Tuesday 8 January 2013

[wanabidii] Mwandishi wa Radio Kwizera Issa Ngumba akutwa amekufa porini Kakonko

Mwandishi wa Radio Kwizera wilayani Kakonko mkoani Kigoma Issa Ngumba
ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha mwili wake
umepatikana katika pori la Mlima Kajuluheta .

Mwandishi huyo aliondoka nyumbani majira ya saa 1 jioni Januari 5,
mwaka huu baada ya kumuaga mkewe Rukia Yunus kwamba anakwenda madukani
na tokea hapo hakuweza kurudi mpaka mwili wake ulipopatikana leo
asubuhi baada ya jitihada za wananchi kuanzisha msako wa siku mbili.

uchunguzi wa Daktari umebaini kuwa Marehemu alinyonga shingo kisha
akapigwa risasi mkononi, simu zake mbili, fedha pamoja na bastora
inayodhaniwa kutumika kumshambulia imekutwa eneo la tukio.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment