Friday 25 January 2013

Re: [wanabidii] Re: Sitta: Nafaa kuwa Rais

Kaka Hamisi unasema hayo baada ya kusoma vipi huyu mzee alivyotaharuki baada ya kuukosa U-speaker?
Hivyo kama angelikuwa honest kweli angelibabaika kama alivyobabaika pale alivyoukosa huo U-speaker?
To many of us he is just like any other politician (including yourself) in this country - chakula cha simba!

//John Nkumbaruko.


From: Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, January 25, 2013 3:01:24 PM
Subject: Re: [wanabidii] Re: Sitta: Nafaa kuwa Rais

Katika wanasiasa wachache waliopo huyu Mzee vana kiwango cha juu sana cha kuwa 'honest'...akigombea atawasumbua sana wenzake...ana akili nyingi sana huyu Mzee. Atanipa taabu kuchagua baina yake na wengine wawili ninaowapenda, kama watajitokeza nao ofcoz...


2013/1/25 Said Issa <saidissa100@yahoo.com>
Fredy, uyasemayo ni kweli.
Yatamkuta, kwasababu kwanza safari hii urais ni zamu yetu Wazenj.
Pili, tumesahau jamani mara ile nini alitueleza Dr Slaa juu ya Sitta?
Hebu jamani tujikumbushe kidogo kabla hatujamtaja tena huyu Nd. Sitta kwa position ya urais wa nchi yetu tukufu:


...bin Issa.


From: Fredy Lema <fredylema@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, January 25, 2013 2:39:41 AM
Subject: Re: [wanabidii] Re: Sitta: Nafaa kuwa Rais

Yaliyomkuta katika uspika katika chama chake kwa karata ya mwanamke yatamkuta pia kwenye uraisi sijui amejiandaaje na hilo.

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, 25 January 2013, 9:40
Subject: [wanabidii] Re: Sitta: Nafaa kuwa Rais

Asububiri mchakato wa kumpata mwakilishi wa chama chake akajieleze ,
wamkague , vyombo vya ulinzi na usalama vimkubali .

On Jan 25, 8:45 am, Fred Alphonce <fredrick197...@yahoo.com> wrote:
> SOURCE http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1674756/-/bo3nriz/-...
> WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kwamba anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania na anafikiria kugombea 2015, iwapo dhamira yake itaridhika na mazingira na upepo wa kisiasa wa wakati huo.
> Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili juzi, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri.a
> Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong'ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
> "Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee," alisema Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge.
> Hata hivyo, alisema hana mkakati wowote sasa wa kuendesha harakati za kutafuta nafasi hiyo kwa udi na uvumba kama baadhi ya wengine (bila kuwataja), wanavyofanya... "Sina sababu za kuanza kutafuta support (kuungwa mkono) wala uundaji wa kamati za ushawishi kwa watu sasa," alisema Sitta.
> Badala yake alisema atasubiri hadi muda wa kuchukua fomu za kugombea utakapofika ndipo atakapojitathmini na kusema endapo atabaini kuwa Watanzania wengi wanamuunga mkono, atachukua uamuzi wa kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho.
> Aitahadharisha CCM
> Waziri huyo aliwahadharisha wanachama wa CCM kwamba wasipokuwa makini, wanaweza kuipoteza nafasi hiyo ya urais na kwenda kwa vyama vya upinzani.
> Alionya kuwa iwapo watamteua mtu asiye mwadilifu, Watanzania hawatamchagua na badala yake watampa nafasi hiyo mgombea yeyote kutoka vyama vya upinzani.
> Alisema Watanzania wengi wana werevu wa kutosha kujua watu ambao ni mafisadi na ambao wamekuwa wakitumia fedha zao chafu kwa ajili ya kutaka wakubalike mbele ya macho ya Watanzania. Alisema suala la uadilifu ni moja ya vigezo muhimu ambayo CCM wanapaswa kuvizingatia ili kupata ushindi wa kiti cha urais mwaka 2015.
> "Ndiyo maana nilipokuwa mbele ya Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba niliweka wazi kwamba Tanzania tunahitaji kuwa na jopo la kuhoji viongozi na wananchi wawe na fursa ya kuwachambua," alisema Sitta.
> Alisema kinachohitajika Tanzania ni mfumo ambao utajenga mazingira ya kuwa na viongozi waadilifu katika ngazi zote.
> Alisema hali hiyo itaepusha mfumo unaoonekana sasa wa viongozi kwenye ngazi mbalimbali kuishi kiujanjaujanja, kujinufaisha na kutojali athari kwa uchumi wa nchi na Watanzania kwa ujumla.
> Alitoa mfano wa uzembe uliofanywa na viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambao umesababisha Bandari ya Dar es Salaam kupoteza uaminifu kwa nchi mbalimbali zinazopakana na Tanzania.
> Alisema uzembe huo umeifanya Bandari ya Dar es Salaam kuingiza Sh38 bilioni kwa mwezi tofauti na Mombasa ambayo inaingiza Sh300 bilioni.
> CCM ni imara?
> Akizungumzia miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM, mbunge huyo wa Urambo Mashariki alisema anaamini kwamba chama hicho kimefanya vizuri licha ya kuchafuliwa na watu wachache kutokana na tabia zao za ufisadi.
> Alisema CCM kinakubalika kutokana na sera zake, lakini pia sifa za kada mmojammoja zinawavuta Watanzania wengi kwenye chaguzi mbalimbali.
> Alitoa mfano wa CCM kuendelea kuwa na wabunge wengi, alisema hali hiyo inatokana na wale wanaogombea kuwa na heshima ya kipekee kwa jamii.
> "Ninaamini CCM bado itaendelea kuwa na wabunge wengi japo imetetereka wakati fulani kutokana baadhi ya makada kutuangusha," alisema Sitta.
> Alisema anaamini kuwa sasa CCM itajisafisha na kuondokana na sifa hiyo mbaya kupitia uongozi wa sasa ambao wamepewa jukumu la kukirejeshea heshima.
> Rushwa kwenye chaguzi
> Akizungumzia kuhusiana na rushwa kwenye uchaguzi, Sitta alisema ipo haja ya sheria kuweka wazi suala hilo kutokana na kuingiliana na ukarimu wa kawaida ambao ni utamaduni ya Waafrika kutafsiriwa kama ni kosa.
> Alitoa mfano wa mgombea akipata wageni nyumbani kwake asubuhi na ikabidi aandae chai nyingi kuwatosheleza waliomtembelea, inaweza kutafsiriwa kuwa ni rushwa. Hata hivyo, alipinga baadhi ya watu wanaotaka wagombea waidhinishiwe kutoa usafiri kwa watu wanaokwenda kwenye mikutano yao.
>
> Fred
> MATURITY does not come with age, it begins with acceptance of Responsibility
> Change is Essence to maturation

-- 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment