Saturday 19 January 2013

Re: [wanabidii] Re: MAANDAMANO MAKUBWA MTWARA - 19.01.2013



Mawazo yako mazuri Yona, lakini mzizi wa tatizo sio wanachi wa Mtwara na Lindi kudai gesi ni yakwao, mzizi ni uongozi mbovu wa nchi yetu,

Ninaposema uongozi mbovu ninaongelea mfumo wa kiutawala wa nchi yetu, mfumo wetu ni wa TOP-DOWN APPROACH  na sio BOTTOM-UP APPROACH.

TOP-DOWN APPROACH- ni mfumo wa kiutawala ambao hauhusishi watu wa chini (grass root people) katika maamuzi, mfumo huu hautaki kujua na hauna haja ya kujua nini athari ya maamuzi tunayotaka kufanya kwa jamii husika, au ni athari gani zitawapata wanajamii husika (katika impact area). Mfumo huu hautangulizi mbele mawazo ya wananchi na hautaki kujua machungu au hisia za wananchi, viongozi wakaa bungeni, vikaoni wanapitisha sheria hat bila kujali mwazo ya wananchi wa nchi wanayoiongoza.

Mfumo huu unasifa zifuatazo - Viongozi wake wana 'team-work' (Ushirikiano) wa kula rushwa kwa hali ya juu (Corruption syndicates), na kwa hiyo maamuzi yoyoyte kabla hayajafanyika lazima yaonyeshe kwanza uwezekano wa kupata 10% Commision, hata kama maamuzi hayo ni ya kuokoa maisha ya raia wanaowaongoza!! hata ikiwa ni misaada lazima ionyeshe dalili za 10%commission kabla haijakubaliwa au la haitakubaliwa.

Sifa ya pili, Policies na mikakati ya kitaifa yote inapangwa kwa kuangalia kwanza maslahi ya wachache walio juu (viongozi) elite group interest kwanza. iko mifano mingi tu likiwemo suala la kutaka kuamrisha pensheni za zisitoke ispokua mfu akifika umri wa miaka hamsini/sitini. n.k.

Sifa ya tatu, Wasomi wa nchi husika hawapewi nafasi ya kushiriki katika mikakati ya kuandaa policies na mikakati ya nchi yao, japo wamesomeshwa kwa kodi za wananchi wa taifa lao, hawahusishwi kuchambua, kufanyia upembuzi yakinifu na kushauri mustakabalii wa nchi yao. mawazo ya wasomi hayahitajiki, japo wamesomeshwa kwa gharama za nchi hiyo hiyo. Mfano Dr. Mkumbo Kitila na wengine, wataendelea kushauri mashirika ya uma tu sio serkali.

Sifa ya nne, Wabunge katika mfumo huo hupatikana kwa rushwa na maamuzi wanayoyapitisha  (Zikiwemo sheria za nchi) ni kwa rushwa huku wakijali kurudisha gharama zao walizozitumia katika uchaguzi kuingia bungeni.  n.k. Mifumo hii imetawala zaidi katika nchi za Sudan, DRC, Mali, Nigeria, n.k. na huu ndio mfumo unaotutafuna sisi hapa TANZANIA

Sifa ya tano, wananchi wa chini 'grass root people' hawajui kabisa kinachoendelea katika taifa lao! nani raisi hawajui, nini haki yao kutoka kwa serika yao hawajui, kusoma na kuandika hawajui, lini utafanyika uchaguzi hawajui, nani viongozi wa taifa lao hawajui!!! na wananchi wa kati nao hawaruhusiwi kujua mikataba ya serikali yao inayoingia au kusaini pamoja na wawekezaji au na mataifa makubwa kiuchumi wanaochuma mali asili za taifa lao. mikataba ya kitaifa na ya rasilimali za taifa ni siri. mfano, Mikataba ya madini, Gas, Mafuta, Richmond, TRL, RIGHTS, n.k.  

Madhara ya nchi kuwa na mfumo wa aina hii, ni kuwa Uchumi wa nchi utakua mikononi mwa wawekezaji na maamuzi makubwa ya kitaifa yatafanywa na wawekezaji kwa faida yao wenyewe na sio kwa faida ya wananchi wa nchi husika.

Pili, wakiwa na mali asili nyingi, wataimba midomoni mwao kuwa taifa lao ni tajiri ili hali wao wenyewe (80% ya wananchi wao) ni masikini wa kila kitu.

Tatu, taifa lao likiingia vitani wawekezaji wataishia kulinda maeneo yenye vitega uchumi vyao tu na sio taifa zima walimowekeza. mfano DRC na Sudan nk

Nne, Jamii zao/ wananchi wa nchi hizo hujaa hofu ya kufanya mapinduzi katk serikali zao, huku wakupata taizo lolote husingizia nchi jirani

Tano, huwa marafiki wakubwa wa mataifa tajiri duniani. na huwa na chuki kubwa na mataifa yenye mfumo tofauti na wa kwa wa BOTTOM-UP APPROACH kwa kutumiwa na

 



2013/1/19 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Waachiwe waandamane ni haki yao ya msingi kuandamana na kusema mawazo
yao wako huru kabisa .

Uhuru wao unaishia pale wanapoanza ubinafsi wa kwanza hiki ni chetu
sio cha watanzania , watanzania wengine hawaruhusiwi kunufaika na hivi
na vile hiyo sio sahihi .
Lazima watambue maeneo ya kusini yanafaidika zaidi na mradi wa gesi na
mafuta kwa kipindi kirefu kijacho nitatoa mfano kidogo chini .

Bandari zao zitapanuliwa na kuwa kubwa kwa ajili ya biashara hii ya
mafuta na gesi , wataweza kuuza sio dsm tu maeneo mengine ya nchi na
nchi jirani haswa kusini mwa nchi kama Malawi , Zambia , msumbiji .

Kuna hoteli n huduma nyingine mbalimbali zitajengwa na zimeanza
kujengwa kutokana na sekta hii ya mafuta maeneo ya kusini kwa ajili ya
wafanyakazi na wadau wengine wa biashara maeneo hayo .

Vyuo vya ufindi na mashule yatajengwa kutokana na vipato vinavyotokana
na sekta hii kwa ajili ya kuandaa wafanyakazi wa sekta hii na nyingine
zinazofanana kwa kipindi kirefu .

Sasa wananchi wakianza maandamano sasa hivi na virugu wajue fursa
nyingi watapoteza , wawekezaji wanaotoa mitaji yao kwa ajili ya ujenzi
na miundombinu ya mafuta na mengine wanapenda kuhakikishiwa usalama
wao na wa mali zao kwanza ndio mengine yaendelee .

Waangalie wasije wakakosa vyote , wasipoangalia itakuwa kama north
mara na maeneo mengine ya migodi kwenye vurugu ambapo makampuni
yanaweka mageti makubwa walinzi na silaha wao utawaona kwenye ndege
kutoka na kuingia tu .


On Jan 19, 1:41 pm, Sylvanus Kessy <frke...@yahoo.com> wrote:
> Ndugu wanabidii
> Mzimu wa Gas unaendelea kuitafuna nchi, ukianzia huku Mtwara. Leo wananchi wamehamasishana Wilaya zote, za Lindi na Mtwara ili kupinga GAS ISITOKE  Mtwara.
>
> Hakika Elimu na makubaliano yanahitajika. Viongozi wanaohusika watafute Hekima ya hali ya juu kutatua tatizo hili. Tukiendelea kusema ni wahuni watafanya mambo ya kihuni na tutapata hasara kubwa zaidi!
> sylvanus

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment