Monday 7 January 2013

[wanabidii] Rais Kikwete amu-endorse Kigwangala na matumaini yake ya baadae

Rais Jakaya Mrisho Kikwete yuko kwenye ziara yake ya kazi mkoani
Tabora toka jana alipoianza akitokea mkoa wa Singida. Jana alipokelewa
mkoani hapa akitokea Singida.

Akiwa kwenye mkutano wa hadhara alitoa fursa ya wabunge kuongea kuhusu
kero za wananchi na hapo Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangala hakufanya
makosa na alianza kwa kumpongeza Rais Kikwete kwa kutekeleza ahadi
zake kubwa mbili kati ya tatu alizotoa na huku akimuoamba aisukume
hiyo ahadi yake ya tatu ya kupeleka maji Tabora kupitia Nzega. Ahadi
nyingine ni pamoja na mradi wa kupeleka umeme vijiji 28 vya wilaya ya
nzega na ujenzi wa barabara ya lami ya nzega - tabora. Tayari umeme
unawaka hadi sasa na ujenzi wa barabara za lami umeanza japokuwa kwa
kusuasua kwa kuwa wakandarasi bado hawajalipwa pesa ya kutosha.
Mheshimiwa Kigwangala alitumia fursa ile kumuomba Rais Kikwete asaidie
kusukuma mradi huu upewe pesa za kutosha na barabara ziishe kabla ya
2015. Aliongea kwa kujiamini huku akishangiliwa na wananchi wa Nzega
waliojaa viwanja vya parking, mjini hapa.

pamoja na mambo mengine, Kigwangala aliwagusa zaidi wananchi pale
alipomalizia kwa kumuomba Rais Kikwete aondoke na mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Nzega Ndugu Kyuza Kitundu kwa kosa la
kuwadharau wananchi na viongozi wao, alisema: 'Mhe Rais tunafurahi leo
umefika na tunashukuru umetupa nafasi hii......mimi kwa niaba ya
wananzega naomba nikwambie kuwa huyu mkurugenzi wa haamshauri ya
wilaya hatumpendi na uondoke naye, anawadharau wananchi, anawadharau
wawakilishi wao na ndiyo kiini cha kukwama kwa maendeleo ya
nzega.....sisi tuliishamaliza wajibu wetu, tuliishamkataa kwenye vikao
halali vya halmashauri, sasa tunashangaa kwa nini bado yupo
hapa...tunakuomba tafadhali ondoka naye....ni dharau yake
inayosababisha wananchi kukosa maji safi na salama ya kutumia maana
hafuati ushauri wetu....yeye anafanya ya kwake tu...' Alisema maneno
hayo huku akishangiliwa na wananchi maelfu waliokuwepo eneo la
mkutano.

Katika hatua nyingine Mh John Pombe Magufuli alikazia kwa kusema
'natoa maelekezo kuwa bodi ya mainjinia Tanzania imnyang'anye kibali
mhandisi huyu wa maji ambaye ameshindwa kurekebisha mitambo ya
kusafisha maji na matokeo yake amewanywesha wananchi maji machafu kwa
zaidi ya miaka mitano...' wananchi walishangilia sana. Naye Waziri wa
maji Prof. Jumanne Maghembe alisema 'mhandisi wa maji wa hapa Nzega
ninaondoka naye namrudisha wizarani na wiki ijayo tutaleta mhandisi
mwingine atakayeweza kurekebisha mitambo hii ili wananchi wapate maji
safi na salama'. Pia waziri wa maji alitoa sh milioni themanini kwa
ajili ya kurekebisha mitambo hiyo ya kusafisha maji.

Mh Rais Kikwete alijumuisha hotuba zote kwa kumfagilia sana Kigwangala
pale aliposema, huku wananchi wa Nzega wakishangilia: 'wananchi wa
Nzega mna Mbunge mzuri, kijana, sema wakati mwingine ana spidi sanaa,
inabidi kumtuliza kidogo na kumpa ushauri, uzuri ni msikivu sana na
ana matumaini makubwa huko mbeleni kushika nafasi kubwa za uongozi wa
Taifa letu, endeleeni kushirikiana naye, muungeni mkono katika kazi
zake.'

Kesho Rais Kikwete atazindua mradi wa barabara ya Nzega - Tabora
kwenye kijiji cha Puge, ambapo pia atahutubia wananchi, na baada ya
hapo ataendelea kuelekea Tabora kukamilisha ziara yake ya siku tano.

Source: Jamii Forums

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment