Thursday 10 January 2013

[wanabidii] Fw: [Tanzania Correspondent Jounalists] Itakuwaje, wazinza,wakurya na wasukuma...


----- Forwarded Message -----
From: Sarya Sogildick <notification+i5wjd7ji@facebookmail.com>
To: Tanzania Correspondent Jounalists <145522512244997@groups.facebook.com>
Sent: Wednesday, January 9, 2013 3:32 PM
Subject: [Tanzania Correspondent Jounalists] Itakuwaje, wazinza,wakurya na wasukuma...

Facebook
Itakuwaje, wazinza,wakurya na wasukuma...
Sarya Sogildick 3:32pm Jan 9
Itakuwaje, wazinza,wakurya na wasukuma watakapoamua kuandamana?
Na Mobini Sarya
HUUI tata wanee! Itakuwaje itakuwaje,siku wakurya na wasukuma kutoka Mikoa ya Mara,Shinyanga na Geita watakapoamua kuandamana kuzuia Madini ya dhahabu na Almasi yatumike kwao tu?
Itakuwaje kama leo Wakerewe na wazinza wataamua kuandamana kuzuia pato la samaki aina ya sangara liisiingizwe kwenye pato la taifa ambalo husambazwa hadi kwa wamakonde?
Inakuwaje wakurya wanavumilia kupigwa risasi na Polisi kila mara wakituhumiwa kuwa ni wavamizi wa mgodi wa north Mara ambao unatoa dhahabu halisi lakini wasiizuie isisafirishwe kwenda ulaya?
Inakuwaje wasukuma wameruhusu viwanda vya kuchenjulia almasi vijengwe japani badala ya usukumani ambapo wangeajiliwa vijana wao,He mbona hata wazinza na wakerewe wameruhusu viwanda vya Sangara kujengwa Mwanza badala ya kwao?
Inakuwaje Maneneo mengi ya wazinza wanaokalia wilaya ya sengerema na visiwa vyake hayana huduma zozote mhimu kijamii kama barabara nzuri,zahanati wala vituo vya Polisi lakini samaki aina ya sangara wanaovuliwa kwao ndio wameijenga Mwanza?
Jamani ubaguzi huu wa watu wa kusini umetoka wapi, wamelishwa maneno kwa masilahi ya wanasiasa au ni laana ya ubaguzi inataka kutokea mtwara?
Eti nini wamakonde na wamwera? Ni kweli ni mumeamua kuungana na kuamua kuandamana kupinga gesi asili kusafirishwa kwenda jijini Dare s Salaam?
Narudia tena kuwauliza ni kweli mmetumwa kabisa na dhamira zenu kuandamana au mmesukumwa na hisia za kisiasa ili muandamane?
Nauliza hivyo kwa sababu hapa Tanzania hatuna sera ya ukanda , hakuna rasirimali inayogawana kwa misingi ya ukanda kama baraza la mawaziri.
Inakuwaje leo wamachinga wa Mtwara ambao walifika katika jiji la Dar es Salam, wazaramo wakawafundisha maana ya Musa hassani badala ya mcha-hachani leo wawageuke na kuwaona maadui zao?
Nahoji na ntaendelea kuhoji lakini kabla ya kutimisha hoja yangu ni bora nianze leo kuhoji kwa kumpunguzia maswali msomaji.
Baadhi ya watanzania waliozaliwa na kukulia katika utawala wa Mwalimu Julias K.Nyerere hawamini kilichotokea Mtwara baada ya kusikia kuwa wananachi wa mikoa ya kusini wameandamana kuzuia gesi isisafirishwe kwenda jijini Dar es Salaam.
Hawakuamini kwasababu ni majuzi tu Tanzania ilikuwa inaadhimisha miaka 51 ya uhuru wake kipindi ambacho hotuba maarufu ya Mwalimu Nyerere inayopinga ubaguzi ilikuwa inarushwa kwenye redio na Televisheni.
Katika hotuba hiyo Mwalimu Nyerere alijaribu kuwaonya wazanzibar wanao wabagua wenzao wa bara kwa kuwaita watanganyika na wao wanzanzibari.
Aliwaaambia nje ya muungano hakuna mzanzibari wala mtanganyika kwani wale waliowabagua wenzao wataendelea kubaguana tu.
Hivyo leo wamakonde na wamwera wanaposhirikiana kuzuia gesi asilia kusafisrishwa kwenda jijini Dar es Salaam, wakiwa na mabango yameandika kuwa 'Gesi ni ya wamakonde na mafuta ni ya wa kwere' hiyo ni dhambi mbaya.
Hivi wanadhani kuwa wanamkomoa Mtoto wa Bagamoyo,Rais Jakaya Kikwete ambaye ni mkwere wala wasidhani wanamkoamoa Prof.Sospiter Mhogo ambaye ni waziri wa Nishati na Madini.
Watakuwa wanajikomoa wenyewe, kwani baada ya kufanikiwa kuzuia gesi hiyo isiende kwenye nchi ya wakwere kama wanavyodai,ubaguzi huo utakwenda hadi kwenye makampuni ya kuchimba na kusafirisha gesi.
Wenyeji wa kusini wataanza kuchoma mitambo ya wawekezaji wakihoji kuwa mbona makampuni hayo hayajawaaajiri vijana wa kimakonde badala yake wameajiriwa wachaga, wachina na wazaramo.
Dhambi hiyo itakapofikia hapo vijana wa kimakonde watalishwa sumu ya ubaguzi wataanza kuchoma na kutekeza mitambo ya wawekezaji,hatua itakayohitimisha uwekezaji huo na gesi watabaki wanaisikia kwenye bomba tu.
Kwanza ni vizuri wananchi wa mtwara wakatambua kuwa kwa mjibu wa taratibu za nchi hii Gesi,madini na ardhi ni mali ya serikali tafauti wanavyofikiria wao.
Hayo wanayotaka kuyafanya wenzao kutoka mokoa ya kanda ya ziwa walijaribu wakashindwa sasa dhahabu inajulikana ni mali ya serikali ndio inauza pato linagawanywa kwa taifa zima hata watoto wa kimakonde wanalipiwa ada chuo kikuu bila ubaguzi.
Ni wazi kuwa suala la wananchi wa Mtwara kuandamana kuzuia gesi isisafirishwe kwenda kinyerezi jijini Dar es Salaam,kwa ajili yakuzalisha umeme wa Mg.990 ambao utatumika nchi limeandaliwa na kuibuliwa na CHADEMA.
Hayo maandamano bila kuficha wala kumung'unya maneno yameratibiwa na chadema kama mtaji wao binafsi kutokana na sababu nitakazoziweka hapa nchini.
Kwanza ni wazi kuwa kwa muda mrefu mikoa ya kusini imekuwa ni ngome ya kisiasa inayoongozwa na chama cha wananchi CUF, mara kadhaa Chadema imejaribu kuingia hapo imegonga mwamba.
Pili ni chama cha Chadema chenye sera ya majimbo katika ilani yao ya uchaguzi iliyonadiwa Mwaka 2010 ilitamkwa wazi kuwa kama Chadema wangepata nafasi ya kuongoza dola wao wangegawa nchi katika ukanda ili kila eneo wafaidi rasilimali zao.
Hapo ndipo yanapoibuka maswali kuwa kama wamakonde watafaidi gesi yao wakurya na wasukuma watakatalia madini yao,Wachaga watang'ang'ania Kilimanjaro, je wagogo na wahehe watafaidika na nini?
Ni kweli kuwa viongozi wa Chadema ndio walioratibu maandamano hayo ili wapate nafasi ya kuiteka ngome hiyo na viongozi wa CUF bila kujua au kwa kujua kuwa huo mchezo wa Chadema wakaamua kuunga mkono hayo maandamano kwa kutoa tamko.
Kama viongozi wa CUF wangefanya tathimini vizuri wala wasingejisumbua kutoa tamko tena siku tatu baada ya maandamano hayo,wangeng'amua mapema wangeepukana na mtego huo.
Tunachoshangaa wengine ni kwamba mwenyekiti wa Cuf, Profesa Ibrahim Lipumba ni mchumi mzuri anajua maana ya kukuza uchumi wa pato la taifa, anajitokeza na kuwaunga mkono viongozi wa Chadema ambao lengo lao ni tofauti anapotoka.
Baaada ya tamko lake alilodhani kuwa Cuf ikilitoa wananchi wa Mtwara hawatakiasi , Chadema wao wanaendelea kusherehekea ushindi kwamba hata CUF wameunga mkono sera yao ya ukanda maana hiyo siyo sera ya CUF.
Ni vizuri chama cha wananchi Cuf kingesimama na kutoa ushauri wake kitaalam,atahari ambazo zinawezakupatikana kiuchumi endapo Gesi ya Mtwara itasitishwa isiendelee kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam,na faida ya kufanya hivyo.
Tulitarajia Prof.Lipumba atoke na takwimu za kiuchumi ili amsaidia Prof.Mwezake namna ya kuweza kuelimisha wananchi wa mtwara kuachana na fikra za kisiasa ambazo kama zikifuatwa nchi haitakalika.
Tayari tumemsikia mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party,Agoustine Mrema akisema kuwa wananchi wa Mtwara wakifanikisha kuzuia gesi hiyo isiendelee kuchimbwa nay eye atawashawishi wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kuzuia rasmali zao zisitumiwe na wananchi wan je ya mkoa huo.
Kama tukifikia hatua hiyo nchi haitaweza kutawalika kwasababu serikali itashindwa kupata rasilimali za kuendeshea nchi inaweza kutumia nguvu ambazo zinaweza kule athari kubwa hata kiuchumi kama wananchi wataamua kulipa kisasi kwa kuhujumu miundombinu.
Hayo yatakapotokea anayekomolewa sio rais Jakaya Kikwete wala waziri wa Nishati,Prof.Muhogo bali ni sisi wenyewe kwasababu nishati ya umeme itazidi kupanda bei wanaumia kwakununua umeme bei ghali ni sisi tunaosukumwa na wanasiasa kwenda kwenye maandamano.
www.mobinday.blogspot.com 0753 399579

View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.


0 comments:

Post a Comment