Tuesday 8 January 2013

Re: [wanabidii] TAARIFA YA BAVICHA KUWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE

Aliyesema malaria imeanza kupanda nilimuuliza kupanda wapi- Kichwani alikataa kunijibu.
Nimeanza kupata jibu mwenyewe

--- On Tue, 1/8/13, hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com> wrote:

From: hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] TAARIFA YA BAVICHA KUWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, January 8, 2013, 4:48 AM

Hatujadili Kigwangalla hapa, tunajadili CDM. Hata hivyo kuna mengine aliyoyasema kuwa ana matumaini makubwa sana kwangu huko siku za mbele kwenye uongozi wa Taifa letu. Hilo nalo hukulisikia?
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: josephludovick@gmail.com
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 8 Jan 2013 12:43:22 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] TAARIFA YA BAVICHA KUWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE

Kama wewe usivyokuwa na Impact yeyote ile.umemsikia Mungu wako jana aliposema unakuwa wakati mwingine na kichaa hivyo wanakudhibiti na yale makofi ya polisi?
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: hkigwangalla@gmail.com
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 8 Jan 2013 12:38:59 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] TAARIFA YA BAVICHA KUWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE

Kwa nini hawakuanza na msaliti nambar wan.....Slaa na kadi yake ya CCM? Au yeye ni untouchable? Si nilisikia kuwa yeye ndiye mwenye mchango mkubwa kwenye chama na hivyo analipwa mshahara mkubwa sana kushinda ule wa Ubunge eti kwa kuwa walimlazimisha kugombea Urais huku wakijua hatoshinda, sasa wanam-compensate!? Only to find that he is into both parties! Kwa nini mnahangaika na hawa vijana wapiga siasa za dot.com? Hawana impact yoyote ile!

Regards,
HK.
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 8 Jan 2013 01:19:59 -0800 (PST)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] TAARIFA YA BAVICHA KUWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE

Inapanda wapi? Kichwani? Utafungiwa?!

--- On Mon, 1/7/13, KULWA MAGWA <magwakulwa12@gmail.com> wrote:

From: KULWA MAGWA <magwakulwa12@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] TAARIFA YA BAVICHA KUWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, January 7, 2013, 8:27 PM

Malaria sasa inaanza kupanda polepole na tusubiri tuone

2013/1/7 ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Kati ya mambo ambayo CHADEMA wanastahili kuigwa hi hili la kutomuonea aibu mtu. Ninafikiri wakiwa madarakani hawawezi kumheshimu waziri kwa uwaziri wake akafanya uharibifu wakakaa kimya.

--- On Mon, 1/7/13, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] TAARIFA YA BAVICHA KUWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, January 7, 2013, 11:38 AM

Taarifa kwa Vyombo vya habari juu maamuzi ya kikao cha Kamati Tendaji ya Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA)

Ndugu waandishi wa habari, baadhi yenu mnafahamu kuwa Baraza la Vijana la Chadema Taifa (BAVICHA), limefanya kikao cha kawaida cha Kamati Tendaji, juzi 5 Januari 2013, katika Hotel ya Benzi Garden jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, kilijadili masuala matatu mazito.

Kwanza, Kamati Tendaji ilijadili kwa kina suala la kuporomoka kwa elimu nchini, ambapo serikali imepunguza alama za viwango vya kufaulu, jambo ambalo limesababisha mamia ya wanafunzi waliochaguliwa kutokuwa na sifa.

Pili, Kamati Tendaji ilijadili jinsi Bavicha itakavyoshiriki katika maandilizi ya utekelezaji wa maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema yalioeleza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma.

Tatu, Kamati Tendaji ilijadili kwa kina "Tuhuma za usaliti na njama za kuvuruga chama, kutukana viongozi wakuu wa chama na kuvuruga wanachama wa Chadema na Baraza kwa ujumla."

Ndugu waandishi wa habari, yapo baadhi ya vyombo vya habari jana na leo vimeripoti kwa upotoshaji mkubwa wa baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na kikao hicho. 

Kwa mfano, gazeti moja la kila siku limemtaja mwanachama wetu mmoja kuwa ndiye aliyekuwa mtoa taarifa wetu muhimu na kusema mbunge mmoja wa CHADEMA alijadiliwa katika kikao hicho kuwa ni miongoni mwa kundi hili la MASALIA na kufika mbali zaidi kwa kusema, "…sasa amekalia kuti kavu."

Lakini ukweli wa kilichojadiliwa kikaoni ni huu ambao tunaueleza sasa:

Kwanza, kuhusu ajenda ya kuporomoka kwa elimu: Kamati Tendaji imeagiza kuwa utafiti uliofanywa na BAVICHA katika ngazi ya sekondari, ambao umegundua madudu mbalimbali, uongezwe hadi shule za Msingi na taarifa yake ililetwe kwenye kikao kijacho cha Kamati Tendaji.

Kwenye ajenda ya pili: Kamati ya Utendaji BAVICHA, ilipokea na kujadili agizo la Kamati Kuu ya Chama iliyoeleza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma. 

Katika ajenda ya tatu juu ya tuhuma za usaliti na njama za kuvuruga chama, kutukana viongozi wakuu wa chama na kuvuruga wanachama wa CHADEMA, na Baraza, Kamati ya Utendaji ilipokea taarifa ya Kamati Ndogo ya Kamati Tendaji iliyoundwa Septemba mwaka jana kwenye kikao chake kilichofanyika mjini Morogoro. Kamati ilipewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha kazi hii.

Katika hili, watuhumiwa wakuu walikuwa ni kama ifuatavyo:

  1. Juliana Shonza, Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa
  2. Habib Mchange, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA
  3. Mtela Mwampamba, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA
  4. Gwakisa Burton Mwakasendo, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA
  5. Joseph Kasambala, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA

Aidha, baada ya Kamati iliyoundwa kuwahoji baadhi ya watuhumiwa na wanachama wengine mbalimbali, ilibaini kwamba wapo baadhi ya wanachama wa BAVICHA ambao wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika tuhuma hizi. Hao ni pamoja na Ben Saanane – maarufu kama Eight Oclock.

Katika orodha hiyo, wakatajwa pia Exaud Mamuya lakini kamati ikashindwa kumpata Mamuya kwa kuwa hakukuwa na mawasiliano ya kutosha.

Ndugu waandishi wa habari, hizi sasa ni tuhuma za kila mmoja:

Ndugu Juliana Shonza:

Alituhumiwa akiwa katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA, amekuwa akishirikiana na baadhi ya watu kupanga njama na kufanya usaliti dhidi ya Baraza, Chama na vijana wenzake wapenda mabadiliko nchini.

Amekuwa akifanya mikutano na vikao vya siri, kwa manufaa ya CCM, akiwakusanya vijana wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali waliosimamishwa masomo au kufukuzwa vyuoni kwa kutimiza wajibu wao wa kudai haki zao za msingi na uwajibikaji wa serikali na ambao ni wanachama wa CHASO. 

Juliana alifanya kazi yake hiyo kwa ushawishi wa hongo, ili wakubali kuitisha mkutano na waandishi wa habari, watoe matamko machafu dhidi ya CHADEMA na viongozi wake wakuu, akiwamo Dk. Willibrod Slaa na Freeman Mbowe.

Mfano dhahiri hapa ni kikao alichofanya Baa ya Highland iliyoko maeneo ya Makumbusho, majira ya saa 9 hadi saa 11, ambapo aliwaita viongozi wa CHASO, akawashawishi kuwa watakuwa na maisha mazuri, watarudishwa vyuoni na kutunzwa vizuri hapa mjini kama anavyoishi yeye, endapo tu watakubali kufanya press conferences na kuisema CHADEMA kuwa inawavuruga vijana walioko vyuoni.

Tarehe 6, Desemba, 2012 Hotel MIC, kuanzia saa 10 hadi saa 12, aliwaita baadhi ya vijana ambapo yeye na wenzake walipanga njama za kukichafua chama na kutukana viongozi, kwa manufaa ya CCM.
Ifuatayo hapa chini ni moja ya sms ambazo Juliana Shonza alikuwa akiwaandikia vijana katika ushawishi wake wa usaliti kwa mapambano haya ambayo chama chetu kinafanya, kuwapigania Watanzania maskini na wanyonge katika nchi yao;

"jembe chukua bodaboda basi jamaa washatia timu hela yako yakulinda mfuko wako utaikuta tumempa eddo mnaetoa naye tamko tutalindana tu jembe usijali."

Huu ni moja tu kati ya ushahidi mwingi, wa meseji, simu, sauti, video, picha na vikao kadhaa katika maeneo mbalimbali, unaomwingiza Shonza na wenzake wengine katika sifa mbaya ya usaliti wa chama, baraza na viongozi wake na wanachama wenzao na umma wa Watanzania kwa ujumla. 

Hapo alikuwa akimwandikia mmoja wa viongozi wetu ili ashiriki katika press conference ambayo yeye Makamu Mwenyekiti kwa kushirikiana na wenzake wengine, walikuwa wameiandaa kwa nia ya kuchafua chama, kulichafua baraza, kutukana viongozi waandamizi pamoja na kuvuruga na kuchonganisha wanachama wa CHADEMA.

Matokeo ya kikao hicho cha MIC Hotel, yalionekana siku moja baada ya kikao hicho, ambapo mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Edo Mwamalala, aliyeshiriki kikao hicho cha MIC Hotel, aliitisha mkutano na waandishi wa habari, akijitambulisha kuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA, cheo ambacho hakuwa nacho. 

Aidha, Shonza amekuwa akikutana na kufanya vikao vya siri na wenzake, wakipanga njama za kufanya kazi na majukumu ya CCM kuhujumu BAVICHA pamoja na CHADEMA. Mikakati ya kuvuruga baraza, kuchonganisha wanachama na kutukana chama na viongozi wakuu, kwa siri na hadharani, imekuwa ikipangwa katika vikao hivi. 

Amebainika kukiuka kipengele cha 10.1(x) cha Maadili ya Viongozi, cha Katiba toleo la mwaka 2006, kinachomtaka kiongozi yeyote asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali, kwa kuzingatia taratibu na kanuni za chama.

Ameonesha ubaguzi wa kikabila na kikanda kupitia maandiko yake kwenye mtandao kwa kutumia jina lake, anapungukiwa na sifa muhimu na mahsusi za kuwa kiongozi, kwa mujibu wa kipengele cha 10.1(iv) kinachomtaka kiongozi yeyote asijihusishe na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini au ukanda vinavyolenga kuleta ubaguzi ndani ya chama.

Kwa kushiriki vikao vya kuanzisha chama kipya kinachoitwa CHAUMMA, kushiriki katika makundi yaitwayo MASALIA na PM7 ambayo yote yalikuwa na lengo la kuvuruga chama na wanachama, kukosanisha na kutukana viongozi wa chama, ndugu Shonza amevunja kipengele cha 10.1(i),(viii)(ix) na ibara ya 10.2(iv).

Kwa kushiriki vikundi hivyo hapo juu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya BAVICHA wamejiridhisha pasi na shaka kuwa Shonza haendani na katiba, falsafa, sera na maadili ya chama makini na tumaini la watu, CHADEMA. Hivyo kwa mujibu wa ibara ya 5.1.4 na 5.1.5 anakosa sifa za kuwa mwanachama wa Baraza la Chama.

Kwa kutoa tuhuma za uongo dhidi ya wanachama na viongozi wenzake, ameendelea kuvunja kanuni za uendeshaji kazi za chama ibara ya 10.1(viii). 

Amehusika katika kuanzisha, kujihusisha na kuratibu moja kwa moja kundi la vijana waliokuwa wakizunguka mikoani na kushawishi viongozi wa vijana kutoa matamko kwa kutumia jina la CHADEMA kufanya kazi na majukumu ya CCM ya kukichafua chama, kugombanisha wanachama na kumtukana Katibu Mkuu kwa kutumia propaganda za CCM.

Kamati Ndogo ilimuita Ndugu Shonza ili kumhoji. Lakini aligoma kwa madai kuwa haitambui kamati hiyo na wala hajui kuwa kuna mgogoro, jambo ambalo limetushangaza wengi kwa kuwa Ndugu Shonza alikuwapo katika kikao cha Morogoro kilichounda Kamati hii.

Ndugu Shonza pia hakuhudhuria kikao cha Kamati Tendaji cha juzi kwa madai kuwa amebanwa na shughuli za familia. Baada ya kupitia maelezo yote hayo, Kamati Tendaji iliamua yafuatayo:

Ndugu Juliana Shonza, amepoteza sifa na uhalali wa kuwa mwanachama wa Chadema kwa kukiuka ibara ya 5.3.4 na ibara ya 10.1(ix) ya katiba ya CHADEMA na hivyo imeamua kumuondoa katika nafasi yake ya makamu mwenyekiti na kumfuta uwanachama wake. 

Hivyo basi, kwa maamuzi hayo ya Kikao cha Kamati ya Utendaji ya BAVICHA, kuanzia juzi tarehe 5 Januari 2013, Ndugu Juliana Shonza, si mwanachama wa BAVICHA na hivyo moja kwa moja amepoteza sifa za kuwa kiongozi wa baraza na kwa nafasi yake aliyokuwa nayo ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara. 

Habib Mchange:

Huyu alituhumiwa kutoa tuhuma za uongo, zikiwemo za mauaji, kinyume na maadili ya Wanachama (kipengele cha 10.3(3); kuunda vikundi vinavyojulikana kwa majina ya MASALIA na PM7 – Pindua Mbowe.

Pia Ndugu Mchange alituhumiwa kuwavuruga wanachama, kuwachonganisha na kuwatukana viongozi, kisha kushiriki vikao vya kuanzisha chama kingine cha siasa cha CHAUMMA.

Alituhumiwa pia kupotosha maamuzi halali ya vikao vya chama na Baraza hivyo kuendelea kukipaka chama matope.

Kamati ilimuita Mchange, na kumhoji juu ya tuhuma zinazomkabili. Hakufika. Badala yake, aliandika barua kueleza kuwa hana imani na kamati:

Aidha, pamoja na Mchange kugoma kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Kamati Tendaji, Sekretarieti ya Kamati Tendaji Taifa, ilimuita Ndugu Mchange kuhudhudhuria mkutano wa Kamati Tendaji ili kujibu tuhuma zinazomkabili. 

Mwaliko huu ulifanywa kwa njia ya barua na simu. Njia hizo ndio zilizotumika kualika wahusika wote wakiwamo wajumbe wa Kamati Tendaji, 

Ndugu waandishi wa habari, baadhi yenu mnafahamu kwamba Ndugu Mchange alikuwa miongoni mwa wanachama wa BAVICHA waliotaka kuwania nafasi ya uenyekiti wa taifa wa baraza hili. Jina lake liliondolewa na Kamati Kuu ya CHADEMA, kutokana na kukosa maadili ya uongozi.

Kamati Tendaji baada ya kusikiliza hoja yake hii, ikajiridhisha kuwa mtuhumiwa ameamua kuibuka hoja hiyo ili kutaka Kamati Tendaji isimjadili ili aendeleze mradi wake wa kukichafua chama akiwa ndani ya chama.

Hivyo Kamati Tendaji imefanya yafuatayo: Imempata na hatia ya kuvunja ibara ya 10.3(iii) na kwenda kinyume na kanuni za uendeshaji wa chama ibara ya 10.3(4), kinyume na Maadili ya Wanachama (kipengele cha 10.3(3); uendeshaji wa chama ibara ya 10.3(4) na kwamba mambo yote haya yanadhihirisha kuwa Ndugu Mchange hayuko tayari kushirikiana na viongozi wake kama mwanachama, hivyo kukiuka katiba ya chama ibara ya 5.3.4 na kuafikiwa uamuzi wa kumfukuza uwanachama wa Bavicha na Chadema.

Mtela Mwampamba:

Huyu ametuhumiwa kutoa tuhuma nzito za uongo hadharani, zikiwemo za mauaji, kinyume kabisa na Maadili ya Wanachama (kipengele 10.3(3).

Kuvunja katiba ya chama ibara ya 5.3.4 na Kanuni za Uendeshaji kazi za chama Ibara ya 10.3(4) kwa kupotosha maamuzi halali ya vikao vya chama na baraza na kukipaka matope chama pamoja na kudhihirisha kuwa hayuko tayari kushirikiana na viongozi wake kama mwanachama.

3.Amevunja Katiba ya CHADEMA ibara ya 5.3.3 na 5.3.4 kwa kutoa kauli za kichochezi dhidi ya chama, kuwachonganisha wanachama na kuwatukana viongozi.

4.Kwa kujiunga na vikundi vinavyoitwa MASALIA NA PM7 na baadae kushiriki vikao vya kuanzisha chama cha CHAUMMA, Ndugu Mwampamba amevunja ibara ya 10.3(iii).

5.Kinyume na ibara ya 5.3.3 na 5.3.4 ya Katiba ya CHADEMA na Ibara ya 4.3(g) na (i) ya kanuni za BAVICHA, zinazopinga ubaguzi wa aina yoyote ile, Ndugu Mwampamba ameonesha hisia za ubaguzi wa kikabila na kikanda.

Gwakisa Burton Mwakasendo:

Huyu amekuja kwenye kikao na kukiri kutenda makosa yake ambayo takriban yote ni sawa yanayowahusu watuhumiwa waliotangulia hapo juu. Mbele ya kikao cha Kamati ya Utendaji alikiri kushiriki vikao, akisema kuwa 'lakini' alilazimika 'kuikimbia' dhambi kwa kuondoka katika baadhi ya mikutano na watu hao, wakati mwingine hata nyumbani kwake hakuweza kulala akihisi 'dhambi' hiyo anayoikimbia itamfuata nyumbani.

Kamati Tendaji, iliamua kumpa adhabu ya kuwekwa chini ya uangalizi kwa mwaka mzima, katika wakati wote huo amezuiwa kugombea nafasi yoyote ndani ya BAVICHA na onyo kali la barua.

Ben Saanane:

Huyu pamoja na kwamba hakuwa miongoni mwa watuhumiwa alipewa adhabu ya onyo kali na uangalizi wa miezi 12, kutokana na makosa yafuatayo. Kutoa tuhuma nzito, zinazomhusu pia Kiongozi wa juu mwandamizi wa chama, Ben amekiuka Maadili ya Wanachama (kipengele 10.3(3).

Kukiri kuwa mmoja wa waanzilishi wa vikundi vinavyoitwa MASALIA na PM7 na kisha kushiriki vikao vya kuanzisha chama kingine cha CHAUMMA, amevunja ibara ya 10.3(iii), kwa nia ya kuvuruga chama na kutukana viongozi wake:

Mbele ya Kamati Tendaji, Ben alikiri makosa na akaomba radhi.

Aidha, Ben alitoa ushirikiano mkubwa kwa Kamati Ndogo jinsi ya kupatikana kwa taarifa na ushahidi wa namna wanachama wa BAVICHA walivyokuwa wanafanya kazi za kundi hili la MASALIA na PM 7 na hasa juu ya majina wanayotumia katika mitandao mbalimbali ya kijamii, wakifanya juhudi za kuivuruga CHADEMA, kuvuruga BAVICHA, kutukana viongozi na kuwavuruga wanachama, lakini kikubwa wakionesha kila dalili ya tabia ya usaliti.

Exaud Mamuya:

Huyu hajapata nafasi ya kusikilizwa kwenye vikao. Hivyo suala lake litaendelea kufanyiwa kazi na uongozi wa BAVICHA.

Aidha, kikao cha Kamati ya Utendaji pia kilipitisha kwa kauli moja, moja ya maazimio ya BAVICHA Mkoa wa Mwanza, waliopendekeza kufukuzwa uanachama kwa aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Mwanza, Salvatory Magafu, kwa tuhuma za kukiuka Kanuni ya 10.1(xii) kwa kutoa tamko kwenye vyombo vya habari kwa nia ya kumfarakanisha Katibu Mkuu na wanachama wa CHADEMA na umma wa Watanzania, ikiwa ni sehemu ya uratibu wa kundi lililokuwa likiendeshwa na watuhumiwa wengine hapo juu.

Kamati ya Utendaji pia ilimkuta na makosa ya kiuongozi katika tuhuma zilizowasilishwa vikaoni na kufanyiwa kazi na Kamati Ndogo, Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Mbeya, Joseph Kasambala na hivyo amepewa adhabu ya onyo kali. 

Hitimisho
Tunaomba kuwahakikishia vijana wenzetu wa CHADEMA na wengine wote wapenda mabadiliko nchini, hakuna kijana mwanachama wa BAVICHA, atafanya kazi za kuhujumu baraza na chama kwa ujumla na kusaliti matumaini pekee ya Watanzania, akifanya kazi za mahasimu wetu, kisha akaachwa. 

Ni lazima na muhimu tuoneshe kuwa tuna uthubutu kwa kuchukua hatua kadri inavyotakiwa, pale panapotakiwa. Tuliopewa dhamana za uongozi, tutatimiza wajibu kuhakikisha hakuna mtu ataonewa wala kupunjwa haki yake katika kusimamia utendaji na utoaji utumishi bora wa baraza kwa wanachama wake na chama kwa ujumla. 

Daima tutasimamia katiba ya chama, maadili, kanuni, taratibu, itifaki na miongozo ya mabaraza. Baraza hili halitakuwa tayari kuwa sehemu ya kuruga matumaini makubwa ya Watanzania waliyonayo juu ya CHADEMA. 

Baraza liko imara. Wanachama wetu wasifadhaishwe na upotoshaji unaofanywa na wasaliti kuwa tumevurugika au 'kumechafuka'. Hatuwezi kuchafuka wala kuvurugika kwa kuchukua maamuzi dhidi ya watu wabinafsi wanaotaka kukwamisha mapambano ya awamu ya pili, kupigania mabadiliko ya kweli ya kimfumo na kiutawala, kwa ajili ya Watanzania.

Historia inatuonesha kuwa mara zote ambapo mapambano yamefikia hatua ya juu ya kutimiza malengo, ndipo ambapo wasaliti hujitokeza. Hivyo vikwazo hivi vya baadhi yetu kuanza kugeuka nyuma ni dalili za mwisho mwisho kuwa ushindi unakaribia. Ni lazima kama vijana tuendelee kujenga imani na matumaini ya Watanzania waliyonayo juu ya CHADEMA kutukabidhi dola mwaka 2015.

Mwisho

Imetolewa leo Januari 7, 2013, Dar es Salaam na;

John Heche
Mwenyekiti wa Taifa, 
Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA)

--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment