| Kwanza kwa sasa sidhani kama utapata ardhi Mtwara mjini. Yale maplot makubwa ya majumba ya zamani ya serikali, NHC etc kuna mahoteli. Ukanda wa bahari-mahoteli, peninsula za bahari ya Hindi Lindi hao customary owner waliopo huko na vibanda na vimnazi vyao naona watauza ardhi kwa mabilioni watu waweke mahoteli makubwa. Mtwara kumejaa wahindi, wachina, wasomali na kila jamii ya binadamu wanaotafuta kuwekeza. Mahelikopta ya huo utafiti wa mafuta na airwing yao ni tofauti na miaka ile. Utalii kuunganishwa na ule wa Kilwa Kisiwani-Mafia, Mikindani. Wale waliokando ya bahari Mikindani watanunuliwa watapata pesa za mtaji na wakitaka kuwa wabia. Mtwara-Lindi kuna maembe mengi anayonunua Bakhresa kwa sasa. Wakipanda mengi ya muda mfupi, kukazana na kilimo endelefu na ufuta na mtama unakuwa vizuri watauza value added crops. Bandari na daraja barabara kwenda Msumbiji na meli, lorries kwenda DSM hapo ni juhudi yao tu. Wakikazana na miradi ambayo ipo sasa kule ya Aga Khan, CONCERN, FAO, Janegoodal etc watafika mbali. Ila tu waache kukaa barazani kutwa longolongo. Bado hela za Mkuhumi. Wakianza uharibifu-watafukuza hawa wageni itakula kwao. +255762544553/754763803 --- On Sat, 19/1/13, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment