Monday 7 January 2013

[wanabidii] Eng. Ezron Mashamba Amefariki.

TANZIA     TANZIA      TANZIA
 
Kwa Jumuiya ya Wahandisi wote Serikali za Mitaa, wahandisi wote nchini, Watumishi wote Serikali za Mitaa na watanzania wote;
 
Napenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha kuwa Mhandisi Mashamba aliyekuwa Mhandisi wa Ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu amefariki leo majira ya mchana katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kulazwa katika Hospitali ya Kolandoto – Shinyanga.
 
Marehemu alipelekwa Hospitali ya Mkoa Shinyanga baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya kutokea jana tarehe 06.01.2013. Bado hatujajua mazishi yatafanyika wapi kwa vile alikuwa na makaazi mjini Shinyanga lakini nyumbani kwao ni Bariadi - Mkoani Simiyu.
 
Kama ilivyo kawaida yetu tutashiriki msiba huo kwa kutoa rambirambi zetu za shs: 30,000.00 kwa kila mwanachama wa ALGETA na kiasi chochote kwa wale wote watakaoguswa na msiba huu. Mchango huu utapitia kwa Wahandisi wa Mikoa yote nchini kwenye Sekretarieti za Mikoa ambao wataziwasilisha kwa Mhandisi wa ALGETA ili kupata uratibu wa jinsi ya kuzifikisha kwa walengwa.
 
Kwa nafasi hii pia nawaomba wahandisi wote walioko Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu kutoa uwakilishi unaostahili katika maandalizi hatimae mazishi ya Mhandisi mwenzetu Eng. Mashamba.
 
Eng Mashamba alipata usajili wake kupitia mpango wa SEAP ambapo alikuwa kwa Meneja wa Tanroads Shinyanga. Alikuwa ni mojawapo ya wahandisi wachache waliopata uzoefu wa haraka kupitia mafunzo hayo yanayoratibiwa na ERB.
 
Ameacha mke na watoto ambao kimsingi walikuwa wanamuitaji sana kipindi hiki cha hali ya kiuchumi ya ulimwengu inayumba.
 
Kwa niaba ya Jumuiya ya Wahandisi katika Serikali za Mitaa Tanzania bara – ALGETA napenda kutoa pole kwa wafiwa wote, ndugu na jamaa wote, watumishi wote wa Wilaya ya Kishapu na Jumuiya nzima ya Watumishi wote walio Serikali za Mitaa Tanzania.
 
MUNGU ametwaa jina lake libarikiwe. Ukipata taarifa hii wajulishe na wengine.
 
AMINA
 
Eng. Kunyaranyara, E.M.S.
KATIBU MKUU
ALGETA.

0 comments:

Post a Comment