Yona,
Sahihisho kidogo. Kwangu mimi salamu hiyo au salamu nyingine yeyote, sina tatizo nayo. LAKINI unachotakiwa kujua ni kuwa tofauti ya uislam na ukristo ni kwamba ukristo ni maisha ya kiroho, uislam ni mfumo wa maisha ya kila siku. Ni mfumo unaoelezea mwana-Adam aishi vipi, avae vipi, serikali iendeshwe vipi. Ndiyo maana huwezi kutofautisha uarabu na uislam. Ndiyo maana asalam aleikum ni salamu ya kiarabu na hivyo ni salamu ya kiislam. Au Yona unaijua salamu ya kiislam zaidi ya asalam aleikum.
Mimi najiuliza, hata kama nikisalimiwa kwa salamu ya kiislam au kilokole au hata ya kijadi inanidhuru au kuniathiri nini. Kwangu sioni tatizo kama ninajua namna ya kuitikia. Lakini kwa Shekifu ambaye kusalimia kwa salamu ya kiarabu/kiislam wakati yeye mwenyewe si muislam wala mwarabu, anaowasalimia si waislam wala waarabu, is very awkward. Ningeweza kuelewa kama ambaye aliitoa salamu angekuwa muislam/mwarabu akiwasalimia wakristo au waswahili, au mkristo akiwasalimia waislam/waarabu, au muislam/mwarabu akiwasalimia waislam/waarabu. Kwa mkristo kuwasalimia waislam kwa salamu ya kiislam au kinyume chake inapendeza maana inaonesha jinsi jamii yetu ilivyochanganyika, inavyoheshimiana na kuthaminiana katika kile ambacho mwenzie anakiamini.
Bart From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, January 8, 2013 12:12 AM
Subject: [wanabidii] Re: Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani *
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, January 8, 2013 12:12 AM
Subject: [wanabidii] Re: Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani *
Mbunge shekifu hakuwa na sababu yoyote ya kuomba radhi kwa kutamka
asalam aleikum , Hii sio salamu ya kidini ni salamu ya lugha ya
kiarabu inayotamkwa dunia nzima na kwa maeneo kama ya Tanga ukanda wa
pwani hiyo imezoeleka sana .
Naungana na ndugu Matinyi alivyosema watu kutanguliza utaifa badala ya
dini na makabila .
On Jan 7, 11:23 pm, Edgar Mbegu <emb...@hotmail.com> wrote:
> Matinyi
> Huyu bwana alienda Kanisani siku ya Jumapili, na si katika Mkutano wa hadhara aliouitisha yeye. Kanisani kuna salamu zake ambazo si za "kishabiki" au za "kipumbavu" kama unavyodai wewe, maadamu zinatolewa mahali panapohusika. Si ndiyo uhuru wa kuabudu huo kadiri ya Katiba yetu ambao hata wanasiasa wanao?
> Kama unadhani alipaswa kuwasalimu kwa salamu za "kitanzania" , angeitisha mkutano wa hadhara na kuwasalimu watu kwa salamu hizo. Kama ni mwanasiasa tu na hana dini alikwenda Kanisani kufanya nini? Maadamu alienda Kanisani, siku ya Jumapili katika Ibada, na yeye pengine ni muamini wa Kanisa hilo, alipaswa kuwasalimu kwa salamu ya Kanisa husika; na waamini walimzomea kwa sababu alitoa salamu ambayo huwa haitumiki Makanisani hata kama maana yake ni nzuri namna gani. Isipokuwa, katika vyombo vya habari vya taifa, unasikia mtangazaji kabla ya kuanza kipindi anatoa salamu zinazohusika na dini fulani, hapo nadhani siyo mahali pake. Au katika semina za kiserikali... hapo salamu hizo hazihusiki. Mimi naona, aliyekosea ni yule aliyemualika huyo bwana aongee katika hadhira ile, kama nani? Kama ni muamini wa kanisa hilo, si alienda kusali tu kama wengine? Kwa nini apewe nafasi ya pekee ya kusalimia au kuongea? Ina maana katika Kanisa hilo kila mgeni hupewa nafasi kama hiyo?
>
> From: mati...@hotmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: RE: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani *
> Date: Mon, 7 Jan 2013 16:43:13 +0000
>
> Musa Juma,
>
> Suala la dini ya Shekifu halina maana yoyote hapa. Suala kwamba alikuwa na nia njema halina maana yoyote hapa. Suala kwamba waumini walimzomea lina maana kubwa, kwamba wanahisi alifanya kosa, aliwaudhi. Lawama zote zinapaswa kwenda kwa Shekifu kwa sababu hakupaswa kutumia salamu ya dini yoyote pale kanisani (hata ya kikristo) kutokana na hadhi yake ya uanasiasa.
>
> Mchungaji au padri angetumia salamu au kauli mbiu za kishabiki kama Asifiwe Bwana Yesu - mara sijui Tumsifu Yesu - hilo lingekuwa ni tatizo lake yeye na kanisa lake lakini huyu Shekifu ni kiongozi wa Watanzania wote kwenye jimbo lake, hivyo alipaswa na anapaswa kutumia salamu za Watanzania wote.
>
> Kuleta salamu zenye harufu ya udini ni ukosefu mkubwa wa busara katika zama hizi za udini kuinyemelea nchi yetu. Huyu mtu aache salamu za kipumbavu hizi. Hakuna lugha laini hapa - hizi ni salamu za kipumbavu. Wanasiasa wanaozitumia wapaswa kuzomewa kokote kule. Uanasiasa haufi mtu akiingia kwenye nyumba ya ibada.
>
> Kwani sisi Watanzania hatuna salamu za tamaduni zetu katika lugha ya Kiswahili? Hatuna???
>
> Matinyi.
>
> Date: Mon, 7 Jan 2013 15:43:19 +0300
> Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani *
> From: mussas...@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> SHEKIFU hakukosea.
>
> WADAU katika mjadala huu, Mbunge huyu, hakukosea kwani salamu hiyo haina tatizo, kwa tafsiri yangu ndogo Mtu kusema: Asalam Aykum humaanisha rehema na amani iwe juu yenu,ukiitikia wa alaykum salama, kipifu na wewe pia.
>
> Sasa hapa hakuna udini
>
> ni muhimu watu kupunguza jazba katika mambo madogo madogo kama haya kwani hayajengi na kikubwa zaidi Shekifu ni Mkristo sasa kumzomea kwa salamu tu nadhani hajatendewa haki;
>
> Wadau mjadala huu ni funzo kuwa sasa Taifa liendapo sio salama sisi tuwe watoa elimu sahihi kwani chuki za kidini zimeanza kunutafuta.
>
> Mussa
> Arusha
>
> On Thu, Jan 3, 2013 at 1:07 PM, magreth Mulokozi <m.mulok...@gmail.com> wrote:
>
> This message is eligible for Automatic Cleanup! (m.mulok...@gmail.com) Add cleanup rule | More info
>
> Duu anatafuta kura za 2015 sasa , duu pole sana Nd Shekifu
>
> 2013/1/3 mati...@hotmail.com <mati...@hotmail.com>
>
> ....alikariri.....siyo alikalili.
>
> T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
>
> ----- Reply message -----
> From: "adeladius makwega" <makwadelad...@googlemail.com>
> To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Subject: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
> Date: Thu, Jan 3, 2013 4:46 am
>
> Shekifu aunza mwaka mpya Vibaya
>
> Mbunge wa Lushoto Hendry Shekifu ameuunza mwaka wa 2013 vibaya
> baada ya kuzomewa Kanisani na waamini katika sherehe za mwaka
> mpya baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimu washirika wa Kanisa Kuu la
> KKKT Lushoto Tanga.
>
> Ibada hiyo ya kuukaribisha mwaka mpya ilianza kwa waumini kupokea
> mahubiri ya mwaka mpya yaliyohubiriwa na Mchungaji Walelaza na
> baadae kufuatiwa na ibada ya ubatizo ambapo watoto wawili kutoka
> familia mbili walibatizwa.
>
> Mara baada ya ubatizo huo ibada ilifuatiwa na utoaji wa Sadaka
> huku mbunge huyo wa Lushoto akionekana kushiriki kikamlifu
> katika ibada hiyo .
>
> Akiwa amevalia suti ya rangi nyeusi yenye mistari midogo
> midogo miyeupe Mbunge Shekifu ambaye aliwahi kushika nyadhifa
> mbalimbali zikiwamo ukuu wa mkoa alipewa nafasi ya kusimama mbele ya
> waamini mithili ya kasisi.
>
> Nafasi hiyo ilitolewa wakati wa Matangazo huku mchungaji
> akiwaomba waumini hao kumsikiliza Mbunge wao ili awasalimu. Basi
> Mbunge Shekifu alisimama huku akiweka vizuri koti kwa kujifunga
> vifungo vya koti hili ambalo lilionekana kuutosha mwili wake
> mkubwa uliojengeka vizuri.
>
> Alikisogelea kipaza sauti mara alianza kuongea kwa
> kujiamini."Aslaam Aleikumuuu…" Duu utangulizi huo uliharibu hali ya
> hewa ya kanisa hilo wauumini kuanza kuzomea na kuguna kutokana
> salaam hiyo iliyotolewa mwanzoni katika sehemu isiyo sahihi.
>
> Hali hiyo iliwafanya waumini hao kuibua munkali huo kutokana na
> kitendo cha mbunge huyo pengine kukalili namna ya kusalimia watu
> katika majukwaa ya kisiasa bila ya kujua kuwa sasa madhari
> aliyokuwa nayo ilikuwa ya salaam moja tu kama sikosei ni Bwana
> Yesu asifiwe au Tumsifu Yesu Kristu.
>
> Hekima ilitumika pengine huku yule aliyempa nafasi ya kuwasalimu
> wauumini wake akijilaumu kuitoa nafasi hiyo iliyotia shubiri
> kanisani hapo na kuibua zomeazomea hiyo ambalo sio jambo la
> kawaida kwa waumini kufanya hivyo.
>
> Mchungaji Walelaze ilibidi kuinuka na kusema waziwazi kuwa Ndugu
> Shekifu umekosea sana kwanza ulitakiwa kujitambua kuwa wewe
> japokuwa ni Kiongozi pia wewe ni mkiristu lolote utakalo fanya
> popote pale tambua unamajukumu mawili kwanza ukiristu wako
> na pili kuwa kiongozi. Hapa ni kanisani ulitakiwa kuwasalimia
> waashirika kwa salaam yao siyo salaam hiyo uliyoitoa hapa.
>
> Basi mchungaji huyo alimaliza mtafaruku huo huku mbunge huyo wa
> Lushoto akishuka katika mimbari ya kanisa hilo kwa fedhea na
> kurejea katika kiti chake ambacho kilikuwa jirani na mlango wa
> kutoka nje ya kanisa.
>
> Mara baada ua ibada hiyo ya mwaka mpaya mbunge huyo alionekana
> kuwa mtu wa mwisho kuondoka kanisani mara baada ya washirika wote
> kuondoka lakini washirika hao walisema kuwa mbunge huyo
> amekalili kusalimia kwa salaam hizo ndiyo maana alipitiwa.
>
> "Mimi nilitaka Mbunge aombe msamaha kwa alilolifanya sio
> kuondoka kimya kimya tu hawa wanasiasa hawana adabu kabisa wanakuja
> na mbwembwe alafu wanapata aibu."alisema mama mmoja
> aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Mama Sarah.
>
> Mshirika mwingine alimuunga mkono mchungaji Waleleza kwa kumkumbusha
> Mbunge huyo kuwa makini sana akiwa kanisani na kuheshimu salaam
> za ibada za makanisa sio kuja na salaam za nyumba zingine
> za ibada.
>
> "Pengine inawezekana Mbunge huyu asipewe tena nafasi ya
> kuwasalimu waumini kanisani kutokana na kosa hili," aliserma mzee
> mmoja wa makamo ambaye alidai kuwa hilo ni kosa baya.
>
> Mwishoni alionekana Mbunge Shekifu akiingia ndani ya gari yake
> nyeupe yenye Bendera ya CCM ikipeperuka mkono wa kushoto. Ndani ya
> gari hiyo kukiwa na akina mama watatu ambao walionekana wakifunga
> milango na dereva wa gari hilo akiondoa gari katika eneo la
> kanisa hilo.
>
> Wasalaam Adeladius Makwega
>
> --
> Jobs in Africa -www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs -www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> --
> Jobs in Africa -www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs -www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> --
> Jobs in Africa -www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs -www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> --
> Jobs in Africa -www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs -www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented ...
>
> read more »
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment