Tuesday 22 January 2013

[wanabidii] Re: MKUTANO NA WAANDISHI MAKAO MAKUU YA CHADEMA JANUARI 22, 2012

CHADEMA wamekosa focus kwenye mambo muhimu na tatizo kubwa ni kwenye
Idara yao ya Habari na uenezi inayosimamiwa kwa kiasi kikubwa na
Tumaini Makene , Hili tamko litakuwa na Baraka za Tumaini Makene .

Ndugu Tumaini Makene .

Wananchi hawataki Mipasho , wanataka kuelezwa mambo muhimu kuhusu nchi
yao na harakati nyingine za chama hizo katika kujiimarisha na angalau
mafanikio iliyofikiwa kwa mwaka mmoja uliopita na matarajio ya mwaka
huu ulioanza karibuni tu .

Kupambana na CCM kwa njia hii hamtafika popote mnajipotezea muda na
kupotezea wananchi muda haswa wale wananchi wanaowaamini na
waliochukuwa kadi zenu za uwanachama .

Tunataka mambo na vitu tofauti , Tumechoka uzushi , Majungu na
Undumiwa Kuwili .

On Jan 22, 10:59 pm, Bariki Mwasaga <bmwas...@gmail.com> wrote:
> Kama mipasho vile. Siasa za Tanzania zinahitaji kuhuishwa kwani kwa hali
> hii sioni mbele kukoje!
>
> 2013/1/22 Yachama Gabriel <yachama2...@gmail.com>
>
>
>
>
>
>
>
> > Statement kwenye point (iii) inakubaliana kuwa chadema nacho kinakufa.
> > Sasa mbona maneno yanayofuata anakanusha tena? Je, ni madhumuni ya
> > mwandishi kusema hicho au kiswahili ni tatizo kwake?
> > Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Zantel Etisalat Tanzania.
>
> > -----Original Message-----
> > From: Abdalah Hamis <hamis...@gmail.com>
> > Sender: wanabidii@googlegroups.com
> > Date: Tue, 22 Jan 2013 10:20:14
> > To: Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
> > Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
> > Subject: [wanabidii] MKUTANO NA WAANDISHI MAKAO MAKUU YA CHADEMA JANUARI
> > 22, 2012
>
> > MKUTANO NA WAANDISHI MAKAO MAKUU YA CHADEMA JANUARI 22, 2012
>
> > NDUGU waandishi wa habari,
>
> > Kuna mambo mengi yamezungumzwa kuhusu CHADEMA. Nanyi waandishi wa
> > habari mmekuwa mkitupigia simu, mmoja mmoja kutaka ufafanuzi na
> > msimamo wa chama chetu kuhusiana na masuala hayo. Leo tumeamua kuwaita
> > hapa ili kuwapa ufafanuzi mkiwa pamoja badala ya kila mmoja kuuliza
> > akiwa kwenye chumba chake cha habari.
>
> > Kwanza, CCM kupitia kwa viongozi wao waandamizi, akiwemo Nape na
> > Mwigulu, wanazunguka zunguka huko, kuwaambia Watanzania kuwa CHADEMA
> > inakufa, tena wanatengeneza hata sababu za kifo, wanasema ni ubaguzi
> > na kutokana na laana ya Mwalimu Nyerere.
>
> > Tunataka kuwaambia hivi: Kwamba CHADEMA haina ubaguzi na hivyo haiwezi
> > kufa leo wala kesho, mpaka iwe imetimiza kazi yake ya kuwakomboa
> > Watanzania. Na bahati mbaya, CCM wanaona CHADEMA kitakufa, wanasahau
> > kuona kuwa chama chao tayari kinakufa tayari sasa.
>
> > Kama suala ni laana ya Nyerere. Laana hiyo haiko CHADEMA; iko ndani ya
> > CCM kwa sababu tatu.
>
> > (i) Mwalimu wakati wa uhai wake, kwa kushirikiana na waasisi wengine,
> > alijenga misingi ya utaifa wetu, ambapo CCM wameamua kuivunja kwa
> > maslahi ya wachache. Akiwa bado hai, Mwalimu alitunga hata kitabu
> > akasema CCM kimeoza na kinakuka rushwa. Akaongeza CCM kuna kansa ya
> > uongozi na uchaguzi ndani ya chama hicho, ni gulio la wala rushwa.
> > Maneno hayo ni laana tosha.
>
> > (ii) CCM kinapata laana ya Mwalimu kwa sababu kimerasimisha ubaguzi
> > kwa wanachama wao, viongozi wao na Watanzania kwa ujumla. Ni hawa hawa
> > CCM wanaoeneza uongo wa hatari, wakiwatisha wananchi kwa kusema
> > CHADEMA kina ukabila, mwaka 2005 walimzushia Dk. Salim Ahmed Salim
> > uongo kuwa ni Mwarabu na alihusika na kifo cha aliyekuwa mmoja wa
> > wasisi wa taifa hili, Abeid Amani Karume. Uchafu ulifanywa na wana CCM
> > wa kundi la wanamtandao ambao leo ndiyo wanaongoza chama na serikali
> > na ubaguzi huu dhidi ya Dk. Salim ndiyo uliowafanya washinde.
>
> > (iii) CCM kinakufa pia kwa sababu ya laana ya ubaguzi wa kukiuka haki
> > za raia. Ninyi ni mashahidi namna ambavyo baadhi ya makundi ya
> > wafanyakazi yamekuwa yakibaguliwq katika kupata stahiki zao. CCM na
> > serikali yake, imekuwa ikijibu kwa kauli za kejeli na vitisho, ikiwemo
> > kutekwa na kuteswa kwa viongozi wa wafanyakazi na kisha kutupwa katika
> > Msitu wao wa Mabwepande na baadaye kulinda wahalifu kwa visingizio
> > vingi vya kulindana huku wakichezea maisha na uhai wa Watanzania
> > wenzetu.
>
> > Hivi unaweza kuielezea vipi hali ya serikali ya CCM kutowalipa wazee
> > wastaafu waliokuwa watumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kama si
> > ubaguzi! Wazee ambao wametumikia taifa hili kwa uwezo wao, akili zao
> > na miili yao, wenzao wote katika nchi nzingine zilizokuwa zikiunda EAC
> > wakati ule, walishalipwa, isipokuwa hapa Tanzania ambapo chama
> > kinachotawala kimeamua kufanya ubaguzi wa haki za watu, nani apate na
> > yupi asipate.
>
> > Itakumbukwa kuwa wazee wale kutokana na kuyumbishwa na kubaguliwa
> > katika kupata haki zao, waliamua kuvua nguo barabarani, pia kwa kiburi
> > na ukosefu wa heshima ya serikali ya CCM kwa wananchi, wakawachapa
> > viboko wazee wale! Laana ya wazee hawa inakiua CCM.
>
> > Hivyo basi, CCM kinakufa kutoka na laana hiyo na uongo uliosababisha
> > na kushindwa kutekeleza ahadi zake za maisha bora, ajira kwa vijana na
> > kuwezesha wanawake.
>
> > CCM wajiandae kufuata njia za vyama vya KANU ya nchini Kenya, UNIP ya
> > Zambia na chama cha ukombozi nchini Malawi.
>
> > Ndani ya CHADEMA kuna baraka za Mwalimu Nyerere. Hakuna laana. Ninyi
> > ni mashahidi kuwa kabla ya Mwalimu kufariki dunia, alikimwagia sifa
> > CHADEMA kwa kusema ni chama makini.
>
> > Tofauti ya CCM na CHADEMA
>
> > Kwenye mikutano yao, sasa CCM wamejipatia majukumu wasiyoyamudu ya
> > kujifanya ni maofisa waenezi wetu na moja ya majukumu waliyoamua
> > kujipachika na kuyafanya ni kuwaonesha Watanzania, moja ya tofauti
> > kati yetu na wao, ambazo ni uwezo wa kuchukua hatua na kuwa na sera
> > sahihi mbadala kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Watanzania.
>
> > Kwenye mkutano wao uliomalizika hivi karibuni na kwenye shughuli zao
> > za kila siku, CCM sasa wameamua 'kuimba' sera za CHADEMA, hasa zile za
> > elimu bure na kushusha bei ya vifaa vya ujenzi. Mambo ambayo miaka
> > miwili tu iliyopita walikuwa wakiimba kinyume chake. Bahati mbaya
> > hawana uwezo wa kuzitekeleza, kwa sababu si mawazo yao na hawana
> > utashi huo.
>
> > Hili la pili la kuchukua hatua…bahati mbaya kwa sababu ya kuelemewa na
> > kansa ambazo tumezitaja hapo juu, CCM wanaona kuchukua hatua ni
> > 'kufukuzana', maneno ambayo hata jana wakati wakizungumza na waandishi
> > wa habari wameyarudia. Hawawezi kuona kwa sababu wote ni wachafu,
> > wanaishi hivyo kwa kukubaliana.
>
> > Ndugu wanahabari, hii ni moja kati ya tofauti nyingi zilizopo kati ya
> > vyama hivi viwili, ambazo zimeifanya leo CHADEMA ndiyo tumaini la watu
> > wanaodai haki na uwajibikaji, tumaini la watu katika kupigania uhuru
> > na mabadiliko ya kweli nchini, kimbilio la watu wasafi dhidi ya
> > ufisadi, wanaopinga ubadhirifu na dhuluma ya CCM, ni tofauti hizo
> > zinakifanya CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani na mbadala
> > kinachoaminiwa na Watanzania kukabidhiwa dola.
>
> > Tukiwa chama imara na makini kinachoaminiwa na kubeba matumaini ya
> > Watanzania, tutachukua hatua mbalimbali, dhidi ya makosa tofauti
> > tofauti, kulingana na uzito wake, kama vile uzembe, udhaifu,
> > ubadhirifu, ufisadi na usaliti.
>
> > Tuwachukulia hatua hata wale ambao wametumwa na CCM kuja kufanya kazi
> > ya chama hicho kupitia kwa jina la CHADEMA.
>
> > Ni uwezo na uthubutu wa kuchukua hatua mbalimbali, ndiyo umekuwa moja
> > ya sababu kubwa ya Watanzania kuiunga mkono CHADEMA kila tunaponyoosha
> > mkono kuikemea CCM na serikali yake juu ya ufisadi, ubadhirifu na
> > uminyaji wa haki za Watanzania.
>
> > Zamani, CCM kilipokuwa bado chama cha siasa hasa, ambapo kilikuwa
> > kinasimamia misingi ya umoja wa kitaifa bila kujali dini ya mtu,
> > kabila au rangi; kilipokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi
> > rushwa na ufisadi, yaani CCM ya enzi za Mwalimu Nyerere na waasisi
> > wengine waadilifu, hakika kilikuwa na uwezo wa kufukuza kila
> > aliyeonekana kwenda kinyume na misingi yake.
>
> > Ni katika kipindi hicho, CCM kiliwavua uongozi na uanachama baadhi ya
> > waliokuwa viongozi wake. Kwa mfano, Maalim Seif Shariff Hamad, Hamad
> > Rashid Mohammed, Sudi Yusuf Mgeni, Fortunatus Lwanyantika Masha na
> > wengineo. Baadaye mwaka 1984 kilimfukuza uongozi (msisitizo uongozi)
> > aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,
> > Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi, kwa kukiuka misingi yao.
>
> > Lakini leo hii, CCM hakiwezi kuchukua hatua hiyo hata kwa katibu wa
> > tawi. Kwa sababu, hiki si chama cha siasa tena. Hili ni genge la
> > wahuni, waliojikusanya pamoja na kujiita chama cha siasa. Ni wezi wa
> > raslimali za taifa, waliotayari kulirejesha taifa kwenye utumwa kwa
> > maslahi yao binafsi.
>
> > Ndiyo maana wameshindwa kuwafukuza mafisadi, badala yake ndiyo
> > wanaoongoza chama na kuwatawala. Walisema wanataka kujivua gamba (la
> > nyoka) baadae wakagundua kuwa gamba lao halisi (ufisadi) ni gamba la
> > kombe, ambalo ili livuke ni lazima kobe afe!
>
> > CCM ya sasa, hakiwezi siyo tena kutetea wafanyakazi na wakulima.
> > Hakitetei tena maslahi ya wanyonge. Kimebeba na kukumbatia ufisadi na
> > mafisadi wa kila aina, na wabadhirifu wa mali za umma, ambao
> > wameyafikisha maisha ya Watanzania na nchi yao hapa yalipo.
>
> > Lakini CHADEMA inachukua hatua kwa sababu hiki ni chama sikivu na
> > kinachobeba matumaini ya wananchi. Hivyo, hatuko tayari kumuacha mtu
> > yeyote ambaye anafanyakazi za CCM ndani ya CHADEMA, kisha kujiita yeye
> > ni mwana-Chadema. Tutamfukuza.
>
> > Huwezi kuzusha uongo kwa viongozi wako na chama chako, kisha ukataka
> > uachwe. Usijadiliwe. Usiguswe. Tutakujadili na tukibaini kuwa una
> > makosa, tutakuomba ujirekebishe. Ukikataa, tunakuambia hutufai.
> > Ondoka. Ukishindwa, tunakufukuza.
>
> > CCM kupitia mawakala wao wanasema: CHADEMA kinapokea ruzuku kubwa,
> > lakini kimepanga ofisi. Hii nyumba ni mali ya Chadema. Lakini mbona
> > hao mawakala wa 'status quo' hawasemi kuwa CCM haina ofisi? Maana ile
> > inayoitwa ofisi ya CCM Makao Makuu Dodoma, ni mali ya Mamlaka ya
> > Ustawishaji Makao Makuu (CDA).
>
> > Huyu Nape hana hata maadili ya uongozi. Alifukuzwa kwenye UV-CCM baada
> > ya wenzake kumwambia amezusha uongo. Baada ya kuitwa kujitetea,
> > akasingizia kuwa alilishwa maneno na waandishi wa habari. Kumbe
> > wenzake walikuwa na mkanda wa hotuba yake aliyoitoa pale Peacock
> > Hotel. Wakampa aisikilize. Eti ndipo akakiri na kuomba radhi. UV-CCM
> > chini ya Emmanuel Nchimbi, ikamwambia hutufai. Muongo wee. Ikamfukuza.
> > Sasa mtu ambaye amethibitishwa na chama chake kuwa muongo, atawezaje
> > kutusumbua CHADEMA?
>
> > Wala tunachofanya hapa siyo kujibu maneno yake, bali tunaweka rekodi
> > zake sawasawa. Tunataka umma umfahamu vizuri, kwa sababu wasiomjua
> > wanaweza kuamini maneno yake.
>
> > Kauli za Mwigulu Nchemba
>
> > Tunataka kuwaambia wahusika wa usalama na ulinzi nchini, hususan Rais
> > Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema na
> > Mkurugenzi
>
> ...
>
> read more »

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment