Saturday 19 January 2013

[wanabidii] TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI HUJUMA DHIDI YA CHADEMA WILAYA YA LUSHOTO

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
(CHADEMA)
WILAYA YA LUSHOTO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HUJUMA DHIDI YA CHADEMA WILAYA YA LUSHOTO


1.1 UTANGULIZI

Ndugu Wanahabari

Kwa kuwa nchi yetu imekubali kuridhia mfumo wa demokrasia ya vyama vingi nchini ambao unatoa, pamoja na haki zingine, haki ya usawa, haki ya uhuru wa mawazo na uhuru wa mtu kushirikiana na wengine na kwa kuwa viongozi wa CHADEMA wilaya ya Lushoto tunatambua kwamba ushindi na uhalali wa kisiasa unatokana na nguvu ya hoja katika msingi wa mamlaka na nguvu ya umma, hatuna budi kuwa taarifu watanzania juu hujuma na mizengwe inayokiuka misingi ya kidemokrasia ili umma wa watanzania kuchukua maamuzi sahihi kupitia sanduku la kura.

1.2 HUJUMA DHIDI YA CHADEMA

Ndugu Wanahabari,
Kwa kuwa kwa muda mrefu sasa CCM wilaya ya Lushoto wamekuwa wakifanya hujuma ambazo ni kinyume cha kanuni za kidemokrasia ikiwepo vitisho dhidi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA tumeona ni muda muafaka kuwahabarisha watanzania juu ya mpango huu unaolenga kudhoofisha nguvu ya CHADEMA. 

Tarehe 13/01/2013 CHADEMA wilaya ya Lushoto ilifungia jalada la kesi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) juu ya ung'oaji wa bendera kwenye matawi ya CHADEMA na kupewa RB No. LUSH/RB/65/2013 kutoka kituo cha polisi wilaya ya Lushoto. Kesi hii ilimuhusisha Mwenyekiti ya Vijana wa CCM (UVCCM), Bwana Antipus Mbuguni na Bwana Faustine Mndolwa, mtoto wa mjumbe wa NEC wa wilaya ya korogwe vijijini, Dr.Edmund Mndolwa. 

Aidha uongozi wa wilaya ya Lushoto wamepata malalamiko ya aina hii toka kwa wanachama na wafuasi wa CHADEMA kata ya Milingano jimbo la Bumbuli. Vilevile ung'oaji huu ulifanyika wakati wa chaguzi ndogo za udiwani kata ya Funta na Tamota jimbo la Bumbuli mwaka 2012. Na ung'oaji juu unafanyika kwenye kata mbalimbali za jimbo la Lushoto.

Mwaka 2010 hujuma kama hizi zilifanywa pia na Mbunge wa Jimbo la Lushoto na Mwenyekiti mpya wa mkoa wa Tanga Dr. Henry Daffa Shekifu kwa kushirikiana na viongozi na wanachama wa CCM kwenye kata ya Mlola na kusababisha vurugu kubwa ambayo ilisababisha Mwenyekiti wa CHADEMA wa kata Marehemu Salim Kibacha kupigwa vibaya na wafuasi wa CCM. Vilevile uhuni huu ulifanyika kata ya Lushoto kitongoji cha Milemeleni.

Kwa kuwa jambo hili ni dhahiri kwamba halifanyiki Lushoto tu bali maeneo mengi ya Mkoa wa Tanga, viongozi wa wilaya ya Lushoto tumeamua kwa dhati kulifanyia kazi ili haki iweze kupatikani kwani viongozi na wanachama wa CHADEMA hatuwezi kushindana kung'oa bendera za CCM kwa kuwa tunatambua huu ni uhuni na ufinyu wa kifikra dhidi ya misingi ambayo CHADEMA kama chama cha siasa kinasimamia. Ieleweke kwamba adui yetu mkubwa si bendera, rangi au sura za viongozi wa CCM bali sera mbovu za Chama Cha Mapinduzi.

1.3 MATAMKO YA VIONGOZI WA CCM


Ndugu Wanahabari,

Kwa kurejea kauli ambazo zinatolewa na Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Tanga Dr.Henry Daffa Shekifu ni dhahiri kwamba mipango hii inasukwa kwa umahiri mkubwa kuhakikisha vyama vya upinzani ikiwepo CHADEMA hafurukuti mkoa wa Tanga. Vilevile kupitia habari ya gazeti la Mwananchi la tarehe 12/01/2013 toleo namba 4583 lilitoa habari iliyomhusu Katibu wa Itikadi, uenezi na siasa mkoa wa Tanga Bwana Mathew Maganga akihabarisha kuhusu mkakati wa kuusambaratisha vyama vya upinzani mkoa wa Tanga.

Kwa kuzingatia uwajibikaji wa pamoja na usalama wa viongozi na wanachama wa CHADEMA tumeona tutoe taarifa hii kupitia vyombo vya habari ili mamlaka husika zifanye kazi kwa kuzingatia haki na wajibu wa kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanajamii. 

1.4 MAJIBU YA JESHI LA POLISI 


Viongozi wa CHADEMA wilaya ya Lushoto wamekuwa wakifuatilia jambo hili kwa karibu kuhusu mashtaka haya na kupewa majibu yafuatayo:


  1. Faili la mashtaka limepelekwa kwa RPC mkoa wa Tanga 
  2. Faili hili baada ya kutoka kwa RPC Tanga litaenda kwa mwanasheria wa serikali mkoa wa Tanga ili afanye maamuzi kwamba jambo hili linaweza kupelekwa mahakamani au vinginevyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya polisi faili hili litarudishwa baada ya siku 14 tangu taarifa ilipotolewa polisi.

Ndugu Wanahabari, haya ndio majibu ya polisi wilaya ya Lushoto.

1.5 MWISHO


Ndugu Wanahabari,
Tunaomba tuwakumbushe viongozi na wanachama wa CCM, wajifunze kuwekeza kwenye siasa za akili, wajifunze kuwekeza kwenye nguvu ya hoja.

Viongozi wa CHADEMA wilaya ya Lushoto tunaamini kwamba, nguvu, ubabe na misuguano yoyote isiyotawaliwa na busara, hekima na uvumilivu haina maana yoyote katika ustawi wa jamii ya watanzania, ni za muda mfupi tu.

Aidan Singano


Kaimu Mwenyekiti [W]
CHADEMA Wilaya ya Lushoto

Imetolewa Tarehe : 18/01/2013


--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment