Tuesday 8 January 2013

Re: [wanabidii] TAARIFA YA BAVICHA KUWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE

who is next?!ZK?!

On Tuesday, January 8, 2013, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
> Tatizo ni njaa zinazowasumbua hawa akina chumia tumbo kwa kukubali kununuliwa na maasidi wa CHADEMA. Nawapa heko CHADEMA kwa kubaini nyoka hawa na kuwatimua. Binafsi nashindwa kuelewa siasa za namna hii kama zina maisha marefu, bila shaka ni kutapatapa kwa mfa maji. Chama hakiwezi kuimarika kwa kuvivuruga vyama vingine bali ni kuyashughulikia matatizo ya wananchi. Mchezo huu ulianzia kwa chama cha NCCR Mageuzi, Ukaingia TLP na sasa upo CHADEMA.
>
> Nguvu za vyama vya upinzani zinatokana na madudu yanayofanywa na CCM. Siku CCM ikiacha madudu vyama vyote vya upinzani vitakosa nguvu. Mbinu wanazotumia CCM hazina msaada wowote kwa vile kiini cha nguvu kiko palepale hakijaguswa. Ipo siku watu wataamua kuingia barabarani bila hata kutumia chama chochote.
>
> Watu wanajiunga na vyama vya upinzani kwa sababu wanaona chama kilichopo madarakani kimeshindwa kuwaletea maendeleo wanayotarajia na badala yake kinawadhoofisha. Kama sababu ni hizo CCM haiwezi kufanikiwa kuwarudisha wanachama kwa ghiriba hizi za kitoto. Kama fedha ya kutuhonga watu wote ipo ileteni tuitafune na kuwaunga mkono lakini kama ni hiyo ndogo ya kuwapa akina chumia tumbo au tia mchuzi pangu pakavu wa BAVICHA tatizo litabaki vilevile
>
> Waviache vyama vya upinzani vifanye kazi, waache woga wa ushindani kimsingi wanayo nafasi nzuri maana karibu kila kitu wanacho wao. Inashangaza mtu anapokuwa na nguvu kama hiyo lakini anaogopa ata ata kivuli cha mpinzani wake. Mtu wa namna hiyo ni dhaifu sana japo kwa umbo la nje anaonekana ni mwenye nguvu. CHADEMA endelea na fagio lenu hadi uchafu wote uishe
>
> 2013/1/8 paul lawala <pasamila292000@gmail.com>
>
> Safi sana
>  
> Polepole tunaanza kujenga taifa la uwajibikaji na kutooneana haya, hizi hatua zinazochukuliwa zina faida kubwa si kwa CHADEMA tu bali kwa taifa zima
>
> 2013/1/7 KULWA MAGWA <magwakulwa12@gmail.com>
>
> Malaria sasa inaanza kupanda polepole na tusubiri tuone
>
> 2013/1/7 ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
>
> Kati ya mambo ambayo CHADEMA wanastahili kuigwa hi hili la kutomuonea aibu mtu. Ninafikiri wakiwa madarakani hawawezi kumheshimu waziri kwa uwaziri wake akafanya uharibifu wakakaa kimya.
>
> --- On Mon, 1/7/13, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
>
> From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
> Subject: [wanabidii] TAARIFA YA BAVICHA KUWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE
> To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Monday, January 7, 2013, 11:38 AM
>
> Taarifa kwa Vyombo vya habari juu maamuzi ya kikao cha Kamati Tendaji ya Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA)
>
>
> Ndugu waandishi wa habari, baadhi yenu mnafahamu kuwa Baraza la Vijana la Chadema Taifa (BAVICHA), limefanya kikao cha kawaida cha Kamati Tendaji, juzi 5 Januari 2013, katika Hotel ya Benzi Garden jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, kilijadili masuala matatu mazito.
>
> Kwanza, Kamati Tendaji ilijadili kwa kina suala la kuporomoka kwa elimu nchini, ambapo serikali imepunguza alama za viwango vya kufaulu, jambo ambalo limesababisha mamia ya wanafunzi waliochaguliwa kutokuwa na sifa.
>
> Pili, Kamati Tendaji ilijadili jinsi Bavicha itakavyoshiriki katika maandilizi ya utekelezaji wa maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema yalioeleza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma.
>
> Tatu, Kamati Tendaji ilijadili kwa kina "Tuhuma za usaliti na njama za kuvuruga chama, kutukana viongozi wakuu wa chama na kuvuruga wanachama wa Chadema na Baraza kwa ujumla."
>
> Ndugu waandishi wa habari, yapo baadhi ya vyombo vya habari jana na leo vimeripoti kwa upotoshaji mkubwa wa baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na kikao hicho. 
>
> Kwa mfano, gazeti moja la kila siku limemtaja mwanachama wetu mmoja kuwa ndiye aliyekuwa mtoa taarifa wetu muhimu na kusema mbunge mmoja wa CHADEMA alijadiliwa katika kikao hicho kuwa ni miongoni mwa kundi hili la MASALIA na kufika mbali zaidi kwa kusema, "…sasa amekalia kuti kavu."
>
> Lakini ukweli wa kilichojadiliwa kikaoni ni huu ambao tunaueleza sasa:
>
> Kwanza, kuhusu ajenda ya kuporomoka kwa elimu: Kamati Tendaji imeagiza kuwa utafiti uliofanywa na BAVICHA katika ngazi ya sekondari, ambao umegundua madudu mbalimbali, uongezwe hadi shule za Msingi na taarifa yake ililetwe kwenye kikao kijacho cha Kamati Tendaji.
>
> Kwenye ajenda ya pili: Kamati ya Utendaji BAVICHA, ilipokea na kujadili agizo la Kamati Kuu ya Chama iliyoeleza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma. 
>
> Katika ajenda ya tatu juu ya tuhuma za usaliti na njama za kuvuruga chama, kutukana viongozi wakuu wa chama na kuvuruga wanachama wa CHADEMA, na Baraza, Kamati ya Utendaji ilipokea taarifa ya Kamati Ndogo ya Kamati Tendaji iliyoundwa Septemba mwaka jana kwenye kikao chake kilichofanyika mjini Morogoro. Kamati il

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment