Tuesday 1 January 2013

[wanabidii] Re: [PK] VYAKULA VYA GMO MADUKANI KWETU



---------- Forwarded message ----------
From: Haidari BENN <benntz@yahoo.co.uk>
Date: 2013/1/1
Subject: Re: [Wanazuoni] Re: [PK] VYAKULA VYA GMO MADUKANI KWETU
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>


 

Mr. Yona,
God has created his creatures to survive in their own climates. He also created the products according to the climatical position. This means we who live in Tropical countries need those products in the tropical countries to survive accordingly.
Kwa hivyo sioni sababu yeyote kuwa vyakula vyetu vya kiasili havifai hivi sasa. Tunadiganya ikiwa tutaanza kuabadilisha maadili yetu like fastfood na humbugers awu pizza.
Katika uchunguzi tuliofanya magonjwa tunayoyapata hivi sasa Africa like Diabetes, etc. ni kwasababu tumebadili vyakula vyetu. We  have to come back to our roots so that we can have better health.
regards,
 
Benn Haidari
Klintvägen 16 C 36
22100 Mariehamn
Åland
Suomi-Finland
Author of Modern Zanzibar Cuisine
Tel/Home: +358.18.13665
Mobile: +358.457.3424826

From: Mathew Bukhi <bukhimathew@gmail.com>
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Cc: wanazuoni <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Sent: Monday, 31 December 2012, 23:59
Subject: Re: [Wanazuoni] Re: [PK] VYAKULA VYA GMO MADUKANI KWETU

 
Halafu ni hatari kwa nchi kama yetu isiyo na taasisi imara za kusimamia na kudhibiti vyakula vya namna hiyo. Nchi za Ulaya zimekataa upuuzi huo wa GMO. 

Baruani, ina maana huyo profesa haoni kama mataifa ya Ulaya yana sababu za msingi za kukataa GMOs?

Tanzania yetu tumevamia na kuingia kichwa kichwa katika hiyo laboratory based genetic selection and modification. Nafikiri kuna taasisi moja ya masuala ya kilimo pale Mikocheni, inajihusisha na GMOs.

Hiyo hoja ya GMOs kuwa suluhisho la njaa katika bara la Afrika, haina mashiko sana. Vipi kuhusu uduni wa zana za kilimo katika bara hili, kama moja ya sababu kubwa ya mavuno hafifu? Vipi kuhusu uwezo wa wakulima wa bara hili katika 'kupata' - 'kuaccess' pembejeo na miundombinu ya msingi ya kilimo, kama sababu ya mavuno hafifu? Vipi kuhusu sera za IMF/WB zilizohimiza serikali zetu kupunguza matumizi, hivyo kupelekea uhaba wa wataalamu wa kilimo, kama sababu ya  mavuno hafifu? Wataalamu hao kilimo wangeweza kutoa elimu na ushauri kwa wakulima juu ya namna ya kupata tija katika mavuno.

Kwa kujenga hoja kwa misingi ya ustahimilivu wa GMO crops katika ukame na wadudu tu, bila kuangalia dimensions zingine zinaziweza kusababisha mavuno hafifu ya mazao ba njaa,wanaifanya hoja iwe narrow na biased.

Wasalaam,

Bukhi.


Sent from my iPhone

On 31 Des 2012, at 21:43, Baruani Mshale <baruani.mshale@gmail.com> wrote:

 
Ni vizuri pia kuelewa kuwa 'genetic modification" imekuwa ikifanyika kwa karne nyingi sana. Kwa mfano, kitendo cha mkulima kuchagua mbegu bora toka ktk mavuno yake kwa ajili ya kupanda msimu unaofuatia ni kwamba anafanya "genetic selection" ambayo itabadili mazao misimu inayofuatia. Mashabiki wa GMO wanadai kuwa tofauti ni kwamba, sasa genetic selection inafanyika kitalaam zaidi na kwa muda mchache kuliko zamani.
 
Ugomvi upo kwenye laboratory selection and manipulation of genes. Wale wanaofanya genetic modification wanadai kuwa GMO products hazina madhara yoyote na anayedai kuwa zina madhara atoe ushahidi wa madai yake. In English, they have shifted the burden of proof on to the GMO opposers to prove harmful effects. Wanadai kuwa ni kawaida kwa jamii kuwa na hofu isiyokuwa na msingi pale teknolojia mpya inapokuja. wanatumia mifano ya zipu na vifungo, chai na kahawa, margarine na butter, n.k. Kwamba vifungo vilikuwako kabla ya zipu na kwamba zipu si nzuri kwani zinaweza kufunguka zenyewe na kumdhalilisha alovaa nguo yenye zipu. Kanisa katoliki likatumika ktk kupinga ugunduzi na matumizi ya zipu. Mashabiki wa GMO wanasema, je zipu zimewadhalilisha wavaaji? Vile vile kwamba kahawa ni kinywaji cha shetani kwa kuwa kahawa ilikuja baada ya chai, vivyo hivyo kwa butter na margarine, na mengineo mengi. Kwangu mimi ni ya kipuuzi tu.
 
Mjadala huu unaendelea na bidhaa za GMO zinazidi kuzagaa kwa walaji na watumiaji. Baadhi ya skimu za kuhakiki kama bidhaa ni za GMO ama la, zimegundulika kuwa na walakini mkubwa.
 
Mashabiki wa GMO wanadai kuwa GMO itasaidia kukabiliana na tatizo la njaa kwa Afrika kwa kuwa zitapatikana mbegu zinazokabili ukame, magonjwa, wadudu, na kutoa mazao mengi ambazo zinakomaa kwa muda mfupi zaidi. Terminator seeds ni mfano mmojawapo na baadhi mnatambua athari zake za kiuchumi, kitamaduni, kijamii n.k. Of particular importance is the increased dependence on multi-national corporations in industrialized nations and loss of agro-diversity (I wrote a term paper on this topic for a class and got marked down because i was against GMO and the professor is a pro-GMO, it got really hot. He wanted a social-scientist like myself to prove scientific harmfull effects of GMO, and I argued that psychological effects among consumers and effects on biodiversity are as important as health effects that i cannot prove).
 
Nadhani ni wakati sasa tunahitaji taarifa zote ziwekwe hadharani ili tuweze kujadili kwa kina.
 
Baadhi yetu tumejikuta tukishambuliwa sana pale tulipojaribu kuingia kwenye mijadala dhidi ya GMO foods na kujikuta hatuna ushahidi wa kuthibitisha madhara yake na kuonekana kana kwamba tuna wasiwasi unaotokana na hisia tu na sio scientific proof. Nilifarijika nilipofahamu kuwa wafanyakazi wa kampuni kubwa ya GMO iliyoko Minnesota, USA waligoma kula vyakula vinavyozalishwa na kampuni yao na kudai wawekewe organic foods kwenye cafeteria zao: Monsato.
 


2012/12/31 Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
 
Ni vyakula vinavyotokana na kurekebisha (kuboresha?) vinasaba (i.e. genes) vya mmea/mbegu eti ili vyakula hivyo viwe bora zaidi kuliko vya asili - kirefu cha GMO ni Genetically Modified Organism.
 
-------
My mission is to acquire, produce and disseminate knowledge on and about humanity as well as divinity, especially as it relates to Africa, in a constructive and liberating manner to people wherever they may be.

Address: 41 Banks Street # 1, Cambridge, MA 02138 USA
Cellphone: US = +1 (857) 413 - 9521/TZ = +255754771763
Skype: chambi100
Twitter: @Udadisi


 
Vyakula vya GMO ni vyakula gani, vina sifa ipi? tuelewesheni.

2012/12/29 Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
 
Ndugu Benn Haidari

Ahsante kwa mchango wako , nina swali moja kwako .

Je unadhani vyakula asili vinavirutubisho vya kutosha vinavyoweza kupambana na hali ya sasa ya kimaisha ?

Je vipi kuhusu ubora wa vyakula hivi kuanzia kwenye ardhi inayopandwa , maji yanayotumika kunyeshea na aina nyingine ya utunzaji kufananisha na  Hivi vya kisasa ?

2012/12/29 <benn.haidari@aland.net>
Waheshimiwa,
Wiki iliyopita kabla ya Christmas, nilialikwa kuwa mgeni rasmi huko visiwa vya Komoro kwa kujadili masuala haya ya vyakula kutoka pande za ulaya ambavyo vimepigwa marufuku huku Ulaya kwaajili ya madhara mbali mbali.
Katika mijadala hiyo ambayo ilikuwa kwenye semina na workshops mbali mbali mbali za wiki 2 tulijaribu kutiliya mkazao vyakula vyetu vya Kiswahili ambavyo Wazee wetu walikuwa wakivitumiya kwa karne nyingi.
Katika semina hiyo, tulikuwa na wataalamu mbali mbali kama Professor Bakri Othman from U.S.A. ambawo wameonesha kitaalamu kuwa nchi nyingi za Kiaafrrika zinatumiwa kuwa jaa la vitu vilivyooza huku Ulaya.
Kwa hivyo sijastaajabu kuona mjadala huu, hapa kwenye mtandawo, na itabidi serikali zetu watiye mkazo kutumiya local products zetu zaidi katika mikahawa yetu,  madukani na nyumbani pia. Ni muhimu sana kuwasomesha watoto wetu kupenda vyakula vyetu vya jaddi ambavyo vina siha zaidi kuliko hivi vyakula vya ulaya.
Katika vitabu vingi vyangu vya mapishi ambavyo vinapatikana kwenye Amazon.com, nimeonesha ule ustaarabu tulikouwa nawo miaka mingi iliyopita, ya vyakula, na ustaarabu huu unapoteya.
 
From: Yona Maro
Sent: Saturday, December 29, 2012 6:45 PM
Subject: [PK] VYAKULA VYA GMO MADUKANI KWETU
 
Ndugu zangu

Nilikuwa natafuta vyakula Fulani Fulani vya watoto na moja ya kitu nilichokuwa naangalia kwenye kila bidhaa ni kama vyakula hivyo vina nembo zenye kuonyesha kama ni GMO au la , Nilipata bidhaa kama 3 hivi zilizokuwa na chapa inayosema NON GMO kwa zile bidhaa zinazotoka nje ya nchi haswa Ulaya Na Marekani .

Bidhaa hizi nimezikuta katika duka la shoprite mlimani city ,hii imekuwa ishara nzuri maana tumejadili mara kadhaa kuhusu bidhaa kuwekwa nembo kama ni GMO au la hii nimeiona kwa mara ya kwanza hapo Shoprite .

Hili sio Tangazo la biashara ila ni kuleta mjadala huu mpana zaidi kuhusu bidhaa zinazotokana na GMO haswa vyakula ambavyo inasemekana vipo nchini na watu wanatumia na tumekuwa tukisikia au kusoma kuhusu madhara ya bidhaa hizi sehemu mbalimbali duniani .

Kama una ushuhuda wowote kuhusu GMO kwa kanda ya afrika mashariki au popote ulipo tunaweza kutupa kutumia mtiririko wa mjadala huu au tuma kwenda wanabidii@googlegroups.com kama wewe sio mwanachama wa Wanabidii na wengine wataweza kusoma mchango wako .

Karibu tuendelee kujadiliana huku tukijenga nchi zetu .

Unaweza kusoma au kujifunza zaidi kuhusu GMO kwa kutembelea





--
*************************************************************************************************
Geniuses Training and Business Services
Certificate and Diploma in Teaching, Training, Business Management & Entepreneurship, Legal Studies, Social Media & Marketing, Project Management, Multimedia Development, English and Literature Studies, Children Studies, Psychology, ICT Foundation Course
Call 0705297307 or 0786695083 or Email to: info@geniusesltd.com
 
*************************************************************************************************
TO ADVERTISE HERE: email: amosogal @ gmail.com
*************************************************************************************************
To subscribe:progressive-kenyans+subscribe@googlegroups.com:
Unsubscribe:progressive-kenyans+unsubscribe@googlegroups.com
 
 
--
*************************************************************************************************
Geniuses Training and Business Services
Certificate and Diploma in Teaching, Training, Business Management & Entepreneurship, Legal Studies, Social Media & Marketing, Project Management, Multimedia Development, English and Literature Studies, Children Studies, Psychology, ICT Foundation Course
Call 0705297307 or 0786695083 or Email to: info@geniusesltd.com
 
*************************************************************************************************
TO ADVERTISE HERE: email: amosogal @ gmail.com
*************************************************************************************************
To subscribe:progressive-kenyans+subscribe@googlegroups.com:
Unsubscribe:progressive-kenyans+unsubscribe@googlegroups.com
 
 







--
Baruani Mshale
Doctoral Program
SNRE
University of Michigan


__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (7)
Recent Activity:
.

__,_._,___

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment