Pamoja na mvua kubwa iliyonyesha Geita lakini tulifanikiwa kufanya mkutano wa ndani katika ukumbi wa kanisa katoliki Geita kama ambavyo ulipangwa. Mvua hiyo ilianza majira ya saa 8:45 hadi saa 10 alasili muda ambao wafanyakazi wengi walikuwa njiani kuelekea kwenye viwanja vya kanisa katoliki ambapo mkutano wa TAMICO ulipangwa awali ufanyikie. Hata hivyo baada ya hali ya hewa kubadilika tuliamua kuutumia ukumbi ambao ulihimili watu zaidi ya 250 walikuwa wameishafika kwenye mkutano. Mgeni rasmi, Mheshimiwa Suleiman Said Jaffo mbunge wa Kisarawe aliwahakikishia wafanyakazi hao waliohudhuria mkutano huo kwamba habari zilizosambaa migodini na kusababisha wafanyakazi kuacha kazi si za kweli kwani kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kuandaa mswada wa marekebisho kwa maelekezo ya bunge ili uletwe bungeni kwa kujadiliwa. Na kwa utaratibu mswada unatakiwa kusomwa mara mbili pasipo kujadiliwa na mara ya tatu ndio unasomwa na kujadiliwa na hatimaye unapitishwa na kusubiri Rais ausaini kuwa sheria na baada ya rais kusaini, waziri mwenye dhamana anautungia kanuni na kutangaza tarehe ya sheria kuanza kutumika kwenye gazeti la serikali. Kwa mchakato huo, hakuna ukweli wowote kwamba mswada uletwe kwenye kikao cha mwezi February 2013 na kuupitisha. Na hata kama mswada utapitia hatua zote hizo na bado serikali ikaweka kipengele cha fao la kujitoa namna ambavyo kinapigiwa kelele bado wabunge watakuwa na fursa ya kukipinga kwa kuzingatia hoja mbali mbali zilizokwisha wasilishwa na wadau katika nyakati tofauti zikipinga kipengele hicho kutokana na upekee wa sekta binafsi hususani migodi,NGO's na sekta zingine zenye changamoto zinazofanana na hizo. Pia alitoa angalizo juu ya wimbi la wafanyakazi migodini kuacha kazi ambalo limepelekea wafanyakazi zaidi ya 300 kuacha kazi katika migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu,Geita, North Mara,Tulawaka na Buzwagi katika kipindi kisichozidi miezi miwili. Mgodi wa Bulyanhulu ndio umeathilika zaidi ambapo wafanyakazi zaidi ya 200 tayari wameishaacha kazi na athali za uzalishaji tayari zimeanza kujitokeza.Alionya kama wimbi hili litaendelea la kuacha kazi kwa uvumi tu basi tutarajie nafasi hizo kuchukuliwa na wageni kutoka nje na kunyima fursa vijana wa kitanzania. Mwisho, aliahidi kuifanyia kazi hoja iliyoibuliwa kwenye mkutano ya ya black listing inayofanyw na waajiri migodini kumzuia mfanyakazi aliefukuzwa au kuachishwa kazi mgodi mmoja ashindwe kuajiriwa mgodi mwingine hata kama ameachishwa kazi kwa kuonewa au kusingiziwa jambo ambalo kiuhalisia hakulifanya. Kuna wasiwasi mkubwa kama jambo hili lisipofanyiwa kazi kikamilifu hata hawa wanaoacha kwenye wimbi hili la fao la kujitoa wakakumbwa na kikwazo hiki pale ambapo watapata tena fursa ya kuajiliwa tena katika mgodi mwingine au huo huo waliotoka. Aidha aliwashauri wafanyakazi kuchangamkia fursa mbali mbali zilizopo nchini kwa ajili ya ustawi wao wenyewe na taifa kwa ujumla. Aliwaasa kila mfanyakazi ajiwekee lengo la kumiliki ardhi walao heka tano na kuhakikisha wanamiliki viwanja katika miji ambayo tayari imeishaunganishwa na mtandao wa barabara. Thomas Sabai Katibu wa TAMICO- Tawi la GGM
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment