha nyama cha mtu anaedhaniwa kuwa
na ugonjwa wa ukoma au kwa mgonjwa wa ukoma ili kujua ni aina ipi ya
ukoma inayomsumbua.

MATIBABU:
Tiba inapatikana bure kwenye hospitali zote za serikali ambapo
wagonjwa hupewa dawa za kuua bakteria na dawa za kuzuia na kupunguza
kuvimba kwa mwili.

Serikali pia hugharamia viatu maalumu kwa wagonjwa wa ukoma ili kuzuia
athari na kupunguza ulemavu utokanao na kuharibiwa kwa mishipa ya
fahamu, huduma za marekebisho ambazo ni pamoja na huduma za upasuaji,
viungo vya bandia, magongo na viti mwendo.

Kugundua ugonjwa mapema ni muhimu sana. Matibabu ya mapema huzuia
athari za ukoma, na kuzuia mtu mwenye ukoma kusambaza kwa wengine na
kumsaidia mtu kuwa na maisha ya kawaida.

ATHARI ZA UKOMA:
Mwili kuwa katika umbo la ajabu mfano miguu kuvimba sana, mwili
kuchoka, tatizo la kudumu la neva kwenye mikono na miguu, kupoteza
nguvu ya kuhisi vitu. Watu wenye tatizo la kudumu la ukoma wanaweza
poteza uwezo wa kutumia mikono au miguu yao kutokana na majeraha
kwasababu wanakosa hisia ya maeneo hayo mfano wanaweza kuungua moto
bila ya wao kujua.

MUDA GANI SAHIHI KUFIKA KWENYE HUDUMA ZA AFYA:
Fika kwenye huduma za afya pale unapopata dalili za ukoma hasa kama
umewahi kugusana na mtu mwenye ukoma. Dalili muhimu ni baka au mabaka
kwenye ngozi yasiyo na hisia ya mguso ambayo huambatana na ganzi
kwenye mikono na miguu.

KUZUIA:
Kujikinga na ukoma kunahusisha kutogusana na mtu mwenye ukoma ambaye
hakutibiwa. Pia watu walio katika matibabu kwa muda mrefu hawawezi
kusambaza Ukoma


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2JBJTtg4n

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment