Thursday 10 January 2013

Re: [wanabidii] Wazanzibari wasema - " Ahsante Chadema"!

Tatizo la wanaojiita wazanzibari wengi hawaelewei wanachokidai na kwa nini wanakidai. Ukiwauliza karibu wote watakwambia wananyonywa na bara, sasa sijui ni kipi kilichopo zanzibar ambacho hakipo bara na ambacho kinafaidisha bara kuliko zanzibar. Wengine wanadai wanatawaliwa na hapa ndipo nnapokuwa na utata na definition yao ya kutawaliwa. Nnachoamini kuna kakundi kadogo ka watu zanzibar ambao wanaelewa nini hasa wanakitafuta kwa maslahi ya wanachama wa hicho kikundi. Ili kufanikisha malengo wanatumia uelewa duni wa wazanzibari wengi kwa kutumia sababu tofauti kutokana na ukweli kwamba sababu halisi haziwezi kusemwa hadharani.
 
Suala kama hili la kuvunja muungano linahitaji utafiti wa ndani  "detailed assessment" na wa muda mrefu tena na wataalamu na sio wanasiasa wala mambumbumbu wenye kujua kupiga kelele. Utafiti uonyeshe  faida na hasara za wakati huu wa muungano na baada ya kuvunika kwa muungano kwa zanzibar na wananchi wake. Utafiti ulinganishe faida na hasara kwa nyakati hizo mbili ila usitoe mapendekezo yake ili maamuzi ya wakati upi mzuri ubaki kwa mwananchi. Mwisho utafiti uwe wazi kwa wazanzibari wote halafu wapewe nafasi ya kuamua (referendum) huku wakijua nini hasa matokeo ya uamuzi wao (informed decision).
 
Lakini hili la kuwalisha sumu wananchi ambao wengi hawajafika hata darasa la saba ni uonevu kwa sababu wanakuwa wanashabikia kitu wasichokifahamu kwa kina. Hakuna kitu kibaya kama kujutia maamuzi yaliykwishafanyika.
 
Vile vile kuna ukweli kwenye maelezo ya Matinyi someni vizuri.
 
Nnachokiona BAADHI ya wazanzibari wamepokea haya mapendekezo kama vile ndio yamepitishwa. Jamani Tanzania ina watu wengi wenye mitazamo na uelewa tofauti. Wengine ni wana Chadema lakini si lazima mtazamo wako ufanane na wa uongozi wako ambao kwao vile vile kunaweza kuwa na tofauti ila demokrasia tu imetumika i.e. wengi wape.

On Thursday, January 10, 2013 10:55:17 AM UTC+3, Said Issa wrote:
Kaka Matinyi,
 
>sisi tunataka NDOA kamili.

Kama unataka ndoa kamili, basi bora utafute mwari mwengine, kwani huyu keshatoroshwa!
 
...bin Issa.

From: Mobhare Matinyi <mat...@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wana...@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, January 9, 2013 10:59:14 PM
Subject: RE: [wanabidii] Wazanzibari wasema - " Ahsante Chadema"!

John, nenda kawape wenzako jibu hili linaloanza hivi:
 
Jamani Watanzania wenzangu, huku ni kuchanganyikiwa ingawa kunatia moyo kwamba watu bado mnautaka Muungano wetu.
 
Mfumo wa serikali tatu kama shirikisho ni sera ya vyama vyote vya upinzani na baadhi ya Watanzania na hata CUF wamekuwa wakiihubiri kwa miaka yote hadi pale Maalim Seif alipobadilika na kuanza kuuhubiri muungano wa mkataba kana kwamba kuna miungano isiyokuwa na mikataba.
 
Hoja ya muungano wa mkataba inataka mambo ambayo yakitekelezwa huu muungano hautakuwepo na ndicho ambacho watu wa Tume - akina Warioba - huwa wanawauliza wanaoutaja muungano wa mkataba kwamba wanamaanisha hivyo au vinginevyo.
 
Mfano wa muungano wa mkataba unaotolewa eti ni EU na hiki kilichosemwa na Chadema hakina sura ya EU bali sura ya shirikisho kama yalivyo mashirikisho ya nchi nyingi duniani, mfano Nigeria, Sudan, Ujerumani, India, Kanada, Brazil, Marekani, n.k. Mashirikisho haya pamoja na hili la Chadema yana "sovereign state" moja yenye serikali zaidi ya moja LAKINI huu muungano wa mkataba unaosemwa eti utakuwa na sovereign states zaidi ya moja na hakutakuwa na serikali ya shirikisho bali mfumo kama wa EU ambao ni kama huu wa AU na huu si muungano kamili bali ushirikiano tu.
 
Hii ni tofauti kubwa mno na kama watu hamuijui, basi ni kweli kwamba hata mnachokidai hamkijui.
 
Tofauti ya shirikisho la Chadema na haya ni kwamba shirikisho la Chadema lina serikali kuu dhaifu mno inayozungukwa na serikali mbili zenye nguvu. Huwezi kudumu katika mfumo wenye serikali kuu dhaifu kiasi hiki na pengine tujiulize kwa nini serikali za mashirikisho mengine duniani hazina hii sura? Kumbukeni Muungano wa Kisovieti, kwamba pale ulipokuwa na serikali ya shirikisho dhaifu ndipo hapo ulipovunjikilia mbali.
 
Huo muungano wa mkataba unaodaiwa bila kueleweka na hata wanaousema ni mwepesi kuliko mfumo uitwao "confederation" ambao huziunganisha nchi katika masuala ya ulinzi na sera za nje/uhusiano wa kimataifa, kama zile jamhuri za iliyokuwa USSR. Mkishakuwa na sovereignty states zaidi ya moja, na hamna vitu hivi viwili vya pamoja, basi mnaweza kweli mkawa kama EU au AU iwapo mtakubaliana kushirikiana lakini huo si MUUNGANO tunaoutaka siye wengine; sisi tunataka NDOA kamili.
 
Matinyi.
Date: Wed, 9 Jan 2013 09:51:07 -0800
From: nkumb...@yahoo.com
Subject: [wanabidii] Wazanzibari wasema - " Ahsante Chadema"!
To: wana...@googlegroups.com

Default Wazanzibari wasema - " ahsante chadema"!

Dear All,
Wazanzibari wameishukuru CHADEMA kwa dhati kabisa kwa kumfunga na kumziba mdomo yule mwanachama wao anaeitwa Mzee Mwanakijiji ambae alikuwa akikebehi na kusema kuwa hauna mantiki yoyote Muungano wa Mkataba unaotaka serikali tatu.
Shukrani hizo zilitolewa jana baada ya Chadema kuwasilisha waraka wa maoni juu ya Katiba Mpya kuhusu Muungano - maoni ambayo ni sawa na yale ya Muungano wa Mkataba ambao Wazanzibari ndio wanaoutaka.
Tarehe 16 December, 2012 lile blogu la Wazanzibari lijulikanalo kama Zanzibar Ni Kwetu (ZNK) lilichapisha barua moja kutoka kwa Mzee Mwanakijiji ambayo ilibeza mantiki ya kuwepo kwa Muungano wa Mkataba ambao jana chama cha Mzee Mwanakijiji kiitwacho Chadema kiliupendekeza kwa kutaka Muungano wa Shirikisho kama ule wa European Union ambao ndio ulikuwa nyimbo na ngoma ya Wazanzibari siku zote hizi.
Katika barua hio, Mzee Mwanakijiji aliwasulubu Wazanzibari kwa kuandika kuwa..."hoja wanayoitoa ni ile ya kutaka Zanzibar kwanza, dola kamili, ikiwa na mamlaka yake yote. Hoja hii kwa Kiingereza inaweza kufupishwa kwa maneno mawili tu "FULL SOVEREIGNTY" yaani "HAKIMIYA KAMILI". 
Aliendelea Mzee Mwanakijiji..."Katika historia ya dunia jamii za watu zinapodai 'DOLA KAMILI' wakimaanisha dola yenye hakimiya kamili maanake ni kuwa jamii hizo zinatawaliwa na wengine....", aliandika Mzee Mwanakijiji.
"Chama cha Mzee Mwanakijiji (Chadema) jana kiliwasilisha mapendekezo kadhaa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba; mojawapo ilikuwa ni kutaka kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika, ambayo itakuwa HAKIMIYA KAMILI na MAMLAKA KAMILI ya Rais. Suala kwa Mzee Mwanakijiji ni hili: Chadema kutaka serikali yenye hakimiya kamili kwa Tanganyika, je, Tanganyika inatawaliwa na nani?". Aliuliza Mzanzibari mmoja alipokuwa akihojiwa na Wagagagigikoko, huku akiwa hana mbavu kwa kucheka kama vile Mzee Mwanakijiji alikuwa mbele yake.
" Mzee Mwanakijiji can now see the meaninglessness of his earlier assertions when he now refers to the official stand of his own party", aliendelea Mzanzibari huyo, huku akionywa kutotumia kimombo katika mahojiano hayo.
"Hayo hayo waliyoyatamka Chadema ndio ambayo tunayasema sisi Wazanzibari kila siku. Tukisema sisi tunafanyiwa nongwa na tunaelezwa tutoke na tutalipwa TSHS Bilioni 400, sasa leo Mzee Mwanakijiji atasema nini baada ya chama chake mwenyewe kuyatamka rasmi hayo hayo, tena hadharani? Atakiaga bye bye chama chake au vipi?". Aliendelea kuuliza Mzanzibari huyo.
"Strategy yetu Wazanzibari wote hivi sasa ni kukipigia kura Chadema katika 2015, kwasababu tunajua kuwa sisi na Chadema tunakuenda kwa pace moja." Alimalizia huyo jamaa.
Juhudi za kumtafuta Mzee Mwanakijiji kwa simu ili kumuuliza nini 'mantiki' ya mapendekezo ya Chadema au nini ilikuwa tofauti baina ya Muungano wa Mkataba na huu wa Shirikisho wanaoutaka Chadema hazikufanikiwa, kwani simu yake ilikuwa imezimwa. 
"Vyenginevyo, sisi Wazanzibari tutamsaka Mzee Mwanakijiji mpaka tumpate ana kwa ana ili atuombe radhi kutokana na barua zake za nyuma za kiburi alizokuwa akizitawanya kila pahala kuhusu juhudi zetu za kuigomboa nchi yetu", alimalizia msomaji mmoja wa Zanzibar Ni Kwetu.

Chanzo: Jamii Forums.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment